Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
"Tulianza safari kama majira ya saa moja hivi, sasa wakati tuko njiani kilomita kama 20 kutoka Kisasa, mimi nilianza kusinzia nikiwa seat ya mbele (kiti), marehemu akaniambia hapo huko safe (salama), hama rudi nyuma kalale kwenye kiti."


Huu ni mwanzo wa simulizi wa ajali hiyo mbaya ya gari ndogo aina ya Toyota Corolla Limited, ambayo imesababisha kifo cha Wangwe na kushtua taifa na kusababisha majonzi makubwa kwa Watanzania, wa kada mbalimbali.

Malya anasema wakiwa njiani kabla ya ajali, marehemu alisimama sehemu kununua muda kwa maongezi ndipo yeye akarudi kiti cha nyuma kama alivyokuwa ametahadharishwa na marehemu Wangwe.

"Baada ya kusimama, mimi nikarudi nyuma huku nasinzia, lakini nikiwa nimefunga mkanda, kisha akawa anaendesha gari akiniambia tungelala Morogoro ili leo (jana), tuanze safari ya Dar es Salaam kuwahi msiba wa mzee Boke Munanka," anasema na kuongeza:

"Yeye akiwa anaendesha katika mwendo wa kasi lakini haikufika 120, sasa ghafla tukiwa eneo la Pandambili, nilisikia mshindo mkubwa huku gari ikiwa imefunikwa na vumbi jingi kiasi kwamba sikuweza kujitambua mara moja."

"Wakati nikijiangalia, nikamkuta marehemu ametoka kiti chake cha mbele akatupwa hadi nyuma kwangu nilikokuwa nimekaa, kichwa chake kikawa katika miguu yangu akapasuka eneo la kichwa na kifua kisha akatokwa na damu nyingi sana."



source: Mwananchi Communication

Sina kumbukumbu nzuri, siku mbili kabla ya ajali ya Chacha nilipita barabara hiyo, kwa mwendo wa kasi, si rahisi kusimama kununua vocha ya simu eneo la kabla ya Pandambili, hasa kama giza limeanza kutanda. Sehemu kubwa ya maelezo ya Mallya yana utata mkubwa na sasa polisi wamefanikiwa kumfanya aseme ukweli. Mallya amekutwa na vitu vingi vyenye utata mkubwa. Tusubiri tuone.

Kuhusu Zitto, ndugu zangu HALI SI NZURI HATA CHEMBE..... Nasema pasi shaka kwamba, Zitto alikua katika hali mbaya sana wiki iliyopita na kama barua yao inavyojieleza suala hilo liliripotiwa kwa IGP hata kabla ya ajali ya Wangwe, sasa hapo sidhani kama Chadema wanatumia tishio la Zitto kukwepa jambo, na HAKIKA hawana cha kukwepa kwani uchunguzi wa polisi hata kama miongoni mwao watahusika wachukuliwe hatua, jambo ambalo wananchi wanalitaka, SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE hata kama ni watu ndani ya CHADEMA, ndani ya Usalama, ndani ya CCM, Makampuni ya madini, Wanaotaka jimbo na kadhalika. Nimetumia neno ndani kwa kuwa Chadema, CCM, Usalama, makampuni ya madini, ni taasisi ambazo haziwezi na wala hazina sera ya kuua
 
"Tulianza safari kama majira ya saa moja hivi, sasa wakati tuko njiani kilomita kama 20 kutoka Kisasa, mimi nilianza kusinzia nikiwa seat ya mbele (kiti), marehemu akaniambia hapo huko safe (salama), hama rudi nyuma kalale kwenye kiti."


Huu ni mwanzo wa simulizi wa ajali hiyo mbaya ya gari ndogo aina ya Toyota Corolla Limited, ambayo imesababisha kifo cha Wangwe na kushtua taifa na kusababisha majonzi makubwa kwa Watanzania, wa kada mbalimbali.

Malya anasema wakiwa njiani kabla ya ajali, marehemu alisimama sehemu kununua muda kwa maongezi ndipo yeye akarudi kiti cha nyuma kama alivyokuwa ametahadharishwa na marehemu Wangwe.

"Baada ya kusimama, mimi nikarudi nyuma huku nasinzia, lakini nikiwa nimefunga mkanda, kisha akawa anaendesha gari akiniambia tungelala Morogoro ili leo (jana), tuanze safari ya Dar es Salaam kuwahi msiba wa mzee Boke Munanka," anasema na kuongeza:

"Yeye akiwa anaendesha katika mwendo wa kasi lakini haikufika 120, sasa ghafla tukiwa eneo la Pandambili, nilisikia mshindo mkubwa huku gari ikiwa imefunikwa na vumbi jingi kiasi kwamba sikuweza kujitambua mara moja."

"Wakati nikijiangalia, nikamkuta marehemu ametoka kiti chake cha mbele akatupwa hadi nyuma kwangu nilikokuwa nimekaa, kichwa chake kikawa katika miguu yangu akapasuka eneo la kichwa na kifua kisha akatokwa na damu nyingi sana."


source: Mwananchi Communication

Haya maelezo ya huyu kijana ni ya kupanga kabisa...Eti alikuwa anasikia usingizi na kuamuwa kulala nyuma baada ya kuambiwa na marehemu...Sasa marehemu ndiye alikuwa na haraka ama ni yeye aliyemuamsha kwa simu hata licha ya kujuwa hali yake si nzuri?

Unaweza kuta kijana alimlazimisha marehemu aendeshe kwa kujifanya hawezi ama an usingizi mzito na marehemu kwa huruma ya mtoto huyo....

Akaamuwa kuendesha gari licha ya maruwe ruwe na ugonjwa ambao alishindwa hata kuamka asubuhi na mapema licha ya kugongewa kwa nguvu na mtoto wake wa kumzaa anyeitwa Zakayo.

Simu ya nyoka mtoto anayeitwa Deus Mallya ndiyo iliyomuuwa Wangwe!

Ama kweli Wangwe alikuwa ni SHUJAA!

Mungu atusamehe sana...Ila na sisi tujifunze kuwa watu wenye misimamo isiyoyumba ili tusiingie mitegoni..Na pia kuwa werevu!

Ndio maana hata Zitto aliponea...Na ndio maana watu kama kina Slaa bado ni wazima kwani ni Mungu anawasaidia kwa kuwa ni watu wanaotabirika...wao huyasimamia MASLAHI YA TAIFA..PERIOD.

Sasa tumempoteza mpiganaji...Lakini haina maana vita tumeshindwa.

Kauli za huyo Deus ni za kupangwa na hao watu walio onekana naye kwenye gari ni wakukamatwa mara moja.

Na huyo Deus aseme ni nani aliyetoa msisitizo wa kuamshwa kwa Wangwe kwani inaonekana huyo aliyetaka asafiri kwa namna yoyote ile ni huyo aliyejuwa ratiba yake.Huyo aliyekuwa akiwasiliana naye ndiye huyo wa kukamatwa.

Na hiyo autopsy ijumlishwe na vipimo vya kitaalamu ili kujuwa ni nini kilipasua tairi...Kwani kama tairi likichomoka kwasababu ya nati ni tofauti na tairi kupasuka.

Na huyo kijana ametengenezwa kama shahidi tu.
 
CHADEMA hao wanataka kujivua wao lawama na kupeleka kwa wengine.

Waacheni polisi wafanye uchunguzi wao bila kuingiliwa na wanasiasa.

Hiyo ni ajali tu na sidhani kama kuna mkono wa mtu yeyote.

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza hapo, je dereva alifunga mkanda? Kwanini madereva TZ hawapendi kufunga mikanda?

Tutaendelea kutafuta wachawi kwenye vifo vya ajali na kuacha sababu za msingi ambazo zinajulikana na tunashindwa kuzifanyia kazi.

Mtanzania naelewa concerns zako ulizokuwa nazo kuhusu chadema walivyo-handle mgogoro wa kiuongozi. Unasema hii ni ajali tu na hapohapo unasema "chadema hao wanataka kujivua wao lawama..", ni lawama gani hasa?

Na je,pamoja na kwamba tunajua Wangwe kafariki katika ajali, huoni kwamba mpaka sasa hatujui mazingira ya ajali hii? Katika mazingira ambayo hata dereva wa gari lililopata ajali hajulikani na aliyeshuhudia ajali hajulikani mahusiano yake na marehemu, yaani huoni umuhimu wa uchunguzi wa kina? Huoni kwamba haya ya kukataa uchunguzi ndio yanasababisha hizi conspiracy theories kusambaa?

Kulikuwa na fununu nyingi kuhusu mazingira ya ajali ya Salome Mbatia, tukalumbana, tukabuni na kutoa kila aina ya hisia, na ikaishia hivyohivyo, sasa huoni kwamba kuna haja ya kuachana na hizi conspiracy theories kwa kuweka ukweli sawasawa?

Above all, wewe unajua vizuri sana kwamba tatizo likitokea ndio huwa mara nyingi ni mwanzo wa kutatua tatizo hilo in the long run. Sasa hizi ajali zinatokea kila siku, tunapiga kelele na kutoa kila aina ya utabiri na kisha yanapita, huoni kwamba wakati umefika kufanya uchunguzi wa kina wa chanzo cha ajali kama hizi ili tuweke mikakati ya kujaribu kuzizuia?

Kwa mfano, ni nani anayejua ni kwa kiwango gani hizi ajali zinasababishwa na kutofunga mikanda, kunywa na kuendesha, ubovu wa magari, ubovu wa barabara, n.k. Hizo zote ni sababu tunazoweza kuzibuni kadri ya uzoefu (anecdotal evidence) lakini hatujui kipi ni kipi hasa. Sasa katika mazingira haya huoni kwamba ni muhimu pakawa na a thorough investigation?
 
hold on!!! Hivi yule dereva aliyemgonga Mbatia na akatokomea gizani mwenye jina la mwisho Mangula alipatikana?
 
Wangwe alizuiwa na familia yake asisafiri
Waandishi Wetu Dodoma, Dar na Tarime
Daily News; Wednesday,July 30, 2008 @00:01

Wanafamilia wa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe (52), ambaye alikufa kwa ajali ya barabarani mkoani Dodoma juzi walimsihi asisafiri wakiamini kwamba muda huo haukuwa mzuri, imefahamika. Kwa mujibu wa wanafamilia hao, sababu nyingine ya kumzuia ni kuwa alikuwa akipata matibabu ya malaria, lakini hata hivyo aliwakatalia.

Wangwe alikufa papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kwa safari ya kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam kupinduka katika eneo la Pandambili saa 2.55 juzi usiku. Watoto wa marehemu waliwaeleza waandishi wa habari nyumbani kwake Dodoma jana, kwamba wakati baba yao akijiandaa kuondoka saa moja usiku kwa safari ya Dar es Salaam, walimbembeleza aahirishe safari hiyo hadi jana lakini alikataa akisema kwamba shughuli zilizokuwa zinampeleka huko zingekwama.

Mtoto wa kiume wa marehemu, Zakayo Chacha (19) alisema mara ya mwisho alipomwona baba yake ilikuwa saa moja juzi jioni akitoka gereji kutengeneza gari lililobainika kuwa na hitilafu baada ya kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam na kurudi njiani eneo la Ihumo na yeye na mdogo wake, Bob (18) walitumia nafasi hiyo kumwomba akubali ushauri wao na wa mama yao, Mariam, wa kuahirisha safari lakini alikataa.

Kwa mujibu wa watoto hao, hofu yao kubwa ilitokana na jinsi baba yao alivyokuwa akiugua malaria kwa siku tatu mfululizo za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kiasi cha kulazimika kupata dozi, kulala kitandani huku akitetemeka mara kwa mara na kula kwa taabu. Walisema awali, walifichwa habari za kifo cha baba yao kwa kuambiwa kwamba alikuwa amepata majeraha madogo tu hadi walipoona idadi kubwa ya wabunge wakifika kwao na kuwapa mkono wa pole muda mfupi baada ya saa tatu usiku.

Ilibainika pia jana kwamba vibaka katika kijiji ambako Wangwe alipata ajali, walikwapua bidhaa na mali nyingine kutoka kwenye gari lililopata ajali. Kwa mujibu wa Deus Mallya, ambaye alisafiri na marehemu Wangwe na aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, anachokumbuka alisikia kishindo na alipogutuka alikuta gari limeshapata ajali na Wangwe alikuwa amekufa. Alisema muda mfupi baadaye vibaka walifika na kuanza uporaji hadi alipolazimika kupiga simu Polisi.

Mapema asubuhi Bunge lilizizima kwa majonzi na wabunge kadhaa kutokwa machozi baada ya Spika Samuel Sitta kutangaza rasmi kifo cha Wangwe. Baada ya kutoa taarifa hiyo na wakati akijaribu kutaarifu juu ya kufanyika kwa kikao cha kamati ya uongozi, Sitta alizidiwa na uchungu na kuangua kilio. Mara baada ya kuona hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda naye alianza kulia na wakafuata wabunge wengine.

Akitangaza kifo hicho bungeni Dodoma baada ya kusoma dua la kuombea Bunge, Spika Sitta alisema; "Waheshimiwa wabunge kwa mara nyingine nalazimika kutangaza katika kikao hiki cha tisa kuwa Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe amekufa kwa ajali saa 2.55 usiku katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam. Alipata ajali akiendesha gari lake aina ya Toyota Corolla ambalo lilipinduka eneo la Pandambili na kubiringika na kugonga miti hivyo aliumia na kufa papo hapo.

"Wangwe alikuwa na mtu mwingine aliyetambulika kwa jina la Deus Mallya ambaye amesalimika, yuko Hospitali ya Dodoma, hatuna maelezo ya ziada. Kwa niaba yangu na yenu, tunatoa pole kwa familia, wapiga kura wa Tarime na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mwenyekiti na wote walioguswa na msiba huo. "Kutokana na kanuni 149 ambayo inasema, endapo mbunge atafariki wakati shughuli za Bunge zikiendelea, Spika anaweza kuahirisha shughuli za Bunge kwa ajili ya kutoa nafasi ya shughuli za maombolezo, kwa kanuni hiyo naahirisha Bunge hadi saa sita mchana."

Bunge lilipokutana muda huo wabunge walitaarifiwa taratibu za kuuaga mwili wa marehemu baadaye jioni katika shughuli iliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete. Wakati wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge huku wakitokwa machozi, baadhi walikuwa wameshikiliwa na wenzao kutokana na kusikitishwa na msiba wa mbunge huyo. Wabunge kadhaa waliohojiwa walielezea kushtushwa na kifo cha ghafla cha Wangwe na wengi wao walieleza kuwa wamepoteza mwanamapambano, huku kambi ya upinzani ikieleza kupata pigo kubwa.

Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema Wangwe alikuwa na mchango mkubwa katika kambi ya upinzani kwani alikuwa mtetezi wa wananchi. Mbunge wa Viti Maalumu Lucy Owenya (Chadema), alisema ameshtushwa na kifo cha Wangwe hasa akizingatia juzi asubuhi alikuwa naye bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu. Kwa mujibu wa Owenya, Wangwe alikuwa na mchango mkubwa bungeni na kwamba kambi ya upinzani na Bunge kwa ujumla wamepoteza mwanamapambano.

Naibu Spika, Anne Makinda, alimsifu Wangwe hasa kwa tabia yake ya kupenda kutumia vifungu vya katiba anapotaka kueleza jambo bungeni. Akizungumza kwa masikitiko alisema, Ijumaa iliyopita Wangwe alimweleza kuwa anataka kuwasilisha maelezo yake binafsi na kwamba alimueleza kuwa nafasi hakuna hadi Jumatatu. "Alitaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu ugomvi wa wafugaji Tarime na wizi wa mifugo na kuomba polisi wasitumie nguvu wanapotaka kuhamisha wananchi. Jana (juzi) alinikumbusha asubuhi nikamwambia unaweza kupata nafasi baadaye," alisema.

Hata hivyo, Makinda alisema baada ya hoja ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo kupitishwa, muda ulibaki na Spika Sitta alimtuma Ofisa wa Bunge, Japhet Sagasii kumtafuta Wangwe lakini hakuonekana na huo ndiyo ukawa mwisho wa mbunge huyo. Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM) alisema kifo cha Wangwe kilimshtua na kwamba kimewasikitisha wabunge wote bila kujali itikadi. "Tutamkumbuka Wangwe, yeye katangulia lakini wote tutafuata," alisema.

Maziko ya Wangwe yatafanyika wilayani Tarime kesho na wabunge kadhaa watashiriki. Bunge limekodi ndege ambayo itapeleka maiti, ndugu na msafara wa wabunge 20 kwenda Tarime leo kwa maziko. Ujumbe wa Bunge utaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo Wangwe alikuwa mjumbe, William Shellukindo. Kwenye msafara huo watakuwamo wabunge wote wa Mkoa wa Mara, wabunge watatu wa kambi ya upinzani akiwamo kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashid Hamad na wabunge wengine kwa kuzingatia maeneo na jinsia.

Katika hatua nyingine, Chadema imetangaza bendera zake zote nchi nzima kupeperushwa nusu mlingoti kwa kipindi cha wiki moja kuanzia jana, ikiwa ni kuomboleza msiba huo. Sambamba na hilo, makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni Dar es Salaam, jana kuliwekwa kitabu cha maombolezo ambako watu mbalimbali walimiminika kukisaini, miongoni mwao akiwamo Mbunge wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi na Mjumbe wa Baraza la Udhamini, Muslim Hassanali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa kikao cha Sekretarieti ya chama hicho, Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Vijana, John Mnyika alisema kuwa chama hicho kimepokea taarifa hizo kwa masikitiko na mshtuko. Alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alikwenda Afrika Kusini kwa ziara ya kisiasa Jumapili iliyopita kwa wiki moja, amekatisha ziara hiyo na anatarajiwa kurejea nchini leo na kuendelea na safari hadi Tarime kwa ajili ya kuungana na waombolezaji.

Viongozi wengine watakaohudhuria maziko hayo yatakayofanyika kesho ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye aliondoka jana na familia ya marehemu iliyokuwa Dar es Salaam na Dodoma kuelekea Tarime. Wengine watakaohudhuria ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, Ofisa Mwandamizi wa Ulinzi na Usalama, Hemed Sabula, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na mafunzo, Benson Kigaira ambaye ndiye mratibu wa mazishi hayo na wenyeviti wa chama hicho wa mikoa ya Mwanza, Kagera na Shinyanga wakati Mkoa wa Mara utawakilishwa na Katibu wa Mkoa.

Kutokana na msiba huo, Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Bunge, wananchi wa Tarime na Chadema ambako amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko. Naye Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema mbali na kusikitishwa kupata taarifa hizo, kifo chake kimeacha pengo kwa Chadema na Bunge hasa kambi ya upinzani kutokana na Wangwe kuwa nguzo katika shughuli za siasa ndani ya chama na bungeni.

Wangwe ameacha wajane watatu ambao ni Jacqueline, Dotto na Maryam na watoto tisa ambao wanaume ni wanne na wanawake watano. Na Makubo Haruni anaripoti kutoka Tarime kuwa kifo cha Wangwe kimewaliza watu wengi hususani wakazi wa Tarime ambao tangu taarifa itolewe na vyombo vya habari wamekuwa wakikusanyika makundi kwa makundi, wengine wakilia na kububujikwa machozi na kila mmoja akiwa na hisia tofauti, kwamba kina mkono wa mtu huku wengine wakisema ni kazi ya Mungu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kuwa wamepoteza Mbunge aliyekuwa akiwatetea hata kufanya sungusungu waliokuwa wakiwapiga na kuwanyang'anya mali zao kukoma kutokana na msimamo wake usioyumbishwa. Wakati wananchi wakilia kumpoteza waliyedai kuwa ni mpiganaji kama aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Chama Cha Mapinduzi kimesema kimepokea taarifa ya kifo hicho cha ghafla kwa masikitiko makubwa, kwa maelezo kwamba alikuwa mdau muhimu wa changamoto za kisiasa.

Katibu wa CCM wa Wilaya za Tarime na Rorya, Iddi Stambuli, amesema kuwa Jimbo la Tarime limeondokewa na kiongozi ambaye alikuwa mwenye msimamo wa kutetea wanyonge. Hata hivyo, amewataka Watanzania na wakazi wa Tarime kutolihusisha tukio la kifo cha Wangwe na mkono wa mtu, na kuanza kunyosheana vidole kwa maelezo kuwa kifo hicho ni mapenzi ya Mungu.

Kwa upande wa Chadema Wilaya ya Tarime imesema kuwa licha ya kupata pigo kubwa la kuondokewa na mpambanaji wa siasa wilayani hapa asiyekubali uonevu, pia wamepunguza nguvu ya kisiasa ya kidemokrasia na kwamba itachukua muda kumpata mtu mwenye kupendwa na watu wengi kama Wangwe. Katibu wa Chadema, Joseph Anton alisema: "Baada ya kifo hicho watu wengi wamekuwa wakitupigia simu wakidai kuwa hiyo ajali ina mkono wa Chadema, huku wengine wakidai kuwa ni wa CCM. Msimamo wetu ni kwamba Mbunge huyo amekufa kifo cha kawaida na si vinginevyo na sasa tunaandaa mazishi yake kijijini kwake Kyamakorere."
 
Ka nzi ka KLH Kamepeperuka...

Nimepatiwa majibu yafuatayo. Bado mengine tunaweza kusahihisha kwa kadiri nzi anavyoruka ruka. So, right now I'll give the following info 80% ya usahihi.

3.Huyu kijana yeye ndio alikuwa wa kwanza kuipigia polisi simu na kuwataarifu kuhusiana na msiba huo. Sasa hapa panaleta utata mkubwa sana ;

a) Alipata wapi number za simu za polisi?Tena hapo hapo?
b)Ni kwanini awapigie polisi wa kwanza ,na je?yeye kama alikuwa na simu za Wangwe aliwezaje kuzipata kwa hali gari lilivyokuwa?
c)Huyu kijana aliwapigia simu watu wa Tarime na kuwafahamisha kuwa Wangwe amefariki ,na mmoja wapo ni aliyekuwa rafiki wa karibu wa Chacha ambaye alikuwa katibu wa CHADEMA wilaya ya Tarime aliyehamia CCM.
D) Alimpigia simu mke wa Marehemu pamoja na ndugu zake marehemu, ila hakupiga simu kwa kiongozi yeyote wa CHADEMA ,ile hali kama alikuwa anatumia simu za Wangwe basi number za simu za viongozi wa CHADEMA zilikuwepo.
e) Mkuu wa wilaya ya Kogwa alienda eneo la ajali in 30 minutes time ,baada ya ajali na ndio alimfahamisha Mkuu wa Mkoa ,then Waziri wa mambo ya ndani na then Spika.....
f) Zitto alipigiwa simu na waziri Masha, na baada ya simu kukatika alimpigia spika na spika akasema hata yeye kayasikia hayo .

4.Huyu kijana Mallya ,kwa taarifa za leo ni kuwa amekubali kuwa yeye ndio alikuwa anaendesha gari ,na hilo kalisema polisi .

5.Huyu Mallya kuna taarifa kuwa ameiharibu simu yake na ameondoa simu card yake pamoja na kingine kikubwa na cha kustaajabisha ni kuwa ameondoa memory card ya simu yake .

Sasa hili la memory card linatupa wasiwasi zaidi na hatujui ni kwanini hilo limefanywa hivyo na hii inaonyesha kuwa aliyefanya hivyo lazima atakuwa ni expert mzuri sana .

6.Kwa taarifa za kiuchunguzi ni kuwa huyu Mallya alikutwa na bastola, na alisema kuwa ni ya kwake ,sasa hatujui kama hili polisi watalisema kwani hilo limesemwa na watu ambao walikuwepo wakati polisi walipokuwa wamefika eneo la ajali na kuanza upekuzi.

7.Huyu Mallya ,inasemekana kuwa alikuwa na mtu mwingine kwenye gari ambaye wanakijiji wa pale hawakuweza kumfahjamu mara moja, na haijulikani alipo.

8,kwenye eneo la tukio mzee wa pale kijijini ambaye alisaidia kumtoa Wangwe kwenye gari anasema kuwa huyu wangwe alikuwa amekaa kiti cha abiria mbele ,na alikuwa amefunga mkanda, na huyu mzee ndio alimtoa huop mkanda na kumtoa nje.

My Take:
- The burden of proof, iko kwa Polisi kumuweka kijana huyo kizuizini. My gut tells me something about assassination. It is just my gut and I probably am very wrong.
- Kama kweli Mallya alikuwa na bunduki, was it discharged for any reason even "accidentally"?
- Kuna mtu aliomba lift aidha walipoenda kununua "voucher" kutokana na ushauri wa Mallya. Huyo mtu wa tatu hakuwepo mwanzo wa safari, na kwa hakika hakuwepo mwisho wa safari. Who is he?
 
Malya the Mysterious Crook.
Sasa hapa tunaweza kuona this was very clearly planned.I have maintained a very strong stand kumuhusu huyu mtu na sasa naona my speculations were pure and true.Sasa tuone kama polisi watafanya kazi yao ama watakuwa vibaraka.IGP Mwema waonyeshe Watanzania you can do it even if you have to intervene and question him personally?Electrecute him if you have to and slice bits of him until he confesses who ordered him to do such a merciless thing.
Mwema prove to us you are not among the dirtiest but a servant of the people and a real patriot.Get the names and have them prosecuted maliciously.
 
...duuuh!

huyo jamaa (Malya) akiyasikia yanayosemwa na wananchi 'naona' atawish tu bora naye angekufa kuliko anavyoonekana amekula njama za kumuua Mheshimiwa!

scenario 2; Hivi angekufa Malya, Chacha Wangwe atoke unscathed, hadithi ingekuwaje?

Kumbe ndio maana VIPs Mh.Mudhihir, na Mh.Prof Kapuya hawana hatia kwenye ajali zao eeh?

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Lakini kama kweli jamaa ameweza kuona kila kitu, kidogo inatia shaka. Watu wengi ambao wanapata ajali mbaya kama hizo mara nyingi watakuambia (baada ya fahamu kuja) kuwa alisikia taili limepasuka, then vumbi then baada ya kupata fahamu akajikuta na damu kibao. Anyway, nami nampa the benefit of doubt!!!

Kama alivyosema bwana Kitilya huko nyuma inawezekana kabisa bwana Deusi ndiye alikuwa dereva sasa anajaribu kuficha ukweli ili aisije akafunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusudia.

Otherwise, hii ni ajali tu wala hakuna mkono wa mtu. Kama matatizo ya gali yeye mwenyewe alishayajua, hali yake ya afya haikuwa nzuri kwa nini aliamua kusafiri? Tatizo ni may be ni Deus kutuficha kuwa nani alikuwa anaendesha.
 
MMKJJ

.. patakuwa hapatoshi! Hao Polisi wawe waangalifu huyu kijana asije kututoka kama Balali.
 
Je, hiyo bastola ilikuwa na risasi ngapi na kuna ambazo zilitumika siku hiyo ya ajali hasa ukitilia maanani inasemakana kwamba Wangwe alitoka damu nyingi kichwani? Huyo Mallya inasemekana anaishi Masaki, Dar. Je, ilikuwaje kuwaje hata akawa Dodoma?Na alikuwa na uhusiano gani na Wangwe? tangu lini?
 
Hizo ndio politics bwana za Mheshimiwa Mnyika... Hongera Dogo ... ni kikao gani cha CHADEMA kimepitisha hiyo nia ya kuchunguza... na viongozi wangapi wanahitaji huo ulinzi na kwa nini?

Mpaka leo hakuna sehemu niliona au kusikia kwamba Zitto alikuwa na Ugomvi na Marehemu Chacha Wangwe... neither Dr. Slaa.

Unless useme ulikuwa unatumia hayo majina kwa ajili ya Mbowe kupewa Ulinzi.

Lakini waTanzania tuna-create problems ambazo hazipo...

Mpaka leo, familia ya Balali haijawahi kulalamikia kifo cha ndugu yao, lakini Dr. Slaa na CHADEMA wamelalamika wee...akina ndg yangu MwanaKijiji wamelalamika weeeee.....

Sasa hili nalo... linaletewa spinning.
 
Hapa ukweli utajulikana tu kwani clue zipo tena zipo wazi. Huyu kijana ni lazima aseme huyo mtu wa 3 ni nani? Makampuni ya simu yasaidie kutrace mawasiliano ya imu ya huyo Mally.
Tutaomba polisi wafanye kazi yao vizuri, mungu ibariki Tanzania.
 
I'll tell you one thing. Anayedhania Polisi are willing, able, and determined to find out the truth anaota njozi. Tukubali tu yaishe. Believe me, "mapenzi ya Mungu" yataimbwa kama wimbo wa "Kasuku". You know what, I'm so done, sitoingia zaidi ya nilivyoingia, it is very dangerous.

Anayeamini ajali aendelee asiyeamini lwake!
 
Mtanzania naelewa concerns zako ulizokuwa nazo kuhusu chadema walivyo-handle mgogoro wa kiuongozi. Unasema hii ni ajali tu na hapohapo unasema "chadema hao wanataka kujivua wao lawama..", ni lawama gani hasa?

Na je,pamoja na kwamba tunajua Wangwe kafariki katika ajali, huoni kwamba mpaka sasa hatujui mazingira ya ajali hii? Katika mazingira ambayo hata dereva wa gari lililopata ajali hajulikani na aliyeshuhudia ajali hajulikani mahusiano yake na marehemu, yaani huoni umuhimu wa uchunguzi wa kina? Huoni kwamba haya ya kukataa uchunguzi ndio yanasababisha hizi conspiracy theories kusambaa?

Kulikuwa na fununu nyingi kuhusu mazingira ya ajali ya Salome Mbatia, tukalumbana, tukabuni na kutoa kila aina ya hisia, na ikaishia hivyohivyo, sasa huoni kwamba kuna haja ya kuachana na hizi conspiracy theories kwa kuweka ukweli sawasawa?

Above all, wewe unajua vizuri sana kwamba tatizo likitokea ndio huwa mara nyingi ni mwanzo wa kutatua tatizo hilo in the long run. Sasa hizi ajali zinatokea kila siku, tunapiga kelele na kutoa kila aina ya utabiri na kisha yanapita, huoni kwamba wakati umefika kufanya uchunguzi wa kina wa chanzo cha ajali kama hizi ili tuweke mikakati ya kujaribu kuzizuia?

Kwa mfano, ni nani anayejua ni kwa kiwango gani hizi ajali zinasababishwa na kutofunga mikanda, kunywa na kuendesha, ubovu wa magari, ubovu wa barabara, n.k. Hizo zote ni sababu tunazoweza kuzibuni kadri ya uzoefu (anecdotal evidence) lakini hatujui kipi ni kipi hasa. Sasa katika mazingira haya huoni kwamba ni muhimu pakawa na a thorough investigation?

Kitila,

Nilichomaanisha mimi ni kwamba kuna watu watawalaumu uongozi wa CHADEMA kwasababu
ya mgogoro uliokuwepo. Ni kawaida ya Watanzania kutafuta mchawi.

Naona ni kama CHADEMA nao wanajitahidi mno kusukumia lawama kwa watu wengine. Kwa mfano huyo kijana ameumia lakini sasa ni kama watu wanamwona muuaji wakati hakuna ushahidi wowote. Watu hawaamini alichosema huyo kijana.

Mimi nashauri tuwaachie polisi wafanye uchunguzi wao bila kuingiliwa na wanasiasa. Wakishindwa basi tutakuwa na kila haki ya kulalamika na kuandika barua.

Binafsi naamini hiyo ni ajali na wala hakuna mkono wa mtu. Matatizo ya ajali TZ yanajulikana ila hatutaki kujifunza na tunakimbilia kutafuta wachawi.

Kila nikisoma maelezo yaliyotolewa mpaka sasa ni kama mheshimiwa Wangwe hakufunga mkanda.

Tupiganie kwenye kuhakikisha sheria ili kulinda raia barabarani. Kama mpaka sasa viongozi wetu wakuu wanaweza kuendesha/kupanda magari bila kufunga mikanda, hii ni dalili mambo ya kufuata sheria kwetu ni shida kabisa.

Sokoine alikufa bila kufunga mkanda lakini mpaka leo bado kuna Watanzania wengi tu wanendesha/kupanda magari bila kufunga mikanda. Vifo vikitokea tunaanza kukimbilia wachawi.

Hata kwenye kifo cha Mbatia niliandika hivyo hivyo hakuna haja ya kutafuta mchawi, ile ilikuwa ajali.
 
I'll tell you one thing. Anayedhania Polisi are willing, able, and determined to find out the truth anaota njozi. Tukubali tu yaishe. Believe me, "mapenzi ya Mungu" yataimbwa kama wimbo wa "Kasuku". You know what, I'm so done, sitoingia zaidi ya nilivyoingia, it is very dangerous.

Anayeamini ajali aendelee asiyeamini lwake!

Mzee umepokea kitisho mara hii? nakushauri usikate tamaa endelea ku-dig in pia nadhani tuwape chance polisi huenda wakafanya kazi nzuri otherwise familia au CHADEMA itafute independent investigators.
 
Malya the Mysterious Crook.
Sasa hapa tunaweza kuona this was very clearly planned.I have maintained a very strong stand kumuhusu huyu mtu na sasa naona my speculations were pure and true.Sasa tuone kama polisi watafanya kazi yao ama watakuwa vibaraka.IGP Mwema waonyeshe Watanzania you can do it even if you have to intervene and question him personally?Electrecute him if you have to and slice bits of him until he confesses who ordered him to do such a merciless thing.
Mwema prove to us you are not among the dirtiest but a servant of the people and a real patriot.Get the names and have them prosecuted maliciously.

we jamaa unachafua hadi mada na huo mdomo wako wa kidemu. hivi huwa hausikiii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom