Kesi ya ugaidi wa Mbowe: Uamuzi wa Jaji wa pingamizi la upande wa utetezi kesho unaweza kuja na haya....

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Leo kumejitokeza utata mwingine tena mahakamani kwa shahidi No. 8 wa Jamhuri Askari Polisi aitwaye Jumanne.

Kwamba, alipowakamata watuhumiwa na kuwapekua aka - seize [akachukua] mali za watuhumiwa kinyume cha sheria inayoongoza tendo hilo.

Sasa upande wa utetezi ume - OBJECT tendo hilo na kuitaka mahakama isiupokee ushahidi wa shahidi huyo kwa sababu umepatikana kinyume cha sheria.

Yaani utaratibu unamtaka aongozwe kutenda tendo hilo kwa sheria au kifungu cha sheria A yenye akatumia kifungu au sheria B. Hii kisheria inaitwa "wrong citation of the law"

Jaji amepata home work nyingine tena. Je, atawabeba Jamhuri tena kama Jaji Siyani alivyofanya katika pingamizi la kwanza na kumpelekea ajitoe kusikiliza kesi hii...?

NINI KITATOKEA IWAPO UAMUZI UKAWA KINYUME CHA SHERIA?

Mnaukumbuka wito wa Godbless Lema wa kutaka mawakili wa M/Kiti Freeman Mbowe kujitoa ktk kesi ili Jaji ahukumu apendavyo yeye kwa kadiri ya kile kinachodaiwa kuwa "kupokea maelekezo toka juu?"

Nadhani maamuzi ya Jaji kwenye OBJECTION hii yanaweza KUTIMILIZA HILI KESHO...!

Let's see and wait...
 
Niko nasikiliza #MariaSpace natumai kabla haijaisha Lema atazuka ili kuja kusisitiza tena umuhimu mkubwa wa kuondoa Mawakili kesho kama Jaji atafanya maamuzi kinyume na sheria za nchi.

Huyu jaji alishaanza kujichanganya toka juzi kwakuwa anatembea na hukumu ya serikali mfukoni, ila tulisema lazima ajae kwenye 18. Kesho ni lazima ajichanganye, hapo ndio maamuzi ya kuisusia mahakama yachukuliwe ASAP.
 
Niko nasikiliza #MariaSpace natumai kabla haijaisha Lema atazuka ili kuja kusisitiza tena umuhimu mkubwa wa kuondoa Mawakili kesho kama Jaji atafanya maamuzi kinyume na sheria za nchi.
Kabisa, hakuna haja ya kuwaendekeza hawa wahuni. Wanatembea na hukumu za kihuni hivyo ni bora kuwaumbua mapema.
 
Jaji leo amekumbana na mtego je nayeye ataitema kesi kama wengine? Kundi la Kina Kibatala ni kama kesi nzima wanaijua. Yaani maswali na hoja wanazotoa ni kama vile CD nzima ya kesi wanayo wanatupia mulemule yaani.

Citation ya sheria ambayo haipo ktk sheria zetu za nchi ni kosa lingine la dhahiri litamtia mashakani Jaji
 
 
Niko nasikiliza #MariaSpace natumai kabla haijaisha Lema atazuka ili kuja kusisitiza tena umuhimu mkubwa wa kuondoa Mawakili kesho kama Jaji atafanya maamuzi kinyume na sheria za nchi.
BAK please Marià space unafanuaje kuisikiliza? Napitwa na mengi
 
Lema huyu wa wizi wa magari ndio mnasubiria tamko lake

Huyo huyo ndiyo tunamsubiri, na hata asingesema tayari hiyo kesi tulishajua kuwa ni uhuni wa kitoto uzeeni. Ww endelea kula tikitimaji na cocacola hapa, lakini hiyo kesi ni uchafu kama uchafu mwingine.
 
Mimi nasikiliza kupitia Twitter. Inabidi uwe na account kule. Kuna pia wanaosikiliza kupitia utube na telegram lakini huko utaratibu wake siujui. Ukishakuwa na account Twitter basi mfollow Maria kule na kila siku za Jumatatu na Alhamisi utapata notification kuhusu uwepo wa Maria Space. Maria Space huanza 8:00pm EAT na kuendelea wakati mwingine hadi 01:00am au hata zaidi.

BAK please Marià space unafanuaje kuisikiliza? Napitwa na mengi
 
Back
Top Bottom