Waziri Simbachawene: Saini feki za Katibu Mkuu UTUMISHI na TAMISEMI zinatumika kuhamisha watumishi vituo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Serikali imebaini baadhi ya watumishi wa umma wanatumia njia za udanganyifu na nyaraka za kughushi mtandaoni, ili kufanikisha uhamisho wa vituo vya kazi pasipo kuridhiwa na mamlaka husika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Wilaya ya Geita.

Amesema taarifa za awali zinaeleza watumishi wanaofanya vitendo vya aina hiyo hushirikiana na maofisa wa wizara wasio waaminifu, ambapo ufuatiliaji unaendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria.

“Tumeanza na tumeshagundua wenye uhamisho feki, wengine wanapewa ruksa kwa kupigiwa simu na watu wanaojifanya wapo Tamisemi, wengine wanapigiwa simu na watu wanaojifanya wapo Utumishi.

“Saini zinazotumika ni za makatibu wakuu wawili, Katibu Mkuu Utumishi na Katibu Mkuu Tamisemi, lakini uhamisho huo ni feki, na kinachokuja kusumbua ni pale wanapotaka kuhamisha mshahara,” amesema.

Amebainisha uhamisho wa aina hiyo unakuwa hautambuliki na haujaridhiwa na Katibu Mkuu Tamisemi na Katibu Mkuu Utumishi.

Pia soma

# TAMISEMI tufahamisheni, lazima Mtumishi alipie fedha ili apate uhamisho?
# Hongera Mchengerwa kuwa waziri TAMISEMI. Nakuomba yatazame haya, vibali vya uhamisho vina urasimu mkubwa
 
Back
Top Bottom