Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Wanatumia mbinu hizi chafu ili kupata jimbo, wenzetu akili yao iko kwenye ruzuku wanajua kuondoka kwa wangwe ruzuku imepungua. wampeleke TUNDU LISSU akagombee kwani ndiye alisema kuwa alimsaidia Wangwe kuwa Mbunge.

Sasa nimeamini kuwa wewe sio tu unaukabila mkubwa unakusumbua moyoni bali pia unadharau kubwa sana kwa watu wa Tarime. Yaani Tarime hakuna mtu bali Tundu Lissu pekee ndiye anaweza kugombea?

Kuwa na heshima kwenye msiba wa wenzako. Hii sio kitu kikubwa cha kuuliza toka kwako.
 
mgagagigikoko unaonekana wazi kwamba umetumwa au unatumwa na fikra zako ambazo zinaweza kuwa siyo sahihi. Wenzako bado hatujajua ni nani mhusika ila tunatambua na kukubali kwamba kunawatu au vikundi vingi tunavyoweza kuvihisi, lakini wewe umekomalia chadema tu thats why nahisi umetumwa.
KAMA MBOWE anavyomtumia MNYIKA kufanya kazi za Chadema na kumkana makamu mwenyekiti wake Wangwe.
Nziku ni wewe ambaye unaandikia Tanzania Daima kila jumatano?
 
Muongo wewe, HAKUNA KIONGOZI WA KITAIFA WA CHADEMA ALIYEONGOZANA NA MAITI TOKA DODOMA HADI MUSOMA, hakuna SLAA wala Mbowe.nipe ushahidi?

Mwili wa Marehemu ulipotolewa Dodoma uliongopzana na ndugu wa Marehemu tuu na mtu aliyepata nafasi ambaye sio ndugu wa marehemu ni Mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Tarime.

Ndege hiyo ilipangwa ratiba na Bunge sasa waulize Bunge ni kwanini ujumbe wa wabunge ulipangwa kuwa wanaenda kwenye msiba leo?

Pili wakati msiba unatokea unajua kuwa Mbowe alikuwa Afrika ya Kusini akiongoza ujumbe wa TCD ambao ni muunganiko wa vyama vya CCM,CUF,CHADEMA,NA TLP, ulitaka aweze vipi kuongozana na mwili wakati aliweza kuingia nchini jana mchana baada ya kuahirisha safari?

Fanya kazi nyingine hii unayofanya inahitaji watu au mtu mwenye IQ kubwa sana ,sio kama ya kwako,ashakumu sio matusi....
 
mbowe Alisema Hayuko Tayari Kufanya Kazi Na Wangwe Anayevujisha Siri Za Chadema. Walijaribu Kumnyamazisha Kidemokrasia Wakashindwa, Sasa Wameenda South Africa Kumtafutia Sangoma La Kumuondoa.

Dogo Hebu Wacha Kuvuruga Watu Kumu Ndani
 
Muongo wewe, HAKUNA KIONGOZI WA KITAIFA WA CHADEMA ALIYEONGOZANA NA MAITI TOKA DODOMA HADI MUSOMA, hakuna SLAA wala Mbowe.nipe ushahidi?

Kwani kuongozana na maiti ndio kushiriki msiba? Kama hivyo ndivyo, basi wabunge wengi sana hawajashiriki msiba wa Chacha Wangwe! Kwa maana hiyo hata Spika na Naibu wake hawajashiriki msiba wa Wangwe!
 
Taarime naijua vizuri

Taarime hua wanaamua kumweka mtu wanayemtaka na ndio maana ni halimashauri hiyo tu ambayo CHADEMA inaongoza na kwanini isiwe DODOMA, DAR, Shinyaga,Kigoma,Karatu ,singida ama Moshi?

Kumbe wewe ni mwongo na mzushi namna hii, sikukujua. Kwa taarifa yako CHADEMA inaongoza halmashauri tatu, acha uvivu tafuta na hizo zingine mbili-achana kuandika mambo kwa hisia!
 
Hapa nimeshangaa kitu kimoja wakati watu wanataka uchunguzi hili familia angalau waweze kujua nini kilitokea na wajiridhishie naona kuna walioletwa mahususi kwa ajiri ya siasa kama kawaida yao.

Nawapeni pole maana wanavyozidi kuleta janja ndivyo watu wanazidi kuwagundua. Nafikiri kifo cha Mpiganaji Chacha wangwe kinaweza kutuonyesha Mengi yaliyopo katika jamii zetu.
 
Sasa nimeamini kuwa wewe sio tu unaukabila mkubwa unakusumbua moyoni bali pia unadharau kubwa sana kwa watu wa Tarime. Yaani Tarime hakuna mtu bali Tundu Lissu pekee ndiye anaweza kugombea?

Kuwa na heshima kwenye msiba wa wenzako. Hii sio kitu kikubwa cha kuuliza toka kwako.

Msikilize Tundu Lissu akisema kwa kauli yake kuwa ndiye aliyemfanya Chacha Wangwe awe mbunge wa Tarime, unaweza kuyasikia mahojiano yake na Mwanakijiji nenda www.klhnews.com halafu listen show utaona mahojiano ya Chacha Wangwe unaweza kuyasikia.

Mimi nampenda sana Wangwe na watu wa Tarime toka alipofukuzwa nakuwa akisimangwa kama mtoto yatima hapa JF ni mimi niliysimama kidedea kuhakikisha analindwa kwa nguvu zote kiasi cha members wengine humu kunibatiza jina la Wangwe, mie sijaonesha unafiki wa kumthamini marehemu baaada ya kufa nilimpa heshima toka mwanzo na nimekuwa very active toka day one Wangwe alipobambikiwa kesi. furaha yangu ingetimia wakati angechukua uenyekiti Chadema.

wewe ulikuwa wapi siku zote kumsaidia Mwana Tarime Mwenzako? acha unafiki. wanajulika waliompa heshima wangwe kuna Mtanzania, Mkandara, Mkamap WAKIONGOZWA na mimi.
 
Kumbe wewe ni mwongo na mzushi namna hii, sikukujua. Kwa taarifa yako CHADEMA inaongoza halmashauri tatu, acha uvivu tafuta na hizo zingine mbili-achana kuandika mambo kwa hisia!

Kitila,

Huyu ni mzushi tu hapa na alikuwa anataka sana kuona watu wa Tarime wakipigana na kumwaga damu na sasa ameaibika. Anajifanya kuwa ni mtu wa Tarime wakati hata hakui kuiandika hiyo Tarime yenyewe.

Watu badala ya kuwa na heshima kwenye msiba huu wao wanaleta upuuzi wa kisiasa. Inasikitisha sana kuleta ushabiki wakati wengine tuko kwenye uchungu mkubwa sana.
 
wanatumia Mbinu Hizi Chafu Ili Kupata Jimbo, Wenzetu Akili Yao Iko Kwenye Ruzuku Wanajua Kuondoka Kwa Wangwe Ruzuku Imepungua. Wampeleke Tundu Lissu Akagombee Kwani Ndiye Alisema Kuwa Alimsaidia Wangwe Kuwa Mbunge.

Sijakutana Na Watu Walio Chini Kama Huyu Jamaa Dah ( Wakazi Wa Tarime Wameshaapa Kuwa Hawatothubutu Kumchagua Mbunge Bwa Chama Tawala Na Ni Bora Wasimamishe Mbuzi Au Jiwe Then Walipigie Kura Kuliko Kuchagua Chama Tawala
 
Naamini kuwa kuna watu wameletwa hapa kuja kuvuruga mjadala ambao ulikuwa centred kwenye kuibua mambo mapya na kila hatua tulikuwa tunajua nini kinatokea ,ila hapa kuna watu wameletwa na sasa tunashindwa kupata kinachojiri huko Tarime .

Wana JF tusijibizane tena na hawa watu ila tupeane taarifa za huko na nini kinaendelea.
 
Kwa kuanzia tu, jina la record la wilaya yetu ni Tarime na sio Taarime. Wewe unaongelea Tarime ipi?

wewe naye!!!
Nipe jina mbunge wa mwaka 1990 ,mkuu wa wilaya wa mwaka 1996 na mkuu wa polisi wa mwaka 1998 na Mbunge kabla ya Chacha anatoka kijiji gani? maana nawasi wasi na wewe kidogo.

CHADEMA ndipo sehemu ya kuanzia kuchunguzwa.

1.CHACHA alikua ktk mchakato wa mwisho kukipeleka CHADEMA mahakamani ili waeleze na kuthibitisha waliyomzushia.

2. Wangwe alivuliwa umakamu na CHADEMA kwa kua ni mzigo na anayemega siri zao

3. MBOWE alisema hawezi fanya kazi na mtu kama CHACHA

4.CHACHA alikituhumu chdema kwa kufisadi fedha

5. Ktk uhai wake watu wa chadema walidai apigwe risasi na kweli dalili za mwanzo zinaonyesha CHACHA kapigwa RISASI mbili za kichwa.

Hata ktk hali ya kawaida mtu akikwambia aisii wewe subiri nitakuchoma kisu cha tako ,na baada ya siku kadhaa kweli ukachomwa kisu ,polisi wanakuja moja kwa moja kwa yule jamaa aliyetamka hakuna cha kujadiliana hapo.

Sehemu ya kuanzia ni CHADEMA ndio waende kwingine unless labda ajali hiyo ni ya kawaida kama ajali zingine.
 
Msikilize Tundu Lissu akisema kwa kauli yake kuwa ndiye aliyemfanya Chacha Wangwe awe mbunge wa Tarime, unaweza kuyasikia mahojiano yake na Mwanakijiji nenda www.klhnews.com halafu listen show utaona mahojiano ya Chacha Wangwe unaweza kuyasikia.

Mimi nampenda sana Wangwe na watu wa Tarime toka alipofukuzwa nakuwa akisimangwa kama mtoto yatima hapa JF ni mimi niliysimama kidedea kuhakikisha analindwa kwa nguvu zote kiasi cha members wengine humu kunibatiza jina la Wangwe, mie sijaonesha unafiki wa kumthamini marehemu baaada ya kufa nilimpa heshima toka mwanzo na nimekuwa very active toka day one Wangwe alipobambikiwa kesi. furaha yangu ingetimia wakati angechukua uenyekiti Chadema.

wewe ulikuwa wapi siku zote kumsaidia Mwana Tarime Mwenzako? acha unafiki. wanajulika waliompa heshima wangwe kuna Mtanzania, Mkandara, Mkamap WAKIONGOZWA na mimi.

Acha unafiki wako, kumuunga mkono Wangwe sio lazima uandike pumba zako mtandaoni. Kuna watu wanafanya vitendo zaidi ya maneno. Maneno yako ya chuki na dhihaka kwenye msiba huu yanaonesha jinsi gani usivyojali feelings za watu wa Tarime.

Heshima ni kitu cha bure, ungepungukiwa na nini kama ungesubiria siku chache tu wenzako tukaomboleza na kuzika ndio ulete unafiki na upuuzi wako hapa?
 
Kumbe wewe ni mwongo na mzushi namna hii, sikukujua. Kwa taarifa yako CHADEMA inaongoza halmashauri tatu, acha uvivu tafuta na hizo zingine mbili-achana kuandika mambo kwa hisia!
Rais karibu sana mheshimiwa, kwanza omba radhi kwa sisi wapenzi wa Wange uliposema kuwa marehemu ni mzigo mzito ndani ya chadema.
kumsaidia MKAMAP kuna halmashauri ya KARATU kwa mzee Slaa ambayo mnaiongoza kabla hata ya wewe kuingia Chadema. kama sikosei na Kigoma.
karibu Rais wetu. RAIS.. RAIS.. RAIS..
 
wewe naye!!!

5. Ktk uhai wake watu wa chadema walidai apigwe risasi na kweli dalili za mwanzo zinaonyesha CHACHA kapigwa RISASI mbili za kichwa.

Wewe ni laghai na mzushi sana, na uzushi wako unatisha mno! Ni mtu gani wa chadema alisema Chacha apigwe risasi? Hivi huu uzushi unamtumikia nani na kwa manufaa gani, au una-abuse anonymity yako hapa?

Unafikiri kwa kuwa unatumia jina bandia basi una uhuru wa kuropoka na kupayuka unavyotaka?
 
.....

Hata ktk hali ya kawaida mtu akikwambia aisii wewe subiri nitakuchoma kisu cha tako ,na baada ya siku kadhaa kweli ukachomwa kisu ,polisi wanakuja moja kwa moja kwa yule jamaa aliyetamka hakuna cha kujadiliana hapo.

Bado unaleta stereotype kwa watu wa Tarime. Hakuna watu wanaoongea kwa kutishia watu kwa visu katika Tarime ninayoijua mimi. Tafadhali sana Mkamap, weka heshima na subira kwetu wakazi wa Tarime badala ya kuleta maneno ya dharau kwa maelfu ya wakazi wa Tarime wanaomboleza kifo cha mbunge wao waliyempenda.
 
Hii misiba ambayo inasimamiwa na serikali na kuzuia wafiwa wasimkague ndugu wao ninakuwa na mashaka nayo toka alipouliwa Dr.Omar ALi Juma nasema aliuliwa kwani serikali ilikataza mtu yeyote kumfunua au kumkagua na hata alipopelekwa Pemba Ndugu zake hawakuruhusiwa kuagana nae alipelekwa kaburini moja kwa moja na walihusika kuuzika mwili huwa ni usalama wa taifa kama majeshi au polisi ndio haohao,wahusika walitakiwa kukaa mbali na maiti eti wanazika kitaifa hadi hii leo nasikia kaburi lake kuna gadi ,kwani serikali inaamini watu wanaweza kwenda kulifukua ili kujua kama walizika mtu au gogo,ni utata mtupu lakini kweli itajulikana tunangojea kuanguka kwa CCM kila kitu kitaanikwa uwanjani na wahusika kama kufa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria labda wawahi kufa ,lakini hili litazuka tu kama wanasikia yule wa mauaji ya Sebrenika Bosnia yupo kizimbani akijibu masuala basi na hawa waache wachelewe kufa tuone ,hii itakuwa ishu ya kisiasa uhai ukiwepo.
 
Mbowe Alisema Hayuko Tayari Kufanya Kazi Na Wangwe Anayevujisha Siri Za Chadema. Walijaribu Kumnyamazisha Kidemokrasia Wakashindwa, Sasa Wameenda South Africa Kumtafutia Sangoma La Kumuondoa.

JF imeingiliwa na wagagagigikoko, my God na nilikuwa nafikiri JF ni kijiwe cha walio nazo. What a big disappointment and what a contrast between Tarime and Ugagagigikoko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom