Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
RIP Chacha

life is too short whether kwa mapenzi ya Mungu au mapenzi wa mtu.
 
RIP fighter.Ni pigo kubwa kwa demokrasia yetu changa.Jina la Bwana lihimidiwe.

Mungu awajaalie faraja wanafamilia,marafiki na wanatarime woote.
 
RIP Chacha Z Wangwe. Tutakukumbuka kwa ujasiri wako
 
Kitila.. tangu jana mara tu baada ya ajali nimekuwa nikiuliza maswali fulani na nimewauliza watu wengi kweli; na kati ya majibu ambayo hayakupatikana ni suala la muda. Sisemi nini chaweza kuwa kimetokea, lakini suala la muda ni muhimu sana kwani ndilo litaweza kujibu mara moja na daima kuwa hii ni ajali tu. Wasipojibu suala la muda, wamejichimbia shimo kubwa tu la maelezo. Ninaposema "wamejichimbia" sijui ni kina nani. Nitaanza kuyauliza maswali hayo hapa, na mwenye majibu anisaidie kutuliza udadisi wangu.

a. Nani alikuwa wa kwanza kufika eneo la ajali?

Kwa mujibu wa maelezo ya yule jamaa aliyesalimika, wa kwanza kufika walikuwa ni vibaka ambao waliwapora kila kitu walichoweza kupora. Baadaye wakaja wasamaria wema na yeye alipotolewa lwenye gari aliwasiliana na polisi ambao walifika MUDA MFUPI baadaye.
 
Wanakijiji ndiyo walikuwa wa Kwanza Kufika Katika eneo la ajali.Hawa wanakijiji wa Pandambili.

b.Nani alikuwa akiendesha Gari?

Chacha ndiye alikuwa akiendesha na Malya anasema kuwa hakufunga mkanda.
Malya anasema yeye alikaa kiti cha nyuma kutokana na ushaur wa wangwe. Alimuambia ahamie kiti cha nyuma baada ya kumuona anasinzia
 
Kwa mujibu wa maelezo ya yule jamaa aliyesalimika, wa kwanza kufika walikuwa ni vibaka ambao waliwapora kila kitu walichoweza kupora. Baadaye wakaja wasamaria wema na yeye alipotolewa lwenye gari aliwasiliana na polisi ambao walifika MUDA MFUPI baadaye.

very good. hivyo aliweza kuwa na simu karibu baada ya ajali, usiku, katika eneo baada gari kurushwa "mita chache" na kusababisha kifo papo hapo... na aliweza kutolewa ndani ya hilo gari baada ya vibaka kufika kwanza ndani ya muda mfupi... kuna muda gani kati ajali na Polisi kufika?
 
very good. hivyo aliweza kuwa na simu karibu baada ya ajali, usiku, katika eneo baada gari kurushwa "mita chache" na kusababisha kifo papo hapo... na aliweza kutolewa ndani ya hilo gari baada ya vibaka kufika kwanza ndani ya muda mfupi... kuna muda gani kati ajali na Polisi kufika?

Dakika 55.inawezekena simu ilikuwa ndani ya gani hivyo kwa kutumia Tochi waliweza kuiona hiyo simu,ama Ujumbe wa Simu ulilia.
 
so kama saa moja baadaye... Polisi walifika baada ya Mkuu wa Polisi kupata taarifa au kabla ya mkuu wa Polisi kupata taarifa?
 
SIKU 6 ZA MWISHO NA MAREHEMU CHACHA ZAKAYO WANGWE
na Hebron Mwakagenda

Tumekuwa marafiki na Marehemu Chacha Zakayo Wangwe aliyekuwa Mbunge wa Tarime mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Disemba 14, 2005 baada kuapishwa bungeni na kurudi kwenye chama Makao Makuu ambapo mimi nilikuwa msaidizi wa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na yeye akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama ilikuwa mapema Januari 2006 tukakutana naye na kuanza kuwa karibu. Nimemshuhudia akijenga hoja zake kwenye Kamati Kuu na Baraza Kuu la chama kwa nyakati tofauti tofauti.

Nimekutana naye katika nyakati tofauti Dodoma na Dar es salaama kwenye shughuli za bunge na chama. Tumekuwa karibu zaidi mara baada ya yeye kushinda uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambapo nilimpigia simu kumpongeza na kumuunga mkono kama ilivyo desturi yetu wanasiasa. Matatizo yalipoanza kwenye chama kati yake na viongozi wenzake alinipigia simu kujua mimi nasemaje nilimwambia tukutane tuongee. Tulikutana naye Kunduchi Beach Hotel kwenye Semina ya wabunge kuhusu madini iliyofanyika mwezi Aprili 2008 tulipoonana asubuhi akaniambia mchana wake alikuwa anaenda kuonana na kamati maalum ya wazee wa chama iliyokuwa imeundwa ili kutatua kilichosemekana kuwa ni mgogoro kati yake na viongozi wenzake.

Jioni aliporudi tulikuwa na sherehe fupi hapo hotelini Kunduchi Beach ambapo mgeni rasmi alikuwa rafiki yake wa zamani Wakili Tundu Lissu, mimi nilikaa naye meza moja pamoja na mke wake ambaye ni binti ya Marehemu Meja Jenerali Warden akanisimulia kwa ufupi kilichojili kwenye kikao chake na Wazee wa chama, baada ya siku 2 kabla hajaenda Dodoma kwenye bunge alipita ofisini kwangu mjini akaniachia nakala ya makaratasi yote na miniti za vikao na maamuzi yaliyokuwa yamefikiwa na kikao cha kamati ya Wazee. Baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Dodoma nilimtafuta kwenye simu bila mafanikio baada ya siku kadhaa akanipigia na kunieleza kuwa kilichotokea alikitegemea kwahiyo lazima tukutane ili tushauriane.

Zilipita siku kadhaa akiendelea kujibizana na wenzake kwa njia ya vyombo vya habari nikampigia simu nikamwambia kwa ufupi sana uko wapi? akanijibu kuwa yuko Dar! nikamwambia “Mbona unaonyesha silaha zote kwa adui? kwenye Baraza Kuu utaongea nini kama yote unaongea na vyombo vya habari” akasema kabla hajarudi Dodoma lazima tuonane na kujipanga upya.

KIKAO CHETU CHA MWISHO na Marehemu Chacha Zakayo Wangwe

Ilikuwa Jumatano iliyopita tarehe 23/7/2008 muda wa saa 6 alinipigia simu na kuniuliza niko wapi nikamwambia niko Mikocheni akasema nakuja nikamwambia usije kwanza nakuja mjini nakutana na mtu fulani halafu nitakupigia akasema angependa tuonane nje ya mji kidogo ili tuwe na utulivu nikamwambia sawa nikimaliza ningemfuata kokote atakakokuwa. Nikaenda mjini saa 9.30 nilitoka katikati ya mji na kuelekea barabara ya Bagamoyo nilipofika Oysterbay Polisi nikampigia akaniambia nirudi yupo Namanga niliporudi Namanga nikamkuta amepaki gari yake ndogo mbele ya duka la dawa linaloitwa Hoots the Chemist Limited ndani ya gari akiwa na mtu mmoja mwanaume akanitambulisha mimi lakini hakuniambia yule ndugu anaitwa nani akatoka kwenye gari akaomba kifimbo chake kwa yule ndugu ambaye alikuwa bado yuko ndani ya gari akampa akaaanza kuzungumza nikamwomba tutafute sehemu yenye faragha kidogo tukaingia kwenye sehemu inayouza chakula na vinywaji hapo hapo Namanga inaitwa Anne Shop tukakaa chini na kuanza mazungumzo yetu yaliyoanza kwenye saa 10.00 jioni na yaliyotuchukua kama muda wa saa 1.30 bila kula wala kunywa chochote.
Kwanza nilitaka kujua kilichojili Dodoma kwenye kikao cha Kamati Kuu kutoka kwake mwenyewe kwasababu nilikuwa na taarifa kutoka kwa watu wengine, akanieleza baada ya kumuuliza nasikia ulifanya haya na haya akawa mkweli kunieleza kila kitu kilichotokea Dodoma, nikamuuliza sasa unataka nini baada ya hapo? Akaniambia yafuatayo:-


“Mpiganaji jina langu limechafuka sana nataka nisafishwe jina langu kwanza” hata jimboni siwezi kwenda katika hali hii lazima niende mahakamani.
Pili nataka Demokrasia ndani ya chama chetu iongezeke
Tatu nataka hii dhana ya ukabila iliyojengwa na maadui zetu ndani ya chama chetu ifutike
Nne nataka ruzuku ya chama iende wilayani hilo nitapigania hata nisipokuwa kiongozi wa kitaifa katika chama.
Tano nataka tuchukue madaraka ya nchi haraka iwezekanavyo naona tunachelewa sana.

Tulipomaliza tukakubaliana kujiandaa kwa uchaguzi ndani ya chama na kuwa makini tunaongea nini na vyombo vya habari, nikamsindikiza kwenye gari yake na alionyesha kuwa angesafiri aidha siku hiyo jioni au kesho yake kwenda bungeni Dodoma.

Katika kipindi kifupi nilichomjua Marehemu Chacha Zakayo Wangwe alikuwa na tabia mbili ambazo tutazikosa ndani ya chama chetu kwanza ni Ujasiri wa hali ya juu alikuwa hamuogopi mtu yeyote ila alikuwa anawaheshimu watu wote. Tabia ya pili ni kusema kila anachoona ni sawa hata ukimbembeleza vipi ukampa msimamo wa chama kabla ya kikao kama hakubaliani nao lazima ataongea anavyoona yeye inafaa akitofautiana na msimamo wa chama kwenye kikao husika. Tumempoteza mpiganaji na mpambanaji mahiri katika medani ya siasa za Tanzania.

Tunashukuru Bw. Mwakagenda kwa taarifa nzuri. Kitila tunashukuru kwa kuiposti.

Ushujaa wa Wangwe utajulikana tu hata kama ni kutoka kwa watu wasio na majina makubwa. Kwa wale wasiokuwa wamemuelewa marehemu Wangwe, ningewaomba wafungue macho na kusaidia kutimiza yale aliyokusudia marehemu kupigania. Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi.
 
I call for an independent investigation by the Scotland Yard...
 
Not easily accepted, but CZW is gone,
RIP.
 
Je,Dennis Malya baada ya ajali alikua ameumia kiasi cha kutojitambua ama alikua na fahamu za kutosha? Na wakati ajali inatokea,kwa kuwa alikua ktk siti ya nyuma alikua macho? maanake kuna member mmoja amechangia hapo juu na kudai Marehemu alimshauri Malya arudi kukaa nyuma baada ya kuonekana anasinzia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom