KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

tulijua tu mwisho wa story tutasikia waliohusika ni usalama wa taifa au police.
 
Hypothesis yangu ni kuwa waliofanya tukio hili na lile a Ulimboka ni wahalifu na sio serikali kutokana na hiyo unayoiita Modus Operandi.

Kwa vile jamii ilijengwa kuamini kuwa ni serikali, ndio maana wahalifu wakachomekea vile vile ''Afande mshuti''

Ni mazuzu tu watakaoamini kirahisi kwamba hao ni maafande. Hao huenda walikuwa rafiki zake tangu zamani ila wakabadilika kuwa mahasimu. Acha FBI na CIA wahusishwe.


.......

Ungekuwa right serikali ingeshawashika hao wahalifu. Kigugumizi cha nini? especially kwenye kesi ya Ulimboka alitoa all the details ambazo zingefanywa wahusika washikwe, lakini alishikwa mtu, hapana. ooh mkenya.

Sasa Kova anakuja na mpya kwamba hao sio wahalifu ni kwamba walikuwa wana kisasi naye kwahio hapo ndiyo mwisho wa uchunguzi. Nilidhani kazi ya polisi ni kulinda raia wake kumbe nilijidanganya.
 
Hilo neno la afande ni mtihani kubwa. Limeficha mengi sana. Ila ukweli utajulikana tu. Ingawa mimi kuna washkaji wananiitaga kamanda sijui wanakuwaga na maana gani.
 
Tume tume tume,kila siku tume jamani tumecoka na tume hizi ambazo matokeo yake huwa hatuyajui wala kuambiwa.

mwishowe watateu mitume kuchunguza, hawa viongozi wetu wajinga sana..... ile ya kubenea,ulimboka na nyinginezo zimeishia wapi?
 
Very interesting especially ukishasema ni mystery! Ukisema watu walioko serikali hawatumii hata 5% ya 10% (i.e 0.5% < 1%) nakataa on the basis kwamba hiyo quantification ni subjective.

Sidhani kama masuala ya uwezo wa kutumia ubongo utayazungumza subjectively hata kama upimaji wa uwezo huo ni tata. Haya yanazungumzika vyema in a relativity manner.

Hivyo, ndio maana nilisema watendaji wa serikali yetu wengi wao hawatumii hata asilimia 5 ya asilimia 10. Kwani nikiangalia watendaji wa serikali zingine wanavyofanya kazi, inakuwa rahisi kutambua uwezo mdogo sana wa watendaji wetu.

Huo uhalifu wa namna hiyo unatokea hata katika nchi ambazo wewe unaamini kwamba wanatumia hiyo 10% yao yote mfano Marekani na Uingereza!

Ndiyo. Lakini unatokea bila ya 'mkono wa serikali' kuonekana dhahiri i.e. untraceable.
Kumbuka hapa tunaongelea hypothesis ya ushiriki wa serikali katika tukio. Kwa wenzetu kama serikali ikishiriki kufanya umafia huo, inahakikisha haichi alama yoyote itakayoweza kuihusisha. Si hapa kwetu, ndiyo maana nikasema, si ajabu kwamba alichosema Kibanda juu ya kusikia 'afande' akielekezwa kushuti, ikawa ni kweli.

All in all ni kuwa ume over react kwa kuwashambulia wote walioko serikali, kitu ambacho nafikiri sio sawa.

Ni sawa. Ingekuwa si sawa, basi tungekuwa tunaona utendaji wenye tija kutoka kwao. Nitasemaje sawa wakati kila sekta iliyo chini ya serikali ipo hoi bin taabani. Si usafirishaji, si elimu, si kodi na makusanyo yake, si usalama, si michezo, si siasa n.k.

Hili swala huenda likawa ni zaidi ya siasa, Tuwe objective kwenye kujadili mambo zaidi ya kiuweka upinzani wetu wa kisiasa mbele kwa kila jambo.

Sasa chifu, upinzani wa kisiasa umeingiaje hapo? Umejuaje mimi ni mwanasiasa ama mwanachama wa chama chochote cha siasa? Sitaki kuamini kama nawewe unamwona yeyote anayeikosoa serikali kuwa mpinzani, tena mwanachama wa chama cha upinzani!!

Fikra hizo ndizo zinakwamisha maendeleo kwa namna fulani kwa sasa. Kwani hata ukiwa mfanyakazi wa serikalini, ukitoa wazo mbadala (lenye kuleta maendeleo na mabadiliko) unaonekana 'wewe ni CHADEMA tu'.
 
Ungekuwa right serikali ingeshawashika hao wahalifu. Kigugumizi cha nini? especially kwenye kesi ya Ulimboka alitoa all the details ambazo zingefanywa wahusika washikwe, lakini alishikwa mtu, hapana. ooh mkenya.

Sasa Kova anakuja na mpya kwamba hao sio wahalifu ni kwamba walikuwa wana kisasi naye kwahio hapo ndiyo mwisho wa uchunguzi. Nilidhani kazi ya polisi ni kulinda raia wake kumbe nilijidanganya.

Mkuu polisi haifanyi kazi kwa hisia za watu, ni uchunguzi huwa unafanywa.

Initial assessment huwa inakubalika ni kama vile Nchimbi alivyosema mauaji ya padri ni tukio laugaidi.

Usisiasishe kila kitu.
 
ni bora mtu mmoja aangamie kuliko Taifa zima kuingia kwenye machafuko,kama mtu mmoja anataka kuondoa ''AMANI''nchini,kwa njia yoyote ile,hasa kwa kutumia vyombo vya habari ni bora akapotea atuachie nchi yetu
 
Mkuu polisi haifanyi kazi kwa hisia za watu, ni uchunguzi huwa unafanywa.

Initial assessment huwa inakubalika ni kama vile Nchimbi alivyosema mauaji ya padri ni tukio laugaidi.

Usisiasishe kila kitu.

Basi ni sawa na kusema hawafai maana wameshindwa kuwapata hao wahalifu
 
Nchi ya kung'oana meno
na kucha bila ganzi. Watanzania masifa sana, eti nchi ya amani, aha
nani kakwambia!



Mkuu tatizo la hawa polisi-ccm na usalama wa taifa-ccm, hawana hakili, na ndio maana style yao ya utekaji, kumpa mtu kichapo na kumtelekeza imebakia hiyo hiyo miaka nenda rudi....
Naona hii ndio style yao ya kushikishana adabu hapa mujini, wanakung'oa meno na kucha, kisha wanakutupa mabwepande, kama msitu wa mabwepande huko mbali, wanakutupa pembeni ya nyumba yako...
 
"CHADEMA YAANZA MIKAKATI YA MAUAJI"""

Na Comrade sambala Feat Kimeta.........

CHADEMA INAHUSIKA 99% NA UMWAGAJI DAMU NA UVAMIZI WA MWANDISHI HUYU WA HABARI

Usiku wa kuamkia jana pametokea tukio la kushambuliwa vibaya na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF).

Ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari (2006) LTD ndugu Absalom Kibanda.

Ambaye kwa sasa amesafirishwa nchini Afrika ya Kusini kwa Matibabu zaidi na juu ya maumivu makali aliyoyapata.

MASWALI YA KUFIKIRISHA NA KUJIULIZA NA KUFIKIRI ZAIDI.

*...Tukio kama hili ni karibu la tatu ama la nne kutokea hapa nchini kwa kipindi cha miaka 5 ama sita.

mwaka 2008 Saed Kubenea alimwagiwa Tindikali.

2011-Vijana Waandamananji waliuawa kwenye Maandamano ya Chadema Arusha.

2012-Kijana aliuwa Kwenye Vurugu za Chadema morogoro.

2012-Dk Ulimboka alitekwa na kuumizwa Vibaya.

2012 Mwandishi Daud Mwangosi aliuwa na Polisi...

Kwa haya Matukio Kadhaa tuliona namana Taifa na hasa wanaharakati na Vyama vya Siasa kulaani sana na kuilamu Serikali.

Je Kuhusu Kibanda...

Kwa Nini wanaharakati hawajalaani wamekaa Kimya...?

Kwa Nini Chadema hawalaani ama kuita CC ya dharura na wamekaa Kimya...?

JE NANI ASIYEJUA KUWA KIBANDA KWA ZAIDI YA MIAKA 8 AMEKUWA MFANYAKAZI WA FREE MEDIA INAYOMILIKIWA NA MBOWE NA DK LILIANI MTEI MBOWE..?

Kwa nini Tukio la Kibanda hatujaona Matamko...?

Kwa nini wana Harakai wapo Kimya....?

Wakati tunasubiri Vyombo vya Ulinzi na Usalama kupata majawabu ya Maswali yetu..

Kwa Sasa nasema FIKIRI ZAIDI na jipe majibu mwenyewe.

MAJAWABU TUNAYASUBIRI..

Think Twice.
 
Na hizi kampuni za ulinzi binafsi hazitumii afande?
It is a setup,someone is trying to flame someone.Hilo neno Afande laweza kuwa limetumiwa makusudi to divert suspiction(sp?) to draw away from the really criminal.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom