Kesi ya Thadey Kweka: Utawala wa sheria, hauruhusu vyombo vya uchunguzi na mahakama, kuvunja haki za kikatiba na sheria, katika utoaji hukumu zake

Emekha Ikhe

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
52
Reaction score
84
Nimesoma HUKUMU ya Kesi ya THADEY KWEKA ambayo imetolewa jana kinyemela hata bila yeye mwenyewe kujitetea au kutetewa na Mawakili wake tangu kukamatwa kwake, Ninasikitika Kuona kwamba hata Mahakama kupitia Hakimu imejielekeza Vibaya Kutoa HUKUMU husika

Raia Wanategemea Mahakama itende Haki na sio kushirikiana na Vyombo Vya Ukamataji na Uchunguzi kuminya Haki za KIKATIBA za Mtuhumiwa kama ambavyo nitaeleza Juu ya Sakata la THADEY KWEKA kama nyaraka zinavyojifafanua, binafsi nitaandika kwa ufupi na straight to the point

Kitendo cha Ofisi ya DPP kufungua kesi dhidi ya Mtuhumiwa (Thadey Kweka) ya kuitaka Mahakama kutoa Amri dhidi ya KWEKA ili atoe Nywila(Password) yake ili Polisi na Ofisi ya DPP kufanya Uchunguzi, na kesi Kusikilizwa na Mahakama hata bila Mtuhumiwa kupewa wito ili kuwepo kwa utetezi au kutetewa na Wakili wake, Kunaibua maswali Mengi ya kisheria dhidi ya Vyombo Vya Uchunguzi pamoja na Mahakama yenyewe

Mosi, Kesi umesikilizwa Upande mmoja kwa hati ya dharura bila mtuhumiwa wala Wakili wake kujulishwa kwa wito wa Mahakama huku kesi iliyofunguliwa ikiwa Inter-Parte Application (Kwamba Mtuhumiwa alipaswa kupewa wito kwa utetezi) na sio Exparte Application (Kwamba kesi isikilizwe Upande mmoja kulingana na nyaraka zilizofailiwa

Ukisoma Wito wa Mahakama( Chamber summons) hauonyeshi kwamba kesi hii ilikuwa ya Kusikilizwa Upande mmoja (Exparte Application) hivyo, Thadei alipaswa kuwakilishwa na Wakili au kujiwakilisha katika utetezi wake ili Kutekeleza Haki ya Asili ya Kusikilizwa inayolindwa na Katiba ya Nchi kabla ya Mahakama Kuja na Uamuzi uliotolewa

Bahati Mbaya sana Hakimu aliyetoa Uamuzi anakili kwamba kesi hii ilikuwa kwa hati ya dharura ili isikilizwe Upande mmoja kinyume na nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani na Hakimu anaamua kesi husika bila kutii Katiba ya Nchi na Sheria zake kama nitavyofafanua hapa;

Mahakama hazina Mamlaka ya ku-dis regard Haki za Msingi za Kikatiba mathalani haki ya Faragha (Right to privacy) bila Kutoa Haki ya Kusikilizwa kwa Mtuhumiwa (Principle of Natural Justice) kama ambavyo Hakimu alivyojielekeza vibaya katika Uamuzi wake unaopswa kukatiwa Rufaa haraka iwezekanavyo

Pia Kifungu cha 32 cha Sheria, Cyber Crime Act, licha ya kwamba Kifungu hiki kimeipa Mamlaka Mahakama Kutoa Amri husika, Sheria husika haijaipa Mamlaka Kufanya Maamuzi kwa KUVUNJA Sheria na Katiba ya Nchi, hususani kukinzana na matakwa ya Katiba juu ya Haki ya Kusikilizwa (Fair hearing) kabla ya uamuzi

Ifahamike kuwa, Polisi na DPP hawezi Kumkamata Mtuhumiwa kwa tuhuma hewa za jinai ( kupublish Taarifa za UONGO (False nformation) bila kuzitaja in specific kama Kifungu cha 32 cha Sheria ya Cyber crime Act kinavyotaka

Ni Bahati mbaya sana Hakimu huyu wa Mahakama(RMC) ametoa HUKUMU ya Amri ya Mtuhumiwa Kutoa nywila zake bila kujua ziitwazo Taarifa za UONGO ni zipi ambazo zilipelekea Mtuhumiwa kukamatwa kama Sheria inavyotaka

Ni takwa la Sheria zetu kwamba,Mahakama katika Kutoa HUKUMU au Uamuzi wake haswa katika kesi ya Jinai inapaswa kuongozwa kanuni ya kuthibitisha bila Shaka (Prove Beyond Reasonable drought), kwenye hili Mahakama imejielekeza Vibaya hivyo Uamuzi husika unapaswa kukatiwa Rufaa haraka

Hatuwezi tukawa na Mahakama ambazo Hakimu anaamua kesi ya Jinai bila kujua in specific( details za kosa (criminal offence), bila kumpa Haki Mtuhumiwa kujitetea au kutetewa na Wakili wake (Fair hearing) na Kutoa Maamuzi

Hii ruling inapaswa kukatiwa Rufaa haraka, Ni Muhimu Mahakama zetu kujiongoza vyema katika Kulinda Haki za Binadamu ambazo zinalundwa na Katiba ya Nchi yetu
 

Attachments

  • inbound6150996344563864447.jpg
    70.7 KB · Views: 10
  • inbound4300967958931106526.jpg
    189.6 KB · Views: 9
  • inbound6074964550284767534.jpg
    241 KB · Views: 9
  • inbound4658300855320504533.jpg
    159.3 KB · Views: 10
  • inbound9018582459540547332.jpg
    276 KB · Views: 7
  • inbound48069550307847023.jpg
    314.6 KB · Views: 5
  • inbound6518991479493533616.jpg
    313.8 KB · Views: 8
  • inbound4527793917683548279.jpg
    252 KB · Views: 13
Sasa mkuu hapo kuna utaratibu wa sheria kweli.

Zama hizi za google, you just need to type ‘the right to be represented by an attorney in tanzania law’ upate mtiririko wa sheria za Tanzania zinavyotaka hivyo.

Talking about theories of justice and the rights of defendants, is beyond many Tanzania lawyers comprehension.

Hawa ni watu ambao hata sheria zinazowaongoza hawazijui. Hili sakata litaisha pale US embassy litakapokomalia haki za raia wake, make no mistake that move is coming.
 
Nia yako ni njema; kutaarifu wasomaji juu ya swala ulilozungumzia; lakini kwa bahati mbaya sana umetumia maneno meeengi mno, ambayo hayakusaidia kamwe kufikisha ujumbe.

Ni kama unaelezea jambo ambalo kila msomaji wa mada yako analifahamu tayari, na wewe ni kama unatoa ufafanuzi tu wa jinsi mambo yalivyoendelea.

Huyo Kweka anashtakiwa kwa kosa gani; kwa mfano??

Ungetumia mstari mmoja au miwili kuhusu taarifa hiyo ya awali ingesaidia wasomaji wako kupata pa kuanzia kuelewa unachokizungumzia kwenye mada.

Nimejitahidi sana kusoma andiko lako hilo refu nikiwa na matumaini kwamba labda nitakutana na taarifa muhimu huko katikati ya andiko. Nilipofika katikati na kuendelea na mizunguko, nikakata tamaa kuendelea huko chini!
 
Sasa mkuu hapo kuna utaratibu wa sheria kweli.
Hivi Tanzania ni sehemu/maeneo gani ambako bado kunatumia/fuata "utaratibu wa sheria"?
Nikitizama taratibu zinazofuatwa na polisi katika utendaji wao, sioni sehemu ambayo wanafuata "utaratibu wa sheria"!

Hayta ukitazama mhimili wa Bunge; taratibu zao huko ni matakwa ya mtawala.

Ni wapi kunafuata taratibu za sheria, wakati hadi Katiba yenyewe (pamoja na ubovu wake wote) watu hawaoni umuhimu wake. Wangeona umuhimu wake pasingekuwepo na mambo mengi ya hovyo yanayofanyika nchini hivi sasa.
Kwa mfano, ni Katiba gani iliyowaruhusu kubadili tu jina la Tume ya Uchaguzi, na kuigeuza iwe "Tume Huru ya Uchaguzi" na kuwateua watu walewale kuwa watu Huru wa kusimamia uchaguzi huru!

Na bado hata hujazungumzia uchafu wa uchaguzi wa serikali za mitaa!
 
Tatizo zaidi viongozi wa kitaifa hawaoni najisi waliyoifanya.

Saa zingine kuna mambo unayaachia fate.
 
Nikitizama taratibu zinazofuatwa na polisi katika utendaji wao, sioni sehemu ambayo wanafuata "utaratibu wa sheria"!
Uko sahihi.
Polisi kiutendaji ni kama vile wako juu ya sheria.
Ukiangalia hata taarifa ambazo ilistahili zitolewe na waziri wa mambo ya ndani zinatolewa na polisi.
 
Hiyo simu wanavyong’ang’ania password zake kwa akili zao wanadhani watakuta mawasiliano yake na akina Maria Sarungi.
 
Wasomi wenzangu siku hizi naona sana neno 'complainant' kwenye case za jinai, mbona kama nazeeka
 
UPDATE 5: Kesi ya Thadei Kweka

December 31, 2025

1. Upande wa Jamuhuri wamepeleka Maombi (Ex-parte) Mahakaman kwa hati ya dharula na yamesikilizwa Upande mmoja bila Thadey Sabinus Kweka kuwepo Mahakaman ukizingatia kuwa yupo mikononi mwao.

2. ⁠Maombi hayo yanahusu kumtaka Thadey Sabinus Kweka kutoa Nywila (password) za simu yake ili Polis wafanye upelelezi.

3. Mahakama imetoa Amri kuwa Thadey Sabinus Kweka anatakiwa kutoa Nywila (password) za Simu yake ili Polisi wafanye uchunguzi.

4. Thadei ameshindwa kutoa password kwa sababu haikumbuki baada ya kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia tokea akamatwe. Zoezi la kutoa password limeshindikana hadi kesho Thadei akikumbuka password yake.

5. Polis bado wamemkatalia Thadei dhamana na kusaini consent forms kutoka ubalozi wa Marekani ili America iwe involved.

6. Thadei anashtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kwenye groups za ”what sup”. What sup hatujui ni Application gani haya Thadei mwenyewe haelewi!

Tutaendelea kuwapa taarifa.

#FreeThadeiKweka

Asante
 
Mkuu Eme, Emekha Ikhe. kwanza asante kwa hoja hii, naunga mkono hoja kwa asilimia 100% chini ya 100%.

Taifa letu tunakabiliwa na tatizo kubwa la wanasheria waliosomea sheria lakini hawaijui katiba, hawazijui sheria, hawajui haki, wala hawaujui wajibu wao, kuanzia mhimili wenyewe wa Mahakama, serikali na Bunge ndio maana kila uchao wanatutungia sheria kibao ambazo ni batili kinyume na katiba!.

Tukija kwenye mhimili wa Mahakama, huko ndio kwenye majanga, tuna baadhi ya mahakimu na majaji majanga wasijua haki kama nilivyoeleza hapa Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Dawa ya kulitibu gonjwa hili, ni mahakimu na majaji kuanzia CJ waombe kazi, wasailiwe, kama wanaijua katiba, sheria, haki na wajibu, wenye sifa ndio wateuliwe, hii itasaidia kupunguza majaji majanga!.

  1. Mtuhumiwa ni foreign subject, huwezi kumkataa raia wa nje, bila kuutaarifu ubalozi wake.
  2. Huwezi kumhoji mtuhumiwa bila legal representation
  3. Huwezi kuingilia his right to Privacy bila kwanza kumwambia tuhuma zake
  4. Makama haiwezi kumlazimisha kutoa password yake bila tuhuma specific
  5. Na hata ikitokea mfano kumtukana rais wa nchi kwa huku kwetu ni kosa la jinai, lakini kwa Marekani sio kosa, hivyo hata kama alimtukana rais wakati akiwa Marekani, alipokuja nchini, huwezi kumshitaki kwa kitu ambacho sio kosa kilipotendeka.
  6. Ila kama hiyo jinai ameifanyia Tanzania baada ya kurejea nyumbani, then ni kosa
  7. Wanatakiwa kuutaarifu ubalozi wake kuhusu makosa ya raia wao na kumpatia haki nyingine zote za kisheria ikiwemo the right to legal representation, the right to be heard, the right to fair hearing in a court of competent jurisdiction
Hii kesi isipokuwa handled kwa makini. sasa hivi nayo inaweza kutuchafua!, unaweza kuwachezea Watanzania kama kuwaua kama panya na usifanywe kitu, lakini huwezi kumfanyia hivi raia na Marekani ukabaki salama!.

P
P
 
Kama mihimili ya sheria yenyewe hafuati sheria unategemea nini?

Ndio hali iliopo nchini, wanaogopa nini kumpa mtuhumiwa haki yake ya kisheria
 

Tunaombwe Comrade, Bila Katiba Mpya itayoweka Misingi ya uhuru wa Mhimili wa Mahakama, hatutatoka hapa
 
Tunasafari Ngumu ya Kujifunga Mkanda Kupata Katiba Mpya itayoweka misingi ya Uhuru wa Mhimili wa Mahakama. Unapoona Mahakama inashirikiana na Wakamataji na Washitaki kwa kupuuza haki za binadamu ni hatari sana
 
Kaka Maridhiano juu ya Damu za watu badala ya Uwajibikaji wa wahusika ni dhambi kuu itayovutia ghafhabu ya MUNGU Kwa Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…