Nakubaliana na wewe mkuu!!! kuweka rekodi sawa ni kwamba tairi mbili za upande mmoja... yaani ya mbele na nyuma ndio zilizokuwa zimepasuka.
Ukubwa wa gari pia una kinga fulani... no wonder wamepewa mikopo ya magari kama nissan patrol na toyota landcruiser gx... haya yako salama zaidi kuliko Toyota Corrola...
Sipendi kusisitizia lakini surely... viongozi wetu wangetumia gari ambazo kidogo ziko salama zaidi... although hakuna 100% security/safety.
Kasheshe,
Unachoandika sio sahii kabisa, inaelekea hiyo ni group thinking ya watu wengi Tanzania na ndio maana viongozi wetu wanaongoza kwa kununua shangingi.
Gari kubwa sio kinga ya ajali. Tembelea hata websites tafuta safest cars.
Gari ndogo ni safe kama utalinganisha gari zilizo sawa kwa ubora na vifaa. Taili zikipasuka, matatizo yanatokana na gari kuviringika. Gari kubwa inaweza kuviringika zaidi ya gari ndogo, wote tumesoma center of gravity na jinsi inavyohama kirahisi kwa kitu kirefu.
Ukiachia Afrika na labda USA, viongozi karibu wote duniani wanatumia gari ndogo.
Faida ya gari kubwa ni kwamba ni comfortable kama unaenda safari za mbali na pia kwa watu wengine ni status, unaonekana uko juu ya watu wengine lakini SIO kweli kwamba magari makubwa ni salama kuliko madogo.
Ondoeni mawazo kama hayo ambayo hayaendani na facts zozote za maana, ni group thinking kama ile ya kwamba Saddam ana silaha kubwa, kiasi kwamba hata waliotakiwa kutafuta facts wakawa wanaandika tu bila uchunguzi.
Kama umeona picha mbalimbali za ajali duniani, utakuta gari ndogo imeharibika kabisa lakini baadhi ya watu wamepona, wakati hizo 4WD ni ngumu sana kupona kama impact ya collision ni kubwa.
Tatizo la Tanzania ni uendeshaji mbaya. Kuna watu wanasema barabara ya Dar - Dodoma ni nyembamba sana. Mnataka hiyo barabara iwe na ukubwa gani? Angalieni hata faida kiuchumi, hiyo barabara ukitafuta average ni kwamba gari linapita kila baada ya dakika kama kumi, matumizi yako chini sana ukiachia sehemu chache za mijini. Mnataka kutumia mabilioni ili kuzuia vifo kama 1000 kwa mwaka? Mna ushahidi gani kwamba hata barabara ikipanuliwa ajali hazitatokea shauri ya uendeshaji mbaya pamoja na magari mabovu? Economically unawezaje kuhalalisha kutumia mabilioni hayo kuokoa ajali kama 1000 huku watu malaki wanakufa shauri ya kukosa dawa? huku wakulima vijijini wanahangaika kwa umaskini shauri hakuna barabara za kufikisha mazao yao mijini? Kwa nchi ambayo robo tatu ya nchi haina barabara, utaongeleaje kujenga barabara kubwa zaidi ya iliyopo kwa Dar mpaka Dodoma?
Ukiachia USA ambako wana barabara kama viwanja vya ndege, hata hapa Europe barabara ndogo ziko nyingi tu hasa huko wilayani. Nimeendesha barabara nyingi tu hapa Europe, kwa mfano ukienda Scotland kutokea England, kuna barabara ndogo na magari ni mengi labda zaidi ya mara 20 ya TZ. Sisikii hata siku moja kwamba kule kuna ajali kuliko barabara za kuelekea London ambazo ni kubwa.
Matatizo mengi ya Tanzania ni sisi watu wake, tunashindwa kufuata sheria. Barabara ya 80km/h watu wanaendesha mpaka 150km/h. Watu wanaendesha wamelewa. dereva mmoja anaendesha hata miles zaidi ya 500 bila kupumzika, hakuna alama barabarani, polisi hawafanyi kazi zaidi ya kuchukua rushwa, magari mabovu, hayatakiwi hata kuwa barabarani. barabara nyingi hazitengenezwi, mashimo yanaibuka bila kuzibwa.
Matokeo yake tunajidanganya kwamba tukiendesha shangingi tutasalimika, sio kweli, hata Mbatia alikuwa na shangingi. Kuna mate wangu mmoja, kijana msomi karudi toka nje akajenge taifa, akagongwa na shangingi lake na hakupona. Kwa Tanzania hata unayefuata sheria bado unaweza kuwa victim maana waendeshaji wengine watakufuata hata kule unakoendesha salama au hata kukugonga ukiwa umesimama.
Tutasubiri mpaka watu wangapi wafe kabla ya kuchukua hatua?