KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

Kwa udhaifu wa serikali yetu inafika pahala hadi tunashindwa kuwa fair kuijaji uhusuka wake. Tujiulize serikali ina maslahi gani katika tukio hili?
Tatizo kubwa naloliona ni udhaifu uliopo ktk serikali yetu. Udhaifu upo mkubwa katika kuzingatia zaidi mambo yasiyo ya msingi na kuacha yaliyo ya msingi. Ni kipindi cha serikali yetu kujipanga vema.
 
Inasikitisha sana. Kama alivyosema Jaji Warioba, hawa sasa sii majambazi tena bali mashambulizi ya kupanga... Taifa lililo huru watu wake wana haki ya kusema. Waziri mambo ya ndani na vyombo vyako vya dola, hii sasa ni aibu kwa taifa, amkeni na jiulizeni kunani? taifa linaelekea wapi? nani wa kulaumiwa?
 

Mbowe na Tanzania Daima wanayo siri ya Kutekwa na Kujeruhiwa kwa Kibanda

Salaam Wakuu,
Tasnia ya Habari kwa sasa imejawa na simanzi kutokana na kitendo cha kuvamiwa na kuumizwa na watu ambao hawajabainika walikuwa na lengo gani.

Mimi kwa ujumla nimesikitishwa sana kutokana na tukio hilo na nawalaani wote waliohusika. Aidha, natumia fursa hii kumuombea ndugu yetu Kibanda apone kwa haraka ili arejee nyumbani salama kuungana na familia yake na hatimaye kuendelea na majukumu yake.

Baada maelezo hayo, naomba kwa pamoja tutafakari mambo yafuatayo;


  1. Juzi Jumanne tarehe 05/03/2013 kulikuwa na kikao cha wadau wa demokrasia nchini kilichoandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini (Tanzania Centre for Democracy – TCD). Wenyeviti wa vyama vyote vya siasa ni wajumbe na walipata barua za mwaliko kuhudhuria kikao hicho. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), FREEMAN MBOWE, ni miongoni mwa wajumbe walioalikwa. Hata hivyo, Mbowe alitoa udhuru ya kutohudhuria kikao hicho kwa madai kuwa atakuwa jimboni kwake, Hai kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri wilaya ya Hai (Full Council). Hizi zote ni facts na mimi nikiwa miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho, nilimsikia ANTHONY KOMU, Mkurugenzi wa Utawala wa CHADEMA ambaye ndiye alimwakilisha Mbowe akitoa maelezo hayo.
  2. Hata hivyo, katika tukio la kuvamiwa na kuumizwa vibaya kwaAbsalom Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri wa New Habari Corporation (2006), Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameonekana Hospitali ya Taifa ya Mhimbili akimjulia hali ndugun yetu Kibanda.
  3. Pia hakuna uthibitisho kuwa Mbowe alienda jimboni kwake kama alivyodai wakati akitoa udhuru wa kutohudhuria kikao cha TCD.
  4. Kwa vile kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa, KIBANDA amekuwa na mgogoro na Tanzania Daima gazeti ambalo linamilikiwa na FREEMAN MBOWE, na kwa vile KIBANDA ana siri nyingi sana za CHADEMA na kwa hali hiyo viongozi wa Chama hicho wanamuona kama ni adui, na kwa kuwa kitendo cha Mbowe kutohudhuria kikao cha TCD kilitumika tu kama ushahidi wa yeye kutokuwepo Dar es Salaam wakati wa tukio hilo na hivyo asiwe mshukiwa nambari moja, kitendo cha yeye kuonekana Hospitali ya Mhimbili akimsalimia KIBANDA, kilinishtua na kuniachia maswali mengi.
Kazi ipo,sikuwa najua kama Kibanda alikuwa na siri za CHADEMA ndio nasikia toka kwako,sasa kama ana siri ndio ashambuliwe?Unataka kuniaminisha kuwa CCM walimuua Horace Kolimba?

 
Tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mhariri ni lakinyama,ndugu wadau naomba mtu mwenye taarifa ni mambo gani Huyu mhariri alifanya katika kazi yake ambayo yanapelekea tukio hilo?
-
NAWASILISHA,
 
Mimi elimu yangu kama ya Mbowe tu, sihitaji kurudia paper acha nibangaize tu mtaani.

Hiyo kauli ya afande mshuti imetumika ili kuwazuga watu kama nyie wenye chuki na serikali kwa vile tu

inaongozwa na CCM. Usifikiri kwamba uhalifu utaondoka kwa kuingia chama fulani madarakani, hapana ni zaid ya hapo.

chadema hawa dhaifu hata kwa kujibu hoja wataweza wapi kuongoza wewe.
 
soma habari kwenye thread nyingine zipo humu au magazet hasa ya jana.acha uvivu
 
Tuache propaganda- Yaani tudanganyike na kauli za neno afande! Halafu afande huwa haamrishwi na askari wa chini yake afanye kitu. Halafu kwanini waji expose kiasi hicho kama sio kuvuruga ushahidi na kurefusha njia za kukamatwa kwao. Hata mhe. Mbowe alikosea sana aliposema kwenye TV moja kuwa '...Kibanda amekuwa akiandika habari zinazoiudhi serikali..' kwa msikilizaji aliyekuwa makini iliimanisha kuwa serikali inahusika na uvamizi huo. Lkn mzee Mengi aliwaasa waandishi waandike habari hiyo kwa utafiti wa kina badala ya kutumia hisia.
 
Yaani hawa polisi wamekidhiri. Kila mtetea haki auawe? Yule Mungu tuliyefundishwa tangu utoto kumwogopa amehama Tanzania? Jamani kama wewe ni mzazi unatoka kumfanyia haya mzazi mwenzio? Unatoka kumfanyia Binadamu aliyofanyiwa Dr. Ulimboka, Ally wa Morogoro? Unaenda kumbaka mama na kumtoboa kizazi kisha alikuwa anakata majani au kuokota kuni za kuwapikia manae wadogo chakula? Hivi mwuumba wetu alienda wapi? Unatoa amri mzazi mwenzio afumuliwe kwa bomu la machozi na kisha mwili wake uachwe umesambaratika vibaya kama wa mnyama huku ukijiondokea kwenda nyumbani kufurahia maisha na mkweo na watoto? Unambambikizia mjane kesi na kumtupa rumande kama mbwa bila kujali wanae wa chini ya miaka mitano eti wewe ni askari polisi na hakuna wa kukufanyia kitu? Je hiyo siku utakapoitwa mbale ya mwuumba utakuwa umevaa uniform za polisi? Watanzania askari wetu wamepitiliza kipimo. Tuwakumbushe kuwa hata wao watakufa na pengine watateseka kwa milele yote kutokana na maovu wanayowatendea wanyonge wa nchi hii hasa wale wasio na hatia.
 

Mbowe na Tanzania Daima wanayo siri ya Kutekwa na Kujeruhiwa kwa Kibanda

Salaam Wakuu,
Tasnia ya Habari kwa sasa imejawa na simanzi kutokana na kitendo cha kuvamiwa na kuumizwa na watu ambao hawajabainika walikuwa na lengo gani.

Mimi kwa ujumla nimesikitishwa sana kutokana na tukio hilo na nawalaani wote waliohusika. Aidha, natumia fursa hii kumuombea ndugu yetu Kibanda apone kwa haraka ili arejee nyumbani salama kuungana na familia yake na hatimaye kuendelea na majukumu yake.

Baada maelezo hayo, naomba kwa pamoja tutafakari mambo yafuatayo;


  1. Juzi Jumanne tarehe 05/03/2013 kulikuwa na kikao cha wadau wa demokrasia nchini kilichoandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini (Tanzania Centre for Democracy – TCD). Wenyeviti wa vyama vyote vya siasa ni wajumbe na walipata barua za mwaliko kuhudhuria kikao hicho. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), FREEMAN MBOWE, ni miongoni mwa wajumbe walioalikwa. Hata hivyo, Mbowe alitoa udhuru ya kutohudhuria kikao hicho kwa madai kuwa atakuwa jimboni kwake, Hai kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri wilaya ya Hai (Full Council). Hizi zote ni facts na mimi nikiwa miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho, nilimsikia ANTHONY KOMU, Mkurugenzi wa Utawala wa CHADEMA ambaye ndiye alimwakilisha Mbowe akitoa maelezo hayo.
  2. Hata hivyo, katika tukio la kuvamiwa na kuumizwa vibaya kwaAbsalom Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri wa New Habari Corporation (2006), Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameonekana Hospitali ya Taifa ya Mhimbili akimjulia hali ndugun yetu Kibanda.
  3. Pia hakuna uthibitisho kuwa Mbowe alienda jimboni kwake kama alivyodai wakati akitoa udhuru wa kutohudhuria kikao cha TCD.
  4. Kwa vile kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa, KIBANDA amekuwa na mgogoro na Tanzania Daima gazeti ambalo linamilikiwa na FREEMAN MBOWE, na kwa vile KIBANDA ana siri nyingi sana za CHADEMA na kwa hali hiyo viongozi wa Chama hicho wanamuona kama ni adui, na kwa kuwa kitendo cha Mbowe kutohudhuria kikao cha TCD kilitumika tu kama ushahidi wa yeye kutokuwepo Dar es Salaam wakati wa tukio hilo na hivyo asiwe mshukiwa nambari moja, kitendo cha yeye kuonekana Hospitali ya Mhimbili akimsalimia KIBANDA, kilinishtua na kuniachia maswali mengi.

JESHI LA POLISI limetoa dau la Tsh milioni 5 kwa mtu ye yote atakayelisaidia kuwezesha kukamatwa kwa waliohusika na unyama huu. mkiristoMwislamu unaonekana kuwa na uhakika wa asilimia 100% kuhusu watu waliotenda unyama huu, Kwa nini basi usilichukue hilo dau?
 
Serikali na Polisi wana issue gani na mwandishi huyo?. Jamani kwa maisha ya sasa ni rahisi sana mtu kujijengea maadui kuliko marafiki.

Inaweza ikawa ni chuki ya kibiashara ama mapenzi ndiyo chanzo. Si vyema kuanza kuishambulia serikali bila ushahidi wa kutosha.

Kuna mtu anaandika makala za kuikosoa na kuikashfu serikali kama mzee mwanakijiji?, mbona yuko salama na huru muda wote?
jidanganye mwenyewe sisi tumeshtuka.
Kwanza mzee Mwanakijiji hakai Tanzania. Na kwenye tukio lazima kuwepo chief suspect,rejea tukio la Ulimboka,kumbuka alimtambua mmoja wa maofisa wa polisi na kumwambia amrudishie pochi yake.Hakubisha bali aliondoka fasta.
Hadi sasa jeshi la polisi halijataka kumhoji kuchelea atamtaja mmoja wao.Hadi leo vyombo vya usalama vya jamhuri ya muungano vimemkamata raia mmoja wa Kenya peke,na akili za kawaida utaona huyo jamaa peke yake asingeweza kutekeleza tukio hili,where are his acomplises?
Na ni nani anayetakiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani?niulizie kwa Kova.
Mwanahalisi katika uandishishi wa kichunguzi likaandika habari inayolandana na maelezo ya Ulimboka na kumtaja ofisa wa ikulu kama mmojawapo wa wahusika.Serikali ikalifungia badala ya kulipongeza.
Rejea Mwangosi aliahidiwa ataona na kweli akakiona tena mbele ya RPC kumbuka wamepongezwa na mkuu wa nchi kwa kazi nzuri.
Kazi hii inafanana na kazi ya akina Rama Ighondu kwa Uli,na wewe unataka tusiishuku serikali sikivu nipe sababu ukizingatia inatakiwa kutulinda na kukamata wahalifu.Kwa nini Ighondu na Ulimboka hawajahojiwa?Hakuna inteligensia?hapana ipo ya kuzuia maandamano ya chadema.
By the way aren't u say Ighondu?was just thinking aloud no offense meant
 
Alikuwa anatoka kuangalia mechi kati ya Man U na Madrid,sio uchaguzi Kenya
 
Akizungumza kwa tabu alipokuwa chumba cha wagonjwa ICU, Hospitalini Moi, alisema, "Nilifika nyumbani kwangu kama saa 6 usiku nikitokea kazini tulikuwa tunafuatilia uchaguzi wa Kenya tukaona hamna la maana.

Nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu... Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kukimbia kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito... niliona kama watu 3 hivi...

Sikufahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti...mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti' ilikuwa kama vile imegoma.

Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha ktk vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba na kunitupa na wakaondoka, badaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.

bila shaka hayo kasemewa na waliotekeleza mpango huo na wameandaa maneno hayo ili watan zania waamini kuwa ni jeshi la polisi limehusika. kumbe ni CHADEMA na Mbowe
 
Vyombo vya usalama sio mpaka vikupe wewe taarifa namna wanavyofanya kazi zao. Kwani kule ZNZ si tunaambiwa kuna FBI wameshakwambia waliokamatwa ni akina nani?

Maelezo ya Ulimboka yalishachukuliwa na polisi na ndio maana suspect akakamatwa.

Sio lazima akamatwe unayemuhisi wewe.

Mimi ninadoubt conclusion za watu kama nyie ambao you directly raise an accusing finger kwa serikali kwamba ndio inayohusika.

Kitu kimoja ninachokikubali ni kwamba tuna tatizo la usalama katika nchi yetu mwanya ambao wahalifu wamekuwa wakiutumia.

Hizi allegations nyingine ni kusiasisha kila kitu kwa ajili ya political gain kitu ambacho hakiwezi kutufikisha popote.

Kuna alternative za kupata habari kaka, polisi huwa mnakurupuka kutoa taarifa za vitu ambavyo hamjafanyia kazi just to cover ur ass but at the end u expose ur front parts. Its like hamna wataalam wa kufanya kazi kitaalam hata just to know what to say its a big problem. Nyie jamaa mnatia aibu na mnadhalilisha jeshi. Hivi huko hakuna wataalam Crime Scene Investigation. The way u collected evedence is shame mnacontaminate scene mwanzo mwisho na mwisho wa siku ndio maana hata kesi mnashindwa hata kwa kesi za moja kwa moja. Uwezo wenu wa kujenga ushahidi wa maana ni tatizo. Labda uniambie jeshi halina budget. Ajirini wataalam wa hizo kaka/afande.
Mwisho mko corrupt mnoooo askari/mwanaCCM. Polisi na wahalifu mnafanana tuu tofauti ni upende upi umesimama. Umeona video ya mwangosi, Kamuhanda amewajibishwa?!!!!
 
JESHI LA POLISI limetoa dau la Tsh milioni 5 kwa mtu ye yote atakayelisaidia kuwezesha kukamatwa kwa waliohusika na unyama huu. mkiristoMwislamu unaonekana kuwa na uhakika wa asilimia 100% kuhusu watu waliotenda unyama huu, Kwa nini basi usilichukue hilo dau?

watu wanaofanya kazi kwa maslahi ya kifedha bwana? utawajua kwa posts zao. lazima waguse mshiko aka mnuso. bila shaka utakuwa mchaga tu
 
Hata wale mgambo wa jiji nao wanaitana maafande

Ukweli utajulikana japo utazimwa usiwafikie walio wengi
 
Let me tell you one thing: swa professional killers inawezekana wakatumia neno 'afande@ ili kupotoukweli yaani watu wafikirie kuwa jeshi ndilo lililofanya unyama wakati sio. Pamoja na yote nchi yetu inakwenda kubaya. Usalama kwa raia unatoweka. it is anarchy na hii ni hatari.
 
aliuwawa mkuu wa polisi wa Mwanza iliundwa tume ya upelelezi na wauwaji walipatikana ndani ya wiki moja. ila wengine wakiuwawa uchunguzi unaendelea mpaka tunasahau au wakiamua kutufurahisha wanatutafutia wakenya, au wagonjwa wa akili na kusema hawa ndio wauwaji. utekwaji wa ulimboka. watekaji walimuuliza kuwa kunamkono wa chadema? tuambie nani yuko nyuma yenu, lakini doctor alikataa ila bado waliendelea kumpiga na wakadhani kuwa amekufa. sasa ni kibanda the day has arrived and the truth shall be known
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom