Kenya: Ndege mbili zagongana angani, wawili wafariki Dunia

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
GH5OKzTX0AA5PF8.png
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya imethibitisha kisa cha kugongana kwa ndege ya abiria ya kampuni ya Safarilink na ndege ya mazoezi.

Uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha ajili hiyo.

‘’Uchunguzi umeanza kupitia mashirika mbalimbali ukiongozwa na Idara ya Uchunguzi wa Ajali za Anga na Huduma ya Taifa ya Polisi kubaini chanzo cha ajali,’’ Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya imesema.

Abiria wawili waliokuwa kwenye ndege ya mazoezi wote wameaga dunia huku abiria 39 na wafanyakazi 5 katika ndege ya Safarilink wakiokolewa hadi eneo salama.

Shirika la ndege la Safarilink imesema kupitia mtandao waX kwamba muda mfupi baada ya kupaa mwendo wa saa tatu na dakika 45 asubuhi saa za eneo hilo, kishindo kikubwa kimesikika.

BBC
 
Ok Shukrani kwa taarifa wapumzike kwa amani huko kuzimu waendako
 
Daah poleni sana Kenya
 
Watu wawili wamefariki dunia katika ajali ya ndege mbili zilizogongana angani leo Jumanne asubuhi muda mfupi baada ya kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Wilson jijini Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa, ajali hiyo imehusisha ndege mbili, Dash-8 Safarilink iliyokuwa na watu 44 na ndege ya injini moja aina ya Cessna 172 inayomilikiwa na Chuo cha Urubani cha Ninety-Nines Flying School iliyokuwa na mwanafunzi wa urubani na mwalimu wake ambao wote wamefariki dunia.

Taarifa ya polisi imesema ndege hizo zimegongana angani huku ndege ya Dash-8 Safarilink ikipata mtikisiko na kuweza kurudi Uwanja wa Wilson kwa ajili ya uchunguzi.

Polisi wamesema mwalimu na mwanafunzi wake walikuwa kwenye kipindi cha kawaida cha mafunzo ya vitendo ya kurusha ndege angani.
 
Nimesikiliza kipindi cha Nipashe asubuhi ya leo 06.03.24 mtangazaji anasema watu wawili wamefariki kutokana na ndege mbili kugongana angani huko Kenya, lakini mtangazaji wa Kenya anasema ajali iliyouwa watu wawili ni ile ya mafunzo ambayo imeua Mkufunzi na mwanafunzi wake, ila hajasikika akisema ndege hizo zimegongana angani kama mlivyosema.
 
😅😅
 
Mkaangaa nyiko 🤣🤣
 
Zimegongana ndio kwani hujaelewa nini hapo?

Ndege ndogo aina ya Cessna 172 skyhawk imegongana na ndege kubwa aina ya Dash8 ya kampuni ya safarilink.

Cessna 172 kaanguka na kuua watu wawili, rubani mwanafunzi na mwalimu wake.

Safarilink plane Dash8 kafanikiwa kutua salama bila kusababisha madhara kwa abiria wake.

Yani hapo ni sawa digidigi kagonga tembo.
 
Ivi kale kamlio kabla ya taarifa ya habari bado n kale kale?

Nakumbuka miaka hiyo ukienda kwa bibi ni radio one tu imesetiwa na haijawahi kubadilishwa, ukitaka ugomvi na bibi fanya kutaka kubadilisha stesheni yake pendwa RADIO ONE.

Ukiwasha redio unachoruhusiwa kufanya ni kuongeza au kupunguza sauti tu.

Bibi hakuwa na saa wala hakujua kusoma ila yupo on time na anayajua majira mno, ile sayansi sijui ni ya aina gani akikwambia washa redio saa saba mchana imefika, ukiwasha kweli n ngoma saba kamili na kama haijafika basi ni kasoro dakika 2 au moja.

Wapumzike kwa amani waliofariki kwa ajali hiyo.
 
Back
Top Bottom