Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
[/SIZE][/COLOR]Kwa maneno yako ni kuwa CHADEMA sio waliomuua kwani sasa watakosa hiyo ruzuku.

maneno yako yana maana kubwa sana sasa nani kamuua?

Wangwe hadi sasa tunatambua kafa kwa ajali lakini uchunguzi ukifanyika mahala pakuanzia ni ndani ya CHADEMA.

Alimua anaweza kua kiongozi ,mtu yeyote ama kibaka aliye pita na fedha zake pamoja na komputa yake.

Lakini uchunguzi lazima ufanywe ktk maeneo yote yanayoshukiwa ,eneo la kwanza ni chadema.
 
this brings me to this question:

Kama baada ya ajali vitu vyote walivyokuwa navyo laptop, masanduku n.k viliibwa na hatujaambiwa kama vimepatikana TBC1 wamepata wapi nyaraka zinazoonesha kuwa katika safari hiyo alikuwa anaenda kufungua kesi na kuzungumza na vyombo vya habari isipokuwa kama na wao TBC walikuwa na taarifa hiyo kabla? au mtu mwingine zaidi ya Chadema alikuwa na taarifa hiyo ya safari?

Shimo hilo hawatatoka salama.

Mkuu,

Nina imani TBC soon itaanza kushangaza watu sana kwa umakini wa habari hasa pale itakapoweza kuleta habari live kupitia correspondents au reporters kutoka eneo la tukio.

Swali je serikali nayo itakuwa tayari kwa haya?

Huu ni mwanzo tu na namwamini mzee Mhando.
 
Mie mnanichanganya tu tangu, nashauri kila message tunayoipata tuitafakari kwa utulivu, ni rahisi sana kuchukuliwa na upepo na mawimbi ya emotions. Pease people, take care. Ni wakati mgumu huu. Na kumbuka, there are always those will want to take advantage kwa emotions zetu. Mie simo
 
Mhh JF napapenda sana,naanza kuelewa kila sentensi zilizokuwa zikitolewa na watu kuhusiana na hili suala la wangwe! BBC wanasema ndugu walifunua maiti na wakaona jeraha kubwa kisogoni ambalo kutokana na uzoefu wa baadhi ya ndugu (nafikiri waliopitia jeshi),jeraha lile limetokana na risasi ambayo ilipigwa mdomoni na kutokea kisogoni. Sasa sijui wana hoja hapo au vipi lakini nafikiri hiyo independent uchunguzi ulioombwa na ndugu wa marehemu utaconfirm beyond reasonable doubt hiyo shaka waliyonayo. Kiukweli napenda kuwapongeza wanaJF wote kwanamna mnavyoweza kudodosa na kuconnect dots. Mungu awabariki wana JF!!
 
Kwa mujibu wa habari hii MBOWE ndiye aliyesababisha vurugu kutokea, kwani alipofika tu ndiyo vurumai ikaanza. kweli watu wa Tarime ni wanaume wa shoka,hawajapumbazwa na barua ya chadema kwa IGP.
 
Hapa kuna kitu ,inawezekana kabisa kuwa wapo kwenye spesho mission kwani haiwezekani watangaze kuwa Mbowe kapewa ulinzi maalum wakati viongozi wote waliokuwepo ndio walipewa ulinzi wa polisi na kuondolewa hapo ,sasa hawa wanakataa kusema ukweli kuwa aliyewatuliza wananchi ni Zitto Zuber Kabwe na sio mwingine,

Hii ilipelekea hata wabunge waliokuwa huko kuondoka na kurudi Dodoma ,sasa hapa kuna kitu kinatengenezwa.

Na kwa maneno ya TBC basi inawezekana kuwa yule mtu wa tatu ambaye alisemwa na wanakijiji wale basi alikuwepo na ndio alichukua Laptop na kuwapelekea TBC ni lazima waseme wamepata wapi hizo yaraka huku ikisemwa kuwa marehemu alikuwa ameibiwa?

Wanaongeza maswali zaidi, kuna kitu kinatengenezwa hapa kwa nguvu ila naamini kuwa ukweli kuna siku utawekwa bayana .

Mallya tunajua kuwa yu hai mpaka sasa kesho wasijesema kuwa amepotea ama kawa Ballali.
 
Kwa mujibu wa habari hii MBOWE ndiye aliyesababisha vurugu kutokea, kwani alipofika tu ndiyo vurumai ikaanza. kweli watu wa Tarime ni wanaume wa shoka,hawajapumbazwa na barua ya chadema kwa IGP.

Ubongo wako hauna tofauti na wa panya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tarime palikuwa na mpango uliopangwa tangia jana kuwa watu wa CHADEMA na haswa Mbowe wazomewe na kujenga image kuwa wanahusika na msiba huo na hilo lingeondoa mpango wao wa kutaka ifanyike independent investigation.

Leo asubuhi walipofika huko wakina Mbowe pamoja na viongozi wengine wa vyama vya upinzani wakapokelewa na hakukuwa na hicho walichopanga, sasa kuna juhudi zinafanywa kwa kumshirikisha RPC atoe statement kuwa wamemnusuru Mbowe kuuwawa ,sasa sijajua kama ataitoa wapi ila najua kuwa kuna waandishi wameitwa kwa ajili ya kupata hiyo statement japo kwa umakini mkubwa.

Vyombo vya habari vimechaguliwa mahususi kuwa ni vyombo gani vihusike kupata hiyo statement.

Mtindo huu wa kutaka kutwist mambo huko yanaweza kuiingiza nchi kwenye matatizo makubwa sana ambayo wanaopanga ,na haswa waliokaa nyumbani kwa waziri mmoja wa serikali mjini Dodoma na kuandaa mpango huo mahususi eti kwa vile Mbowe alimshinda Kikwete kura huko Tarime utakuwa na matatizo kwao binafsi.

Vijana waliokuwa wamendaliwa wamesema kuwa wataweka mambo hadharani na kusema mpango huo na haswa baada ya kuona utata wa kifo hiki.

Nawatakia kila la kheri.

Kiranja,

Je ulichoandika hapo juu ni kweli? Waandishi wa habari sio wajinga, kwa vyovyote kuna watu wengi tu watakuwepo kwenye msiba na yaliyotokea tutajulishwa.

Pamoja na kuchukia mfumo wa siasa wa sasa TZ pamoja na ufanyaji kazi wa polisi, sidhani kama mambo yako hivyo.

Kwa mambo ya TZ, hata ingelikuwa kabila lingine bado yangetokea matatizo kwa mwenyekiti Mbowe maana ugomvi kwenye uhai kwa Tanzania hauishi kwenye msiba.

Miaka zaidi ya 40 ya uhuru wetu haijatusaidia kitu. Tumezidi kuwa wajinga na wajinga ndio maana tunaua Albino tukidhani tutapata utajiri.
 
As am coming all the way from Kemakorere jamani ni tatizo kubwa..yaaani wananchi kama mmesikia vyema kwenye taarifa kuna mwananchi kalopoka kuwa ameuwawa...

Fununu zilizopo nikuwa amepigwa ri...sasa huyo mtu wa tatu aliye kuwepo mallya ammseme tu kwa kweli....njia ya kwenda Kemakorere kutoka nyamongo pitia nyamwaga..juu si heri tena...manager mgodi alikwenda kutoa heshima za mwisho...kwa kuangalia tu hari ilivyo akaamua pitiliza kwenda Tarime mjini .... vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine saa hii....

Msiombe wazee wa pale wapewe nafasi ya kuongea utasikia ambayo hutaaamini..

Stay online....
 
Kiranja,

Je ulichoandika hapo juu ni kweli? Waandishi wa habari sio wajinga, kwa vyovyote kuna watu wengi tu watakuwepo kwenye msiba na yaliyotokea tutajulishwa.

Pamoja na kuchukia mfumo wa siasa wa sasa TZ pamoja na ufanyaji kazi wa polisi, sidhani kama mambo yako hivyo.

Kwa mambo ya TZ, hata ingelikuwa kabila lingine bado yangetokea matatizo kwa mwenyekiti Mbowe maana ugomvi kwenye uhai kwa Tanzania huishi kwenye msiba.

Miaka zaidi ya 40 ya uhuru wetu haijatusaidia kitu. Tumezidi kuwa wajinga na wajinga ndio maana tunaua Albino tukidhani tutapata utajiri.

Maneno yangu ni ukweli mtupu subiri magazeti maalumu ya kesho kaka, haswa......
 
[/size][/color]kwa Maneno Yako Ni Kuwa Chadema Sio Waliomuua Kwani Sasa Watakosa Hiyo Ruzuku.

Maneno Yako Yana Maana Kubwa Sana Sasa Nani Kamuua?
Huo Ulikuwa Mpango Wa Mwanzo Kutizama Ruzuku,lakini Inapokuja Suala La Yeye Kung'ang'ania Uenyekiti Hapo Hakuna Mbadala Tena. Bora Kukosa Ruzuku Na Jimbo Kuliko Kukosa Uenyekiti Taifa.
Hata Dawa Unaanza Na Panadol Ukishindikana Unakuja Na Maamuzi Mazito Ambayo Ni Unpopural Kwa Kauli Za Kitila Mkumbo.
 
Maneno yangu ni ukweli mtupu subiri magazeti maalumu ya kesho kaka, haswa......
Alipofika tu Mbowe kwenye msiba akatimuliwa ilibidi pesa za serikali zitumike kumuokoa,baada ya hapo hali ikabadilika kabisa kwenye msiba.
 
Mwanakijiji elewa jambo moja Chadema walikuwa wakitaka ruzuku za Wangwe kupitia jimbo la Tarime, kwa vile priority ya Chadema ni RUZUKU NA UKABILA wasingeweza kumnyanganya uanachama,angekuwa si mwanachama wa Chadema nao makao makuu wangepata Ruzuku, kwa hiyo kilichokuwa kinambakiza Wangwe chadema ni lile kundi la Tarime linalizalisha Ruzuku Makao makuu.

Wangwe alibaki kuwa Mwanachama kwa ajili ya ruzuku si vinginevyo.

Wewe uongo tu utakuponza leo. Haujui historia ya Chacha na wala hujui nini kilimfanya akahamia Chadema. Punguza chuki binafsi na utajua kinachoendelea Tarime leo hii - mipango ya mazishi ya mbunge wa Tarime.

Ubinadamu unao hata kidogo?
 
Alipofika tu Mbowe kwenye msiba akatimuliwa ilibidi pesa za serikali zitumike kumuokoa,baada ya hapo hali ikabadilika kabisa kwenye msiba.
Acha uwongo. Ulikuwepo Tarime? Na wale waliomwita, rais, rais nao walikuwa wanataka kumdhuru? Uongo hapa si pahala pake.
 
Alipofika tu Mbowe kwenye msiba akatimuliwa ilibidi pesa za serikali zitumike kumuokoa,baada ya hapo hali ikabadilika kabisa kwenye msiba.

Sio kweli kwenye hili. Uliza waliokuwepo msibani wakuambie kilichokuwa Tarime. Mbowe hajafukuzwa na yeyote na hata hao viongozi wa serikali na wabunge waliokimbia msiba wamefanya haraka tu. Watu wa Tarime sio vichaa kama wewe unavyotaka kuwapotray hapa.
 
NImewahi kusikia suggestive messages... hii ya leo ni kilele. mmh! TBC imepata documents zinazoonesha kuwa katika safari yake ya kwenda Dar Wangwe alikuwa afungue kesi dhidi ya Chadema kwa kumsimamisha nafasi ya Umakamu Mwenyekiti.

"Mpango huo wa Wangwe kufungua kesi ulikuwa unajulikana kabla na uongozi wa Chadema"...mwisho wa kunukuu...

Hawa TBC1 wanaleta habari na mtu akiwauliza wanazipata wapi sijui watasema nini. Kama wanadai kuwa vitu vya Chacha viliporwa na vibaka, hao TBC haya ya kufungua kesi wameyapata wapi?

Uchochezi tu na unafiki uliokithiri. Thanks GOD watu wa Tarime wamekuwa smart kuliko huu upuuzi ambao TBC na wenzao walitaka kuuleta Tarime.
 
Alipofika tu Mbowe kwenye msiba akatimuliwa ilibidi pesa za serikali zitumike kumuokoa,baada ya hapo hali ikabadilika kabisa kwenye msiba.

nasema tena kwa mara ya pili wewe umetumwa! si bure. Lakini kumbuka damu ninzito kuliko maji na kwa msiba huu kunakuaibika propaganda hazina msaada.
.... pesa za serikali zimetumika kumwokoa...! ebo
 
Sio kweli kwenye hili. Uliza waliokuwepo msibani wakuambie kilichokuwa Tarime. Mbowe hajafukuzwa na yeyote na hata hao viongozi wa serikali na wabunge waliokimbia msiba wamefanya haraka tu. Watu wa Tarime sio vichaa kama wewe unavyotaka kuwapotray hapa.

MBOWE ASABABISHA MAZISHI KUAHIRISHWA BAADA YA VARANGATI HEAVY KUTOKEA KWA MUJIBU WA ISSA MICHUZI,LABDA LEO HII NDIO IWE MICHUZI NI MNAFIKI KWA KUWEKA UKWELI WA MBOWE KUTIMULIWA.WWW.MICHUZI-BLOG.COM
http://michuzi-blog.com/2008/07/mazishi-ya-wangwe-yaahirishwa-kwa.html#comments
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom