Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
...nadhani hawamtendei haki hata huyo Deus Mallya kumhoji wakati huu. Kama kuna anayebisha basi hajawahi kuiona ajali wala ajali haijawahi kumkumba. Kijana lazima atakuwa kwenye mfadhaiko wa hali ya juu, kwanza kwa kupona kwenye ajali ambayo mwenzake amefariki dunia, pili, lawama, na hukumu ya MAISHA juu yake iwapo itabainika yeye ndiye aliyesababisha ajali ama la!

Sio ajabu unapokumbwa na ajali kupoteza kabisa kumbukumbu wapi ulipokuwa wakati ajali inatokea, na vile vile sio ajabu kabisa baada ya ajali mbaya sana ukatoka bila mchubuko sehemu yeyote ilhali wenzako ni maiti.

mfano; Princess Diana, Dodi na Henry paul walipokufa, mercedes yao ilikuwa nyang'anyang'a, lakini Rhees Jones (Bodyguard) alipona ila kumbukumbu ya tukio ilikuwa 'scrambled' kiasi kwamba ni sawa na ilikuwa deleted kabisa kichwani mwake.

katika kuwatendea haki wanandugu na wanafamilia, badala ya speculations, ni bora tukaukubali tu ukweli, ajali mara nyingi inatokana na poor judgents.
 
Sasa ni kitu gani katika maelezo yangu hapo kinachokufanya kuamini kwamba mimi nafikiri Mallya ndiye aliyemuua marehemu? Na kwani unafikiri una uwezo wa kujua kile ambacho mimi nafikiri?

Mimi sijasema nina uwezo wa kujua nini wewe unafikiri na sidani kama kuna mwanadamu mwenye huo uwezo . Lakini kikubwa nilichofanya ni kujaribu kusoma kati kati ya mstari katika hoja zako haswa pale uliposema haya maneno

"It is getting more complicated na mimi naanza ku-change opinion yangu kwamba huenda hiki kifo ni zaidi ya ajali. "

Sidhani kama tunahitaji rocket scientist ili kuweza kujua ni nini haswa ulichokuwa ukizungumzia . Lakini pia ulisema maneno yafuatayo

"Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu-kutokana na kuumwa malaria-isingewezekana kwamba angekubali aendeshe gari."

Hiyo statement siielewi, ni watu wangapi wanaoumwa na kuendesha gari …jee vipi kama Marehemu alitaka kuendesha gari ? jee vipi kama Mallya naye alikuwa anaumwa ? jee vipi kama Mallya alikuwa amelewa kwa hiyo Chacha akaona ni bora yeye aendeshe? Kitila kaa ukijua ya kuwa simply kwa kuwa wewe ukiwa unaumwa malaria hautaendesha gari aimaanishi ya kuwa wengine nao watafanya hivyo ....

"Sasa swali kwa nini huyu kijana kama yeye ndiye alikuwa dereva anaficha ukweli huu? Je, ni woga wa kukwepa kuonekana ndiye aliyesababisha ajali na kifo hiki au there is something more -this is what the police need to tell us"

Sijui ulikuwa una maana gain hapo? Manake nikisema kitu chochote unadai najaribu kuifanya najua nini unachofikiri.
 
Mimi sijasema nina uwezo wa kujua nini wewe unafikiri na sidani kama kuna mwanadamu mwenye huo uwezo . Lakini kikubwa nilichofanya ni kujaribu kusoma kati kati ya mstari katika hoja zako haswa pale uliposema haya maneno

“It is getting more complicated na mimi naanza ku-change opinion yangu kwamba huenda hiki kifo ni zaidi ya ajali. “

Sidhani kama tunahitaji rocket scientist ili kuweza kujua ni nini haswa ulichokuwa ukizungumzia . Lakini pia ulisema maneno yafuatayo

“Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu-kutokana na kuumwa malaria-isingewezekana kwamba angekubali aendeshe gari.”

Hiyo statement siielewi, ni watu wangapi wanaoumwa na kuendesha gari …jee vipi kama Marehemu alitaka kuendesha gari ? jee vipi kama Mallya naye alikuwa anaumwa ? jee vipi kama Mallya alikuwa amelewa kwa hiyo Chacha akaona ni bora yeye aendeshe? Kitila kaa ukijua ya kuwa simply kwa kuwa wewe ukiwa unaumwa malaria hautaendesha gari aimaanishi ya kuwa wengine nao watafanya hivyo ....

“Sasa swali kwa nini huyu kijana kama yeye ndiye alikuwa dereva anaficha ukweli huu? Je, ni woga wa kukwepa kuonekana ndiye aliyesababisha ajali na kifo hiki au there is something more -this is what the police need to tell us”

Sijui ulikuwa una maana gain hapo? Manake nikisema kitu chochote unadai najaribu kuifanya najua nini unachofikiri.

Mh Rufiji,
Nia yangu si kutafuta malumbano lakini ajali kama hii iliyomhusisha Mh. Wangwe inapaswa yapatikane majibu yakina yasokuwa na shaka hasa ukizingatia matukio kadhaa ya maisha yake tangu amekuwa mbunge hadi mauti yamemfika.

Lolote linawezekana,
Inawezekana ni ajali ya kawaida tu.
Lakini kumbuka kuwa kadri maendeleo yanavyopatikana hapa dunia basi na nyanja nyingine utaalam wake nao hukua kuendana na kasi ya maendeleo hayo.
Mauaji ya kupanga yapo sana, tena hufanywa kwa utaalam wa hali ya juu sana (si maanishi kuwa ajali hiyo imepangwa) Kwahiyo dodoso ndiyo zinazojenga misingi ya kufanya uchunguzi.
Kama nilivyoeleza hapo juu lolote linawezekana, kwa mwanasiasa machachari kama Wangwe kuwa target si jambo la kubeza
 
Mimi sikatai Mwanasiasa kama Wangwe anaweza kuwa target kama ulivyosema, lakini ninachopinga mimi ni kwamba sijaona hoja ya msingi ya kunipelekea mimi kwenye consipiracy theory . Kwa sababu wengine wanazungumzia suala la charger , lakini sidhani kama inatosha kutupa picha ni nani haswa alikuwa akiendesha gari wakati huo !

Mimi ninachoogopa hapa ni kwamba hili suala likiachiwa liendelee hivi hivi tutam-villify mtu ambaye ahusiki kabisa . Watu wengi hapa wameshafika conclusion kuhusu kilichotokea sasa wanajaribu kutafuta supporting evidence itakayomatch na conclusion zao.
 
Nimefarijika mno kuona jinsi WATANZANIA na RAIS wetu walivyompa HESHIMA kubwa marehemu Chacha Wangwe ingawa nadhani alistahili heshima zaidi ya hii wakati alipokuwa hai.
 
Ninakulilia Chacha,
Jemedari umetuacha,
eti ajali ya pancha,
asubuhi haija'cha
Mtetezi katutoka.

Safuyo ilikuwacha,
Mapenzi ikayakacha,
eti wewe ni pakacha,
Utawatia makucha,
Mtetezi katutoka.

Pasi bila ya kuficha,
Msimamo hukuacha,
Ukawatolea na picha,
Zinavyotakiwa kwacha,
Mtetezi katutoka.

Wapo ambao hawakupenda uwe mmojawapo miongoni mwao,
Lakini Mwenyezi Mungu ameonesha mapenzi makubwa aliyonayo juu yako,
RIP Chacha Zakayo Wangwe
 
Mimi sikatai Mwanasiasa kama Wangwe anaweza kuwa target kama ulivyosema, lakini ninachopinga mimi ni kwamba sijaona hoja ya msingi ya kunipelekea mimi kwenye consipiracy theory . Kwa sababu wengine wanazungumzia suala la charger , lakini sidhani kama inatosha kutupa picha ni nani haswa alikuwa akiendesha gari wakati huo !

Mimi ninachoogopa hapa ni kwamba hili suala likiachiwa liendelee hivi hivi tutam-villify mtu ambaye ahusiki kabisa . Watu wengi hapa wameshafika conclusion kuhusu ni haswa kilichotokea sasa wanajaribu kutafuta supporting evidence itakayomatch na conclusion zao.

Mimi ninakubaliana na mawazo yako, lakini katika hali ya kawaida kabisa katika kipindi hiki cha tafakuri inabidi kila mwenye hisia zake aseme, you never know nani anaweza kutoa mwelekeo jadidi ambao utasaidia kupeleka uchunguzi kwenye njia sahihi.

Ninaamini neno ulilolitumia la kuogopa ulikuwa na maana ya tahadhari lakini tafakuri zisisitishwe hadi hapo uchunguzi kamili utapomalizika na taarifa kutolewa.
 
...nadhani hawamtendei haki hata huyo Deus Mallya kumhoji wakati huu. Kama kuna anayebisha basi hajawahi kuiona ajali wala ajali haijawahi kumkumba. Kijana lazima atakuwa kwenye mfadhaiko wa hali ya juu, kwanza kwa kupona kwenye ajali ambayo mwenzake amefariki dunia, pili, lawama, na hukumu ya MAISHA juu yake iwapo itabainika yeye ndiye aliyesababisha ajali ama la!

Sio ajabu unapokumbwa na ajali kupoteza kabisa kumbukumbu wapi ulipokuwa wakati ajali inatokea, na vile vile sio ajabu kabisa baada ya ajali mbaya sana ukatoka bila mchubuko sehemu yeyote ilhali wenzako ni maiti.

mfano; Princess Diana, Dodi na Henry paul walipokufa, mercedes yao ilikuwa nyang'anyang'a, lakini Rhees Jones (Bodyguard) alipona ila kumbukumbu ya tukio ilikuwa 'scrambled' kiasi kwamba ni sawa na ilikuwa deleted kabisa kichwani mwake.

katika kuwatendea haki wanandugu na wanafamilia, badala ya speculations, ni bora tukaukubali tu ukweli, ajali mara nyingi inatokana na poor judgents.

Mchomgoma,
Maelezo yako bado hujamalizia, unganisha hii...je Mzee Mohamed Al-Fayed anaongea nini hadi leo baada ya miaka takriban kumi kupita?
 
Baada ya taarifa rasmi za kifo cha Mh wangwe, ni wakati mzuri pia kuweka hisia zetu ili wahusika waweze kutoa maelezo badala ya hisia hizo kuendelea kujengeka miongoni mwa jamii, mara nyingi watu wenye nyadhifa wakifariki kwa namna yoyote ile basi hayakosekani maneno kadha wa kadha! mf Sokoine Kolimba,Balali, salome Mbatia na wengine kibao, sasa kwakuwa magazeti yalishaandika kuwa wangwe alikuwa na mkakati wa kugombea chadema Taifa(MAJALIWA YA MBOWE MKONONI MWA WANGWE) na muda si mrefu wangwe akasimamishwa U-makamu mwenyekiti wa chadema taifa na baadaye kidogo kifo kwa ajali ya gari, ni wakati mzuri kwa kina Zitto, Mnyika , Slaa na wengineo kuwa nao tuwaweke kwenye makundi ambayo yamekuwa yakishutumiwa kwa hisia hizo za Ki mafia ambazo zimekuwa hazithibitishwi. jibu lolote toka kwa hao litasaidia kupata ukweli juu ya yote ambayo yamekuwa yakisemwa kwa Serikali kuhusika kwa namna moja au nyingine na baadhi ya vifo anuai ya viongozi. naomba kutoa hoja!
 
Last edited:
Wanasema Balali ajafa kwa hiyo bora umuweke kwenye mabano (Anaweza akarudi na tukamfananisha na yesu ,kuna watu hivi sasa wanasaka kabuli lake ,eti wamekwenda kabulini hawamuona)
 
Weka mbali yote hayo ,hawa wakubwa kama umewahi kuona misafala yao huko mabondeni basi hushangai ukiambiwa wamepata ajali ,maana wanamaliza kisahani cha spidi ni hatari sana ,kama hujawahi kuona wanavyokatisha kwenye mbuga basi ulizia upate kuona watu wanavyoluka na magali. Si Mchezo wanakwenda kasi kweli kweli,tena wote hata Raisi nae msafara wake ukikatisha maporini utafikiri wanakimbia kimbunga.
 
Ni wangapi kati yenu mkiendesha magari Tanzania, abiria wako anakaa kiti cha nyuma katika safari ndefu au fupi? Mara nyingi viongozi ndio huketi nyuma wakiwa na dereva. Mliokuwa mnajua Wangwe na madereva wake akiendesha yeye (wangwe) madereva huketi kiti cha nyuma?
 
sijui watakupa majibu gani maana angekuwa kafariki kiongozi wa serikali tena ambaye angekuwa na mgogoro wa aina yoyote na serikali nadhani JF pasingetosha! hii usitegemee kupata lolote hapa pua zimekalia mdomo, na kwa hoja hii wengi umewashika pabaya nenda kalale kaka!
 
Baada ya taarifa rasmi za kifo cha Mh wangwe, ni wakati mzuri pia kuweka hisia zetu ili wahusika waweze kutoa maelezo badala ya hisia hizo kuendelea kujengeka miongoni mwa jamii, mara nyingi watu wenye nyadhifa wakifariki kwa namna yoyote ile basi hayakosekani maneno kadha wa kadha! mf Sokoine Kolimba,Balali, salome Mbatia na wengine kibao, sasa kwakuwa magazeti yalishaandika kuwa wangwe alikuwa na mkakati wa kugombea chadema Taifa(MAJALIWA YA MBOWE MKONONI MWA WANGWE) na muda si mrefu wangwe akasimamishwa U-makamu mwenyekiti wa chadema taifa na baadaye kidogo kifo kwa ajali ya gari, ni wakati mzuri kwa kina Zitto, Mnyika , Slaa na wengineo kuwa nao tuwaweke kwenye makundi ambayo yamekuwa yakishutumiwa kwa hisia hizo za Ki mafia ambazo zimekuwa hazithibitishwi. jibu lolote toka kwa hao litasaidia kupata ukweli juu ya yote ambayo yamekuwa yakisemwa kwa Serikali kuhusika kwa namna moja au nyingine na baadhi ya vifo anuai ya viongozi. naomba kutoa hoja!

Tafadhali sana usilete hapa hisia zako hizi zisizo na ushahidi wowote ule ilhali wakazi wa Tarime tuko kwenye majonzi mazito sana. Watu wengine hamuwezi hata kusubiri Wangwe azikwe bila kuleta unafiki wa kisiasa. Hivi kwenye mioyo yenu hakuna hisia hata kidogo? Au ndio kufa kufaana huku kama wanavyofanya gazeti la majira (habari corp)?

Kuweni na ubinadamu muda mwingine. Hii sio kitu kikubwa kuuliza.
 
... ni wakati mzuri kwa kina Zitto, Mnyika , Slaa na wengineo kuwa nao tuwaweke kwenye makundi ambayo yamekuwa yakishutumiwa kwa hisia hizo za Ki mafia ambazo zimekuwa hazithibitishwi.

this is non sense!!!mbona mi sioni uhusiano wowote hapo???au kwa sababu hao ndio huwa mstari wa mbele kwenye kutetea maslai ya nci??
 
Ni wangapi kati yenu mkiendesha magari Tanzania, abiria wako anakaa kiti cha nyuma katika safari ndefu au fupi? Mara nyingi viongozi ndio huketi nyuma wakiwa na dereva. Mliokuwa mnajua Wangwe na madereva wake akiendesha yeye (wangwe) madereva huketi kiti cha nyuma?

Mwanakijiji,

Kama sijakosea hii safari ilikuwa ya usiku , kwa hiyo ia make alot of Sense labda abiria aliamua kulala ili wabadilishane gari mbeleni ...Vile vile nilisoma ya kuwa walikuwa wakienda Tarime hii kwa hiyo ilikuwa safari ndefu kidogo.
 
Utata uko wapi? Subiri watu wamalize maombelezo uulete huo utata.
 
Mwanakijiji,

Kama sijakosea hii safari ilikuwa ya usiku , kwa hiyo ia make alot of Sense labda abiria aliamua kulala ili wabadilishane gari mbeleni ...Vile vile nilisoma ya kuwa walikuwa wakienda Tarime hii kwa hiyo ilikuwa safari ndefu kidogo.

Rufiji,

Walikuwa wanaenda DSM kwenye mazishi ya Bhoke Munanka.
 
mbona mie naona kama gari haikupata ajali! isipokuwa ilipatishwa ajali baada ya yeye kufa! fikra zangu zinasema kwamba kuna huwezekano aliuliwa kwanza kisha ndiyo wakamuweka kwenye gari na kumsukuma kwenye hiyo miti.
 
Hapo hakuna utata,hiki ni kifo cha kawaida kama vingine.Eneo alilopatia ajali ni eneo baya.Limechukua damu ya watu wengi pale.Binafsi mwaka 2006 tulipata ajali hapo na mtu mmoja akafariki papo hapo.Tulikua kwenye gari ndogo.
Wataalam wanadai kuna upepo mkali hapo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom