Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,271
- 2,025
Wadau nawasalimu, hebu tukumbushane kidogo.
Katiba iliyopo ya mwaka 1977 ilitungwa na kuandikwa na makada 40 wa chama kwa mgawanyo wa makada 20 kutoka Tanganyika na makada 20 kutoka Zanzibar.
Mwenyekiti wa jopo hili alikuwa Sheikh Thabit Kombo na Katibu wake alikuwa Mzee Pius Msekwa. Watu hawa 40 walipomaliza kuandika waliyoyataka wao na chama chao mchakato ukaenda bungeni badala ya kuupeleka kwa wananchi ambao kimsingi ndio wenye Katiba yao ukapitishwa ukawa sheria kwa ufupi ni Katiba ya Viongozi.
Hivi sasa wananchi tunataka Katiba ya Wananchi tuipendekeze wenyewe kwa jinsi tunavyoona inafaa kwetu na kwa viongozi wetu. Katiba ambayo itainua uchumi wa wananchi wote bila ubaguzi Katiba ambayo itatenda haki kwa vyama vyote katiba ambayo itasimamia chaguzi zote kwa haki
Katiba ambayo haitakuwa na upendeleo kwa makundi fulani kimaslahi lakini CCM ni kama haitaki kuwepo kwa Katiba ya Wananchi kwani kumekuwa na tume nyingi zilipendekeza hilo suala Rais Mstaafu Kikwete alianzisha mchakato wa Katiba Mpya lakini nao CCM kupitia wabunge wake wakauharibu.
Magufuli yeye aligoma kabisa kuusikia kwa kusema sio kipaumbele na Mama Samia akaturudisha tena nyuma eti tusome Elimu ya Katiba. Zote hizi ni hila za CCM kukataa Katiba ya Wananchi!
Ukweli wananchi tunataka Katiba ya Wananchi sio ile ya makada 40.