Kenya na Tanzania zarejesheana Vibali vya Safari za Ndege

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeruhusu tena vibali vya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) vya kuendesha safari za ndege za abiria kati ya Nairobi na Dar es salaam chini ya vifungu vya Haki za Uhuru wa Trafiki namba tatu na nne kuanzia January 22, 2024 na imetengua uamuzi wake wa jana.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema wametoa ruhusa hiyo baada ya uamuzi wa Mamlaka ya Anga ya Jamhuri ya Kenya kukubali ombi la Tanzania la Kenya kusafirisha mizigo yao yote kwa kutumia Kampuni ya Air Tanzania kuanzia leo January 16,2024 kwa kuzingatia Haki za Trafiki nambari tano kati ya Nairobi na Nchi za dunia ya tatu.

Itakumbukwa jana baada ya TCAA kutangaza zuio la KQ kutua Tanzania, saa chacha baadaye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba alinukuliwa akisema amefanya mazungumzo na Waziri mwenzake anayeshughulikia masuala ya kigeni Nchini Kenya, Musalia Mudavadi na wamekubaliana kumaliza sakata hilo ndani ya siku tatu.

Pia Soma:
- Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

- Kenya na Tanzania kusuluhisha Mzozo wa Safari za Ndege ndani ya Siku 3

Millard Ayo
 
kwakweli sikutegemea Kenya wasalimu amri mapema kiasi hiki

2E7CFCC2-3CB3-4AA3-B698-FD1902AD6B57.jpeg
A6C21708-FE2E-4402-95BE-F9C00F6C9046.jpeg
 
Yaani Tanzania mambo yetu yanafanyika very unprofessiona. But so far it's working to our advantage ..... Uzuri Kenya wanatuelewa hvyo inabidi twende tu.

Yaani Kenya na Tanzania imekuwa kama vile ni mtu na mkewe waliochokana kila siku vurugu tu.....!!
 
Sukari imepanda Bei kilo 5000. Kiko wapi hii ndio inagusa maisha ya watanganyika mpk vijijini uko.sukari sukari
 
Hivi Hawa wakikuyu huwa wanatuona sisi hamnazo? Hivi hawajui ni kwanini tunaitwa wabongo. Maana ya mbongo ni mtu anayeweza kukuchezea game of mind
Ita kuwa halikuwa agizo la Serikali ya Kenya.
Bali interest ya kikundi fulani. Tusi laumu serikali.
 
Sasa wewe unalamba Matako ya Johari ama ... Hivi wewe unaona ni professional kutoa barua kama hizo as Public Notes .....!!
jaribu kuficha ujinga wako kidogo...sasa ulitaka iwe siri ili wateja washtukizwe kuwa KQ wamekatisha safari za Nairobi-Dar kimya kimya? Watu wanapanga safari zao mapema hivyo ilikuwa muhimu kuwajulisha public ili waamue safari zako kulingana na taarifa waliyopewa....hata juzi hapa tumeona mabasi ya kilimanjaro yalipofungiwa kusafirisha abiria ila kwa kuwa abiria hawakuwa na taarifa walihaha sana wakati taarifa ilishatolewa mapema kwa wananchi.
 
Utaacha lini kuwalamba matako hao wakunya, another smartphone kwenye wrong hand.
Yaani ndege yao ya mizigo ije kwetu halafu ndege yetu ya mizigo wakatae iende kwao!
Wameanza wao sisi tukajibu.
Wakupuuzwa Huyo
 
Habari njema.
Kenya wajifunze kuwaheshimu majirani zake.
Hakuna cha maana tunachitegemea nchi ya Kenya, ingawa wao wana mahitaji mengi toka Tanzania.
 
Back
Top Bottom