Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mimi kifo hiki nakichukulia kama Suicide bila kukusudia kwa upande moja kwa upande mungine najiuliza maswali.. Mtoto wake alieleza vizuri kilichotokea. Baba yake alikua anaumwa, amemeza dose ya malaria, gari bolt or whatever za tyres mbovu, safari usiku kweli tusilaumu mtu hapa. Mtoto alijaribu kumzuia baba yake asisafiri aka insist pamoja nahuyo ambaye hakuumia sana akasema shuguli zinalala!!!!!Ila chakusangaza huyo jamaa mungine anasema alikaa kiti cha nyuma (why) damu zilikokutwa. Mh aligongwa kichwa before overturning??? Ni mawazo tu!!!

CHACHA WANGWE...RIP!!

sasa wewe hapo juu unataka kusema Dennis Mallya ndio hitman mwenyewe? Mallya ni jina la Kichagga..so watakusema kwamba huyu bwana katumwa nani??

Chadema ala ala, hii kitu ipo delicate kama 'ashkrim' kwenye jua la darisalamu..mpira mnao ninyi, sie tupo kwenye sidelines tunapiga 'konoli' kwa ukaribu, hii ni PR ya ninyi ku-lose tafuteni msemaji kabisa juu ya suala hili..lakini haya mambo ya Gobole a.k.a Slaa karopoka nini mara Nyepesi bin Zitto nae atakuja hapa na domo nyenga lake, mara ooooh tafrani tupu na ka-chama kenu katapolea kwenye Bermuda Triangle ibaki historia tu ya kwamba kulikuwa na chama cha nanilii....too late.

Chacha alikuwa kipenzi changu kwa wanasiasa wa bongo...nchi imeoza sana, yaani nimesikitika kuona kwamba hata wabunge tena kwenye mji mkuu bado wanaoga kwa maji ya ndoo! na hii ni karne ya 21, li-Tanzania bado lina jikongoja ktk karne ya 18. Bila hata haya yule mama anasema mambo ya maji ya kuoga kwenye luninga..oooooooops, labda najisahau! OK, ndio hali halisi..wakina Marehemu Chacha wakiwapa ukweli mnanuna, haya tutafika.

Aibu kuendesha SUV kuuubwa wakati unaoga kwa kata!! huu ni upuuuzi...
 
Kwa mujibu wa maelezo ya yule jamaa aliyesalimika, wa kwanza kufika walikuwa ni vibaka ambao waliwapora kila kitu walichoweza kupora. Baadaye wakaja wasamaria wema na yeye alipotolewa lwenye gari aliwasiliana na polisi ambao walifika MUDA MFUPI baadaye.

Masikini vibaka hawana roho hawa. Haya waliporwa baada ya wao kupiga simu au? Inanichanganya juu ya simu ya Mh. haikuibiwa au? .... hata sijui kama nauliza kitu kinachoeleweka... nadhani nimechoka kabisa mwili na roho .
 
Jmushi,
Mbona wewe unachuki na marehemu Chacha kiasi hicho?
Mimi nilidhani kuwa mlikuwa mnapingana kwa hoja lakini wewe unaonyesha dhahiri shahiri kuwa una chuki binafsi!
Kwasababu kila linalosemwa juu ya marehemu Chacha kuelezea uzuri wake wewe unakimbilia kushutumu na kupinga????
Ukweli ni kuwa hata kama alikuwa na mapungufu mengi kiasi gani lakini bado alikuwa na mazuri aliyoyatekeleza na kuyasema na watu wanakubaliana naye.
Habari alizotusimulia hapa FMES ziko wazi kabisa, wale waliopata muda wa kushuhudia shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, kwa njia za televisheni wameona wenyewe.
Na wale waliofika pale kwenye viwanja vya bunge pia ni mashahidi kuwa kifo cha kamanda Chacha kimewagusa watanzania wengi sana.Kujitokeza kwao kuuaga mwili wa marehemu ni sehemu tu ya heshima waliyokuwa wanampa.
Hizo chuki zako binafsi hazikusaidii chochote.Najua unachekea tumboni kwakuwa ulishatamani kumpiga risasi.Kwahiyo kifo chake umekifurahia saaana.
Ila ujue jambo moja kuwa CHACHA WANGWE alikuwa juu sana, wale wenye roho mbaya mnakereka kumuona akizidi kung'ara, kwakuwa mmezoea kuonekana nyie tu katika medani za siasa!
 
Ahsante:-

Dawa ya formalin sidhani kama inahusiana na uvujaji damu, kama ndio unachokiongelea hapa. Isitoshe kuna ishus za credibility juu ya taarifa zinazosema kulikuwa na tatizo la Maiti kuvuja damu Bungeni!

Mbona wewe unachuki na marehemu Chacha kiasi hicho?
Mimi nilidhani kuwa mlikuwa mnapingana kwa hoja lakini wewe unaonyesha dhahiri shahiri kuwa una chuki binafsi!
Kwasababu kila linalosemwa juu ya marehemu Chacha kuelezea uzuri wake wewe unakimbilia kushutumu na kupinga????
Ukweli ni kuwa hata kama alikuwa na mapungufu mengi kiasi gani lakini bado alikuwa na mazuri aliyoyatekeleza na kuyasema na watu wanakubaliana naye.
Habari alizotusimulia hapa FMES ziko wazi kabisa, wale waliopata muda wa kushuhudia shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, kwa njia za televisheni wameona wenyewe.
Na wale waliofika pale kwenye viwanja vya bunge pia ni mashahidi kuwa kifo cha kamanda Chacha kimewagusa watanzania wengi sana.Kujitokeza kwao kuuaga mwili wa marehemu ni sehemu tu ya heshima waliyokuwa wanampa.
Hizo chuki zako binafsi hazikusaidii chochote.Najua unachekea tumboni kwakuwa ulishatamani kumpiga risasi.Kwahiyo kifo chake umekifurahia saaana.
Ila ujue jambo moja kuwa CHACHA WANGWE alikuwa juu sana, wale wenye roho mbaya mnakereka kumuona akizidi kung'ara, kwakuwa mmezoea kuonekana nyie tu katika medani za siasa!
 
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Chacha Wangwe Mahala Pema Peponi
 
It is getting more complicated na mimi naanza ku-change opinion yangu kwamba huenda hiki kifo ni zaidi ya ajali. Achana na maneno ya uswahili ya yule mbunge eti kwamba marehemu alikuwa na dalili zisizo za kawaida na hivyo kuonekana kwamba alijua mauti inakuja, this is more than superstitious, it is even more than a crap. Lakini kuna mambo ya msingi ya kuhoji, mojawapo likiwa hili:

Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu-kutokana na kuumwa malaria-isingewezekana kwamba angekubali aendeshe gari. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba dereva alikuwa huyu kijana anayeitwa Mallya. Sasa swali kwa nini huyu kijana kama yeye ndiye alikuwa dereva anaficha ukweli huu? Je, ni woga wa kukwepa kuonekana ndiye aliyesababisha ajali na kifo hiki au there is something more-this is what the police need to tell us. Yaani hapa ndiyo tunahitaji msaada kweli wa polisi.

Lakini sasa hao polisi wanaweza kutupa ukweli kama waliweza kukataa kuona picha bungeni ambazo kila mtu aliziona? Pengine hapa ndipo kauli ya NN kwamba tunahitaji Scotland Yard inaweza ikageuka kuwa ukweli badala ya utani. Regrettably, it seems, as usual, we shall never know the whole truth!
 
Baada ya kusoma maneno ya mtoto wake nimejua ni nini haswa kilichomwua Marehemu Chacha Wangwe na nina uhakika mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kufikia conclusion niliyofikia mimi.

Ila kifo hiki kimenifundisha kitu kimoja watanzania bado mawazo yetu yako karne ya 17 , na ni lazima tubadilike kama tunataka maendeleo. Suala la maiti kutoa damu kwa wingi halina uhusiano wowote na njama au lah ....Mimi nimeshawahi kushuhudia mtu wa karibu ali-bleed vibaya sana baada ya kifo na sababu za kifo chake zilikuwa zikijulikana.
 
It is getting more complicated na mimi naanza ku-change opinion yangu kwamba huenda hiki kifo ni zaidi ya ajali. Achana na maneno ya uswahili ya yule mbunge eti kwamba marehemu alikuwa na dalili zisizo za kawaida na hivyo kuonekana kwamba alijua mauti inakuja, this is more than superstitious, it is even more than a crap. Lakini kuna mambo ya msingi ya kuhoji, mojawapo likiwa hili:

Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu-kutokana na kuumwa malaria-isingewezekana kwamba angekubali aendeshe gari. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba dereva alikuwa huyu kijana anayeitwa Mallya. Sasa swali kwa nini huyu kijana kama yeye ndiye alikuwa dereva anaficha ukweli huu? Je, ni woga wa kukwepa kuonekana ndiye aliyesababisha ajali na kifo hiki au there is something more-this is what the police need to tell us. Yaani hapa ndiyo tunahitaji msaada kweli wa polisi.

Lakini sasa hao polisi wanaweza kutupa ukweli kama waliweza kukataa kuona picha bungeni ambazo kila mtu aliziona? Pengine hapa ndipo kauli ya NN kwamba tunahitaji Scotland Yard inaweza ikageuka kuwa ukweli badala ya utani. Regrettably, it seems, as usual, we shall never know the whole truth!
Mkuu kitila,

Tuanze kujua ni wapi bwana Malya alinunua Vocha ya simu kama alivyosema?Je tunaweza kupajua..hapo ndipo tutaambiwa ni nani alikuwa akiendesha gari.Pia yule mtoti wake atuambie ni nani alikuwa akiendesha gari wakati safari ikianza

So far mpaka sasa mie bado naamini ni ajali ya kawaida
 
Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu-kutokana na kuumwa malaria-isingewezekana kwamba angekubali aendeshe gari. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba dereva alikuwa huyu kijana anayeitwa Mallya. Sasa swali kwa nini huyu kijana kama yeye ndiye alikuwa dereva anaficha ukweli huu? Je, ni woga wa kukwepa kuonekana ndiye aliyesababisha ajali na kifo hiki au there is something more-this is what the police need to tell us. Yaani hapa ndiyo tunahitaji msaada kweli wa polisi.

Kitila ,

Wewe ulichozungumza hapo ndio crap , kwani argument zako zimejaa assumptions nyingi ambazo umezitumia kufanya conclusion ....

1. Huna uhakika kwamba huyu kijana ndiyo alikuwa dereva

2. Pili unasema huyu kijana ameficha ukweli

Kwa hiyo unafikiri ya kuwa huyu kijana aliamua kuligonga ili gari ili amwue Wangwe then yeye apone ....na wewe unafikiri kabisa kama mtu alitaka kumwua Wangwe then njia ya kumwua ni thru ajali ambayo inaacha foot-prints kila sehemu ...
 
Kitila ,

Kwa hiyo unafikiri ya kuwa huyu kijana aliamu kuligonga ili gari ili amwue Wangwe then yeye apone ....na wewe unafikiri kabisa kama mtu alitaka kumwua Wangwe then njia ya kumwua ni thru ajali ambayo inaacha foot-prints kila sehemu ...
Naamini hauwezi kujua Kitila anchofikiri..hayo ni mawazo yako,Kitila anajenga hoja kwa njia ya kichokonozi kujua nini chanzo cha ajali
 
Naamini hauwezi kujua Kitila anchofikiri..hayo ni mawazo yako,Kitila anajenga hoja kwa njia ya kichokonozi kujua nini chanzo cha ajali

Soma vizuri kile aliachoandika Kitila kabla ya kurukia hoja , amesema " kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kwamba huyu kijana Malya ndiye aliyekuwa akiendesha gari " sasa hiyo inamaanisha nini ? Halafu mbona hamtaki kusikiliza kila mtoto wake alichosema ? au kwa sababu akitawawezesha kufikia conclusion ambazo mmeshazifikia ?

Mtoto kasema Gari lilikuwa bovu , likapelekwa kwa Fundi ....je tumefuatilia kujua gari lilipelekwa kwa fundi gani ? je walifanya kazi kama ilivyo takiwa au walilipua tuu ?
 
Maelezo yanayotolewa kuhusu mazingira ya kifo cha Wangwe yanaonesha kukinzana. Uchunguzi makini wa polisi unaweza kuondoa utata huu. Polisi wana nyenzo zinazohitajika? Au nao wataishia kuwa wapiga ramli tu.
 
Ni kitu gani haswa kinachokinzana ?
 
Kitila ,

Wewe ulichozungumza hapo ndio crap , kwani argument zako zimejaa assumptions nyingi ambazo umezitumia kufanya conclusion ....

1. Huna uhakika kwamba huyu kijana ndiyo alikuwa dereva

2. Pili unasema huyu kijana ameficha ukweli

Kwa hiyo unafikiri ya kuwa huyu kijana aliamua kuligonga ili gari ili amwue Wangwe then yeye apone ....na wewe unafikiri kabisa kama mtu alitaka kumwua Wangwe then njia ya kumwua ni thru ajali ambayo inaacha foot-prints kila sehemu ...

Maybe your are right, mine too could be a big crap. Lakini sasa nafikiri umenifanyia hitimisho ambalo mimi sikulifanya, na hili ni tatizo kubwa sana hapa JF. Kuna watu wanajifanya wana uwezo wa kujua mtu mwingine anafikiria nini, huo ni ugonjwa mbaya sana hapa JF!

Mimi nimetoa maoni yangu kwa mujibu wa maelezo ya watoto wa marehemu. Kama umesoma vizuri, mtoto wa marehemu Zakayo kaongea mambo mawili ya msingi, ninakukumbusha:

i) marehemu alikuwa anaumwa malaria na alikunywa dawa za malaria. Kama unaijua malaria vizuri na unajua athari za dawa za malaria, huwezi kufikiri kwamba mtu angeweza kuendesha gari tena usiku na sidhani kwamba kama ni rafiki yako ungeweza kumshauri aendeshe gari katika hali hiyo. So, kwa kuzingatia kwamba Mallya alikuwa ni rafiki yake kama tulivyokwishaelezwa, na kama Mallya ana akili timamu na kwamba alijua kwamba rafiki yake alikuwa anaumwa malaria na alikunywa dawa za malaria, kamwe asingemruhusu, achilia mbali kumshauri, aendeshe gari, tena kwa safari ndefu kama hiyo;

ii) mtoto wa marehemu Zakayo amesema mara kadhaa kwamba wakati wanaondoka mara zote mbili aliyekuwa anendesha gari alikuwa rafiki yake marehemu, huyo ndugu Mallya.

Ni kwa kuzingatia hizo scenario mbili hapo juu, nimesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba aliyekuwa anaendesha gari alikuwa Mallya. Baada ya kutoa maelezo haya, nikauliza swali: Je, kama kweli Mallya ndiye alikuwa anaendesha gari, kwa nini anaficha? Katika ku-speculate, nikasema, pengine anaogopa kuonekana kwamba yeye ndiye chanzo cha ajali na hivyo kifo hiki. Nikamalizia kwa kusema hapa ndiyo tunahitaji sana msaada wa polisi ili kujua ukweli.

Sasa ni kitu gani katika maelezo yangu hapo kinachokufanya kuamini kwamba mimi nafikiri Mallya ndiye aliyemuua marehemu? Na kwani unafikiri una uwezo wa kujua kile ambacho mimi nafikiri?
 
Soma vizuri kile aliachoandika Kitila kabla ya kurukia hoja , amesema " kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kwamba huyu kijana Malya ndiye aliyekuwa akiendesha gari "

Kwa hiyo kwa uwezo wako wa kufikiri hii ni sawa na kusema kwamba "Kwa hiyo unafikiri ya kuwa huyu kijana aliamua kuligonga ili gari ili amwue Wangwe then yeye apone"?
 
Kifo cha Wangwe utata (Majira)

7538.jpg
Waandishi Wetu, Dodoma na Dar es Salaam

...Bibi Masunga alisema kwa taarifa ambazo alizipata kwa watoto wake marehemu kabla ya tukio, alikuwa akijisikia vibaya kiasi cha kushindwa hata kuweka maji bafuni kuoga.

Aliongeza kuwa watoto wake walimpa msaada kwa kumwekea maji bafuni baada ya kushindwa kufanya hivyo na marehemu aliingia kuoga na alipomaliza kujiandaa, alitoka nje na kuingia ndani ya gari kisha kwenda bungeni.

Katika simulizi zake, mtoto huyo alisema kabla ya kifo chake, baba yake alikuwa anasumbuliwa na malaria.

"Lakini kuanzia Ijumaa jioni baba alikuwa anajisikia vibaya, akanywa dawa, pia Jumamosi. Jumapili usiku alitueleza kuwa alikuwa hajisikii vizuri, akaniambia nimtafutie dawa (Panadol), nikatafuta lakini sikupata," alisema kijana huyo huku akionesha masikitiko makubwa.

Alisema aliwasiliana na mama yake kwa njia ya simu kumweleza kuhusu hali ya marehemu na kutoonekana kwa dawa zilizokuwa zimehifadhiwa kabatini.

Bw. Chacha alisema baadaye, mama yake alimshauri aende kununua dawa hizo katika duka la jirani na kwamba alipokwenda, duka lilikuwa limefungwa kwa kuwa ilikuwa usiku wa manane.

Alisema hata hivyo, muuzaji wa duka hilo alikubali kuwapa dawa alizokuwa amezihifadhi kwa matumizi binafsi.

Alisema baada ya kunywa dawa hizo, alilala usingizi mzito," alisema.

Mtoto huyo alisema ilipofika saa 11 alfajiri mtu aliyetamtaja kuwa ni Bw. Deus Malya, ambaye ni rafiki wa marehemu, alikwenda katika makazi hayo na kumtaka marehemu waondoke.

"Nilimgongea sana mlango wa chumba chake, hakujibu baadaye nikampigia simu akajibu na baadaye wakaondoka na kurudi," alisema.

Alisema juzi marehemu aliamka akiwa amebanwa na mafua makali na kwamba kwa kumwona akiwa katika hali hiyo, alisihi baba yake apumzike badala ya kwenda bungeni.

kwa mujibu wa kijana huyo, marehemu Wangwe pia alimwambia kuwa alipitia hospitalini ambako alipimwa na kukutwa na wadudu watatu wa malaria na kwamba alipewa dawa za mseto ili azitumie.

"Baadaye tulimlazimisha ale chakula halafu apumzike, akasema hajisikii kula, lakini alikuwa ameleta matunda akataka tumtengenezee matunda ambayo alisema angeweza kula," alisema.

Bw. Chacha alisema baada ya muda, alimpa baba yake dawa za mseto na kumtaka apumzike na kwamba alipokwenda kumjulia hali alikumtaka anakoroma.

"Saa 11 jioni alikuja Deus na kumtaka baba waondoke, lakini kabla hawajaondoka kuelekea Dar es Salaam, nilimweleza Deus kuhusu hali ya gari.

"Gari lilikuwa na matatizo nati za matairi ya mbele zilikuwa zimelegea tukajitahidi kuzifunga upya. Baada ya hapo nililijaribu lakini ghafla nati zilichomoka, jambo ambalo kwa kweli nilisema lilikuwa la hatari kama wangesafiri nalo," alinena.

Alisema baadaye alimpa taarifa baba yake ambaye alimshukuru na kumtaka yeye na Deus wakashughulikie gari hilo, ili liwe imara kwa kusafiria.

"Gari lilitengenezwa na wakaondoka likiwa linaendeshwa na Deus. Lakini baada ya muda, baba alinipigia siku kuwa gari limewaharibikia Ihumwa na kwamba wanarejea mjini kwenda kulitengeneza. Nikawa nawatafuta sikuwapata.

(basic forensic)

...mjumuisho wa Malaria kali, Uchovu, mafua makali, kutokula vizuri, Nati za tairi zilizokuwa hazifungi, ...kwa namna moja ama nyingine zimejumuisha poor Judgmnents na kusababisha ajali.

...Swali la kujiuliza, Marehemu alikuwa amefunga mkanda? marehemu alikuwa Under influence of Prescribed Drugs? Marehemu alikuwa fit ku Drive? Iwapo Mallya ndiye aliyekuwa ana drive, sioni ajabu yeye ku survive the Crash, kwani mara nyingi dereva anakuwa alert zaidi kwa kujua gari linavyo behave hata sekunde chache kabla ya ajali.

usijekuta hata hiyo gari ilikuwa haina Airbags zote mbili, upande wa Driver na passenger.

Magazeti na udaku kama kawaida yataleta speculations nyingi juu ya hili, lakini ukweli unabakia mfululizo wa maelezo hayo hapo juu unajionyesha dhahiri Marehemu , kama wengi wanaopatwa na ajali, alifanya poor judgements kusafiria gari hilo lenye ubovu wa tairi, ilhali na yeye mwenyewe hakuwa fit kusafiri wala kuendesha kutokana na hali yake ya kiafya na dawa alizokuwa anatumia.

Mwenyezi Mungu amrehemu.
 
Mkuu kitila,

Tuanze kujua ni wapi bwana Malya alinunua Vocha ya simu kama alivyosema?Je tunaweza kupajua..hapo ndipo tutaambiwa ni nani alikuwa akiendesha gari.Pia yule mtoti wake atuambie ni nani alikuwa akiendesha gari wakati safari ikianza

So far mpaka sasa mie bado naamini ni ajali ya kawaida

Gembe,

According tu maelezo ya mtoto wake, safari ilianza kwa Deus kuendesha gari na hata walipoirudia charger ya simu aliyekuwa anaendesha ni deus. Jana mchana ITV walikuwa wanamhoji mtoto wake na alielezea kama hadithi wala hutachoka kumsikiliza. Isipokuwa baada ya kununua vocha ndio haijulikani exactly but deus anasema hapo yeye ndio alihamia kiti cha nyuma, mtanzania wameelezea.
 
Kama ni kweli aliwasiliana na yule msimamizi wa bunge aliyeingia humo na Chenge...Halafu sijui na Mudhihir...Huku ukweli ukiwa ni fununu za yeye kuwa na mawasiliano na RA.

Ni jambo la kusikitisha sana...Alikuwa mwansiasa machachari...Lakini sijui ni kwanini kulikuwa na mvutano na watu kuwa kama vinyonga na huku wakisema wanayapigania maslahi ya wananchi.

Mimi siko bongo...Ila hapa mtizamo wangu ni huu...Kama kuna uwezekano ameuwawa..Basi inaweza ikawa ni either ccm ama chadema.

Kwasasa siwezi kukisia ni nani kati ya hivyo vyama viwili vinahusika endapo hoja ya mkono wa mtu ni ya kweli.

Kwanza tuwekewe wazi kuhusu umaarufu wake...Kwasababu kama umaarufu wake ulishuka...Na kama ni kweli alitumwa na mafisadi...Basi mafisadi wangeweza kumwua pia kwani in order kwa yeye kurudisha umaarufu wake kwa wananchi...Basi ni wazi asingekuwa na budi kuwageuka mafisadi hao.

Kwa kweli ni bora ukweli wote uwekwe hapa kwani licha ya sisi kumpinga Wangwe kwa nguvu zote..Hilo lilikuwa ni kwa yeye kuonekana kuwa badala ya suluhu yeye alitaka kuwafanya wachagga wote waonekane ni wabaya...Na hata pia kuhusu yeye kuendelea kukutana na RA kwa siri...Na pia ni yeye aliyekuwa chadema...Akaenda nccr...Akarudi chadema...Na kabla ya hapo alikuwa TANU.

Siasa za chuki hatuzitaki kabisa!

Labda huo haukuwa msimamo wake lakini juhudi za Mgaga hazikuwa na wema...Juhudi zilizopolekea MKJJ kuanzisha thread iliyoleta uhasama mkubwa sana!

Pia kwa kumalizia..Kazi yake ya u supervisor wa kampuni ya dhahabu ya Afrika Mashariki na mara baada ya hapo kuingia kwenye siasa ni dalili nyingine kuwa inawezekana makampuni nayo yana watu wengi wa aina nyingi kwenye siasa.

Ni maoni yangu hayo kwa sasa.

Kwahiyo Mushi unakubaliana kuwa Wangwe alistahili kwa aina yeyote apigwe risasi wakati muafaka ukifika?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom