Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Mie nadhani Rais bora kuliko wote ni Silaa, kwani kuchukuwa wake za watu itakuwa RUKSA.


mimi ninakushangaa malaria sugu na hadithi yako ya slaa na wakeze.

mbona una wivu na josephine?

unamtaka slaa?

angalia kijana utaumia!
 
Kumbe ni taka usitake..sawa kwa vigezo vyako..JK ni bora kwa vigezo vyetu..tutakesha hapa mkuu hakuna mshindi..utaishia kusema wamechakachua...crying..

JK anampita kwa mbali Mkapa

Wewe huna jipya! Hahahahahaaaaaaaaa! Kwa lipi? Rais wako hana Jipya! Tunatamani hiyo miaka mitano iishe haraka.
 
Ukifuata matakwa ya wananchi Mkapa ni bora kuliko JK. Mkapa aliingia kwa ushindi wa 61% bila kuchakachua na hata neno uchakachuaji halikuwepo, Mkapa huyo huyo akarudi kwa 80%. JK aliingia kwa 81% bila kuchakachua na JK huyohuyo karudi kwa 61% baada ya kuchakachua kura. Kwahiyo ukifuata kipimo cha wananchi kupitia sanduku la kura Mkapa ni bora kuliko JK.

Mkuu hapa kwa bahati mbaya hamtumjui Mode anatumwa na nani pengine usalama wa Taifa,na kwa niaba ya viapo vyetu.
Please kaka kuhusu kitu uchaguzi mkuu acha kama ulivyo SIRI YA MTUNGI.au kamuulize Mh.Mrema atakupa jibu zuri tu.
 
Kwa kweli naona sasa mnajadili mada za HOVYO HOVYO.. vilaza hawa wawili mnaojadili HAMNA MWENYE umuhimu wa kujadiliwa .... WOOTE HAO HAMNA KITU... ni kama PIPA na MFUNIKO. Tuamieni kwenye thread nyingine.
 
Dunia ya leo, mahali pote, kiongozi mzuri ni mtu anayeweza kufanya wananchi wake waishi vizuri. Na hilo huelezwa kwa uimara wa uchumi na usalama wa Raia.

Kuna nchi ambazo demokrasia zake ni za mashaka sana. Nchi kama za kiarabu karibu zote hazina mifumo ya kidemokrasia inayokubalika kimataifa lakini zinaheshimika na wananchi wake wanaridhika kwa namna fulani kutokana na uchumi imara. Kwa upande mwingine hata ufanye nini kama uchumi wa nchi yako ni dhaifu inakuwa ni vigumu sana kuwashawishi watu kuwa wewe ni kiongozi mzuri.

JK si mdemokrasia ila ni kiongozi mwoga, mwenye uso wa aibu wa kukabiliana na wale wanaotenda kinyume na matakwa yake. Ni hali hiyo hiyo ndiyo inayomfanya asiweze kuchukua hatua za kidekteta moja kwa moja kwa magazeti yanayoandika asiyoyataka kwa hofu tu ya kuonekana vibaya machoni pa mataifa ya nje. Kushindwa kwake kuujenga uchumi imara ni dosari kubwa sana, hata afanye nini, kutokana na kuvurunda kwenye uchumi, kamwe hataweza kuwa kiongozi bora ukimlinganisha na mtangulizi wake.

Mkapa aliweka rekodi katika ulimwengu kwa kuujenga uchumi wa Tanzania baada ya kuparanganyika kabisa katika kipindi cha mwisho cha Mzee Mwinyi ambapo mfumuko wa bei ulipanda mpaka kufika 30%. Mkapa aliushusha mpaka 4%, hiyo ilikuwa ni record ambayo mataifa mengi hayajawahi kufikia.

Udhaifu wa Mkapa ni kuwa alifanya yote kwa utashi wake binafsi lakini hakuondoka akiwa ameacha mfumo imara wa kuhakikisha haturudi alikotuacha Mwinyi. Mapungufu yake mengine ni kwamba ujambaza kipindi cha uongozi wake ulikuwa wa kiwango cha juu sana kiasi cha kuwafanya watu wote kuishi kwa mashaka makubwa.

JK alipoingia, aliendesha mambo kwa utashi binafsi, akapandisha mfumuko wa bei mpaka kipindi kingine kufikia 17%! Mafanikio yake makubwa ni kuwa aliweza kupunguza kwa kiwango kikubwa hali ya ujambazi. Lakini ameonesha kupwaya sana katika mambo mengi kiasi cha kushindwa kueleweka tatizo lake kubwa ni nini maana mambo aliyoyafanya imekuwa ni kama mtu aliyeingia kwenye utawala kwa mara ya kwanza licha ya kuwepo kwenye nafasi mbalimbali kwa miaka mingi.

Kwa kipimo cha uchumi, ukimlinganisha Mkapa na JK, Mkapa ni malaika.
 
kwangu mie naona wote ni bure tu. Hakuna aliyeleta unafuu katika maisha ya mtanzania. Mkapa alipata hela za kuendeshea serikali yake kwa kuuza kila kitu chetu na kumwacha kikwete hana cha kuuza. Kwa vile hawakuwa na mipango ya kujenga cuhumi self sustaining, nchi bado inahanja na itaendelea hivyo mpaka mwisho wa utawala wa Kikwete.
 
katika wote hao MZEE RUKSA ndie bora!alitufumbua macho wananchi wakajenga academic schools tv magazeti vitu tele madukani sikukuu kibao kuzilipia siku za j3 na j4 magari unachagua mwenyewe JABA bot kukusanya gold, saa 4 asubuhi kila mtu anapesa mfukoni na bia sh 200 stella artois mkononi!wacha wee mzee ruksa balaa!mikocheni mbezi beach sinza tegeta tabata zimejengwa wakati wa mwinyi
 
I beg to differ. How do you compare these presidents if Tanzania is still in the same state or worse than it is from the time they took office to the time they left office? Mkapa did well with the economy in his first term but ruined it in his second time. That is the same as building a house then demolishing it. It is the same as having never build it at all. Kikwete so far has done nothing meaningful.

So here I see a president who build a house then demolished it and another president who has not build a house at all. How is one better than the other?
 
Ni wakati gani serikali imeingia mikatba mibovu ya madini? (mkapa)

Ni wakati gani serikali imeuza nyumba zake kwa bei bure? (mkapa)

Ni wakati gani wananchi walioandamana kwa haki kuuwa na polisi? (mkapa)

Ni wakati gani kila mwezi navunja TV kumwona jitu gumu linagombeza watu kwenye TV (mkapa)

Mkapa rais bora sana kupita JK...basi ana roho nzuri, isitoshe wametuambia makasisi hivyo damn

namema wakati wa mkapa hapakuwa na inflation kubwa, hapakuwa na migomo kila kona, hapakuwa na ziara nyingi za nje, hapakuwa na waheshimiwa kuzomewa au kupondwa mawe kwenye misafara etc:brick:
 
tumbili = kima = ngedere..
mkapa = kikwete = pinda



wale wale kasoro majina na form
 
mimi ninakushangaa malaria sugu na hadithi yako ya slaa na wakeze.

mbona una wivu na josephine?

unamtaka slaa?

angalia kijana utaumia!

Duh. Kwanza mimi sio MS hilo umekosea.

Pili, umepatia, nna wivu ile mbaya, kwa exPadrii kuwa na mke wake wa ndoa na mke wa mtu na kanisa limekaa kimya. Kwa hilo, namuonea wivu ile mbaya.

Tatu, la kumtaka Josephine. Duh, hanifai hata chembe, uzuri hana, shepu hana.

Mie nna wangu nyumbani. Bukheyrii, sina haja ya mke wa mtu. Isitoshe, nna Ruksa original ya kuchukuwa kihalali mpaka wanne.
 
Mimi nitapima baada ya jmk kumaliza miaka kumi. Ila kwa mwelekeo jk atamzidi bwm.
 
Mkapa is the best president among tanzania presidents, mtoe Mwl J.K Nyerere
 
Ndani ya CCM hakuna aliyemzidi mwenzake kwani sie tuna msemo tunaosema wanapokezana vijiti. Kumaliza kwa mmoja ndipo kuanza kwa mwingine. Kwa hiyo iliyo bora CCM na si Mkapa wala Kikwete. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE. Tanzania bila CCM HAIWEZEKANIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.

Mkuu naichukia ccm kama kifo ila nimependa jinsi ulivyowakilisha hoja yako. Sio kama kina MS (mfalme wa pumba),DSM,na Topical,wanakazia udini tu.
 
Ndani ya CCM hakuna aliyemzidi mwenzake kwani sie tuna msemo tunaosema wanapokezana vijiti. Kumaliza kwa mmoja ndipo kuanza kwa mwingine. Kwa hiyo iliyo bora CCM na si Mkapa wala Kikwete. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE. Tanzania bila CCM HAIWEZEKANIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
Rais bora alikuwa Mwinyi tuu. Nyerere, Mkapa na Kikwete wote hawajui uchumi
 
Ndani ya CCM hakuna aliyemzidi mwenzake kwani sie tuna msemo tunaosema wanapokezana vijiti. Kumaliza kwa mmoja ndipo kuanza kwa mwingine. Kwa hiyo iliyo bora CCM na si Mkapa wala Kikwete. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE. Tanzania bila CCM HAIWEZEKANIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.

Kumbe siyo mpaka uwe umelazwa milembe ndo watu wajue afya yako, hata fikra kama hizi zinatosha kudhihirisha hali halisi ya afya yako!!!
 
MKAPA ni bora kuliko hawa vilaza wengine, ndo maaana walimuita FARU sasa huyu sijui anaitwa swala au digidig bado sijajua!!!
 
Maybe the simple question would be, yupi kati yao alipunguza umaskini, aka empower the locals ili wamiliki uchumi wa nchi, shilingi ikapanda, akadhibiti rushwa na upotevu wa mali za umma, akapandisha kiwango cha elimu na afya n.k. na mwishowe tukapata maisha bora?
 
Humu JF hata kama JK angefanya nini sidhani kama kuna mtu angesema, kwani wako kidini zaid ndo maana hata Dr. Dau alipopata ISSA-Geneva wakasema amechanguliwa kwa sababu ni waislam wenzao.
Mkapa kafanya mengi mazuri japokuwa madhaifu pia ni mengi kama mauaji ya raia, mikataba mibovu yamadini, kuuza mashira muhimu ya umma (eg NBC) amnbayo yalikuwa yanajiendesha hata kwa faida, ufisadi mwingi.
Kikwete naye anamadhaifu yake kama kuwafumbia macho mafisadi wa mkapa kama akina chenge, lakini kuna mazuri mengi tu aliyofanya kuliko ya mkapa hata hizo barabara, ulizeni watu wa Tanroad, miaka 10 Mkapa alijenga km ngapi za lami na miaka 5 Kikwete amejenga KM ngapi tuache ushabiki wakijinga. uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa vyama vya upinzani na mengine mengi.
 
Wote wawili hawafai hata kidogo! Wameshindwa kukidhi malengo ya watanzania katika kuongeza nishati; miundombinu ya barabara na kuimarisha utafiti. Huwezi kuendelea kwa kutoa 0.05% ya gdp kwenye utafiti.
Mkuu wa nchi huwezi kutoa elfu ishirini ishirini [mabilioni ya kikwete] ukidai unawawezesha wajasiliamali au; huwezi kugawa matrekta [tiller] ukisema unakuza kilimo badala ya kuutangazia umma kuwa umepata soko la zao fulani la kilimo!
We need a structural change of this nation. Tunahitaji kiongozi atakayeingalia tanzania katika miaka hamsini au at least 25 ijayo badala ya hawa wanaoingalia katika miezi sita sita!
 
Back
Top Bottom