Basi la Saratoga lapata ajali Kibaha. Wawili wafariki dunia

wakukurupuka1

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
525
1,182
IMG_7352.jpg


Sizaweza kuleta taarifa kwa sababu bado mamlaka husika zimeficha hii taarifa.

Watu kadhaa wamefariki hapohapo.

--
Ajali Basi la Kampuni ya Saratoga Line lililokuwa likitokea Kigoma nakuelekea Dar es salaam limepata Ajali maeneo ya Tanita karibu na Kibaha kwa Mathias majira ya saa 9 Usiku. Ajali hiyo imehusisha Lori la mafuta mali ya kampuni ya Asasi pamoja Fuso.

--
WATU WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI, LORI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema “Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo (Julai 26, 2023) ikihusisha Basi la Kampuni ya Saratoga Line likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam limegongana na gari lingine Lori aina ya Howo na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo dereva wa basi pamoja na majeruhi watatu.

“Miili imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha majeruhi wamelazwa katika hospitali hiyo wakiendelea na matibabu.

“Chanzo ni uzembe wa Dereva wa Basi ambaye alikuwa akiyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na hivyo kujikuta akiligonga Lori ubavuni lililokuwa mbele yake, kwa asilimia kubwa basi ndilo ambalo limepata madhara zaidi kwa kuharibika sehemu ya mbele.”

 
DEREVA ANAENDESHA OVYO,ABIRIA MMEKAA NDANI TU KAMA MABOGA
MNASHINDWA MKEMEA
NDANI MKIWEKEWA MIZIKI SINGELI AMAPIANO NA MOVIE MMEONA MMEFIKA...
NYIE ENDELEENI KUSEMA AJALI ILIPANGWA NA NI KAZI YA MUNGU

MTAZIDI KUCHINJWA KUNGURUUU NYIEE

ova
 
Back
Top Bottom