Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Pilato2006

Senior Member
Aug 25, 2008
125
225
Mkapa tutamkumbuka kwa yafuatayo
1 Daraja la Mkapa la kuunganisha mikoa ya kusini
2 Uwanja wa michezo wa kisasa
3 Maji ya ziwa victoria kwenda Shinyanga na Kahama
4 Mabarabara mengi yalijengwa kwa kiwango cha rami
5 Uchumi uliimalika
6 Mfumuko wa bei ulipungua
7 Kodi ziliongezeka

Mh. Kikwete katika miaka 4 tumkumbuke kwa yapi? Orozesha hapa!!!
 
Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,183
1,250
Nasisitiza tena kwa yepi hatutamsahau kaka Ben kabla sijamwaga razi hapa.
 
Gelange Vidunda

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
313
195
Mkapa used the first 5 years of his reign to build a legacy, and the last 5 to go into private business knowing well that he had done good the first term.

Kikwete is spending the first 5 years of turmoil, fracas, challenges, and kuwaridhisha waliomuweka pale Ikulu, and the last 5 years is currently unknown but I have a feeling he will come out and build his legacy then (unless you think he and CCM won't get re-elected.....but that's completely another topic nyingine kabisaaa!!)
 
Hume

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
342
250
Mpaka sasa mi sijaona la maana sana ambalo limefanyika kipindi hiki litakalonifanya nimkumbuke Mh Kikwete zaidi ya bla blaa ambazo hazilast!

Zaidi nitamkumbuka kwa maagizo yake ambayo hayatekelezwi na wasaidizi wake na yeye kukaa kimya mfano Elimu: Aliagiza wanaosomea udaktari na Ualimu wapate mkopo 100%, Haikufanyika
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Kikwete alikuta tuna sekondari ngapi kila KATA? Dodoma ilikuwa na Chuo Kikuu? Uhuru wa kuandika, kutoa maoni umekua sana (Mengi na Mafisadi PAPA, Rostam na Fisadi NYANGUMI na mimi naandaa orodha ya Fisadi KAMONGO), jana alionekana akikikumbuka kilimo( ingawa wakulima wenyewe hawakuwepo)....Kumbuka pia kwamba JK hata miaka mitano hajamaliza.
 
MEM ya mkapa hakuna aliyefungwa kwa kushindwa kuchangia, na wala watu hawakubanwa wala kulazimika kuchangia. Uliza Hizo sekondary za kata wangapi walifungwa kwa kukosa hela za kuchanga.

Jana alikuwa anatafuta watu wa kutafuna yale mabililioni ya EPA aliyosema anayapeleka kwenye kilimo, wakulima hawana lao kwani meno wanayo?
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,589

Kwenye bold. Hizo ni siasa hakuna ufuatiliaji!!!!! Je na njia za kuwezesha (funding) kulipa 100% mikopo kwa wanaosomea ualimu na udaktari alitoa (au wataalaam wake??). Siasa bana, we acha tu.
 
Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
6,984
2,000
Mkapa tutamkumbuka kwa yafuatayo
1 Daraja la Mkapa la kuunganisha mikoa ya kusini
2 Uwanja wa michezo wa kisasa
3 Maji ya ziwa victoria kwenda Shinyanga na Kahama
4 Mabarabara mengi yalijengwa kwa kiwango cha rami
5 Uchumi uliimalika
6 Mfumuko wa bei ulipungua
7 Kodi ziliongezeka

Mh. Kikwete katika miaka 4 tumkumbuke kwa yapi? Orozesha hapa!!!

Watu wanaogopa sana kumsifia Mkapa hata pale alipofanya mambo mazuri kabisa,....tuache hizo haki yake tumpe kama tunavyo mpa lawama.

Mazuri ya Jk;
-Kutabasamu mfululizo...inasaidia sana kwa mwenye njaa kujisikia angalau anachekelewa!
-Machinga complex..
UDOM...Chuo kikuu cha Dom
-Kupeleka majeshi comoro kukomboa kisiwa
-Kutowasaidia wapinga ufisadi maana wavuruga utwala wa sheria
-Kutembelea wafungwa
n.k
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
MEM ya mkapa hakuna aliyefungwa kwa kushindwa kuchangia, na wala watu hawakubanwa wala kulazimika kuchangia. Uliza Hizo sekondary za kata wangapi walifungwa kwa kukosa hela za kuchanga.

Jana alikuwa anatafuta watu wa kutafuna yale mabililioni ya EPA aliyosema anayapeleka kwenye kilimo, wakulima hawana lao kwani meno wanayo?
Pamoja na MMEM, Mkapa ameacha shule nyingi tu hazina madarasa, madawati,....JK amekikumbuka KILIMO ambacho ndicho AJIRA na UHAI wa Watanzania walio wengi. Utekelezaji wake ndio utakuwa tatizo kama ambavyo tumeshindwa huko nyuma tukaua mashirika yote ya UMMA, tukaua VYAMA VYA USHIRIKA na sasa isingekuwa ruzuku ya serikali kuu, Halimashauri, miji, manispaa, majiji tungeshayaua! Tufike mahala tusiangalie RAIS pekee yake, tujiangalie na sisi wenyewe.
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,764
2,000
Kikwete anatakiwa kukaza buti,hatuna la kumkumbuka zaidi wanamtandao,na kutoa vyeo kwa ndugu zake na marafiki
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,764
2,000
Kikwete alikuta tuna sekondari ngapi kila KATA? Dodoma ilikuwa na Chuo Kikuu? Uhuru wa kuandika, kutoa maoni umekua sana (Mengi na Mafisadi PAPA, Rostam na Fisadi NYANGUMI na mimi naandaa orodha ya Fisadi KAMONGO), jana alionekana akikikumbuka kilimo( ingawa wakulima wenyewe hawakuwepo)....Kumbuka pia kwamba JK hata miaka mitano hajamaliza.

kumbuka hizo sekondari zimejengwa kwa fedha ya msamaha wa madeni kazi ambayo Mkapa alipambana kuomba wafadhili wafute deni la Tanzania na nidhami aliyoionyesha ya kuanza kulipa madeni

Mkapa ndio aliye ruhusu Jengo la chimwaga liwe chuo kikuu cha Dodoma akaweka na budget ya ujenzi kwa kuanzia

Pamoja na mkapa kuwa mkali wa magazeti hakuwa mwoga wa yanayosemwa kama alivyo kikwete ndio maana akina Rai waliweza kuishi wakaishia baada ya wanamtandao kuingia madarakani

Kilimo kimekufa kabisa na hakuna bidii ya kutumia hata soko la agoa kwa bidhaa za kilimo miaka mitano imeshaisha kwa sababu hatuna hata jina la kumuita kwa mkampa kulikuwa na Ukapa,Ukaja ubinafsishaji,utandawazi mwisho ubabe ,sasa Twambie kwa Kikwete tuna majina gani zaidi ya vurugu zaakina dowans,richmond,epa nk.

Angekuwepo mpaka sasa angekuwa amejiwekea mgodi wa mchuchuma na kiwira lakini barabara ya dar -kigoma pia ingekuwa inazungumzwa
 
Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,347
0
1.Kikwete amemleta Maximo kuinua soka la Tanzania.
2.Kikwete amemleta Rais Bush Tanzania na kutoa msaada mkubwa wa fedha.
3.Kikwete amekuwa Raisi wa kwanza wa Afrika kuonana na Raisi Obama wa Marekani.
4.Pia ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania kutotimia mpaka sasa.
5.Feedback ya mikataba iliyochunguzwa bila bila.
 
Nungunungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2007
311
195
Kwa:
1. Mauaji ya raia wake Bulyanhulu.
2. Mauaji ya ya raia wake Zanzibar.
3. Mauaji ya raia wake Mwembechai.

Nitambukumbuka Mkapa.
 
Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,276
2,000
mazuri ya jk;
-kutabasamu mfululizo...inasaidia sana kwa mwenye njaa kujisikia angalau anachekelewa!
-machinga complex..
Udom...chuo kikuu cha dom
-kupeleka majeshi comoro kukomboa kisiwa
-kutowasaidia wapinga ufisadi maana wavuruga utwala wa sheria
-kutembelea wafungwa
n.k

-na kusafiri safiri nje kwa falsafa ya kuvutia uwekezaji
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom