MYCROPOST
New Member
- Jun 16, 2026
- 2
- 0
Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania baada ya Dar. Ziwa Victoria (Nyanza) ni sehemu ya jiji hili, na ukiwa maeneo mengi ya jiji hili, unaweza kuliona ziwa kwa macho. Cha ajabu, licha ya ziwa hili kuwa karibu na kuwa sehemu ya jiji, kuna uhaba wa maji wa makusudi maeneo mengi ya jiji hili. MWAUWASA (Idara ya Maji) ndiyo mamlaka pekee yenye dhamana ya kusambaza maji katika jiji hili. Lakini ni nadra sana kusikiliza kero za wananchi. Mimi ni mkazi wa Mahina Kati, Nyamagana, Mwanza.
Nimekaa Mahina Kati kwa miaka mitatu sasa, lakini shida ya maji haielezeki. Nimewapigia simu idara ya maji MWAUWASA BUZURUGA lakini hawapokei simu, na ni nadra sana kupokea simu, nimewapigia MWAUWASA makao makuu lakini kila mara nakutana na mdada huyo anatoa majibu malaini na ahadi ati suala langu atalifikisha idara husika, na kila mara majibu ni hayohayo.
Cha ajabu ni kwamba unaweza kukuta maji yanatoka maeneo ya Kanisa la Roma kushuka mpaka Senta, lakini upande wa pili, kushuka kuelekea Igeye, hakuna maji wiki mbili mpaka mwezi, ukiwapigia mafundi wanakwambia leo tutawafungulia maji usiku, na inaweza pita siku mbili wanafungua maji usiku wa manane, ukiamka ahsubuhi kuangalia maji unakuta ndo yanaishilizia, hapo kama hujachota basi mpaka baada ya wiki mbili au mwezi. Mtaani wanadai kuna sehemu wanayafunga maji maeneo ya Kanisa la Roma, ili upande mmoja usipate maji, ni kama kuna mtu wana ugomvi nae wanamkomoa, lakini wanaumiza wengi.
Raia wengi walienda mbali mpaka kuwafuata ofisini na wakaishia kutukanana tu, lakini maji ni shida. Alipokuja waziri wa maji Mwanza, nilidhani kero hii ya maji basi tena, licha ya madai ya kubadili uongozi, lakini mfumo uko vilevile. Shida ni nini? Mbona Mahina Kati senta maji yanaweza kutoka hata siku tatu kwa wiki, lakini upande wa Kusini mwa Kanisa la Roma, njia ya kuelekea Kwa Babu, Igeye, hakuna maji? Kwani MWAUWASA huku ni maeneo ya wazi hakuna wananchi au ni maeneo ya Makaburini hakuna haja ya kupata huduma ya maji? Mbona mnakuja kusoma mita na kutumbambikizia bili ambazo hazieleweki? Iweje huduma ya maji iwe shida wakati matengenezo ya barabara Mabatini yamekamilika?
Kipindi kuna ujenzi wa daraja eneo la Mabatini mlisema shida ni daraja, sasa ni miezi imepita, pako shwari, au maji yanakuja kwa mgao, na iweje huku kwetu ndo kuwe na mgao kila mara? Au ni matenki yanasukuma maji kwa Gravitational Force? Iweje hiyo Gravitational Force haifanyi kazi? Na mbona hampokei simu? MWAUWASA Buzuruga, kuna shida gani?
MAHINA KATI kuna shida ya barabara, hiyo tumeshaizoea, maana huku Hiace ziko tatu tu zinazopitia Bugando kuja mjini kati, nauli ni Tsh. 1,000/- na sijui utaratibu huu kauruhusu nani. Zinaondoka saa moja na nusu ahsubuhi kuja mjini, na jioni mwisho ni saa kumi na mbili, nauli ni hiyohiyo elfu moja, kana kwamba tunaishi nje ya jiji, japo kwa hali ya miundombinu, ni kweli Mahina Kati ni nje ya jiji. Kwani watu wa Mahina Kati hatulipi kodi? Kwani sisi si wananchi wa nchi hii? Nani kawaambia MWAUWASA kwamba sisi wakazi wa MAHINA KATI tumekufa na hatuna haja ya kupata huduma ya maji? Je, mnaubia na wenye visima? Mbona maji yatoke usiku wa manane mnapoamua kuyatoa? Kwanini hamyatoi mchana? Iweje kama kuna shida isitatuliwe miaka yote hiyo? Iweje Shinyanga na Kahama wanatumia maji ya Ziwa Victoria na sisi wa Mwanza hatupati maji?
Jee, viongozi wa wilaya na mkoa, hamlijui hili? Wizara ya maji, mpokee simu na mjibu email. MWAUWASA inakera sana.