Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi ... hawa ni baadhi ya watanzania wachache wapambanaji ambao hawakuogopa chochote.
 
Kipande cha barabara ya Pandambili hadi Gairo - inavyodaiwa na wenyeji - kuna vibwengo vinavyokunywa damu za watu. Katika kipindi cha miezi 3 iliyopita mabasi ya Champion na Happy Nation yalipata ajali maeneo hayo hayo. Na wenyeji hao hao wanakupa uhakika kuwa ukitaka kumfanyizia mtu, sehemu hiyo huwa muafaka sana.
 
RIP Chacha Wangwe, sikuwahi kukusikia ila nakukumbuka siku ulipokuwa unachangia hoja kuhusu Bajeti 2008/2009 kama sikosei na ulipokuwa unajaribu kuelezea mapigano yanayoendelea Tarime. Poleni wafiwa
 
Amefariki muda si mrefu kwa ajali ya gari akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Pandambili (kama sijakosea).

Zaidi nitawafahamisha

poleni sana familia ya chacha.ndugu na jamaa wote.poleni wana tarime.poleni wapigania haki na wanademokrasia makini waliobaki ndani ya chadema...
.....................

hivi.....hii ingetokea kule sisiemu si watu wangeongea sana hapa....
 
Usalama wa barabarani unategemea na vitu vinne tu:

(a) umakini wa dereva wa gari husika
(b) umakini wa watu wengine watumiayo barabara
(c) hali ya barabara yenyewe
(d) hali ya gari lenyewe.

Tairi zote kupata pancha klwa pamoja inaweza kuwa ni tatizo la barabara kuwa ilikuwa na misumari au gari ilikuwa na tairi za kipara. hatujui

Nakubaliana na wewe mkuu!!! kuweka rekodi sawa ni kwamba tairi mbili za upande mmoja... yaani ya mbele na nyuma ndio zilizokuwa zimepasuka.

Ukubwa wa gari pia una kinga fulani... no wonder wamepewa mikopo ya magari kama nissan patrol na toyota landcruiser gx... haya yako salama zaidi kuliko Toyota Corrola...

Sipendi kusisitizia lakini surely... viongozi wetu wangetumia gari ambazo kidogo ziko salama zaidi... although hakuna 100% security/safety.
 
Wanabodi,

Nimeshitusha sana kwa kuona kwamba marehemu alikua akitumia gari dogo kwenye safari yake hiyo.

Mimi binafsi kwa kweli hivi vigari vidogo siviamini kwa usalama...

usiseme hivyo ndugu yangu ajali ni ajali tu...cha muhimu mwombe Mungu akulinde na ajali,majanga na mabalaa yote ili uendelee kumtukuza Yeye siku zote.
kwenye ajali hakuna cha gari ndogo wala kubwa .....usalama wetu upo mikoni mwake yeye Muumba wetu.
 
RIP CZW Mpiganaji

Mengi yatasemwa kama kawaida watanzania kuspeculate utadhania wanaweza kufanya kazi kama Scotland Yard.
Nadhani kama mnaona kuna ombeni msaada wa scotland yard waje wawasaidie kupata ukweli
 
Ndio Sababu Tunasema Wahamie Dodoma, Itapunguza Safari Mara Baada Ya Kazi, Kila Mara Wako Safarini Tuuuu.
Wakae Mahali Mamoja Kama Watu Wengine.
Wakisafiri Iwe Ni Lazima.
 
Nakubaliana na wewe mkuu!!! kuweka rekodi sawa ni kwamba tairi mbili za upande mmoja... yaani ya mbele na nyuma ndio zilizokuwa zimepasuka.

Ukubwa wa gari pia una kinga fulani... no wonder wamepewa mikopo ya magari kama nissan patrol na toyota landcruiser gx... haya yako salama zaidi kuliko Toyota Corrola...

Sipendi kusisitizia lakini surely... viongozi wetu wangetumia gari ambazo kidogo ziko salama zaidi... although hakuna 100% security/safety.

hapo ndipo watanzania wanaponishangaza ...wakinunua hayo mashangingi mnalalamika ...wakiendesha corola na kupata ajali mnataka wanunuliwe mashangingi...kweli siasa ya nji hii anaiweza lyatonga tu....
 
usiseme hivyo ndugu yangu ajali ni ajali tu...cha muhimu mwombe Mungu akulinde na ajali,majanga na mabalaa yote ili uendelee kumtukuza Yeye siku zote.
kwenye ajali hakuna cha gari ndogo wala kubwa .....usalama wetu upo mikoni mwake yeye Muumba wetu.

Kweli mkuu...

Lakini kumbuka kila siku malori yanaanduka lakini madereva wanakuwa poa.!!! lakini pia kumbuka magari mbali mbali ya safety level tofauti...

Hilo tu mkuu
 
Hebu walioko Dodoma waende gereji alikoipeleka gari chacha wangwe kabla ya kuondoka, wamuulize huyo Mallya, kwani gari ilikata stadi wakarudia njiani kabla ya kuipeleka gereji na kuondokea huko moja kwa moja. MWanae mmoja anayesoma form III yuko Dodoma na ndiye mwenye maelezo hayo
 
Nakubaliana na wewe mkuu!!! kuweka rekodi sawa ni kwamba tairi mbili za upande mmoja... yaani ya mbele na nyuma ndio zilizokuwa zimepasuka.

Ukubwa wa gari pia una kinga fulani... no wonder wamepewa mikopo ya magari kama nissan patrol na toyota landcruiser gx... haya yako salama zaidi kuliko Toyota Corrola...

Sipendi kusisitizia lakini surely... viongozi wetu wangetumia gari ambazo kidogo ziko salama zaidi... although hakuna 100% security/safety.

Mkuu heshima mbele.

Hakuna formula inayosema kwamba ukiwa na gari, farasi, trector, moped, lorry au pikipiki kwamba vinatofautiana kiusalama na kwamba eti ukiwa na 4x4 basi una angalau safety fulani hivi.

Vyombo vyote hivi pamoja na huyo farasi vinahitaji kuangaliwa (service) na kuhakikisha vipimo vya matairi viko ok na vipo tayari kwa safari hasa zile ndefu.

Hio ni mbali ya wewe dereva kuhakikisha umefunga mkanda, hujanywa pombe na unaweza kufuata barabara kwa umakini.

Bila hivyo ajali hazitakwisha au kuepukwa.
 
Jaman Spika amelia sana. na sasa wanakutana katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Huduma za Bunge. Kamati ya Uongozi ni kwa ajili ya mambo ya Kibunge na kamati ya huduma ni kwa mambo ya kiutawala
 
Ni sheria ya nchi kwa Mkurugenzi na yeyote yule mwenye mamlaka ya kiutendaji kuwa na driver but ktk hili Mh.Sitta speed zake hazina kiwango. I happened to hear Hon.Mudhihir akilitaka Bunge kuangalia nafasi ya madereva wao, na aliongea kwa uchungu sana pale aliporejea ajali yake na sasa anavyomtegemea sana Dereva ktk shughuli zake. Akasema alipokuwa waziri hakuwa na tatizo maana yule dereva alikuwa wa serikali na akakiri kuwa anaomba msamaha kwa kutolipigia kelele jambo hili huko nyuma.

Kimsingi hapa Serikali ilipaswa itumie fursa hii kuajiri madereva wa kudumu kwa bajeti ya Bunge, mimi nina ushahidi wa waathirika wa hali hiyo, maana madereva wengi wanajikuta wako ktk day work tu kumuendesha mbunge lakini kama ingelitolewa ajira ya mkataba ya miaka 5 kwao mambo mengi yangeliepukika.

Sasa kama Mkurugenzi,mkuu wa Idara wana madereva why not Mh.Mbunge.

Chacha Wangwe ,Komrade , nitadumu kukuheshimu kwa misimamo na uwazi wa maoni yako, CHADEMA this is your chance to reconcile ktk yale ambayo Wangwe aliona hayako sawa sawa ndani yenu, onyo kwenu "Mthibutu kuyadharau maana yatawarudia kama kivuli cha saa sita mchana"

Mwanga wa Milele akuangazie Mtumishi Chacha Wangwe,Upumzike kwa Amani.
Amen.
 
Jaman Spika amelia sana. na sasa wanakutana katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Huduma za Bunge. Kamati ya Uongozi ni kwa ajili ya mambo ya Kibunge na kamati ya huduma ni kwa mambo ya kiutawala
Sisi tulimpenda lakini MUNGU alimpenda zaidi. MUNGU aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi
 
LAKINI AIRBAG SYSTEM YA MASHANGINGI NI BORA KULIKO YA MARK 11...,NDIO MAANA WATAALAMU WA USALAMA WANAPENDEKEZA MASHANGINGI KWENYE OFFROAD AU SAFARI NDEFU.......HATA UKICHUNGUZA MISAFARA YA RAIS..OR THE LIKE KAMA ANAENDA SAFARI NDEFU ZAIDI YA KM 100 AU KWENYE BARABARA MBAYA ..HUPANDA MASHANGINGI..YAPO SECURED ZAIDI...

...AIRBAG INASAIDIA SANA..UKIONA ILIVYOMSAIDIA MTU KAMA KAPUYA ..UTAAMINI ...NA UKIONA NAMNA MAMA MBATIA AMBAYE KWA BAHATI MBAYA ILE NISSAN PATROL YAKE ILIKUWA OLD MODEL KIDOGO NA HAIKUWA NA AIRBAG...INGEKUWEPO ANGEWEZA KUTOKA MZIMA.....hata mtu kama MUDHIHIR alipopata ajali na cruizer yake kama sio AIRBAG zaidi ya kuumia angeweza hata kupoteza maisha...

SIKU ZA KARIBUNI WABUNGE WAMEKUWA HAWAPEWI CHAGUO LA MAGARI AMBAYO WANATAKIWA KUYANUNUA YAKIWA MAPYA..BUT I REMEMBER KABLA ..KILA BUNGE JIPYA LINAPOANZA DEALERS WA MAGARI MAPYA...LANDROVER,TOYOTA,NISSAM,MITSUBISHI ..ets walikuwa wanakaribishwa bungeni na wabunge walitakiwa wachague magari miongoni mwa make zinazoaminiwa na serikali.....baadaye naona huu utaratibu umeachwa na hii imesababisha wabunge wengi kuingizwa mkenge na wauzaji wa USED.....najua wabunge wengi tu ambao sasa hivi magari yao yanawasumbua sana...na hayakidhi mahitaji ya wanakotokea ..kutokana na kuchakaa haraka....

RIP Chacha,Poleni ndugu, marafiki na wana tarime na watanzania.
Pia watu humu tupunguze uzushi, hivi kila bunge likianza wakaenda car dealers na wabunge kuchagua magari hatutasema? mara ngaoi tunawalaumu na kuwanyoshea vidole eti wanaendesha mashangingi bila kujali wapiga kura wao? Tusiwe na double standards.
Chacha kaondoka na bila hiyana ndani ya kikolola chake not even a rav 4. Hakuwa ndani ya gari ya kifisadi.
Hivi mbowe na kambi yake wataenda kwenye mazishi baada ya majungu yote waliomfanyia?
 
Mungu ailaze pema roho ya mwenzetu Chacha Wangwe. Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wanaJimbo wake na wote ambao kwa njia moja au nyingine msiba huu umewagusa!!

Bwana alitoa, Bwana ametwaa.... Jina lake lihimidiwe!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom