kwa sababu kila siku ya Mungu, alikuwa akifuatana na mtoto wake aliyekuwa akimshikia dawa zake maalum za moyo,
Uchunguzi wa mwili wa marehemu ulisema hivyo hivyo kwamba kafa kwa heart attack ambayo ilikuwa ni matokeo ya intensive pressure aliyokuwa nayo kabla na kwenye hicho kikao.
Uchunguzi wa mwili wa marehemu ulisema hivyo hivyo kwamba kafa kwa heart attack ambayo ilikuwa ni matokeo ya intensive pressure aliyokuwa nayo kabla na kwenye hicho kikao. Kama una report inayosema tofauti, tuletee. Wakati anafariki 1997 wengine tulikuwa kwenye hivi vijiwe na suala lake lilijadiliwa vizuri sana kule Tanzanet.
Suala la kuzunguka kila sehemu na mtoto wake ni hearsay, hakuna ukweli kabisa. Ni mtoto gani huyo aliyekuwa anazunguka naye ili kumbebea dawa?
Kolimba alikuwa anaumwa, laiti hata angemwona daktari yoyote wa magonjwa ya moyo angemshauri kabisa asiende kwenye kile kikao akiwa katika hali ile. Au angechukua tahadhari muhimu kabla ya kwenda.
Wacha tuendelee na mambo mengine maana hili la mtoto kuwepo au kuto kuwepo haliongezi tija yoyote. Hata kifo cha Mwaikambo kilikuwa ni ajali tu. Inasikitisha kwamba lazima tuweke mkono wa mtu kwenye kila kifo. Tabia hii inatufanya tusiwe waangalifu maana tunaondoa uzembe kutoka kwetu na kuuhamishia kwa wengine. Badala ya watu kujifunza hapa kuwa na madereva wazuri, watu wanaamua kuwa vilaza bungeni na kutokukosoa mambo wakifikiri hapo hakutakuwa na mkono wa mtu. Hata watu wanaokufa kwa ngoma, tunasema kuna mkono wa mtu, hivi kweli tuko serious?
Mkuu Mtanzania,
Naona unajichanganya mwenyewe, niliposema ugonjwa wa moyo ulikata baadaye tena unasema kuwa alikufa kwa ugonjwa wa moyo, anyways siwezi kuamini maneno ya zaidi ya watoto wa marehemu, kwamba na wao wanadanganya hapana, kwamba eti wake za marehemu wanadanganya? hapana, a day kabla Kibona hajafariki nilikuwa naye nyumbani kwa balozi wetu DC wakati huo akiwa Nyirabu, sio siri kuwa hakuwa sawa sawa kwa sababu dalili zilikuwa wazi,
Mwaikambo, ile ajali walisoema imetokea mbele ya jengo la ubalozi wa Rwanda, nayo pia ilikuwa ni Ze-Comedy of all times, hakuna anayeweka mkono wa mtu, lakini watu wanaowajali marehemu wanapouliza serious questions with evidence, huwezi kuwa-dismiss kuwa ni hearsay, mke wa Rutihinda hawezi kuwa anasema uongo kuhusu kifo cha mumewe, kwa sababu waliomuua then waka-plant story kuwa alikuwa na ngoma, that is unfair kwa familia za marehemu,
Kushindwa kupata ukweli wa vifo vya viongozi wetu kwa sababu ya mazingara yanayokuwa under control ya waliohusika, haina maana kukata tamaa kabisa kwa sababu kuna siku zoezi linaweza kubadilika tukashika power watu wenye uchungu na taifa, tutazifufua kesi zote hizi bro na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria wahusika wote watakaokuwepo, maana wote wanafahamika na ushahidi upo, mkuu nimepoteza a relative na huu mchezo tayari na ninajua deatils zote za kifo chake, ambazo hazikusemwa na serikali, sasa kama wewe unaamini kuwa hawa viongozi wote wanaokufa kwa kutaka mabadiliko hawakuuliwa good for you, ila tu huwezi kuwa dismiss wanaofikiri tofauti eti kuwa ni uzembe wa kutaka kuhamishia kwa wengine mkuu that is very irresponsible statement kwa wenye ndugu waliwahi kufa kwa utata na wanaoujua ukweli, wake wa rutihinda na Kibona hawawezi kuwa wanasema uongo kuhusu vifo vya waume zao,
Waliokufa kwa ngoma wanafahamika haijawahi kuwa siri, Nyanda RIP alikufa kwa ngoma sio siri na kuna walioko kwenye power sasa hivi wana ngoma sio siri kabisa mkuu, kuwepo kwenye hizi forum wakati wa vifo vyao haibadli ukweli kuwa vifo vyao vina utata, halafu hizi precautions measures mnazozisema ingekuwa ni rahisi kujua kuwa leo unaenda kufa hivi ni nani asingezichukua mapema? Unafikiri Kolimba angekubali kwenda kwenye kile kikao? Au Wangwe juzi angekubali kusafiri?
I mean kutokukubali kwako na mijadala yaina fulani haina maana wengine wote tuache kujadili, in fact hiyo ndio hasa sababu tuko hapa JF ni kujadili ishus bila kuziogopa na kuelimishana kutokana na yal tunayoyajua, na tutaendelea kufanya hivyo bila wasi wasi wowote, kama vile tulivyojadili kifo cha Balali wewe ulisema hajafa ambayo ni haki yako na kuna tuliosema amekufa ambayo ni haki yetu pia, the ishu ni uzito wa hoja tu!
Ahsante Mkuu, na week end njema na kwako mkuu!.