Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji,

Kama sijakosea hii safari ilikuwa ya usiku , kwa hiyo ia make alot of Sense labda abiria aliamua kulala ili wabadilishane gari mbeleni ...Vile vile nilisoma ya kuwa walikuwa wakienda Tarime hii kwa hiyo ilikuwa safari ndefu kidogo.

a. Je Mallya alijua kuwa Wangwe alikuwa mgonjwa na hajisikiii vizuri? Kwa sababu kama ni hivyo it'll make a lot of sense kwa aliyemzima kuanza kuendesha wakati mwingine aliyekunywa dawa na ambaye alikuwa hajisikii vizuri kupumzika.
 
we jamaa ni mchafu sana, unaamini mambo ya kishirikina tu moyoni mwako. familia yake yenyewe ilisema alikuwa anaumwa. gari ilikuwa na kipara hadi akaenda gereji kwanza. halafu alikuwa anaendesha gari yeye mwenyewe, au hata kama ni yule kijana, hatujui uzoefu wao kwa safari za masafa marefu kama yale. na kwanini aliacha gari yake,si angeendesha shangingi akiwa na dereva wake? hii inaonyesha kuwa, ni kifo cha kawaida kabisa. walikuwa na mwendo mkubwa wakashindwa kulimiliki gari labda kwasababu hawakuwa na uzoefu nao. au alikuwa anasinzia, au alikuwa amejisahau. ni kifo cha kawaida. kwanza umeambia kuwa, matairi mawili yalipasuka, sasa wewe unataka kuleta zakuleta bwana. nenda huko bwana.
 
Kuna tatizo huko Chadema, yaani Mwenyekiti anazunguka na helikopta nchi nzima Makamu wa Mwenyekiti anatumia Corolla yeye yenye stadds zilizolegea!
 
a. Je Mallya alijua kuwa Wangwe alikuwa mgonjwa na hajisikiii vizuri? Kwa sababu kama ni hivyo it'll make a lot of sense kwa aliyemzima kuanza kuendesha wakati mwingine aliyekunywa dawa na ambaye alikuwa hajisikii vizuri kupumzika.

Mallya yes alijua kuwa Wangwe ni mgonjwa na alimeza dawa za malaria, mtoto wake mara ya mwisho alipokwenda kumuamsha; hakuitika na alihisi kuwa atamsumbua so akamwacha alale na kurudi kumwambia Mallya kuwa baba amelala, amemeza dawa na hiyo ilikuwa mara ya 3 toka wamwamshe, then Mallya akwambia wacha nimpigie simu ndio akapiga na simu ikaita sanaaaaaaaaa then akapokea na Mallya akaanza kwa kusema "Mzee kazi zinalala amka" ndio akwambia ok. Maelezo haya ameyatoa mtoto wake jana mchana live ITV....
 
Kweli isije ikawa wamemuua halafu mwili ukakalishwa kwenye gari, gari ikawashwa accelerator jiwe ikajibamiza huku na kule hadi likawa nyang'a nyang'a. Yule kijana Deus Malya anastori za kutusimulia.
 
a. Je Mallya alijua kuwa Wangwe alikuwa mgonjwa na hajisikiii vizuri? Kwa sababu kama ni hivyo it'll make a lot of sense kwa aliyemzima kuanza kuendesha wakati mwingine aliyekunywa dawa na ambaye alikuwa hajisikii vizuri kupumzika.

Mallya alikua akiendesha gari. Full stop. Sana sana aseme alikua na nani mwingine, maana walioshuhudia wanasema walikua zaidi ya watu wawili katika hiyo gari na Wangwe alikua abiria. Huyu Mallya ni nani hasa kihistoria? ametokea wapi? alikua anafanya kazi wapi? amefikaje Chadema?
 
...haya, kwa mujibu wa magazeti yetu ya Bongo haya ndio maelezo ya Bwana Deus Mallya mwenyewe...

Speaking to reporters who paid him a visit at the hospital, Malya said Wangwe told him to move to the back seat to rest.

``� cannot forget what took place at the scene (of the accident). I don't believe that I have escaped death and I am still alive,`` he said.

``I was seated in the front seat and was dozing off before the accident, but he advised me to move over to the back seat because it was not safe where I was seated,`` he said.

Malya said they stopped over on the way to buy recharge vouchers before they proceeded with their journey.

``We were at Pandambili when I heard a great bang and saw a cloud of dust. It is then that I realised that the car`s tyre had burst. The vehicle was engulfed in dust. Wangwe moved from where he was seated to the place where I was with his head touching my legs. His seat had squeezed me as my seat belt was tight,`` he explained.

He said by the time he wanted to see more on what had taken place, he realized that Wangwe's head had sustained a fracture and a lot of blood was coming out.

``My body was soaked in blood, but that blood was not mine but Wangwe`s,`` he said.

Commenting on Malya`s condition, Dodoma Regional Medical Officer Dr Godfrey Mtei said it was improving, adding that he was still undergoing treatment.

source; http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/07/30/119515.html
 
Kuna tatizo huko Chadema, yaani Mwenyekiti anazunguka na helikopta nchi nzima Makamu wa Mwenyekiti anatumia Corolla yeye yenye stadds zilizolegea!

Hapo nimekupata tatizo ni hilo ndio lililosababisha ajali ya kumuondoa chacha duniani. Utata umekwisha. Tumuombee Chacha makazi mema na ya pumziko la milele.
 
Tumefika huku?

Mie nataka Zitto aje hapa atuelezee CHADEMA wanasema nini kuhusu hili,nimeona ushabiki wa hili jambo umekuwa sana toka jana na leo hivyo hivyo.

Mwanakijiji,
Say what you want coz you was the one who who talk about time...

Mie simo
 
a. Je Mallya alijua kuwa Wangwe alikuwa mgonjwa na hajisikiii vizuri? Kwa sababu kama ni hivyo it'll make a lot of sense kwa aliyemzima kuanza kuendesha wakati mwingine aliyekunywa dawa na ambaye alikuwa hajisikii vizuri kupumzika.

kwa mujibu wa taarifa rasmi toka kwa mwanae anasema huyu Mallya alijua kabisa na mtoto wa Wangwe alimweleza amwache mzee apumnzike.
 
MKJJ Hapo ndipo penye utata wenyewe...Kwangu binafsi nafikiri huyo kijana ni shahidi mzuri sana tu.
Kwanza kabla ya kuanza kuzungumzia haya...Ni bora tuanze na wale ambao wanaweza kunufaika na kifo chake.
Kama huyo kijana alidai kuwa kazi zinalala...Ni kazi gani zilizokuwa zinalala?
Si walikuwa wakienda msibani?
Je ni nani mwingine aliyekuwa akijuwa kuhusu kazi yake ya huko msibani?
Alikuwa akienda kumwakilisha nani kwenye msiba wa Bhoke?
Chama,ama familia ama ni yeye binafsi?
Pia inabidi tuzungumzie issue ya yeye kupambana na Barrick huko kijijini kwake...Hivi mnaijuwa Barrick nyie watu?
Huyu mtu ni kweli alikuwa mpambanaji...Tatizo ni tamaa ya madaraka...Na kutokuwa mwangalifu kwenye siasa zetu...Sasa anaweza akawa ameuwawa na mafisadi kwa namna ambayo italeta vurugu kwenye jamii...!
Marehemu Wangwe ni kweli alikuwa akiyapigania maslahi ya wananchi wake wa jimboni...Na alihamia chadema kwani wananchi walishachoshwa na ccm.
Sasa na yeye huo ukaribu wake na ccm bila kuwa mwangalifu halafu akiwa anawapinga tena kuhusiana na Barrick?
Si alikuwa kinyume kabisa na mkuu wa Polisi wa mkoa na kuu wa mkoa mwenyewe?
Yeye kama mbunge alikuwa tishio...Lakini at the same time...Tamaa ya madaraka ilimponza na hakuchukuwa maamuzi ya busara licha ya nia nzuri aliyokuwa nayo!
ccm wasilete UNAFIKI kabisa kwani huyu mtu alikuwa akipinga sana unyanyasaji wa serikali huko kwenye migodi kwa kuwatumia polisi na hata hoja yake aliyokuwa akitaka kuiwakilisha ilizimwa kwa kila namna na wakati akikaribia kuiwakilisha ndio akafa.
Na ili kumuenzi wabunge wanadai kuwa hoja yake hiyo ya mapigano hayo ya koo ifanyiwe kazi na isomwe bungeni.
Hoja hiyo ikisomwa pia tutapa clues nyingi sana.
Na ndio maana nikasema makabila mengine jamani tujifunze kuishi kama watanzania...Sasa unaweza kukuta labda hizo koo huko mara zinagombea ardhi yenye madini..Sasa dunia ya sasa ukoo wa kiafrika unamiliki madini ya Wananchi...wapi na wapi.
Hizo ardhi wanazogombea huko hao wanaojiona ni machifu si ni za Tanzania?
Tunataka mtuletee issues hapa na si kuletea assumptions ambazo hazina kichwa wala miguu!
Kwanza hizo tairi unaweza kuta zilipigwa risasi.
Na kwa uzoefu wangu mimi...Marehemu Wangwe nayeye inanishangaza sana alipoamuwa kuendelea na safari licha ya dalili zote hizo!
Ni wazi alijuwa ana mess na something BIG!
Lakini inaonyesha alijitowa MUHANGA!
Kitendo cha nuts kulegea kwenye gari yake kilitosha kumfana ajiulize maswali mengi kwani si kitu cha kawaida kuwa na nati zisizofiti na ama kutight kama kweli gari hilo ni lake na analitumia kila siku!
Na huyo kijana na historia ya jinsi walivyojuwanan iwekwe hapa!
Huyo kijana kule Kilimanjaro huwa wanaitwa NYOKA.
Hawa Nyoka kazi yao ni kuhakikisha mambo yote ni sawa ikiwa na uzima wa gari na kila kitu!
Sasa ika vipi NYOKA akalala nyuma na Bosi kuendesha?
Tena MH MBUNGE?
Pana UTATA HAPO!
Wangwe alikuwa akienda kukutana na nani?
Nani mwingine aliyekuwa akijuwa ratiba yao?
Kabla ya ajali na safari na mara baada ya ajali...Hizo namba zote za simu zilizopigwa na nyoka kwa kutumia simu yake na ya Wangwe zichunguzwe.
Nyendo zao wote zichunguzwe
Kwa sasa tuanzie hapo.
INASIKITISHA SANA!
MACHOZI YA MAMBA YA ccm YATAWACOST kama haki isipotendeka kwani wao ndio wanao miliki dola na wananchi wanataka majibu.
 
Hili ni gari la Chacha
2.JPG
Laiti kama angekuwa na shangingi tungeongea mengine.
Wakuu hivi ile mikopo ya mashangingi kwa wabunge inaendelea?
Safari ndefu kwa gari dogo kama hili ni hatari sana.
 
Mallya alikua akiendesha gari. Full stop. Sana sana aseme alikua na nani mwingine, maana walioshuhudia wanasema walikua zaidi ya watu wawili katika hiyo gari na Wangwe alikua abiria. Huyu Mallya ni nani hasa kihistoria? ametokea wapi? alikua anafanya kazi wapi? amefikaje Chadema?

Mkuu Halisi, hapa unaleta clue nzuri sana kwamba WALIOSHUHUDIA waliwaona watu zaidi ya WAWILI. Sasa hawa watu wa ziada mbona wanafichwa? Hawa mashuhuda pamoja na Mallya hope wataisaidia polisi ili kupata ukweli.

Poleni wafiwa na wanaCHADEMA.
 
kwani huyo Mallya ameumia kiajari ama amejiumiza makusudi?? wakimukagua vizuri watatambua kama ameumia ndani ya gari ama nje ya gari.
 
kwani huyo Mallya ameumia kiajari ama amejiumiza makusudi?? wakimukagua vizuri watatambua kama ameumia ndani ya gari ama nje ya gari.

Nadhani maelezo ya huyo kijana yanajitosheleza , tatizo hapa watu tumeshafika conclusion .

Hivi ni ajali ngapi tumeona baadhi ya watu wanakufa na wengine wanapona ? Unless watu

watakuja na ushahidi mwingine ...mimi nitaendelea kuamini ya kuwa hii ilikuwa ni ajali Period.
 
Mukiiangalia hii barua ya Chadema kwenda kwa IGP munagundua kuwapo kitu kilichofichika wiki moja kabla hata ya kifo cha Chacha Wangwe. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alitishiwa maisha, alizushiwa kifo na hilo si jambo dogo, Je, polisi wanasema nini?

C/HQ/ADM/SG/02/185 30 Julai, 2008

MKUU WA JESHI LA POLISI,
P.O.BOX DAR ES SALAAM ,
TANZANIA.

YAH; KIFO CHA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE MBUNGE WA TARIME.

Kutokana na ajali iliyotokea tarehe 28 Julai 2008 katika eneo la Pandambili Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, ninalazimika kukuandikia rasmi kuhusiana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini juu ya utata ambao umekighubika kifo hicho na haswa mazingira ya ajali yenyewe. Katibu Mkuu wa CHADEMA, katika mahojiano yake na TBC1 katika mahojiano yake kwenye kipindi cha Jambo Tanzania alielezea pia utata huo na kutaka Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina.

Maelezo ya Ndugu Deus Mallya ameyatoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na jinsi ajali hiyo ilivyotokea na eneo ambalo yeye alikuwa amekaa wakati ajali inatokea , pamoja na kusema kuwa yeye alikuwa amekaa kiti cha nyuma huku Dereva wa Gari akiwa ni Marehemu Chacha Wangwe yameongezea kwenye utata huo.

Taarifa ambazo zimetolewa na watoto wa Marehemu kama walivyohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuripotiwa na vyombo hivyo na haswa maelezo yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), na vituo vingine vya Television, pamoja na Habari za Magazeti mbalimbali ya tarehe 30-07-2008 ,kama vile Magazeti ya The Guardian, Nipashe, Tanzania Daima ,Mwananchi na mengineyo ambayo yaliandika kuhusiana na maelezo aliyotoa Ndugu Deus Mallya pamoja na watoto wa Marehemu yakilinganishwa na maelezo ya Deus Mallya yanahitaji kupatiwa majibu ya kina, jambo ambalo CHADEMA kama mwathirika wa ajali hiyo isingeliweza kulifumbia macho.

CHADEMA , tumefuatilia kwa kina sana kuhusiana na maelezo hayo ambayo yametolewa kwa nyakati tofauti na watu tofauti kuhusiana na ajali hiyo na hatimaye msiba huo.

Hivyo basi , Chadema kama Chama kilichoathirika kwa kumpoteza Mbunge wake, Mwenyekiti wake wa Mkoa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na hivyo kuwa na maslahi ya karibu sana katika uchunguzi huu, tunalitaka Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vingine vya Usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na mambo yafuatayo;

1. Kujua huyu ambaye alikuwa (Deus Mallya) na Marehemu kwenye gari lake wakati anafariki ni nani na anafanya shughuli gani.
2. Deus Mallya alienda Dodoma kufanya shughuli gani na ana uhusiano gani na Marehemu na au Familia ya Marehemu.
3. Ndugu Deus Mallya alikuwa amekaa kwenye kiti gani wakati ajali inatokea.
4. Ni nani alikuwa anaendesha Gari wakati ajali na hatimaye umauti unamkuta Mheshimiwa Chacha Wangwe.
5. Ni mazingira gani yaliyopelekea na au kusababisha ajali hiyo kutokea .
6. Tunataka Polisi wachukue hatua stahiki za kisheria ili Deus Mallya akaisaidie Polisi na kuhojiwa kwa kina juu ya suala hili kwani maelezo yake yana utata mkubwa sana.
7. Jeshi la polisi liitoe ripoti ya uchunguzi huo mapema na kuiweka ripoti hiyo hadharani.

Tunapendekeza hatua hizo zichukuliwe mara moja kwani tunaamini kuwa kifo hiki kimeghubikwa na utata mkubwa sana na haswa kutokana na maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyeshuhudia ajali (Deus Mallya) pamoja na watoto wa marehemu.

Tunaamini kuwa utatupatia ushirikiano wa kina ili kuhakikisha kuwa hatua za haraka na za dharura zinachukuliwa mara moja kwa ajili ya kuujua ukweli wa kifo hiki tata.

Pamoja na hayo, hivi karibuni wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakipata taarifa za vitisho pamoja na kuzushiwa vifo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi na ujumbe huo kusambazwa sana kama ilivyoripotiwa kwako na Mheshimiwa Zitto Kabwe (MB).

Tunaomba wabunge wetu wapatiwe Ulinzi na pia taarifa hizo zifanyiwe kazi kwa kina.

Nakutakia kazi njema.

Wako katika ujenzi wa Demokrasia na Utawala Bora.

……………………
John Mnyika - 0754694553,
Kaimu Katibu Mkuu,
Na Mkurugenzi wa Vijana Taifa ,

Nakala:
1. Mhe.Lawrence Masha – Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
2. Mhe.Dr. Willbrod Slaa (MB) - Katibu Mkuu CHADEMA .
3. Robert Manumba -Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai.
 
Last edited by a moderator:
MKJJ Hapo ndipo penye utata wenyewe...Kwangu binafsi nafikiri huyo kijana ni shahidi mzuri sana tu.
Kwanza kabla ya kuanza kuzungumzia haya...Ni bora tuanze na wale ambao wanaweza kunufaika na kifo chake.
Kama huyo kijana alidai kuwa kazi zinalala...Ni kazi gani zilizokuwa zinalala?
Si walikuwa wakienda msibani?
Je ni nani mwingine aliyekuwa akijuwa kuhusu kazi yake ya huko msibani?
Alikuwa akienda kumwakilisha nani kwenye msiba wa Bhoke?
Chama,ama familia ama ni yeye binafsi?
Pia inabidi tuzungumzie issue ya yeye kupambana na Barrick huko kijijini kwake...Hivi mnaijuwa Barrick nyie watu?
Huyu mtu ni kweli alikuwa mpambanaji...Tatizo ni tamaa ya madaraka...Na kutokuwa mwangalifu kwenye siasa zetu...Sasa anaweza akawa ameuwawa na mafisadi kwa namna ambayo italeta vurugu kwenye jamii...!
Marehemu Wangwe ni kweli alikuwa akiyapigania maslahi ya wananchi wake wa jimboni...Na alihamia chadema kwani wananchi walishachoshwa na ccm.
Sasa na yeye huo ukaribu wake na ccm bila kuwa mwangalifu halafu akiwa anawapinga tena kuhusiana na Barrick?
Si alikuwa kinyume kabisa na mkuu wa Polisi wa mkoa na kuu wa mkoa mwenyewe?
Yeye kama mbunge alikuwa tishio...Lakini at the same time...Tamaa ya madaraka ilimponza na hakuchukuwa maamuzi ya busara licha ya nia nzuri aliyokuwa nayo!
ccm wasilete UNAFIKI kabisa kwani huyu mtu alikuwa akipinga sana unyanyasaji wa serikali huko kwenye migodi kwa kuwatumia polisi na hata hoja yake aliyokuwa akitaka kuiwakilisha ilizimwa kwa kila namna na wakati akikaribia kuiwakilisha ndio akafa.
Na ili kumuenzi wabunge wanadai kuwa hoja yake hiyo ya mapigano hayo ya koo ifanyiwe kazi na isomwe bungeni.
Hoja hiyo ikisomwa pia tutapa clues nyingi sana.
Na ndio maana nikasema makabila mengine jamani tujifunze kuishi kama watanzania...Sasa unaweza kukuta labda hizo koo huko mara zinagombea ardhi yenye madini..Sasa dunia ya sasa ukoo wa kiafrika unamiliki madini ya Wananchi...wapi na wapi.
Hizo ardhi wanazogombea huko hao wanaojiona ni machifu si ni za Tanzania?
Tunataka mtuletee issues hapa na si kuletea assumptions ambazo hazina kichwa wala miguu!
Kwanza hizo tairi unaweza kuta zilipigwa risasi.Na kwa uzoefu wangu mimi...Marehemu Wangwe nayeye inanishangaza sana alipoamuwa kuendelea na safari licha ya dalili zote hizo!
Ni wazi alijuwa ana mess na something BIG!
Lakini inaonyesha alijitowa MUHANGA!
Kitendo cha nuts kulegea kwenye gari yake kilitosha kumfana ajiulize maswali mengi kwani si kitu cha kawaida kuwa na nati zisizofiti na ama kutight kama kweli gari hilo ni lake na analitumia kila siku!
Na huyo kijana na historia ya jinsi walivyojuwanan iwekwe hapa!
Huyo kijana kule Kilimanjaro huwa wanaitwa NYOKA.
Hawa Nyoka kazi yao ni kuhakikisha mambo yote ni sawa ikiwa na uzima wa gari na kila kitu!
Sasa ika vipi NYOKA akalala nyuma na Bosi kuendesha?
Tena MH MBUNGE?
Pana UTATA HAPO!
Wangwe alikuwa akienda kukutana na nani?
Nani mwingine aliyekuwa akijuwa ratiba yao?
Kabla ya ajali na safari na mara baada ya ajali...Hizo namba zote za simu zilizopigwa na nyoka kwa kutumia simu yake na ya Wangwe zichunguzwe.
Nyendo zao wote zichunguzwe
Kwa sasa tuanzie hapo.
INASIKITISHA SANA!
MACHOZI YA MAMBA YA ccm YATAWACOST kama haki isipotendeka kwani wao ndio wanao miliki dola na wananchi wanataka majibu.

Wenye kunufaika na kifo chake ni wale wote walitaka afe kwa njia yoyote, including wale waliotaka kumpiga risasi wakati akiwa hai.
 
b. Kama maelezo kuwa kichwa cha Wangwe kiliharibiwa sana hadi kushindwa kutambulika kuwa ni Wangwe; na kama Malya alikuwa amepoteza fahamu kwa muda hadi "vibaka" wakaja kukusanya masanduku, laptop n.k na kutokomea navyo;

i. Nani alimtambua Wangwe (kama kichwa chake kiliharibika vibaya?)
ii. Nani aliyepiga simu mwanzoni kutoa taarifa ya ajali? haiwezekani kuwa ni Malya..
iii. Mtu huyu aliyepiga simu alisema "nani kapata na ajali" kama alisema ni Wangwe angalia (i) ina maana aliweza kumjua mara moja licha ya kichwa kuharibika.
iv. Sijui voucha zinatumikaje kwenye simu; unaiingiza pale unapoinunua au unaweza kuingiza wakati unataka kutumia simu? Nani aliyekuwa anaendesha gari wakati wa kununua voucher na wakati wa ajali pamoja na commotion yote hiyo Malya aliweza vipi kupata simu yake, na voucher (assuming haikuwa tayari imeingizwa kwenye simu) ukizingatia na yeye alikuwa ni mhanga wa ajali.
Swali hili ni la Omar Mganga, nani aliyempigia simu kuwa kumetokea ajali na nani alimtambulisha kuwa aliyefariki ni Chacha Wangwe?

v. Hiyo Cliniki ya karibu hapo huwa inakuwa na gari la wagonjwa masaa 24? Na polisi wanakuwa eneo la Pandambili usiku huo kwa kawaida au walikuwa assigned kuzunguka eneo hilo wakati huo? Nina maana it is too coincidental kuwa na ambulance karibu, polisi karibu, simu karibu n.k

vi. Simu ya Wangwe imekuwa recovered? I would like to know the last call that went to that phone not the one that went from it.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom