Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Tunamkumbuka: Ni mahali pa kukumbuka maneno, vitendo na maisha ya Wangwe. Focus ni Zakayo Wangwe, maisha yake kwa kukumbuka wema wake na si mapungufu yake.

HABARI ZA KIFO CHA WANGWE - CLICK

Baadhi ya nukuu zake za kukumbuka:


Mzigo wa hoja za wananchi wa jimbo langu naubeba mwenyewe kwa kuwa kila mtu kachaguliwa mwenyewe jimboni mwake na kila mtu ana uhuru wa kutoa hoja yake, hivyo hili halinibabaishi, nitaendelea kutetea watu wangu wa Tarime ambao wanatambua mchango wangu kwao - Wangwe (akizungumza wiki mbili zilizopita)


Namtaka aachane na mambo ya CHADEMA na badala yake ajiulize ya CUF kwa nini haina wabunge Bara na aone upungufu uliopo - Akielekeza kwa kiongozi wa Upinzani Bungeni

Nami kwa kuwa nimesimama katika misingi ya haki na ukweli na wananchi wananiunga mkono, sitaogopa kupambana na maovu ndani ya chama. - Kuhusu msimamo wake ndani ya CHADEMA

ongeza unayokumbuka....
 
Mkuu MMJJ,

Samahani maana mimi nitakuwa kidogo tofauti na wewe, nadhani tutakuwa tayari kuiga yale mazuri lakini pia tusiepuke ukweli kwamba alionyesha utata sehemu fulani fulani ambako inatubidi tujifunze kwamba huo sio mfano mzuri wa kuigwa na yeyote anayeangalia Taifa letu linaelekea upande upi.
 
semeni mema ya mwanadamu mwenzenu; hayo mabaya yaandalieni kwingine. Kama huna jema la kusema usiseme lolote. That is the meaning of a tribute.
 
Natoa shukrani zangu za dhati kwa wananchi wa Jimbo langu la Tarime, kwa kusimama imara kuitetea Demokrasia ya kweli katika nchi hii, bila kujali vitisho, majeraha na mauaji wakanichagua mimi mnyonge mwenzao na kukataa takrima ili niwe sauti ya wasiokuwa na sauti hapa Bungeni. Waliopoteza maisha yao, Mungu awarehemu

hiyo aliitoa tarehe 10 julai 2006
 
Endapo kama maji ya ziwa victoria yatatumiwa vema kwa shughuli za umwagiliaji, basi Tanzania inaweza kabisa kuondokana na adha ya kuomba omba chakula.

hiyo aliiongea kipindi cha mwaka jana akichangia bajeti ya mwaka 2006/7.
 
Pundit, since when umeanza kujicontradict mwenyewe namna hii... ?

This is my saying all along, I will say the same thing the day the devil himself dies, if there is such a thing.Note I am not saying all people, but all beings, including vinyamkera vyote and the very devil himself, if you believe in that kind of mythology.
 
Tunamkumbuka: Ni mahali pa kukumbuka maneno, vitendo na maisha ya Wangwe. Focus ni Zakayo Wangwe, maisha yake kwa kukumbuka wema wake na si mapungufu yake.

HABARI ZA KIFO CHA WANGWE - CLICK

Baadhi ya nukuu zake za kukumbuka:

ALIKUWA JASIRI,KAKAMAVU ASIYEPENDA UKABILA WALA UDINI NA ALIPENDA KUONA KATIKA MAISHA YAKE CAHDEMA INAKUWA CHAMA CHA SIASA KAMA TAASISI NA SI NGO YA WATU WA KILIMANAJARO.
NI KIONGOZI ALIYEKUWA NA MVUTO WA HALI YA JUU KWANI ALISHINDA UCHAGUZI WA UMAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA LICHA YA WENYE CHAMA KUWA NA MGOMBEA WAO(ALFU). ALIMFANYA MBOWE AACHE MASOMO ILI KUKABILIANA NAE.

WANGWE NI MFANO WA KUIGWA NA ILI KUMUENZI, SISI WANACHADEMA INABIDI KUYAFANYIA KAZI YALE YOTE MABAYA ALIYOYASEMA NDANI YA NGO HII.
TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA USHUJAA WAKO KAMANDA MPAMBANAJI CHACHA ZAKAYO WANGWE.
 
R.I.P Chacha Zakayo Wangwe.

Ama kwa hakika kifo chako kimekuja wakati mbaya sana.

Katika mazingira kama haya yaliyopo sasahivi imesababisha walikuwa wanakuunga mkono pamoja na wapinzani wako wameendelea kulumbana hapa JF.

Yawezekana kweli hata wale waliokuwa mahasimu wako wakatoa salaam za rambi rambi kwa dhati ya mioyo yao(wenye roho za ubinadam) lakini pia wapo ambao wameendelea kukushambulia ilhali umeshatangulia mbele ya haki.

Lakini kwa kuwa kila mtu ana uhuru wa kusema na kutenda yale anayoyaamini na kuyafahamu,sisi tuliobaki tutaendelea kukumbuka kwa yale yote uliyoyafanya na kunuia kuyafanya.
Na kwa hakika ulijipambanua kwa namna yako ya kipekee, pamoja na kukutana na vikwazo mbalimbali bado uliweza kumudu kusimamia kile ulichokiamini na kukifahamu.

Napenda kuchukua fursa hii kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki, wapiga kura wako wa tarime, mashabiki wako ndani ya tanzania na hata nje ya tanzania bila kuwasahau wanaCHADEMA wote na watanzania wote kwa ujumla.

Pumzika kwa amani ''MURRA CHACHA OWANGWE''.
 
Tunamkumbuka: Ni mahali pa kukumbuka maneno, vitendo na maisha ya Wangwe. Focus ni Zakayo Wangwe, maisha yake kwa kukumbuka wema wake na si mapungufu yake.

HABARI ZA KIFO CHA WANGWE - CLICK

Baadhi ya nukuu zake za kukumbuka:

ALIKUWA JASIRI,KAKAMAVU ASIYEPENDA UKABILA WALA UDINI NA ALIPENDA KUONA KATIKA MAISHA YAKE CAHDEMA INAKUWA CHAMA CHA SIASA KAMA TAASISI NA SI NGO YA WATU WA KILIMANAJARO.
NI KIONGOZI ALIYEKUWA NA MVUTO WA HALI YA JUU KWANI ALISHINDA UCHAGUZI WA UMAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA LICHA YA WENYE CHAMA KUWA NA MGOMBEA WAO(ALFU). ALIMFANYA MBOWE AACHE MASOMO ILI KUKABILIANA NAE.

WANGWE NI MFANO WA KUIGWA NA ILI KUMUENZI, SISI WANACHADEMA INABIDI KUYAFANYIA KAZI YALE YOTE MABAYA ALIYOYASEMA NDANI YA NGO HII.
TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA USHUJAA WAKO KAMANDA MPAMBANAJI CHACHA ZAKAYO WANGWE.
Hizo zako naziona kama za KIMCHOCHEO vile, sio wakati wake wala mahala pake. Ukipitia wengi hapa ni "tributes" na wala sio malumbano. Kumbuka mwenzetu keshawahi hata kama alikuwaje lakini hakuna la ziada na ikishafika wakati kama huu itikadi huwekwa pembeni na kumuangalia muumba wetu, labda kama wewe huamini hayo nadhani siku yako ya kufa tutakumbuka ulivyokuwa mvurugaji wa mambo...!
 
Habari nilizozipata sasa hivi ni kwamba Mwili wa marehemu Wangwe, leo umewekwa bungeni kwa siku nzima, na hata ninapoandika bado upo bungeni, kwa sababu wananchi wamekuwa wengi sana waliojitokeza kumuaga,
Mwanzoni ilitegemewa kuwa watakuwa wabunge tu, lakini wananchi wamemiminika mno hata protokali imebidi zivunjwe, na wananchi wa kawaida waingie ndani ya bunge, kuuaga mwili wa marehemu, tunasema hewala kwa hilo kwa serikali yetu,

According to the dataz ni kwamba mwili wake mpaka sasa bado unavuja sana damu, haya yamesemwa na walio uona na kwamba inasikitisha sana, kwa sababu kama mpaka sasa bado mwili unavuja damu, ina maana this was a very violent death, Mungu amuweke mahali pema peponi, Maiti itaondoka kesho asubuhi kuelekea kwao Tarime, ambako according to the dataz mazishi ni lazima yafanyike kesho, kutokana na hali mbaya ya mwili wa marehemu,

However, tayari kale kamdudu kameanza minong'ono, kwa kweli tuta-spare mpaka baada ya mazishi, betweeen jana na leo tumekusanya a lot of dataz very soon tutazichambua kwa kina, tena hapa hapa JF, na bado pia tunaendelea kuzikusanya na kuzi-verify, ninasema nothing but just our commitment kuhabarishana ndani ya hii forum, ili kuweka record straight kama kawa!

Again Mungu Amuweke Mahali Pema Peponi Marehemu Wangwe, kwa kweli baada ya kuskia kutoka kwa waliouna mwili, machozi yamenitoka na huwa kwangu sio rahisi kutokwa na machozi, pamoja na kwamba nilikuwa simjui marehemu.

Ahsante Wakuu
 
Mungu ailaze roho yake peponi. Amin. Chochote kilichotokea jana usiku, kimeanza kuzua maswali mengi sana hapa leo. Kuna mambo ambayo hayaelezeki. Tunasubiri kusikia msimamo wa Polisi tu. Lakini, aliyetoa habari za mwanzo aidha alipotosha watu hakujua watu wengine wanajua nini.

Asanteni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom