Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Vitu vingine vinakuwa kama mchezo wa kuigiza hivi! si ni huyu jamaa alikuwa anaanza kungaa kwenye siasa? Halafu all of sudden anakufa,,,, simple! Kweli binadamu siyo kitu.
Kwa Wantazania wote tumempoteza kijana ambaye alikuwa ni mojawapo ya wanaharakati shupavu. Kwa kuwa Yeye aliyetupa ndiye aliyemtwaa, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN
 
RIP Chacha Wangwe,nimemsikia mtoto wa Chacha Wangwe akizungumzia namna alivyokuwa anamshauri aliyekuwa anaendesha gari hiyo Dennis Malya kuhusiana na uendeshaji wake wa rough wa gari.Inasikitisha sana!
 
Kwa walio na uwezekano wa kuona ITV ni vizuri wakaangalia hivi sasa.Kuna kipindi(recorded) kutoka katika eneo ambalo nadhani ni hospitali ulipo mwili wa marehemu.Wabunge na maofisa mbalimbali wa bunge wanahojiwa.Sorry kama kuna mtu atakuwa amekwishatoa habari hii tayari kwani sijaweza kuisoma thread yote.RIP Wangwe.
 
Aksante mwakyj kwa habari. Masikini inasikitisha but watanzania tushikamane katika huzuni hii. Tuhuzunike pamoja
 
Kwa kweli ni pigo sana kwenye harakati....za demokrasia nchini...kwa waliokuwa wanamchukia sababu zao binafsi...hawajui tu ila tumekosa na kumpoteza shujaaa wa kweli kabisa asiyeogopa vitisho .....RIP
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI,

Mheshimiwa Spika,

Nimepokea taarifa ya kifo cha Mbunge wa Tarime, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kwa masikitiko makubwa.

Kupitia kwako, napenda unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa wabunge wa Bunge lako Tukufu kwa kumpoteza mbunge mwenzao katika kipindi hiki ambacho wako katika kutekeleza majukumu yao waliyotumwa na Watanzania, ya uwakilishi.

Kwa masikitiko makubwa napenda kutoa salamu zangu za pole kwa wana familia, ndugu, wananchi wa Jimbo la Tarime, wanachama wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) na Watanzania wote.

Kifo huleta masikitiko na majonzi mengi katika familia na jamii, naungana nanyi ndugu zanguni katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo,

Mwenyezi Mungu awape imani na subira katika kipindi hiki kigumu na huku tukimuombea ndugu yetu, Chacha Wangwe mapumziko mema peponi.

Amina.


Wenu,





Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
29 Julai, 2008




NB: Lile ombi la wanaJF kwa ikulu kubadili email limesikilizwa! Angalia attachment.
 

Attachments

[B]mazishi ni alhamis na sio jumatano. kessho jtano asbh ndo mwili utasafirishwa kwa ndege maalum kwenda tarime. msafara utakuwa wa wanafamilia pamoja na wabunge wawili. then alhamis ndo msafara wa wabunge wengine utakwenda kwenye mazishi na kurudi the same day.[/B]
 
RIP Chacha Wangwe

Natoa mkono wa pole kwa familia na ndugu wa Marehemu Mh. Chacha Wangwe. Ninawaombea mwenyezi Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

Amina
 
Kwa hakika nimepatwa na mshtuko na mfadhaiko mkubwa baada ya kusoma taarifa ya kifo cha Mh. Wangwe.
Kwangu mimi Mh. Wangwe nilimwona kama mtu ambaye alikuwa tayari wakati wote kutetea maslahi ya walio wanyonge na kupiga vita ukabila, ubwanyenye na kutaka umoja na mshikamano wa makundi yote.
Kwa kawaida mpigania haki yeyote hawezi kupendwa na hilo Marehemu Wangwe alilifahamu na bila ya kuogopa aliendelea kupigania haki na maslahi ya watanzania na wanachadema wenzie waliokuwa ni wahitaji.
Vita kama hiyoinanikumbusha watu majasiri kama vile Edward Moringe Sokoine ambaye uhai wake ulimalizika katika barabara hiyohiyo kwenye ajali Aprili 12, 1984.
Lakini juu ya yote hakuna jambo la kupuuza, kwani siku za hivi karibuni Mh Wangwe alikuwa amejijengea maadui wengi hata ndani ya chama chake na hata wengine kudiriki kusema kuwa apigwe risasi, lolote linawezekana na lisemwalo lipo na huenda lilikuwepo na sasa limeshakuwa, si lazima apigwe risasi inawezekana akamalizwa kiaina kwani mafia ni wengi.
(Haya ni maoni yangu binafsi)
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI,

Mheshimiwa Spika,

Nimepokea taarifa ya kifo cha Mbunge wa Tarime, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kwa masikitiko makubwa.

Kupitia kwako, napenda unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa wabunge wa Bunge lako Tukufu kwa kumpoteza mbunge mwenzao katika kipindi hiki ambacho wako katika kutekeleza majukumu yao waliyotumwa na Watanzania, ya uwakilishi.

Kwa masikitiko makubwa napenda kutoa salamu zangu za pole kwa wana familia, ndugu, wananchi wa Jimbo la Tarime, wanachama wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) na Watanzania wote.

Kifo huleta masikitiko na majonzi mengi katika familia na jamii, naungana nanyi ndugu zanguni katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo,

Mwenyezi Mungu awape imani na subira katika kipindi hiki kigumu na huku tukimuombea ndugu yetu, Chacha Wangwe mapumziko mema peponi.

Amina.


Wenu,





Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
29 Julai, 2008




NB: Lile ombi la wanaJF kwa ikulu kubadili email limesikilizwa! Angalia attachment.

MegaPyne,

Shukrani; mimi nina kaushauri tu kadogo!!! Waambie jamaa wa-ikulu ni muhimu kufanya kama policy kwamba document zote za kutoka ikulu zitoke kama pdf format.
 
RIP CHACHA WANGWE. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe
 
SIKU 6 ZA MWISHO NA MAREHEMU CHACHA ZAKAYO WANGWE
na Hebron Mwakagenda

Tumekuwa marafiki na Marehemu Chacha Zakayo Wangwe aliyekuwa Mbunge wa Tarime mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Disemba 14, 2005 baada kuapishwa bungeni na kurudi kwenye chama Makao Makuu ambapo mimi nilikuwa msaidizi wa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na yeye akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama ilikuwa mapema Januari 2006 tukakutana naye na kuanza kuwa karibu. Nimemshuhudia akijenga hoja zake kwenye Kamati Kuu na Baraza Kuu la chama kwa nyakati tofauti tofauti.

Nimekutana naye katika nyakati tofauti Dodoma na Dar es salaama kwenye shughuli za bunge na chama. Tumekuwa karibu zaidi mara baada ya yeye kushinda uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambapo nilimpigia simu kumpongeza na kumuunga mkono kama ilivyo desturi yetu wanasiasa. Matatizo yalipoanza kwenye chama kati yake na viongozi wenzake alinipigia simu kujua mimi nasemaje nilimwambia tukutane tuongee. Tulikutana naye Kunduchi Beach Hotel kwenye Semina ya wabunge kuhusu madini iliyofanyika mwezi Aprili 2008 tulipoonana asubuhi akaniambia mchana wake alikuwa anaenda kuonana na kamati maalum ya wazee wa chama iliyokuwa imeundwa ili kutatua kilichosemekana kuwa ni mgogoro kati yake na viongozi wenzake.

Jioni aliporudi tulikuwa na sherehe fupi hapo hotelini Kunduchi Beach ambapo mgeni rasmi alikuwa rafiki yake wa zamani Wakili Tundu Lissu, mimi nilikaa naye meza moja pamoja na mke wake ambaye ni binti ya Marehemu Meja Jenerali Warden akanisimulia kwa ufupi kilichojili kwenye kikao chake na Wazee wa chama, baada ya siku 2 kabla hajaenda Dodoma kwenye bunge alipita ofisini kwangu mjini akaniachia nakala ya makaratasi yote na miniti za vikao na maamuzi yaliyokuwa yamefikiwa na kikao cha kamati ya Wazee. Baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Dodoma nilimtafuta kwenye simu bila mafanikio baada ya siku kadhaa akanipigia na kunieleza kuwa kilichotokea alikitegemea kwahiyo lazima tukutane ili tushauriane.

Zilipita siku kadhaa akiendelea kujibizana na wenzake kwa njia ya vyombo vya habari nikampigia simu nikamwambia kwa ufupi sana uko wapi? akanijibu kuwa yuko Dar! nikamwambia "Mbona unaonyesha silaha zote kwa adui? kwenye Baraza Kuu utaongea nini kama yote unaongea na vyombo vya habari" akasema kabla hajarudi Dodoma lazima tuonane na kujipanga upya.

KIKAO CHETU CHA MWISHO na Marehemu Chacha Zakayo Wangwe

Ilikuwa Jumatano iliyopita tarehe 23/7/2008 muda wa saa 6 alinipigia simu na kuniuliza niko wapi nikamwambia niko Mikocheni akasema nakuja nikamwambia usije kwanza nakuja mjini nakutana na mtu fulani halafu nitakupigia akasema angependa tuonane nje ya mji kidogo ili tuwe na utulivu nikamwambia sawa nikimaliza ningemfuata kokote atakakokuwa. Nikaenda mjini saa 9.30 nilitoka katikati ya mji na kuelekea barabara ya Bagamoyo nilipofika Oysterbay Polisi nikampigia akaniambia nirudi yupo Namanga niliporudi Namanga nikamkuta amepaki gari yake ndogo mbele ya duka la dawa linaloitwa Hoots the Chemist Limited ndani ya gari akiwa na mtu mmoja mwanaume akanitambulisha mimi lakini hakuniambia yule ndugu anaitwa nani akatoka kwenye gari akaomba kifimbo chake kwa yule ndugu ambaye alikuwa bado yuko ndani ya gari akampa akaaanza kuzungumza nikamwomba tutafute sehemu yenye faragha kidogo tukaingia kwenye sehemu inayouza chakula na vinywaji hapo hapo Namanga inaitwa Anne Shop tukakaa chini na kuanza mazungumzo yetu yaliyoanza kwenye saa 10.00 jioni na yaliyotuchukua kama muda wa saa 1.30 bila kula wala kunywa chochote.
Kwanza nilitaka kujua kilichojili Dodoma kwenye kikao cha Kamati Kuu kutoka kwake mwenyewe kwasababu nilikuwa na taarifa kutoka kwa watu wengine, akanieleza baada ya kumuuliza nasikia ulifanya haya na haya akawa mkweli kunieleza kila kitu kilichotokea Dodoma, nikamuuliza sasa unataka nini baada ya hapo? Akaniambia yafuatayo:-


"Mpiganaji jina langu limechafuka sana nataka nisafishwe jina langu kwanza" hata jimboni siwezi kwenda katika hali hii lazima niende mahakamani.
Pili nataka Demokrasia ndani ya chama chetu iongezeke
Tatu nataka hii dhana ya ukabila iliyojengwa na maadui zetu ndani ya chama chetu ifutike
Nne nataka ruzuku ya chama iende wilayani hilo nitapigania hata nisipokuwa kiongozi wa kitaifa katika chama.
Tano nataka tuchukue madaraka ya nchi haraka iwezekanavyo naona tunachelewa sana.

Tulipomaliza tukakubaliana kujiandaa kwa uchaguzi ndani ya chama na kuwa makini tunaongea nini na vyombo vya habari, nikamsindikiza kwenye gari yake na alionyesha kuwa angesafiri aidha siku hiyo jioni au kesho yake kwenda bungeni Dodoma.

Katika kipindi kifupi nilichomjua Marehemu Chacha Zakayo Wangwe alikuwa na tabia mbili ambazo tutazikosa ndani ya chama chetu kwanza ni Ujasiri wa hali ya juu alikuwa hamuogopi mtu yeyote ila alikuwa anawaheshimu watu wote. Tabia ya pili ni kusema kila anachoona ni sawa hata ukimbembeleza vipi ukampa msimamo wa chama kabla ya kikao kama hakubaliani nao lazima ataongea anavyoona yeye inafaa akitofautiana na msimamo wa chama kwenye kikao husika. Tumempoteza mpiganaji na mpambanaji mahiri katika medani ya siasa za Tanzania.
 
MegaPyne,

Shukrani; mimi nina kaushauri tu kadogo!!! Waambie jamaa wa-ikulu ni muhimu kufanya kama policy kwamba document zote za kutoka ikulu zitoke kama pdf format.

Kasheshe,

Nitajitahidi kuwafahamisha, lakini wao pia wapo hapa, watakuwa wameupata huo ujumbe.
 
Umenifanya nicheke msibani wewe. Umerahisisha mambo, ila watu wasije waka-spam kwenye hizo barua pepe.

Dogo,

Msiba uko wapi ?kuhusu spam..watapata tu hata zile picha zetu za wakati tutamtumia
 
mwanga wa milele umuangazie Eh Bwana, Roho yake ipumzike kwa amani, RIP CHACHA WANGWE, utakumbukwa kwa mengi, mazuri na mabaya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom