Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
source www.michuzi-blog.com na picha ya MBOWE ipo anakimbikia kama nyambui.

Nimeamini kuwa wewe huna chembe ya ubinadamu na hisia za utu hata kidogo ila nakuhakikishia kuwa unachojaribu kufanya hakitafanikiwa na wakazi wengi wa Tarime ni makini na wenye uwelewa mkubwa kuliko ulivyofikiri.

Itakugharimu nini ukiacha mizaha kwenye msiba ambao maelfu ya wakazi wa Tarime tunalia na kuhuzunika kwa kilichotokea? Hata kama ni kutumwa na watu wenye nia mbaya kwa wakazi wa Tarime, je huwezi kusema NO na kuamua kuwa mstaarabu hata kwa siku moja au mbili?

Hatari kabisa kwa Tanzania kuwa na watu kama wewe wasiojali kabisa maisha na hisia za watanzania wenzao.
 
Autopsy ya kwanza imeonyesha nini ?

Kulikuwa na autopsy ya kwanza ?

Kuhani.. ipo autopsy ya kwanza; zikikubaliana na ya pili independently.. case closed. Hofu yangu ni kuwa mapema kesho watatangaza matokeo ya autopsy hii ya kwanza (iliyofanyika Dodoma chini ya mganga mpya kabisa wa Mkoa ambaye juzi ndiyo ilikuwa siku ya kwanza Dodoma!).
 
RIP Wangwe, jamani naomba tusiseme mengi tusubiri uchunguzi huru utaonyesha nini maana habari zinachangaya sana.
 
Date::7/31/2008
Wangwe ahofiwa kupigwa risasi familia yagoma kumzika
*Wahisi ana alama za kupigwa risasi shingoni
*Mbowe, Zitto wafanyiwa fujo msibani, wakimbilia Musoma
*Mrema, Mbatia, Lipumba wasema wataendelea kubaki

Waandishi Wetu, Tarime

NDUGU wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi Chadema wamegoma mwili wa ndugu yao kuzikwa ili kuruhu uchunguzi wa kifo chake ufanyike kutokana na hisia za wanafamilia kwamba alipigwa risasi hakufa kwa ajali ya gari kama ilivyotangazwa na vyombo vya usalama na ofisi ya Bunge.

Msemaji wa familia hiyo, Prof. Samuel Wangwe alisema kuwa kutokana na kifo hicho kuwa na mashaka mengi familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina ili ijiridhisha na sababu za kifo cha mbunge huyo.

Akizungumza katika hadhira iliyokusanyika nyumbani kijijini Kemakorere, alisema familia imepata mashaka makubwa kutokana na mambo mengi na hasa sababu za kifo ambazo zimedaiwa kuwa ni ajali.

"Mambo mengi yamesemwa sasa kama familia tumeamua kufanya uchunguzi huru na wa kina ili kubaini sababu ya kifo cha marehemu, katika uchunguzi huu familia itatoa daktari wake na serikali," alieleza.

Alisema kuwa familia imeamua kusitisha maziko hayo kutokana na mwili wa marehemu kubainika kuwa na jeraha ambalo wanadhani limetokana na kitu kingine na wala si ajali ya gari kama ilivyoelezwa.

Alipoulizwa na gazeti hili iwapo familia imefanya uchunguzi wa awali na kubainika kuwa kifo cha marehemu kimetokana na kushambuliwa kwa risasi, Prof Wange alisema kuwa ni kutokana na utata huo familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia taratibu na sheria.

"Ni kweli mwili wa maerehemu umekutwa na jeraha, lakini mimi sijaliona, na wala sijui kama ni la risasi, lakini kikubwa tunafanya uchunguzi kesho (leo) ili kuondoa utata wote huo, hii ni haki ya familia tumetaka hivyo na serikali imeridhia," alieleza.

Kwa upande wa serikali, msemaji wa serikali Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, alisema kuwa serikali imeridhia kufanyika kwa uchunguzi huo ambapo familia itatoa wataalamu wa kufanya uchunguzi na serikali kutoa mwakilishi wake.

"Serikali imeruhusu uchunguzi huru ufanyike ambapo utahusisha daktari wao wa familia na sisi kwa upande wetu serikali tutatoa daktari pia," alisema Wasira.

Ndugu mwingine wa marehemu, Kefa Wangwe, aliutangazia umati wa waombolezaji waliojitokeza kwa ajili ya maziko ambayo yalipangwa kufanyika jana kijijini kwao kwamba yameahirishwa ili kuruhu uchunguzi wa sababu za kifo cha marehemu.

Kefa alisema familia yao imeamua kuwa Marehemu Chacha hatazikwa hadi hapo madaktari watakapo uchunguza mwili wake na kubaini kifo cha mwanasiasa huyo kimesababishwa na nini.

Keba alisema familia ya marehemu akiwamo kaka yake Prof. Wangwe, waliamua kuufunua jeneza na kudai kuwa kulikuwa na alama za kupigwa risasi shingoni iliyotokea mdomoni nyingine tumboni na kusababisha kifo chake.

Kefa ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa vipindi viwili hadi 2005 na kaka yao Prof. Wangwe, walisema mdogo wao hatazikwa kwanza hadi tume iundwe ikishirikisha familia ya marehemu, Serikali na madaktari bingwa ili kubaini kifo cha ndugu yao kwani kina utata. Mwili wa marehemu ulitarajiwa kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mkoa Musoma ukisubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Habari ambazo timu ya waandishi wetu walioko Tarime na Kijijini kwa Wangwe walizopata kutoka ndani ya familia zilisema kuwa uchunguzi wa mwili huo ulifanywa na Dk Turwa Mrimi ambaye alibainisha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa ukionyesha kuwa alipigwa risasi mdomoni na kutokea nyuma ya shingo, pamoja na kuwa na jeraha liloonyesha kuchomwa na kitu chenye ncha kali pajani kulia.

Kutokana na hali hiyo, ndugu walilazimika kukaa kikao na kujadiliana hatma ya hali hiyo, huku wakifanya mawasiliano kuagiza daktari mwingine zaidi.

Diwani wa Kata ya Kemambo, Agustino Neto Sasi, alithibitisha kufanyika kwa kikao hicho na kusema "Siwezi kueleza kuhusu taarifa ya utafiti, ninachojua ni kweli daktari ameletwa na familia na mwili umefanyiwa uchunguzi sasa tungoje familia itatoa jibu."

Uchunguzi mpya unataraijiwa kufanywa na timu ya madaktari kutoka hopitali ya Dk. Wilfred Kisuka Machage wa jimbo la Kurya, Kenya.

Prof. Wangwe alisema kuwa Dk. Mrimi ambaye anadaiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu jana hakuwa daktari bingwa anayehusikana na uchunguzi, lakini kutokana na kuibuka utata familia imeamua kumpata daktari mbigwa ambaye ni mtaalamu.

Kutokana na hali hiyo, ibada ya maziko ambayo ilikuwa ianze saa 5 asubuhi ilikwama hali ikizidi kuwa tete na kusababisha wananchi kukaa vikundi wakisubiria hadi pale walipotangaziwa kwamba imeamuliwa kuzuia maziko.

'Baadhi' ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, Manaibu Waziri Gaudensia Kabaka, Dk James Wanyancha na Naibu Waziri wa Miundombinu wa Kenya na ambaye pia ni mbunge wa Kurya, Willfred Machage, na wakuu wawili wa wilaya za Kurya Magharibi na Mashariki Getonga na Ama Shamba.

Wengine waliohudhulia ni wabunge Nimrodi Mkono, Zito Kabwe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Pia wabunge 20 ambao wamewakilisha Bunge.

Katika eneo la nyumbani ambako mwili ulikuwa umehifadhiwa, vurugu zilianza kuzuka huku vijana wakiwa na mabango ambao yanaonyesha kwamba hawaamini kwamba Wangwe amekufa kwa ajali. Mengi ya mabango hayo yalikuwa yakisema kwamba wanataka uchunguzi wa kina kuhusu kifo hicho.

Katika eneo hilo, baada ya kuwa na hisia za kifo hicho kimetokana kuuwawa kwa risasi, iliwalazimu baadhi ya viongozi wa Chadema, akiwamo Kabwe kupewa ulinzi mkali ambapo alikuwa analindwa na mabaunsa watatu.

Katika msiba huo kijijini Kemakorere ambako alizaliwa Wange, Zitto alikuwa na walinzi hao kila mara na kila alipokwenda ambao walikuwa wakimlinda na kumfuata.

Habari zilizopatikana zimeeleza kuwa kutokana na wasiwasi huo mara baada ya kufika Tarime, Zitto aliwasiliana na viongozi wa chama wilaya na Jeshi la Polisi ambapo walikaa kikao cha siri na maofisa wa polisi kuhusu suala la usalama wa viongozi.

Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Wilaya, Anderson Deogratias Chacha, alithibitisha kufika polisi, lakini alisema siyo kwa ajili ya maswala ya usalama wa Zitto wala Mbowe, bali ilikuwa ni kuwapelekea taarifa za hali ya ulinzi na jinsi walivyojipanga kama Chadema.

Alisema Chadema walipanga mkakati wa ulinzi kutokana na kubainika kuwa kuna kundi la watu wamepewa fedha kwa ajili ya kufanya vurugu. Hata hivyo, baada ya Mbowe kufika umati ulianza kusikika ukipiga kelele na kusema wanataka pia kumuua kwa vile Wangwe ameuawa na kudai Mbowe ni muhisika

Kutokana na kelele hizo, kuendelea vijana walizidi kurusha mawe na kuzuka vurugu kubwa hatua ambayo ililazimu polisi kuingia eneo hilo na kuwatawanya watu kwa lengo la kuimarisha ulinzi kwa viongozi wa chama na serikali waliokuwa huko.

Kundi kubwa la wananchi lilikuwa likipita sehemu mbalimbali huku likiimba kuwa Wangwe ni Mandela wao, wengine wakiimba, Barrack Obama.
 
ok sasa wanajichanganya kweli; Habari zitakazokuwa more balanced ni zile zitakazotoka Jumamosi kwani leo kulikuwa na kila aina ya manipulation of the news.
 
Ufuatao ni utaratibu wa ughaibuni kuhusu kuchunguza ajali na hasa za barabarani, ambao ningependa wenzangu nanyi mjue kidogo.

Accident investigation procedure - (how do you get hold of the data, links with local infrastructure/police for data collection preparation, etc):

Nina-assume kwamba mfumo wa kukusanya taarifa umebuniwa na unatumika as a standardised method under legislation ambayo imewekwa na serikali.

The method works effectively when the team arrives at the scene soon after the accident. Any delay in the investigation reduces the quality of the information available, such as the marks on the road surface and in turn the reliability of the reconstruction. The investigation may also be carried out later if the call out is delayed for some reason. A reason for the delay can be, for example, a later fatality after an accident.

The information about the accident will usually be reported by the emergency centre or the local senior police officer to the investigation team. The investigation team leader makes sure that those who raise the alarm are aware that the accidents are within the scope of the investigation programme. Alerting members of the investigation team takes place according to the procedure and order agreed on by the team.

This method of investigation has been designed for an investigation team representing multidisciplinary expertise. The basic members of the team are a traffic police officer, vehicle specialist, road safety specialist, physician and psychologist. They participate in the investigations or the analysis of the accident as necessary and, at the request of the investigation team, may include, among others, a railway, a bus body specialist, and special advisors who represent specialist areas in vehicle safety, commercial traffic, or traffic medicine.

Ntaendelea.
 
ok sasa wanajichanganya kweli; Habari zitakazokuwa more balanced ni zile zitakazotoka Jumamosi kwani leo kulikuwa na kila aina ya manipulation of the news.

Mzee Mwanakijiji,

Kwa sasa mimi sitachukulia kwa maanani kile kitakachoandikwa na magazeti ya Rostam Azizi - majira, mtanzania, na mengineyo. Hawa ni watu ambao hata kule kwenye mazishi walikuwa wanauliza maswali ya kichochezi kwa waombolezaji.

Mipango yao ya kuleta fujo kwa wakazi wa Tarime imeshindwa na sasa wako kwenye mpango wa pili wa kupotosha watu kwa kile kilichotokea. Suala la ulinzi wa polisi ni muhimu sana hasa baada ya baadhi ya viongozi wa serikali na vyama kuondoka msibani kwa habari kuwa watu wa Tarime wangewadhuru.

Watu wanafaidika nini kwa kuchochea fujo na habari za uongo kuhusu watu wa Tarime?
 
sidhani kama gazeti linaweza danganya kua Baada ya Mbowe kufika vurumai ilitokea Hata kichaa hawezi daganya kwa staili hiyo,maana walikuwepo watu wengi.

kitu cha ku manipulate ni kama kifo cha Wangwe mtu anaweza andika atakavyo,lakini hili la vurumai anayebisha sijui tu tumweke kundi gani.

Utaziweka mara mia moja leo maana hiki ndicho ulitaka kitokee Tarime ili upate cha kusema kuhusu wakazi wa Tarime. Asilimia 20 ya share za Mwananchi zina jina la mtu mmoja very familiar. Fuatilia ujue jina lake na utajua kinachoendelea hapa. Swali kubwa ni kuwa, kwa nini huyu mtu anataka sana fujo itokee Tarime?
 
wewe waja kweli Unafiki wenu utawamaliza.
Kitu kama kimetokea kikubali na upambane na changamoto ,mtu akitaka kujua unafiki wako rudi page tano nyuma tu utaona nini ulichokua unasema.

ama ukitaka jua wanafiki wanajifanya kuguswa sana na kupoteza mtu mahili nenda tu ktk ile thread ya RIP chacha Kutimuliwa umakamu ,pia ktk thread hizo ndio utaona msimamo wangu tangu mwanzo.

Unafiki huu umekithiri ndio huo huo unaowatuma watu kutotoa mchango wao wakati mgonjwa akiwa anaomba msaada ili aende hospital lakini akifariki mijamaa minafiki inakuja kutoa rambirambi hata mara elfu zaidi ya pesa alizozihitaji wakati akiwa mgonjwa.

Mimi taarime naifahamu ndio mwanzo tu nilimsihi kua kama watu wameshahisi hivyo bora asiende.Wewe mumamuruki wala hutokei tarime wajibaragua kujifanya waijua tarime.

Kwanza wewe kwanini unatumia ID nyingi hivyo,watu wanadhani jamaa kapotea kumbe unabadilisha ID tu.
 
Inaendelea na mwisho wa mawazo haya.

Na hii ni kuhusu baada ya ajali na namna ambayo kijana Daeu Malya angehojiwa.

Approach hii iliounganishwa pamoja itasaidia kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali husika.

1. Eneo la ajali au On-the-scene:

- Form: a specific form reporting all the general information (location, time, weather, description, etc) will be filled in on the accident scene;- Hii ni kawaida kufanyika.

- Pictures: several pictures will be taken in order to have a description of both the accident location (e.g. brake signs) and involved vehicles.- Sasa badala yake picha tayari zimezagaa kwenye magazeti na zilichukuliwa hata kabla polisi hawajafika.

- Contacts: first contact will be establish with the vehicle occupants in order to carry out a detailed interview in phase 2- Hii ndio inachanganya sana kwani haijathibitishwa ni abiria wangapi walikuwamo ndani ya gari.

2. Retrospective:

- Interviews: a detailed interview will be carried out on the vehicles occupant that gave their availability during phase 1 contact establishment- Hapa Deus Malya bado anachengachenga au labda atawaambia polisi of his true account of events hapo akitulia na sisi hatutaki atulie kama yupo nje ya mahabusu.

- Vehicles analyses: the involved vehicles will be deeply analysed in order to highlight outside and inside deformations. Pamoja na gari kuharibika vibaya bado haizuii uchunguzi kufanyika kuona kwamba limebiringika mara ngapi na kama kabla ya kubiringika je milango ilikuwa wazi au imefungwa.

- Back on the scene: a team of specialist will go back on the accident scene within a very short time period (1-2 days) in order to carry detailed analysis.

This will aim at identifying all the parameters that will be used to perform the accident reconstruction. Hii itakuwa inapigwa danadana tu.

R.I.P Chacha Wangwe.
 
Pigeni kelele weeeee mpaka vidole viume lakini hili litapita tu yamepita mengi.....Chifupa,Mbatia,Balali,Kolimba,sokioine.......ni bora tuiadili mikataba ya madini na makoro koro mengine...
 
Tanzaniaaaaaa!!!!!!!
Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

Kosa lako ni nini? Kila anayekutetea na kukulinda ananyamazishwa kwa namna yoyote. Kosa lako ni mama yangu??
Kosa lako madini na rasilimali nyingine nyingi alizokuwekea Mungu. Ndiyo!!! Mama yangu Tanzania Kosa lako: utajiri wako wa asili. wanautaka waroho. Wana mlango wa kuuchota wanavyotaka wakautumbulie ughaibuni. Leo wanapata fursa ya kuwachonganisha walinzi wako na wanao. Kusudi lao waendelee kupora zaidi

Tanzania Mama yangu kosa lako madini yako na utajiri ulio nao. Mafisadi watawamaliza wanao kwa vifo vya aina mbali mbali ili mradi tu kuondoa kabisa kila kikwazo cha kujichotea mali zako mama yangu Tanzania.
Wanao watamalizwa. Watamalizwa kwa mitutu ya bunduki, watamalizwa kwa njaa. Watamalizwa kwa kutengenezewa vita itokanayo na kuchonganishwa.

Damu yao inamwagika. Kaskazi imefunguka kusi inakunywa damu ya wanao. Kosa lao kuzaliwa kutoka kwako mama Tanzania.

Eeeee Mungu iangaliee Tanzania. Nguvu ya uongo inapotawala sasa. Haki na kweli yako isimame. Wenye haki wako wanapotumbukizwa matesoni. Baba wa Mbunguni wape wana wako haki katika nchi yao. Baba pigana na watesi wa wanao. Amen

Tanzania sasa tuombe tuombe, tuombe sana. Waambie watanzania wengine pia waombe sana.
Ulimwengu omba kwa ajili ya Tanzania. Mlipopata shida mlikimbilia Tanzania.

Sasa mitupora imefikia kupita kwenye vijito vya damu ili kuyafikia madini yetu vizuri na kutumasikinisha kabisa. Waliyofanya hayatoshi: Sasa wanataka hata damu ya wana wa nchi ya Tanzania.
UMEKOSA NINI TANZANIA??
 
..KAMA TAIFA HUU NI WAKATI MUHIMU...TUSIJE KUANZIA VITA HAPA...........NI MUHIMU UCHUNGUZI UANGALIE MAMBO YOTE...........

1]USHUHUDA ULIOTOLEWA NA MWANAKIJIJI ALIYEKUWA WA KWANZA KUFIKA KWA KIASI KIKUBWA UMETOFAUTIANA NA WA BW . MALLYA.....NA MWANAKIJIJI ANASEMA ALIKUTA WATU WAWILI ENEO LA TUKIO ...MMOJA AKATOWEKA ..HALI TATA HII

2]BW MALLYA AMEPATA KUSAFIRI NA MSAFARA WA SERIKALI KWENDA LIBYA ..AKIWA NA VIONGOZI WA CCM[ref.mwananchi leo],baadaye akaenda GENEVA....TUNAWEZA KUAMINI BADO KUWA HUYU NI MTANZANIA WA KAWAIDA??

....MAFIKIRI UCHUNGUZI UANGALIE SEHEMU ZOTE TATA..SERIKALI,CCM,CHADEMA ....BILA KUWASAHAU MAKAMPUNI YA MIGODI HUYU ALIKUWA KAMA MWIBA KWAO......HAWA WATU WA MADINI WANAUWEZO WA KUPIGANISHA VITA ..IE CONGO..SEMBUSE KUMMALIZA MTU MMOJA??
 
Taarifa ya Habari ya TBC1 ya leo ambapo dogo Mnyika alihojiwa imeibua mambo kadhaa:

1. Kuwa TBC wana nyaraka toka kwa Chacha Wangwe, za kesi aliyotaka kufungua(hapa TBC1 hawajui kabisa kuwa kesi alishafungua tayari), tamko la Chacha kuhusu CHADEMA na mambo mbalimbali(hapa TBC lazima waeleze umma wamepataje nyaraka toka kwa marehemu kabla hazijatoka wakati ambapo inaelezwa kuwa nyaraka zote za marehemu ziliibiwa garini pamoja na laptop).

2. TBC1 wanaelekea kuwa na mkakati wa dhati wa kufanya propaganda za kuhusisha CHADEMA na hiki kifo.

3. Taarifa nilizonazo ni kuwa Chacha alishafungua kesi ya kuzuia CHADEMA isimvue uanachama na si kesi ya kutaka fidia ya kuchafuliwa kama alivyodai angefungua baada ya siku kumi na nne. Na tamko lake ambalo alikuwa afanye press conference DSM baada ya kuaga mwili wa Bhoke Munanka lilikuwa ni kueleza kwamba CHADEMA inataka kumtimua uanachama. Alikuwa aelekee kufanya reconcilliation kwa kuwa mikakati yake mingi iligonga mwamba ikiwemo kikao na Makamba Dodoma.

Nasubiri kwamba mpambanaji huyu azikwe halafu nitarejea kwa kina.

PM
 
wewe waja kweli Unafiki wenu utawamaliza.
Kitu kama kimetokea kikubali na upambane na changamoto ,mtu akitaka kujua unafiki wako rudi page tano nyuma tu utaona nini ulichokua unasema.

ama ukitaka jua wanafiki wanajifanya kuguswa sana na kupoteza mtu mahili nenda tu ktk ile thread ya RIP chacha Kutimuliwa umakamu ,pia ktk thread hizo ndio utaona msimamo wangu tangu mwanzo.

Unafiki huu umekithiri ndio huo huo unaowatuma watu kutotoa mchango wao wakati mgonjwa akiwa anaomba msaada ili aende hospital lakini akifariki mijamaa minafiki inakuja kutoa rambirambi hata mara elfu zaidi ya pesa alizozihitaji wakati akiwa mgonjwa.

Tatizo lako unafikiri kuwa kuonyesha urafiki kwa Wangwe ilikuwa lazima mtu aje kuandika hapa JF wakati mgogoro wa uongozi Chadema ukiendelea. Wengine vitendo kuliko maneno ni muhimu zaidi.

Watu kama wewe ambao wanatumia siku ya majonzi kama hii kuwapaka matope wananchi wa Tarime na kuleta uchochezi usio na sababu mtaipeleka nchi yetu kubaya.

Fikiria kuhusu wafiwa na maelfu ya wakazi wa Tarime wanaolia leo kabla ya kuja kuleta maneno yake ya kichochezi na uongo hapa.
 
Taarifa ya Habari ya TBC1 ya leo ambapo dogo Mnyika alihojiwa imeibua mambo kadhaa:

1. Kuwa TBC wana nyaraka toka kwa Chacha Wangwe, za kesi aliyotaka kufungua(hapa TBC1 hawajui kabisa kuwa kesi alishafungua tayari), tamko la Chacha kuhusu CHADEMA na mambo mbalimbali (hapa TBC lazima waeleze umma wamepataje nyaraka toka kwa marehemu kabla hazijatoka wakati ambapo inaelezwa kuwa nyaraka zote za marehemu ziliibiwa garini pamoja na laptop).

2. TBC1 wanaelekea kuwa na mkakati wa dhati wa kufanya propaganda za kuhusisha CHADEMA na hiki kifo.

3. Taarifa nilizonazo ni kuwa Chacha alishafungua kesi ya kuzuia CHADEMA isimvue uanachama na si kesi ya kutaka fidia ya kuchafuliwa kama alivyodai angefungua baada ya siku kumi na nne. Na tamko lake ambalo alikuwa afanye press conference DSM baada ya kuaga mwili wa Bhoke Munanka lilikuwa ni kueleza kwamba CHADEMA inataka kumtimua uanachama. Alikuwa aelekee kufanya reconcilliation kwa kuwa mikakati yake mingi iligonga mwamba ikiwemo kikao na Makamba Dodoma.

Nasubiri kwamba mpambanaji huyu azikwe ndio niseme kwa uwazi zaidi.

PM
 
Taarifa ya Habari ya TBC1 ya leo ambapo dogo Mnyika alihojiwa imeibua mambo kadhaa:

1. Kuwa TBC wana nyaraka toka kwa Chacha Wangwe, za kesi aliyotaka kufungua(hapa TBC1 hawajui kabisa kuwa kesi alishafungua tayari), tamko la Chacha kuhusu CHADEMA na mambo mbalimbali(hapa TBC lazima waeleze umma wamepataje nyaraka toka kwa marehemu kabla hazijatoka wakati ambapo inaelezwa kuwa nyaraka zote za marehemu ziliibiwa garini pamoja na laptop).

2. TBC1 wanaelekea kuwa na mkakati wa dhati wa kufanya propaganda za kuhusisha CHADEMA na hiki kifo.

3. Taarifa nilizonazo ni kuwa Chacha alishafungua kesi ya kuzuia CHADEMA isimvue uanachama na si kesi ya kutaka fidia ya kuchafuliwa kama alivyodai angefungua baada ya siku kumi na nne. Na tamko lake ambalo alikuwa afanye press conference DSM baada ya kuaga mwili wa Bhoke Munanka lilikuwa ni kueleza kwamba CHADEMA inataka kumtimua uanachama. Alikuwa aelekee kufanya reconcilliation kwa kuwa mikakati yake mingi iligonga mwamba ikiwemo kikao na Makamba Dodoma.

Nasubiri kwamba mpambanaji huyu azikwe halafu nitarejea kwa kina.

PM

Hivi hawa ni lini walibadili ile taarifa kuwa Wangwe alikuwa anakwenda Dar kwenye mazishi ya Bhoke Munanka? Mambo mengine yanasikitisha sana kuyasikia.
 
Ok hizo halimashauri kuna nyingine kama sikosei ni ya ZITO ,nyingine sijui

Sasa kumbe ulikuwa hujui kwa nini ulisema kwamba wana halmashauri moja tu ya Tarime? Kwa nini ukasirike ukiwambiwa mwongo wakati umedanganya?

Nao wanachadema waliotaka marehemu apigwe risasi mbona huwataji, na walisme wapi na lini?
 
Taarifa ya Habari ya TBC1 ya leo ambapo dogo Mnyika alihojiwa imeibua mambo kadhaa:

1. Kuwa TBC wana nyaraka toka kwa Chacha Wangwe, za kesi aliyotaka kufungua(hapa TBC1 hawajui kabisa kuwa kesi alishafungua tayari), tamko la Chacha kuhusu CHADEMA na mambo mbalimbali(hapa TBC lazima waeleze umma wamepataje nyaraka toka kwa marehemu kabla hazijatoka wakati ambapo inaelezwa kuwa nyaraka zote za marehemu ziliibiwa garini pamoja na laptop).

2. TBC1 wanaelekea kuwa na mkakati wa dhati wa kufanya propaganda za kuhusisha CHADEMA na hiki kifo.

3. Taarifa nilizonazo ni kuwa Chacha alishafungua kesi ya kuzuia CHADEMA isimvue uanachama na si kesi ya kutaka fidia ya kuchafuliwa kama alivyodai angefungua baada ya siku kumi na nne. Na tamko lake ambalo alikuwa afanye press conference DSM baada ya kuaga mwili wa Bhoke Munanka lilikuwa ni kueleza kwamba CHADEMA inataka kumtimua uanachama. Alikuwa aelekee kufanya reconcilliation kwa kuwa mikakati yake mingi iligonga mwamba ikiwemo kikao na Makamba Dodoma.

Nasubiri kwamba mpambanaji huyu azikwe halafu nitarejea kwa kina.

PM

makabrasha ya malipo ya EPA DR SLAA aliyapata wapi? maana hayakuibiwa BOAT yale original yalibaki kulekule..

Mikataba mibovu ya madini ZITO aliipata wapi? maana original zenyewe hazikuibiwa.

Haya sio yakuanza nayo kabisa ,lazime shilingi uitazame pande zote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom