Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Tofauti ya Mr. Clean na Handsome boy ni uimara na udhaifu wa TZS dhidi ya $.

Ni kweli Kipindi cha Mkwere shilingi ya Tanzania imeshuka sana thamani yake tofauti na enzi ya BWM bei za bidhaa zimepanda kweli kweli.

Kwa ufupi toka Mkwere ashike dola shilingi ya Tanzania imepungua thamani kulinganisha na dola,ukuaji wa uchumi umekuwa ukisua sua sana na maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.Kazi kuuza sura tu
 
Tutmie vigezo tu, vigezo vyenyewe viwe vifuatavyo:
1. Utawala wa sheria na haki...wakati gani raia wameonewa sana bila sababu..kuuwa (1998,2001)?
2. Matumizi mabaya madaraka..Wakati gani pesa za umma zimechotwa sana a.k.a sheria mbovu za madini na mikataba mibovu ya tanesco?
3. Ujenzi wa barabara kiwango cha lami..nenda wizarani uone kilometer zilizojengwa wakati wa Mkapa na JK ..utashangaa mkuu
4. Ujenzi wa shule na hospitali ..utashangaa mkuu...

JK yuko mbali sana Mkapa ..du unahitaji moyo wa chuma kumtetea.
 
You don't know the value of what you have till you loose it.
 
mkapa ni kiboko kwani msingi aliouacha utakumbukwa siku zote katika hii nchi yetu,kulikuwa na heshima kwa serikali sio sasa hivi serikali hadi Raisi anadharaulika kwa kila mtu(zaidi sana baada ya uchakachuaji) ,na hii nchi inaonekana wazi kabisa kuwa haina uongozi kwa sasa labda tusubirie 2015
 
Ni wakati gani serikali imeingia mikatba mibovu ya madini? (mkapa)

Ni wakati gani serikali imeuza nyumba zake kwa bei bure? (mkapa)

Ni wakati gani wananchi walioandamana kwa haki kuuwa na polisi? (mkapa)

Ni wakati gani kila mwezi navunja TV kumwona jitu gumu linagombeza watu kwenye TV (mkapa)

Mkapa rais bora sana kupita JK...basi ana roho nzuri, isitoshe wametuambia makasisi hivyo damn

mwenye akili timamu hapati wakati mgumu kukuelewa unafikiria nini,sana sana kwa maneno matano uliyomalizia nayo. Jitaidi kujibu mada,mwisho karibu JF naona uko active maana una cku3 ila hoja kubwa,ila kuna wa2 wanaongezea: uuaji wa raia,naona hii pia ingekuwa thread maana naona watu wameishikia bango!
 
Tutmie vigezo tu, vigezo vyenyewe viwe vifuatavyo:
1. Utawala wa sheria na haki...wakati gani raia wameonewa sana bila sababu..kuuwa (1998,2001)?
2. Matumizi mabaya madaraka..Wakati gani pesa za umma zimechotwa sana a.k.a sheria mbovu za madini na mikataba mibovu ya tanesco?
3. Ujenzi wa barabara kiwango cha lami..nenda wizarani uone kilometer zilizojengwa wakati wa Mkapa na JK ..utashangaa mkuu
4. Ujenzi wa shule na hospitali ..utashangaa mkuu...

JK yuko mbali sana Mkapa ..du unahitaji moyo wa chuma kumtetea.

Kama kuna doa nalikumbuka na sitalisahau kuhusu Mr. Clean ni suala la 'Wapemba'

Tatizo la Mkwere ni kuwa he is too ceremonial. Ameruhusu wasaidizi wake kucheza naye 'mchezo wa paka na panya'. Anaagiza hivi, wanafanya vile au hawafanyi kabisa.

too bad for him(Mkwere)
 
We vipi
Hata kama ni mgeni wewe umepitiliza.hiyo link una maana ipi

Teh teh teh! Ukifungua hiyo link halalfu ukirudi kuangalia jina la mwanzisha thread, unapata jibu. Naona tuko kwenye mtumbwi mmoja, Maamuma na Mbumbumbu.
 
Ni wakati gani serikali imeingia mikatba mibovu ya madini? (mkapa)

Ni wakati gani serikali imeuza nyumba zake kwa bei bure? (mkapa)

Ni wakati gani wananchi walioandamana kwa haki kuuwa na polisi? (mkapa)

Ni wakati gani kila mwezi navunja TV kumwona jitu gumu linagombeza watu kwenye TV (mkapa)

Mkapa rais bora sana kupita JK...basi ana roho nzuri, isitoshe wametuambia makasisi hivyo damn

mwenye akili timamu hapati wakati mgumu kukuelewa unafikiria nini,sana sana kwa maneno matano uliyomalizia nayo. Jitaidi kujibu mada.

Huyu jamaa Topical ni mdini haangalii hoja analeta udini
 
Kuna maneno ya chini chini mtaani kwangu Tandale Kuzuri kwamba Mkapa alikuwa na utawala bora https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon14.pngkuliko 'handsome adult'.... imekaa vipi kwako???
Ukifuata matakwa ya wananchi Mkapa ni bora kuliko JK. Mkapa aliingia kwa ushindi wa 61% bila kuchakachua na hata neno uchakachuaji halikuwepo, Mkapa huyo huyo akarudi kwa 80%. JK aliingia kwa 81% bila kuchakachua na JK huyohuyo karudi kwa 61% baada ya kuchakachua kura. Kwahiyo ukifuata kipimo cha wananchi kupitia sanduku la kura Mkapa ni bora kuliko JK.
 
Kuna maneno ya chini chini mtaani kwangu Tandale Kuzuri kwamba Mkapa alikuwa na utawala bora https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon14.pngkuliko 'handsome adult'.... imekaa vipi kwako???

Ndani ya CCM hakuna aliyemzidi mwenzake kwani sie tuna msemo tunaosema wanapokezana vijiti. Kumaliza kwa mmoja ndipo kuanza kwa mwingine. Kwa hiyo iliyo bora CCM na si Mkapa wala Kikwete. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE. Tanzania bila CCM HAIWEZEKANIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
 
We Mbumbumbu
Nimekuzuia kujadili watu.Hata hivo kwa vile umeuliza unataka jibu.Ubora kwa lipi? Hesabu magazeti mangapi yalifungiwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Watu wangapi wlinyanganywa uraia kwa kuonekana ni tishio kwa serikali wakati wa Mkapa na Kikwete.Kesi ngapi za ufisadi zilifunguliwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Wtz wangapi waliuawa na polisi kwa sababu za kisiasa na kidini wakati wa Mkapa na Kikwete.Vyuo vikuu vingapi vilifunguliwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Shule ngapi za Sekondari zilianzishwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Majibu ya haya na mengine mengi yatakupa jibu la ni yupi bora

Hakuna aliye bora. Wote ni sawa tu. Uzuri wa Mkapa ni kwamba angalau anaweza kuonyesha kwa mkono na kugusa yale aliyoyafanya. Huyo mwingine atakuonyesha kwenye makaratasi tu.
 
Oya we kiboko sema suuu nikutaje! siamini kama una id mpya...
 
Mkapa was BAD.... JK is WORST!!!!.... Hafai hata kwa kulumangia!!!...
 
Msihangaike kutafuta nani bora kati yao HAKUNA,juzi tu mungu ametupa chance ya kumpata rais bora wa kihistoria tumempoteza kwa ujinga wetu sasa hivi tunabishana kulinganisha vipofu wawili,nonsense wote hao hakuna alie bora ni KOKOTO tu
 
Between two evils I will choose the lesser. Mkapa was the lesser evil.
 
Mie nadhani Rais bora kuliko wote ni Silaa, kwani kuchukuwa wake za watu itakuwa RUKSA.
 
Ila ni hv tusipochukua hatua tutabakia na sera za kulinganisha mafisadi eti nani bora ni ufinyu wa mawazo watanganyika tuamke, huu sio muda wa blablaa,fikiria tz ya kesho itakuwaje
 
Between two evils I will choose the lesser. Mkapa was the lesser evil.

Nakubaliana na wewe Mkuu. Kama ni lazima kuchagua kati ya waovu wawili basi bora Mkapa. Alikuwa anauma na kupulizia kidogo, huyu wa sasa hapulizi hata kidogo, duh!
 
Back
Top Bottom