KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

amepigwa na kuteswa na kikundi kinachosadikiwa kuwa ni cha kigaidi cha alshaabab"Mwisho wa kunukuu
 
Wanapoteza ushahidi upi wakati lengo lilikuwa ni kuua. Je bunduki ingefyatuka hayo maneno tungeyasikia kwa nani?

how sure are you that the gun had a bullet?.Hivi unapotaka kushoot mtu dead unaanza kumng'oa meno na kucha kwanza.au unashoot then unapotea?ukichukulia tukio lenyewe limefanyika nje ya nyumba yake ni mtu mjinga tu anapoanza kumtorture mtu ambae the really mission is to kill him.
The really mission was to commit the crime and flame it to the government police or security apparatus.
 
Afande linatumika karibu kwa majesshi yote Tanzania,
Hivi usalama wa taifa wao wanaitanaje?
 
Mungu ni mkuu,amemponya kwenye kifo,ataendelea kumpigania Absolum Kibanda apone haraka ,
 
I don't buy your thought! Ukiwa biased ni ngumu kuacha akili zako kuwa huru.Fikiria nje ya grid mkuu.

Kama maafande ndio waliohusika, wasingeweza kutamka wakati wanamshambulia kwamba ''afande mshuti''

Mhalifu siku zote huficha utambuliso wake, iwe kwa jina au kwa sura. This is common sense, you dont need a degree!

Ni mjinga tu atakayeamini kwamba hao walikuwa maafande.

Hawa wahalifu inabidi kushughilikiwe.

Sasa mbona hata wewe uko biased, una hakika gani kama sio maafande. Common sense yako iko wapi hapo? Kumbuka sio rahisi kufanya uhalifu bila kuacha clue. Kama sio serikali kuhusika kwa nini hakuna tume iliyoleta majibu kati ya zote zilizowahi kuundwa?
 
kwa akili hata ya shule za voda fasta lazima ujue kama walitamka hvyo hao sio wanausalama,wasingeweza fanya ujinga huo hata kama wangekuwa wapuuz vp,ni watu walotumia udhaifu flan wa wanausalama wetu kumuattack kwa lengo ama la kisiasa au vinginevyo.
 
Sasa tuamke make tataandika kwenye vitabu hadi lini. songs of freedom
 
style ya upigaji-kung'oa kucha na meno mbona kama iliyotumika kwa Dr. Ulimboka? nadhani uchunguzi ungeanzia kwenye ushahidi wa Dr. Ulimboka, inawezekana kuna kikundi maalumu cha kunyamazisha watu
 
Sasa mbona hata wewe uko biased, una hakika gani kama sio maafande. Common sense yako iko wapi hapo? Kumbuka sio rahisi kufanya uhalifu bila kuacha clue. Kama sio serikali kuhusika kwa nini hakuna tume iliyoleta majibu kati ya zote zilizowahi kuundwa?

I repeat, ni mjinga tu atakayeamini kirahisi kwamba polisi ndio waliotumika and at the same time wajitaje kuwa eti ''afande mshuti huyo''.

Piga makelele mpaka kesho! CCM kama chama cha siasa kina mapungufu yake mengi tu, lakini sio kila ujinga tuukubali eti kwa sababu CCM ni dhaifu. Hapana, kama taifa tuna vyombo vya usalama acha vifanye kazi yake bila ya kuwadistract.

Polisi inaundwa na watu ambao wana utashi na vyama vyote unavyovijua, acha nao watumie utashi wao kuwafichua kama waliohusika watakuwa wa chama tawala!
 
Wakuu,ni wakati uliokubalika sasa kuomba msaada wa MOSSAD kama siyo ...............!
 
Hapana, kama taifa tuna vyombo vya usalama acha vifanye kazi yake bila ya kuwa distract.

Chifu, unaongea kwa kufikirika sana! Too theoretical!!

Chifu, tungekuwa na vyombo vya usalama vinavyofanya kazi, 'wahusika' wote wa matukio ya kuteka na kujeruhi raia wangekuwa wamekamatwa. Kwani ni matukio yanayofanywa na watu wasio 'smart'; watu wanaoacha alama nyingi za kuwatambua.

Kungekuwa na vyombo vya usalama vya uhakika, twiga wasingesafirishwa mchana kweupe na dege la kijeshi, bila kukamatwa. Vyombo vya usalama vya uhakika visingeruhusu wizi wa kihuni kwa njia ya EPA; kisha wezi wajulikane, halafu wapewe msamaha kama wakirudisha pesa walizoiba!!

[/B]Polisi inaundwa na watu ambao wana utashi na vyama vyote unavyovijua, acha nao watumie utashi wao kuwafichua kama waliohusika watakuwa wa chama tawala!

Here you go again!! Huko katika dunia ya kufikirika mno chifu!!

Ebu nipe mfano mmoja tu wa polisi kuwafichua wahalifu walio ndani ya CCM! Rushwa hadi kwenye chaguzi za ndani za CCM, lakini nani kakamatwa?

Narudia tena, dili la EPA watu kibao wenye uhusiano na CCM walihusika, lakini ulisikia wakikamatwa na polisi?

Kama tu wastaafu wa polisi wanagombea nafasi za uongozi ndani ya CCM, sasa hapo utasema watu hao walikuwa wapo fair katika kazi zao?!?

Polisi hii ya sasa ina mahusiano ya moja kwa moja na CCM! Aidha kwa kukubali kutumiwa na wana CCM au kwa kujipendekeza kwa wana CCM na serikali yake.
 
Tume ni ya nini? Kwani alivyouwawa RPC huko mwanza iliundwa tume? Pengine nimesahau naomba wana JF munikumbushe. Hawa jamaa ukiona wameanza mambo ya tume ujue ipo namna ni kutupotezea tu. Kama Dk Ulimboka aliwataja watesaji wake, serikali badala ya hata kutudanganya wakaanza uchunguzi na hao aliowataja wakakurupuka na kusema huyo Dk hana fahamu anachosema si kweli. Ndo huyo mtu aliyeitwa mkenya akajitokeza na wao kujifanya wanamshikilia kwa tukio hilo. Jamani tumechoka kujazana ujinga na uwongo kama huu wa tume tume hadi lini?. Nafikiri tukubaliane amani nchi hii hakuna bali ni unyama unyama tu. Tutafakari na kuchukua hatua
 
Akizungumza kwa tabu alipokuwa chumba cha wagonjwa ICU, Hospitalini Moi, alisema, "Nilifika nyumbani kwangu kama saa 6 usiku nikitokea kazini tulikuwa tunafuatilia uchaguzi wa Kenya tukaona hamna la maana.

Nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu... Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kukimbia kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito... niliona kama watu 3 hivi...

Sikufahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti...mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti' ilikuwa kama vile imegoma.

Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha ktk vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba na kunitupa na wakaondoka, badaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.

There is not a shred of doubt kwamba hizi ni ritual tortures, wanaofanya hivi ni lazima watumie njia ya aina moja kwa sababu ni maelekezo maalum ya kutoka kwenye Cult Sect.

Kwa nchi za wenzetu already wangekuwa wameshawakamata suspects kutokana na trails za evidence zilizoachwa, huku kwetu ni more likely kuwa wanaotenda haya ni either mafia waliopo serikalini au watu walio karibu na serikali na ndio maana japokuwa ni rahisi sana kuwa wameshakamatwa mpaka saa hizi vyombo vya usalama havifanyi juhudi za kutosha kuhunt wahalifu.

Kwa wenzetu sasa hivi ingekuwa ni NATIONWIDE MAN HUNT while TV stations zikiwa kwenye Breaking News Mode wakifanya kila liwezekanalo kuwapata wahalifu.
 
Kama Padre aliuliwa na kuleta FBI,CIA na SCOTLAND YARD kuja kuchunguza Kwanini pia wasiletwe MOSSAD,IRGC kuja kuchunguza pia?
 
Wanasiasa Banah!WApo tayari hata kuwaua wenzao hili wapate hoja za kisiasa.Ukiwaona wanavyoshambuliana kwenye majukwaa ya siasa utazani ni maadui,nyinyi mukiuana wao baadae wanakaa meza moja na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa(Zanzibar,Kenya na Zambia).Nitafutieni mwasiasa mmoja kutoka bara jeusi ambae ni mkweli zaidi ya Mandela.
 
Nashawishika kuamini kuwa aliyebuni mkakati huu ndi yule yule aliyebuni mkakati wa Ulimboka! Ipo siku Mungu ataamua kumuweka hadharani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom