JK wetu na digrii yake ya uchumi alishindwa na Mwandishi wa Habari, Ben Mkapa! Kaaazi kweli kweli!
Sometimes najiuliza hivi,
1) Is it a matter of a right person following a wrong route?
2)Is it a matter of a wrong person going through a right route?
Sometimes, nadhani ni matatizo ya Tanzania vile? maana tunachosoma madarasani tunataka kukileta kama kilivyo kuku ukwelini. Na, to be frank, hii inakuwa ngumu kwakuwa many of the vitabu tunavyosoma ni outdated, so by the time tunamaliza kusoma tena kwa lugha ya kigeni huku tukiamini lugha ya kigeni ni bora na sahihi zaidi kuliko yetu tunayoitumia kila siku,tunajikuta tayari mazingira yetu na ulimwengu wetu umesogea hatua moja mbele, some of what we learnt becomes irrelevant. Kama hiyo haitoshi tunakutana na tatizo jingine: To put what we learned in the clasrooms to practices in the real world, in our society, amid our problems and challenges.
Now if you want to see kichekesho, ni pale msomi huyu anavyanza kuhangaika ku-paste alichokiona kwenye makabrasha! matokeo yake..? Mtu anaanza kujibu maswali ya kiuchumi ambayo hayajaulizwa na uchumi wa nchi yetu ilhali yale yanayoulizwa na uchumi wa nchi yetu akiyapuuzia ama akiyafumbia macho na kuyakwepa. Haya yanayoulizwa na uchumi wa Nchi yetu si hajayasoma popote? Si msomi huyu anaamini katika ku-copy na ku-paste? Analysis component kwake yeye si irrelevant na imekufa?
Jumlisha hayo yote na ufahamu kuwa yeye sasa anatakiwa kuwa na nyumba nzuri, gari zuri na mali kibao ili watu wakimuona wajue kwamba yeye kweli ni msomi wa nchi hii, jawabu unalolipata ni SERA MBOVU, UCHUMI MBOVU, MATATZO LUKUKI, NA UMASIKINI WA KUTUPWA WA WANANANCHI WALIO WENGI.
Mwishowe tunakuja kugundua kumbe kuna short-cut ya kutembeza bakuli? basi bakuli linaanza kutembea, linatembea weee, hadi inakuwa tabia. Kila kitu mpaka wafadhili watoe hela. Na wafadhili wnyewe wamechoka, wakagundua kitu kumbe wanaweza kutupatia vijihela na tukawapatia rasilimali zetu? Basi anza kuchukua madini, vitalu vya uwindaji n.k.
Na zaidi sana baada ya kuona hawa wafadhili wanataka tulivyonavyo, tukaona isiwe tabu, kama tunaweza kupata pesa kwa wafadhili ya nini kujihighulisha? Uza na mashirika yote ya umma, toa yote, ili tuwe tunakuja kazini kupiga stori tangu asubuhi hadi jioni lakini hela tunapata! Basi tukaanza kuuza, uza uza uza uza....! Kutahamaki kila kitu tumeacha kufanya, tumewauzia ama tumejitoa katika uendeshaji wake.
BIMA, Shirika la Ndege, Reli, Bandari, Ranchi za taifa, mashamba ya nafaka (ambazo wakati wa Nyerere yalisaidia sana kudhibiti njaa na kazalisha kiasi cha kutosha kuuza nje ya nchi na kujipatia fedha za kigeni), Mahoteli, hadi huduma za afya.
Hebu niambie kwa picha hiyo hapo juu, Mtu anayefanya hivi ni tumwite jina gani zuri linalompendeza zaidi ya
"MVIVU"?
Nani aliwahi kuona mvivu akifanikiwa? Sijawahi kuona, labda ashinde bahati nasibu!
Matokeo yake, kwa kuwa hatuna chakufanya, tunajikuta tunaanza wizi, hujuma, rushwa etc.
Tutapona Watanzania wenzangu???? Nisaidieni...!