Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Pole kwa Watanzania wote wapenda 'DEMOKRASIA' na familia ya marehemu kwa ujumla.

Bwaba alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
 
Watu wasijehusisha hiyo accident na mgogoro wa kiuongozi aliokuwa nao ndani ya CHADEMA.

Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi. Sote ndiyo njia yetu hiyo.

Huu ndio uhuni ambao watanzania sasa hivi tumejiwekea kila kiongozi wa serikali akifariki wakati kuna zengwe watu wanasema kifo sio cha kawaida... aliohoji kifo cha Balali wako akina Dr. Salaa etc... sasa sijui na hiki nacho kina hitaji kuhojiwa...

Usitukane wakunga wakati uzazi ungalipo...

Inna Lillah Wainna Ilaih Raajiun
 
Mungu ailaze roho ya kaka yetu mahara pema pepote, tulimpenda lakini mungu amempenda zaidi.
 
Asubuhi aliongea na Mudhihir na Japhet (mkurugenzi wa shughuli za bunge ambaye pia alituhumiwa kuingia bungeni na Chenge kumwonesha kiti) alisema aliongea naye kuhusu hoja yake bungeni na akamwaga kuwa angeenda Tarime kwa shughuli za msiba.

Baadae Mudhihir akamfahamisha (mtu wa kwanza kutoa taarifa ni Mudhihir) Japhet kuwa mheshimiwa Chacha amepata ajali.

Kwa wakati huu mheshimiwa Japhet yupo hospitali ambako mwili wa marehemu umepelekwa.

You'll connect the dots yourselves.


Haya Bwana.....
 
Ametutoka shujaa mpiganaji wa haki.Poleni kwa sote.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi, Tutakukumbuka!
 
I dont want to appear to superstitious ila kuna uchawi humu na kama hamna basi it was a planned accident.Hivi ni wangapi walishakaa chini wakajiuliza kuhusu kifo cha Salome Mbatia?Mimi nina wasiwasi sana na hili.
May His Soul Rest In Peace and Our God Grant Him Eternal Life.
 
Hiyo Barabara ya Dar Mwanza imeanza kujengwa toka mwaka 1982 na Wataliani wakaondolewa, sijii wakaja kina nani lakini hadi leo hii jamani hata hizo single lane bado nasikia ndio kwanza zimevuka Dodoma na Upande wa Mwanza zimefika karibu na Nzega... lini Zitapanuliwa hata kufikia hadhi ya Highway? Mungu ndio anajua..
Nimesafiri hivi karibuni toka Dar kwenda Mwanza, barabara ni nzuri na ipo katika hali nzuri katika kilometa zaidi ya elfu ni kilometa 90 tu ambazo hazina lami na zipo kati ya wilaya ya Singida vijijini na Manyoni.

Barabara toka Mwanza hadi Shinyanga ipo katika hali nzuri ingawa inahitaji matengenezo katika sehemu chache sana. Matuta katika barabara hiyo ni makubwa na tahadhali kuwa kuna tuta mbele yako inatolewa mita chache kabla ya kukutana na tuta lenyewe. Hii ni hatari kwa dereva ambaye hana uzoefu na barabara hiyo aidha ni hatari zaidi kwa dereva anayesafiri kwa spidi ya zaidi ya km 160 kwa saa. Barabara hii inafaa kwa kwa mwendo wa sio zaidi ya Km 110 kwa saa huku ukiweka taadhali kubwa kwenye matuta.

Barabara toka Shinyanga hadi Singida haina tofauti sana na MZA-SHY, tofauti unapokaribia tuta kuna vituta vidogo maarufu kama rasta hii inasaidia kwa gari ambalo lipo katika mwendo kasi. Zaidi mipaka ya barabara na sehemu za wakaazi imewekwa. Hii inasaidia naitasaidia sana kuhifadhi eneo la barabara na iwapo kunahitajika upanuzi pasiwepo habari ya nyumba kuvunjwa au kulipa fidia.

SGD-DOM, barabara bado inajengwa na inaonekana itakapokamilika itakuwa katika kiwango cha hali ya juu. Mipaka ya barabara ipo, matuta yapo na ni makubwa kama ya SHY- SGD kuna sehemu wameweka rasta na kuna sehemu hakuna, hivyo taadhali ni muhimu. Katika barabara hii ndio kuna km 90 ambazo hazipo katika kiwango cha lami. Ni katika kipande hiki ambacho kinarefusha safari nzima ya DSM-MZA, kwani kukivuka kinahitaji zaidi ya masaa mawili na nusu kwa gari linalotembea kwa km 40-60 kwa saa.

DOM-MOR hii wengi wamepita na hali yake bado ni nzuri, matuta yake sio makubwa hivyo kufanya madereva wengi kwenda spidi kubwa, ni pana,na haina msongamano mkubwa wa magari.
 
R.I.P Chacha. Poleni sana wafiwa. Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kukipita kipindi hiki kigumu. Amen.
 
Tunawapa pole sana wafiwa.
Tutakukumbuka Bw. Chacha Wangwe..

Nirudie waliyosema wengine; kama ukitofautiana mtizamo na mtu akiwa hai, au ukiwa na mtizamo fulani kuhusu huyo mtu akiwa hai; baadae akifa haimaanishi kwamba msimamo wako na mtizamo wako utabadilika kwa sababu tu sasa ni marehemu.
He has passed .. watu wanatoa rambirambi , that 's how it should be regardless na tofauti zao wakati wa uhai wake
 
Wanabodi,

Nimeshitusha sana kwa kuona kwamba marehemu alikua akitumia gari dogo kwenye safari yake hiyo.

Mimi binafsi kwa kweli hivi vigari vidogo siviamini kwa usalama...
 
Chacha Wange:

Amevishinda vita vilivyovikuu, mwendo ameumaliza imani ameishika.

Roho yale ipumzike kwa amani AMEN
 
Marehemu Juma Salum,akiwa mwenyekiti wa Simba aligombana na wenzake wakaitwa Dodoma na waziri Sarungi (then) ili wasuluhishwe,akiwa safarini kurudi Dar akala mzinga,sasa na hii? mmmmhhh,Dodoma hii!
 
Wanabodi,

Nimeshitusha sana kwa kuona kwamba marehemu alikua akitumia gari dogo kwenye safari yake hiyo.

Mimi binafsi kwa kweli hivi vigari vidogo siviamini kwa usalama...

Usalama wa barabarani unategemea na vitu vinne tu:

(a) umakini wa dereva wa gari husika
(b) umakini wa watu wengine watumiayo barabara
(c) hali ya barabara yenyewe
(d) hali ya gari lenyewe.

Tairi zote kupata pancha klwa pamoja inaweza kuwa ni tatizo la barabara kuwa ilikuwa na misumari au gari ilikuwa na tairi za kipara. hatujui
 
Inna Lillah Wainna Ilaih Raajiun. Allah ndio muweza, pole kwa wana familia
 
Usalama wa barabarani unategemea na vitu vinne tu:

(a) umakini wa dereva wa gari husika
(b) umakini wa watu wengine watumiayo barabara
(c) hali ya barabara yenyewe
(d) hali ya gari lenyewe.

Tairi zote kupata pancha klwa pamoja inaweza kuwa ni tatizo la barabara kuwa ilikuwa na misumari au gari ilikuwa na tairi za kipara. hatujui
Kichuguu unasemaje? tairi ZOTE zilipata pancha KWA WAKATI MMOJA? hii kali. haya bwana RIP mpiganaji Wangwe.Sote kwa mola tutarejea.
 
I dont want to appear to superstitious ila kuna uchawi humu na kama hamna basi it was a planned accident.Hivi ni wangapi walishakaa chini wakajiuliza kuhusu kifo cha Salome Mbatia?Mimi nina wasiwasi sana na hili.
May His Soul Rest In Peace and Our God Grant Him Eternal Life.


kwa aliyesikiliza mahojiano ya TVT ....saa moja asubuhi...ndugu na jirani yake muheshimiwa joyce amehojiwa....na alieleza vema..
 
Marehemu Juma Salum,akiwa mwenyekiti wa Simba aligombana na wenzake wakaitwa Dodoma na waziri Sarungi (then) ili wasuluhishwe,akiwa safarini kurudi Dar akala mzinga,sasa na hii? mmmmhhh,Dodoma hii!

Mkuu inaelekea kuwa ni same story lakini hii ni completely different scenarios.

Marehemu Chacha Wangwe alikuwa na ofisi Dodoma yaani bungeni na hakuwa huko kwa ajili ya usuluhishi.

Ondokana na imani haba, Tanzania road safety rules hazifuatwi na watu tukiendelea kuendesha magari hovyohovyo ajali hazitakwisha,period.

R.I.P Chacha Wangwe.
 
Tarime tumepoteza mpiganaji na Mwenyezi Mungu ainue mpiganaji mwingine.
R.I.P Chacha mwana wa Wangwe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom