Magabe Kibiti
JF-Expert Member
- Jan 20, 2008
- 292
- 2
this brings me to this question:
Kama baada ya ajali vitu vyote walivyokuwa navyo laptop, masanduku n.k viliibwa na hatujaambiwa kama vimepatikana TBC1 wamepata wapi nyaraka zinazoonesha kuwa katika safari hiyo alikuwa anaenda kufungua kesi na kuzungumza na vyombo vya habari isipokuwa kama na wao TBC walikuwa na taarifa hiyo kabla? au mtu mwingine zaidi ya Chadema alikuwa na taarifa hiyo ya safari?
Shimo hilo hawatatoka salama.
Swali zuri sana Mzee Mwanakijiji,
Mimi ningekuwa Tido Mhando ningeachana na huu upuuzi wa kutaka kugeuza kifo cha mbunge wa Tarime kupandikiza chuki zisizo na maana kwa wakazi wa Tarime na watanzania kwa ujumla. Hawa TBC wamejifanya kuwa wanacover hiki kifo cha Wangwe kwa muda mwingi lakini ukitazama content ya yote yale wanayotangaza utaona kabisa kuwa wana nia chafu kabisa isiyotakiwa kabisa kwa watanzania leo hii.
Uzushi tu na speculations na habari za uchochezi ndizo wanatoa. Kuna mtu aliwadanganya TBC kuwa watu wa Tarime ni mazezeta na wataanza tu fujo bila kufikiri na sasa wamegundua kuwa watu wa Tarime hatutaki kugawanywa kwa misingi yoyote ile wakati huu wa maombolezo.