Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kama ni kweli aliwasiliana na yule msimamizi wa bunge aliyeingia humo na Chenge...Halafu sijui na Mudhihir...Huku ukweli ukiwa ni fununu za yeye kuwa na mawasiliano na RA.

Ni jambo la kusikitisha sana...Alikuwa mwansiasa machachari...Lakini sijui ni kwanini kulikuwa na mvutano na watu kuwa kama vinyonga na huku wakisema wanayapigania maslahi ya wananchi.

Mimi siko bongo...Ila hapa mtizamo wangu ni huu...Kama kuna uwezekano ameuwawa..Basi inaweza ikawa ni either ccm ama chadema.

Kwasasa siwezi kukisia ni nani kati ya hivyo vyama viwili vinahusika endapo hoja ya mkono wa mtu ni ya kweli.

Kwanza tuwekewe wazi kuhusu umaarufu wake...Kwasababu kama umaarufu wake ulishuka...Na kama ni kweli alitumwa na mafisadi...Basi mafisadi wangeweza kumwua pia kwani in order kwa yeye kurudisha umaarufu wake kwa wananchi...Basi ni wazi asingekuwa na budi kuwageuka mafisadi hao.

Kwa kweli ni bora ukweli wote uwekwe hapa kwani licha ya sisi kumpinga Wangwe kwa nguvu zote..Hilo lilikuwa ni kwa yeye kuonekana kuwa badala ya suluhu yeye alitaka kuwafanya wachagga wote waonekane ni wabaya...Na hata pia kuhusu yeye kuendelea kukutana na RA kwa siri...Na pia ni yeye aliyekuwa chadema...Akaenda nccr...Akarudi chadema...Na kabla ya hapo alikuwa TANU.

Siasa za chuki hatuzitaki kabisa!

Labda huo haukuwa msimamo wake lakini juhudi za Mgaga hazikuwa na wema...Juhudi zilizopolekea MKJJ kuanzisha thread iliyoleta uhasama mkubwa sana!

Pia kwa kumalizia..Kazi yake ya u supervisor wa kampuni ya dhahabu ya Afrika Mashariki na mara baada ya hapo kuingia kwenye siasa ni dalili nyingine kuwa inawezekana makampuni nayo yana watu wengi wa aina nyingi kwenye siasa.

Ni maoni yangu hayo kwa sasa.
 
jmushi... ukifikiria kwenye vyama you'll miss the big picture. Jiulize kama kuna mchezo mchafu, ni nani atanufaika zaidi kule Tarime? Kwa sababu kama wasingemtaka Chadema walikuwa na kila sababu ya kumvua uanachama na hivyo kulipoteza Bunge; Kama Chadema wangemuondoa nina u hakika CCM wangemkumbatia na kumsimamisha tena; lakini what if hakutakiwa awe Mbunge wa Tarime? aha!!!

So, ukiniuliza nitawatoa CCM na Chadema; I'll go further and deeper, even wider

Fate has a very weird way of pleasing the mighty!
 
Pole kwa familia, Wananchi wa Tarime na Chadema.
RIP Wangwe
 
Habari nilizozipata sasa hivi ni kwamba Mwili wa marehemu Wangwe, leo umewekwa bungeni kwa siku nzima, na hata ninapoandika bado upo bungeni, kwa sababu wananchi wamekuwa wengi sana waliojitokeza kumuaga,
Mwanzoni ilitegemewa kuwa watakuwa wabunge tu, lakini wananchi wamemiminika mno hata protokali imebidi zivunjwe, na wananchi wa kawaida waingie ndani ya bunge, kuuaga mwili wa marehemu, tunasema hewala kwa hilo kwa serikali yetu,

According to the dataz ni kwamba mwili wake mpaka sasa bado unavuja sana damu, haya yamesemwa na walio uona na kwamba inasikitisha sana, kwa sababu kama mpaka sasa bado mwili unavuja damu, ina maana this was a very violent death, Mungu amuweke mahali pema peponi, Maiti itaondoka kesho asubuhi kuelekea kwao Tarime, ambako according to the dataz mazishi ni lazima yafanyike kesho, kutokana na hali mbaya ya mwili wa marehemu,

However, tayari kale kamdudu kameanza minong'ono, kwa kweli tuta-spare mpaka baada ya mazishi, betweeen jana na leo tumekusanya a lot of dataz very soon tutazichambua kwa kina, tena hapa hapa JF, na bado pia tunaendelea kuzikusanya na kuzi-verify, ninasema nothing but just our commitment kuhabarishana ndani ya hii forum, ili kuweka record straight kama kawa!

Again Mungu Amuweke Mahali Pema Peponi Marehemu Wangwe, kwa kweli baada ya kuskia kutoka kwa waliouna mwili, machozi yamenitoka na huwa kwangu sio rahisi kutokwa na machozi, pamoja na kwamba nilikuwa simjui marehemu.

Ahsante Wakuu

Chumvi mingi sana..Naomba tusiingize siasa hapa.

Kwenye black highlights...Pia unasema mwili bado unavuja damu...Halafu eti umeharibika vibaya sana kwahiyo unatakiwa uzikwe mara moja!

Huo mwili unawekwa huko bungeni badala ya vyumba vya kuhifadhi maiti?

Hakuna madokta na wataalam wa kuzuia hiyo hali na wanapeleka damu za "maiti" BUNGENI?

Yani kweli FMES Maiti inavuja damu kwa muda wote huo hadi inapelekwa bungeni ikivuja damu unasema ni ubinadamu huo?

Na kusema kifo kilikuwa violent...Na huku ukiwa na conspiracy theory..Then unaanisha ameuwawa kinyama kwa kutumia vitu vingine na wala si ajali.

Ungesema ni fatal accident ambayo hata hivyo ni intentional ungeeleweka.

Kwa kumalizia..Kwenye red higlight..Kunanishangaza...Kwani mara nyingi kuharibika kwa kusababisha maiti izikwe haraka ni kwasababu labda ya harufu..na wala si damu!

Kwani mwili gani huo unaoendelea kutowa damu hadi sasa kama si MWELEKEO WA KIPROPAGANDA?
 
...dah, katika mambo nilojifunza humu tangu nijiunge humu, mmojawapo ni kwamba ukiwa public figure halafu ukafa kifo cha ghafla baada ya kutajwa tajwa sana katika siku za karibuni kifo hicho lazima kitahusishwa na mkono wa mtu, ...haswa kidole kitaelekezwa kwa uliyekuwa unapingana naye.

Nadhani inabidi niwe mwangalifu ninayemtupia jiwe humu kundini, asijekufa ghafla nikaja onekana mchawi!
 
Chumvi mingi sana..Naomba tusiingize siasa hapa.

Kwenye black highlights...Pia unasema mwili bado unavuja damu...Halafu eti umeharibika vibaya sana kwahiyo unatakiwa uzikwe mara moja!

Huo mwili unawekwa huko bungeni badala ya vyumba vya kuhifadhi maiti?

Hakuna madokta na wataalam wa kuzuia hiyo hali na wanapeleka damu za "maiti" BUNGENI?

Yani kweli FMES Maiti inavuja damu kwa muda wote huo hadi inapelekwa bungeni ikivuja damu unasema ni ubinadamu huo?

Na kusema kifo kilikuwa violent...Na huku ukiwa na conspiracy theory..Then unaanisha ameuwawa kinyama kwa kutumia vitu vingine na wala si ajali.

Ungesema ni fatal accident ambayo hata hivyo ni intentional ungeeleweka.

Kwa kumalizia..Kwenye red higlight..Kunanishangaza...Kwani mara nyingi kuharibika kwa kusababisha maiti izikwe haraka ni kwasababu labda ya harufu..na wala si damu!

Kwani mwili gani huo unaoendelea kutowa damu hadi sasa kama si MWELEKEO WA KIPROPAGANDA?

Hivi hiyo ajari amegonga mti ama ameanguka? Na ktk gari hilo walikuwemo watu wangapi?

tuaminini ya kwamba ajari imetokea wala haikupangwa na mtu.Na kama imepangwa OLE MTU YULE
 
Mimi si daktari lakini hii ya maiti kuendelea kutoa damu saa 24 baada ya kifo imeniacha hoi. Yaani pale hospitali alipelekwa kufanyiwa nini?
 
Hivi hiyo ajari amegonga mti ama ameanguka? Na ktk gari hilo walikuwemo watu wangapi?

tuaminini ya kwamba ajari imetokea wala haikupangwa na mtu.Na kama imepangwa OLE MTU YULE

Maneno mazito sana mkuu, ubarikiwe tu!
 
Mimi si daktari lakini hii ya maiti kuendelea kutoa damu saa 24 baada ya kifo imeniacha hoi. Yaani pale hospitali alipelekwa kufanyiwa nini?

Mkuu heshima mbele,

Mara ya mwisho tulipokwenda kumzika ndugu yangu, damu ilikuwa inamtoka sana kichwani, kumbe inatakiwa kuwaacha binadamu wengine hoi hiyo?

Basi siku ile kumbe wengi waliachwa hoi sana! na pia karibu sana mkuu
 
Hivi hiyo ajari amegonga mti ama ameanguka? Na ktk gari hilo walikuwemo watu wangapi?

tuaminini ya kwamba ajari imetokea wala haikupangwa na mtu.Na kama imepangwa OLE MTU YULE

Nakubaliana na wewe....LAKINI NA MIMI NASEMA..OLE MTU YULE..KAMA NI FISADI!
 
FMES,
Nilidhani kazi mojawapo hospitali katika hali kama hiyo ni kudhibiti hiyo damu isiendelee kuvuja. That's why I was wondering. Kwa sababu hapa Marekani that's what they do. Mfanyikazi mwenzangu alipatwa accident na tulienda kuona maiti kabla ya kupelekwa mortuary. The doctors had done a good job.
 
Mpaka rafiki yake, the fair-minded Rev. Kishoka, ame raise concern na credibility ya huyu mtu ujue kweli mchizi kapoteza rep.

Ahsante mkuu kwa haya matusi, ila nina heshima na marehemu Wangwe, kwa hiyo ninawaachia Mods haya matusi yako, lakini nimekusikia na haya matusi yako ya nguoni.

Wakuu Mods naomba kuuliza kuwa haya matusi yanaruhusiwa, kabla sijajibu maana kama yanaruhusiwa nitayajibu sooon!
 
FMES,
Nilidhani kazi mojawapo hospitali katika hali kama hiyo ni kudhibiti hiyo damu isiendelee kuvuja. That's why I was wondering. Kwa sababu hapa Marekani that's what they do. Mfanyikazi mwenzangu alipatwa accident na tulienda kuona maiti kabla ya kupelekwa mortuary. The doctors had done a good job.

Ndio maana nimesema hivi mkuu, kuwa sikujua kuwa ile siku ya mazishi ya mdogo wangu, watu waliohudhuria waliachwa hoi sana sikujua hilo, lakini nimekusikia sana.
 
Ndio maana nimesema hivi mkuu, kuwa sikujua kuwa ile siku ya mazishi ya mdogo wangu, watu waliohudhuria waliachwa hoi sana sikujua hilo, lakini nimekusikia sana.

Rarely, it may happens for Haemophilic people to bleed for several hours after death. Depending on the severity of injuries and the hospital facilities, controlling of each of the wounds on and inside the body could be an impossible task. Otherwise, the clotting process is enough to stop bleeding.
 
Pole kwa watanzania na wanaharakati wote!!!!

Nitakuwa Tarime pamoja na ndugu wa marehemu!!!!
 
kapumzike kijana wetu tutakukumbuka sana kama Mwanaharakati na Mwana Mageuzi.
 
RIP Chacha Wangwe

Awali ya yote wana JF naomba mnielimishe hivi nini maana ya RIP?

Pili Na mimi naomba nijitokeze kutoa rambirambi zangu kwa wana Tarime wote na CHADEMA kwa ujumla. Poleni sana mno.

Kilichobaki sasa ni kuandaa mkakati wa kuhakikisha CHADEMA inashinda ubunge tena Jimbo hilo la TARIME, tukifanya kosa sisiem wakashinda, ujue tumeongeza idadi nyingine ya MAFISADI bungeni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom