KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
135
Akizungumza kwa tabu alipokuwa chumba cha wagonjwa ICU, Hospitalini Moi, alisema, "Nilifika nyumbani kwangu kama saa 6 usiku nikitokea kazini tulikuwa tunafuatilia uchaguzi wa Kenya tukaona hamna la maana.

Nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu... Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kukimbia kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito... niliona kama watu 3 hivi...

Sikufahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti...mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti' ilikuwa kama vile imegoma.

Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha ktk vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba na kunitupa na wakaondoka, badaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.
 
Haya ni maneno yaliyotoka kwenye kinywa cha Kibanda mwenyewe, akieleza kuhusu mkasa uliompata (Source: Mwananchi). Kulingana na maelezo ya Kibanda, kilichomwokoa, ni hiyo bunduki kushindwa kutoa risasi, yaani ili-jam.

Sasa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema Jeshi la polisi limeunda timu ya maofisa 10 kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo, kwamba wanne wametoka Polisi Makao Makuu, watano kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam na mwingine anatoka Mkoa wa Kinondoni.

Kwani wanaosema "afande" zaidi ya polisi na wanajeshi ni nani?

Kwa hesabu ya haraka haraka, iweje hawa "maafande" watumike kupeleleza kitu ambacho ni wazi kiliamuliwa na "afande" mwenzao au wenzao?

Mchawi wa jaribio la kumuua Kibanda yuko ndani ya taasisi inayotumia neno "afande", na basi ni eidha Jeshi la Wananchi au Jeshi la Polisi, na niko tayari kuweka dau kwamba si Jeshi la Wananchi.

Basi kuna 'afande" mkubwa tu alitoa amri Kibanda ashughulikiwe, na sasa bila kujua huyo "afande" ni yupi, inaundwa timu ya "maafande" kupeleleza tukio hili? Vipi kama hiyo timu ndani yake kuna "afande" aliyetoa amri Kibanda ashughulikiwe?
 
Tume tume tume,kila siku tume jamani tumecoka na tume hizi ambazo matokeo yake huwa hatuyajui wala kuambiwa.
 
Jamani haya yanatokea tena hata vidonda mlivyotuachia havijapona......Ee Mungu uwalipe hawa wanyanyasaji stahiki ya matendo yao, kwani hata majonzi na machozi yametuisha.
 
Kuna chama kina makamanda je na wale pia maaskari, tutizame alipojikwaa sio alipoanguka.
 
Akizungumza kwa tabu alipokuwa chumba cha wagonjwa ICU, Hospitalini Moi, alisema, "Nilifika nyumbani kwangu kama saa 6 usiku nikitokea kazini tulikuwa tunafuatilia uchaguzi wa kenya tukaona hamna la maana.

Nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu... Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kukimbia kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito... niliona kama watu 3 hivi...

Sikufahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti...mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti' ilikuwa kama vile imegoma.

Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha ktk vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba na kunitupa na wakaondoka, badaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.

.......

Tunamshukuru Mungu aliyekuokoa na tunazidi kumuomba Mungu ili akuponye haraka.Amen
 
Haya ni maneno yaliyotoka kwenye kinywa cha Kibanda mwenyewe, akieleza kuhusu mkasa uliompata (Source: Mwananchi). Kulingana na maelezo ya Kibanda, kilichomwokoa, ni hiyo bunduki kushindwa kutoa risasi, yaani ili-jam.

Sasa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema Jeshi la polisi limeunda timu ya maofisa 10 kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo, kwamba wanne wametoka Polisi Makao Makuu, watano kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam na mwingine anatoka Mkoa wa Kinondoni.

Kwani wanaosema "afande" zaidi ya polisi na wanajeshi ni nani?

Kwa hesabu ya haraka haraka, iweje hawa "maafande" watumike kupeleleza kitu ambacho ni wazi kiliamuliwa na "afande" mwenzao au wenzao?

Mchawi wa jaribio la kumuua Kibanda yuko ndani ya taasisi inayotumia neno "afande", na basi ni eidha Jeshi la Wananchi au Jeshi la Polisi, na niko tayari kuweka dau kwamba si Jeshi la Wananchi.
Basi kuna 'afande" mkubwa tu alitoa amri Kibanda ashughulikiwe, na sasa bila kujua huyo "afande" ni yupi, inaundwa timu ya "maafande" kupeleleza tukio hili? Vipi kama hiyo tume ndani yake kuna "afande" aliyetoa amri Kibanda ashughulikiwe?

Na hizi kampuni za ulinzi binafsi hazilitumii hili neno?
 
hapa TZ hatujapimana nguvu kutakuwa hamna heshika kati ya raia na watawala let call for the war
 
Tanzania ndivyo ilivyo wanasema wanaunda tume itachunguza miezi hadi watu wasahau baadae mambo yanaisha kiswahili swahili
 
Mwana wa adamu anapigeuka kuwa mnyama ndipo haya hutokea, lakini nawaambia wale wote walioshiriki njama hizi HAKUNA TESO LA MWENYE HAKI LIKAKOSA JIBU.... Mungu ni mwema na hakika yake IKO PAMOJA NAWE uponywe nyama na mifupa yako kwa uweza wa mungu POKEA UZIMA... Poleni familia ni wakati wa kuomba uvumilivu kwa mungu nae yu pamoja nanyi
 
jamani watanzania kwanini tusisimame kwa pamoja na kusema sasa yatosha!! Jamani inawezekana? Tutayaangalia mambo ya kinyama kama haya mpaka lin??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom