saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,173
- 6,157
Siku za karibuni Rais alifanya mabadiliko madogo kwa makatibu wakuu ambapo ndg. Adolf Ndunguru alipelekwa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.
Huyu bwana tangia aingie katika ile ofisi alikuta tayari kuna watumishi walishapata uhamisho hasa wale wa kubalishana vituo vya kazi. Jambo la ajabu amezuia uhamisho husika kwasababu anazojua yeye.
Mtu anapoomba uhamisho ana sababu za msingi, na hasa kama ametimiza masharti na vigezo vilivyowekwa na serikali kwanini atokee mtu moja kwa maslahi yake na kwa jeuri tu kisa ana madaraka anaamua kuzuia pasipo sababu zozote?
Hii ni roho mbaya ya kikatili, ni matumizi mabaya ya madaraka uliyokasimiwa na mheshimiwa rais. Anapata faida gani kuzuia huo uhamisho. Hivi serikali haifanyi vetting ya kutosha kabla ya kuwapa hawa watu madaraka makubwa yanayoumiza maisha ya watu?
Ndg. Adolf Ndunguru katoe hayo majina maisha ya watu yaendelee kwa furaha na amani, iache hiyo kiburi na jeuri huo ni utumishi wa umma na ni wa muda tu.