Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Mheshimiwa Mkapa alipata msaada mkubwa sana kutoka kwenye taasisi za kimataifa na sera zake za uchumi kwa kiasi kikubwa zilifuata matakwa ya hawa ambao wengi wetu tunawaona wabaya. Kumbukeni ule mzigo wa madeni ya nje na miapngo mbalimbali ya kufuzu kwenye unafuu na misamaha yake kama HIPC, MDRI etc. Sasa kwa kifupi nchi isingeweza kufuzu na kuwa katika hali ya kukopesheka tena kama vimasharti kadhaa visingefuatwa. Tafuteni makaratasi yanayohusiana na hii mipango mjionee.

Pia VAT haikuwa mbaya kiasi hicho, tatizo letu tunapenda bwerebwere. Hazina kulikuwa hakuna fedha na BoT hawakuwa na akiba ya kutosha, forodha ilikuwepo ila ilikuwa ni pambo tu. Wakala wa kukusanya ushuru ni lazima apewe vyanzo vya ukusanyaji na huu huu mfumo duni wa kodi tunaoukosoa leo hii ndio uliosaidia kuleta afueni maana kabla yake hali ilikuwa mahututi haswa.

Kama pia mnakumbuka matumizi ya serikali katika mishahara yalipungua sana, watu wengi walipewa ridandansi, wafanyakazi wa umma walipungua kutoka kwenye 355,000 kwa mwaka 1992 mpaka 264,000 mwaka 1998/99, kama hapa chini tunavyojionea,



Tatizo letu kubwa lilianza mara baada ya sera za awamu ya kwanza ya Mkapa kufanikiwa na misaada, wakopeshaji, wafadhili na wawekezaji kuanza kututupia pesa ambazo tulikuwa hatuna uwezo wa kuzitumia kama ilivyopaswa hii ni kuanzia kwenye miaka ya 2001 kuendelea.
 
kikubwa nimeshangaa hakijatajwa ni jinsi mkapa alivyokua hachapishi pesa ovyo, mkapa alianzisha vyanzo vya mapato sio uyu check bob wa sasa, uyu check bob pesa ikiisha au akiwa na deficit yeye anakimbilia kuchapisha pesa na kuziingiza ktk mzunguko as a result pesa inazagaa nyingi mtaani na vitu vinapanda, lakini mkapa alikua hachapishi pesa ovyo! mnakumbuka check bob wetu alichapisha 700bilion alipoishiwa? na ndio pia kilichotokea kwa rais wa awamu ya pili, hajui kutafuta vyanzo vya mapato akawa anachapisha pesa ovyo, mkapa alistabilize, lakini uyu check bob anaturudisha kule kwa mzee rukhsa!
 
Mwaka 1995 Wakati Mkapa anaingia madarakani nyumba za Kariakoo ilikuwa Dollar 20,000 sawa na Tsh Millioni 10 watu walishindwa kuzinunua..Kufikia mwaka 2005 anaondoka madarakani nyumba hizo hizo zilikuwa zikiuzwa Dollar Laki 6 hadi 8 sawa na Tsh Billioni 8 hadi 10..

Saaafi sana kwa uchumi wa nchi, lakini where did the money came from? maanake Uzalishaji haukupanda wala pato la mwananchi halikuongezeka!..kuna siri gani ya kiuchumi iliyotokea..Muhimu tujiulize sisi ikiwa wakati wa Mwinyi kwa mshahara ule ule wa Mkapa (thamani ya Tsh) watu walishindwa kununua au kujenga iweje leo tushangae kwamba Mkapa aliweza kudhibiti Mpasuko wa bei hata kama gharama ilipanda mara 10..Wananchi walikuwa na mifedha isiyojulikana ilitoka wapi...

Kwa Tanzania, kudhibiti all depends na nyaya za kupata mifedha..watu wakiwa na cash wanaweza hata kununua mtu..Kila benki nchini iliibiwa sii chini ya mara 3, Mashirika kuuzwa ovyo ovyo, Ushuru wa kulanguana na mtu wa TRA, Cartel ya Polisi kucheza na Majambazi,wizi hadi BOT jamani still bado mnataka kujua kipi zaidi..
Mzunguko wa fedha ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba Mpasuko wa bei haikuwa big deal..
 
Hebu tuambie, wakati wa mkapa, VAT ilikuwa kiasi gani , wakati wa Mwinyi, wakati wa kikwete. Unafahamu ukiwa kama msomi unatakiwa utoe tarakimu na hoja zilizosheheni.

Mkuu Jaxonwaziri, naona unamsingizia tu kuwa huyu bwana ni msomi...umwombe radhi labda? ha ha haa haa, joking...

 
Mkapa Aliwezaje Kudhibiti Mfumuko wa Bei?

Hili swali aulizwe Mh Yusufu Makamba aka baba Januari; utapata majibu mazuri kuliko ya Bull na utajua kama ni kweli Kikwete ameshindwa kudhibiti mfumuko wa bei au mnamzingizia.
 
mi namkubali sana bwana nkapa, jamaa sirias kinyama,
nchi hii ilipata heshima sana.

huyu wa sasa bado amesimama juu ya mabega ya mkapa, ndo hizo pesa alizoacha mwenzake zinamfanya hatulii nyumbani.

he cannot think beyond the next meal,
bado natafuta nauli, siku nikitokeza huko aliko udugu utakufa na anko!!

Nafikiri wanaJF tungepata angalau neno moja toka kwa Mkapa kuhusu mgombea wa CCM 2010 maana mpka sasa sajiona Rais mteuzi toka SSM
 
Watu wanaogopa sana kumsifia Mkapa hata pale alipofanya mambo mazuri kabisa,....tuache hizo haki yake tumpe kama tunavyo mpa lawama.

Mazuri ya Jk;
-Kutabasamu mfululizo...inasaidia sana kwa mwenye njaa kujisikia angalau anachekelewa!
-Machinga complex..
UDOM...Chuo kikuu cha Dom
-Kupeleka majeshi comoro kukomboa kisiwa
-Kutowasaidia wapinga ufisadi maana wavuruga utwala wa sheria
-Kutembelea wafungwa
n.k

-kuwa rais wa kwanza wa africa kukutana na Obama
 
Mkapa alifanya mengi mazuri, kwa kweli. MAOVU yalikuwa makubwa sana!! Yakafuta uzuri woooooote.

The guy is a crook!! Kana kwamba haitoshi akamua kutuachia the worst PRESIDENT of all history of this country so far!!
 
Mkapa alifanya mengi mazuri, kwa kweli. MAOVU yalikuwa makubwa sana!! Yakafuta uzuri woooooote.

The guy is a crook!! Kana kwamba haitoshi akamua kutuachia the worst PRESIDENT of all history of this country so far!!

Mkuu amatumia maneno makali sana jaman
 
Jokakuu,
Mkuu hizi habari za IMF mbona mnazikuza sana kuonekana kama ni mahitaji yetu makubwa ktk maendeleo hali hiki chombo kimewekwa kwa maslahi ya nchi tajiri?..Je, unajua kwamba swala la EPA limekufa na IMF wenyewe ndio wametuliza ball.. They IMF wamemshauri JK kuchukua hatua hafifu ili mradi tu kupoza majanga yote na mikopo itarudi..Ile ku freeze account za wahusika wa EPA kuhakikisha fedha yao creditors inarudi ndio hatua ya walioitaka IMF. What they care most ni fedha yao sio madhambi yanayofanyika ndani nchini. As long as mikopo ya udhamini wao inalipwa, they careless what happens na Ufisadi.

IMF hawapo kupambana na Grand Corruption ktk nchi maskini hizi ni kamba tu, as a fact wanapenda sana kumweka mtu ktk madeni kwa sababu atazidi kukopa zaidi kama vile Bank wakikupa Creditline hawajali unazitumia vipi..Wanachokiangalia ni uwezo wako kulipa ile basic interest kwa kufuata vipengele vyao vinavyohusiana zaidi policies zenu kwa wawekezaji na Usalama wa nchi..

Lakini kila mnavyozidi kukopa ndivyo wanavyofurahiia utawala huo na kila unavyoshindwa kumaliza deni ndivyo wanavyokusanya zaidi na kukuweka ktk hali mbaya kiuchumi. Mikakati yote toka Mkukuta na sijui Mkurukuta are failure! - Fedha hazifiki ktk ujenzi wa maendeleo na IMF wanaelewa fika kwamba Grand Corruption in Tanzania imefika ktk hali mbaya sana lakini wanachoweza kufanya ni kuendelea kuhakikisha tunalipa madeni yao..

Kama sikosei Mwinyi alianza ku deal na deni la Nyerere ambalo IMF walitaka lilipwe kwanza kabla hatujakaa kuongea lolote. Kwa hiyo Utawala wa Mwinyi ulitumia muda mrefu kulipa deni tulolimbikiza toka wakati wa Nyerere. Tunakumbuka vizuri Nyerere hakukubaliana na IMF toka wakati wa Mtei tukawa blacklisted lakini tulikuwa na deni nao.. mfumo wao hauna tofauti na ule wa credit card, IMF ni kama credit reference Agency wa Banks na financialinstitutions..wana check and ku rate nchi zipate mikopo ya Banks kama WB kwa kutazama usalama wa fedha na interest zahizo Banks na sio maendeleo ya Tanzania au nchi maskini...

Kwa hiyo Mkapa sio tu aliwezakuingia IMF isipokuwa aliwezeshwa na ulipwaji wa madeni na Mwinyi kisha ndio tuka qualify tukaanza na mikakati ya SAP..Where do we stand kiuchumi - ZERO!..Kuingia hivi vyombo means nothing ikiwa hatuna uzalishaji, miundombinu mibovu tukitegemea imports ambazo zinazidi kutuweka ktk madeni..

Katika misaada yote hiyo tazama reli yetu toka mkoloni tumefanya nini? je, unategemea kuuza nje pasipo usafikri mzuri wa ndani! leo hii reli hiyo imesimama miezi mingapi? ilisimamama wakati wa Mkapa miezi mingapi.. Haya hiyo ya Moshi, Mombasa ndio historia kabisa bado mnategemea kuendelea..

Nitarudi kusema kwamba Tanznia hatujaendela hata kidogo!... tunarudi nyuma pasipo kujua..Nchi yetu tumekuwa ki umri tu hivyo maendeleo yoote tunayoyaona ni sawa na mtu aliyekuwa kiumri badala ya kuvaa nepi (wakati wa Mwinyi) leo tunavishwa kaptula... Tulikuwa tukitambaa uchi na nepi wakati wa Mwinyi leo ni toddler tunachechemea ktukivikwa kamptula na viatu..Bado sisi ni wahitaji.. Haya sii maendeleo ya kiuchumi ila ni makuzi ya kimwili..
 
We Mbumbumbu
Nimekuzuia kujadili watu.Hata hivo kwa vile umeuliza unataka jibu.Ubora kwa lipi? Hesabu magazeti mangapi yalifungiwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Watu wangapi wlinyanganywa uraia kwa kuonekana ni tishio kwa serikali wakati wa Mkapa na Kikwete.Kesi ngapi za ufisadi zilifunguliwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Wtz wangapi waliuawa na polisi kwa sababu za kisiasa na kidini wakati wa Mkapa na Kikwete.Vyuo vikuu vingapi vilifunguliwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Shule ngapi za Sekondari zilianzishwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Majibu ya haya na mengine mengi yatakupa jibu la ni yupi bora
 
Namimi nasema

1. Ni wakati gani bei za bidhaa zilikuwa juu na maisha ya wananchi kuwa magumu kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete? Kikwete
2. Ni wakati gani barabara nyingi zimejengwa hadi vijijini hadi Mtwara kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete.? Mkapa
3. Ni wakati gani uchumi ulikuwa toka asilimia 4.5 hadi asilimia 6.3 kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete? Mkapa
4. Ni wakati gani vyama vya upinzani vimekubalika zaidi kuonesha kuwa uongozi ulipo madarakani haufai kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete? Kikwete
5. Ni wakati gani nchi imeingia hasara kutokana na mikataba mibovu ya umeme mfano Richmond ,Dowans kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete? Kikwete
6. Ni wakati gani imetokea Waziri mkuu kujiuzulu kutokana na uongozi mbovu kati ya uongozi wa Mkapa na Kikwete? Kikwete
.
.
.

Mkapa alikuwa Kiongozi bora na makini,hii nchi angechukua Kikwete 1995 ,angeishindwa Mkapa alisafisha mambo mengi ili Kikwete aje kuendeleza ila ndivyo hivyo mafisadi ndio wameishika nchi
 
Ni wakati gani serikali imeingia mikatba mibovu ya madini? (mkapa)

Ni wakati gani serikali imeuza nyumba zake kwa bei bure? (mkapa)

Ni wakati gani wananchi walioandamana kwa haki kuuwa na polisi? (mkapa)

Ni wakati gani kila mwezi navunja TV kumwona jitu gumu linagombeza watu kwenye TV (mkapa)

Mkapa rais bora sana kupita JK...basi ana roho nzuri, isitoshe wametuambia makasisi hivyo damn
 
We Mbumbumbu
Nimekuzuia kujadili watu.Hata hivo kwa vile umeuliza unataka jibu.Ubora kwa lipi? Hesabu magazeti mangapi yalifungiwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Watu wangapi walinyanganywa uraia kwa kuonekana ni tishio kwa serikali wakati wa Mkapa na Kikwete.Kesi ngapi za ufisadi zilifunguliwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Wtz wangapi waliuawa na polisi kwa sababu za kisiasa na kidini wakati wa Mkapa na Kikwete.Vyuo vikuu vingapi vilifunguliwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Shule ngapi za Sekondari zilianzishwa wakati wa Mkapa na Kikwete.Majibu ya haya na mengine mengi yatakupa jibu la ni yupi bora


1. Suala la magazeti kufungiwa ni kawaida kwa kuwa magazeti lazima yafuate sheria na taratibu za nchi,vipindi vyote vya marais kuanzia Mwinyi,Mkapa na Kikwete kuna magazeti mengi tu yamefungiwa,na hicho sio kipimo cha uongozi bora.

2. Walionyang'anywa uraia wapo ni kama Hussein Bashe,Ezechiel Wenje wote hao waliambiwa kuwa si raia.

3. Kiongozi bora hawezi kuwa yule anayemfungulia mtu kesi mahakamani halafu anampigia kampeni achaguliwe ubunge eti ni mtu safi(kiongozi bora hawezi kuwa kigeugeu)

4. Kuuawa raia huko Zanzibar kulitokana na wafuasi wa CUF kuanzisha fujo na kutaka kupambana na polisi wenye silaha za moto,mimi nadhani baada ya kutokea vile viongozi wa CUF wakakaa chini na kuona ni heri kuwepo kwa muafaka.Lazima serikali iheshimiwe na isichezewe na watu wanaotaka kuhatarisha amani ya nchi

5.Huwezi ukasema mtu ni kiongozi bora eti kwa kuwa amejenga shule nyingi za kata ambazo hazina walimu na hazina vifaa vya kufundishia,matokeo yake ndizo zinazofelisha wanafunzi wengi zaidi

Suala la vyuo vikuu hata Mkapa alitoa majengo ya chuo cha Posta Morogoro ili kijengwe chuo Kikuu cha Kiiislam(hapo inajibu hoja kuwa wakati wa Mkapa watu waliuawa kwa sababu za kidini sio kweli hata kidogo)

Dodoma University ni funds toka kwa wafadhili na hata mimi ningekuwa Rais Dodoma University ingejengwa tu.Vyuo vingine vilipandishwa hadhi ambao ni utaratibu wa kawaida tu wa serikali ya Rais yeyote wa Tanzania

Kwa hiyo Mkapa alikuwa kiongozi bora utake usitake
 
1. Suala la magazeti kufungiwa ni kawaida kwa kuwa magazeti lazima yafuate sheria na taratibu za nchi,vipindi vyote vya marais kuanzia Mwinyi,Mkapa na Kikwete kuna magazeti mengi tu yamefungiwa,na hicho sio kipimo cha uongozi bora.

2. Walionyang'anywa uraia wapo ni kama Hussein Bashe,Ezechiel Wenje wote hao waliambiwa kuwa si raia.

3. Kiongozi bora hawezi kuwa yule anayemfungulia mtu kesi mahakamani halafu anampigia kampeni achaguliwe ubunge eti ni mtu safi(kiongozi bora hawezi kuwa kigeugeu)

4. Kuuawa raia huko Zanzibar kulitokana na wafuasi wa CUF kuanzisha fujo na kutaka kupambana na polisi wenye silaha za moto,mimi nadhani baada ya kutokea vile viongozi wa CUF wakakaa chini na kuona ni heri kuwepo kwa muafaka.Lazima serikali iheshimiwe na isichezewe na watu wanaotaka kuhatarisha amani ya nchi

5.Huwezi ukasema mtu ni kiongozi bora eti kwa kuwa amejenga shule nyingi za kata ambazo hazina walimu na hazina vifaa vya kufundishia,matokeo yake ndizo zinazofelisha wanafunzi wengi zaidi

Suala la vyuo vikuu hata Mkapa alitoa majengo ya chuo cha Posta Morogoro ili kijengwe chuo cha waislam(hapo inajibu hoja kuwa wakati wa Mkapa watu waliuawa kwa sababu za kidini sio kweli hata kidogo)

Dodoma University ni funds toka kwa wafadhili na hata mimi ningekuwa Rais Dododma University ingejengwa tu

Kwa hiyo Mkapa alikuwa kiongozi bora utake usitake

Kumbe ni taka usitake..sawa kwa vigezo vyako..JK ni bora kwa vigezo vyetu..tutakesha hapa mkuu hakuna mshindi..utaishia kusema wamechakachua...crying..

JK anampita kwa mbali Mkapa
 
Sio kweli hata kidogo.Mkapa yuko juu kuliko huyo Kikwete wenu
 
Back
Top Bottom