Kuna Mkuu mmoja hapa katoa maoni haya:
Analysis ya video:
1. Je, Rwakatare alikuwa anatoa mafunzo kwa kuruta mpya au alikuwa anatoa maelekezo kwa mtendaji mzoefu? Hebu sikilizeni kwa makini aina ya mazungumzo yanayoongelewa, it is confusing. Mwanzoni anaanza kwa kuelezea aina mbalimbali za uuaji, halafu katikati anakuja kumkumbusha "the to be killer?" matukio waliyotenda sehemu mbalimbali (ni mzoefu?). Au labda ilikuwa ni refresher course?
2. Mandhari ya tukio ni kichekesho kingine. Honi na miungurumo ya magari, watu wakiendelea na maongezi yao (background noise). Halafu the master killers ambao wanajaribu kupanga mipango yao kwa ustadi mkubwa, wanaendelea na plan zao bila wasiwasi, huku mdada anaonekata kukatiza hovyo, mhudumu analeta vikombe (chai?) story zinaendelea tu. Yaani kila mwanadamu aliyemo ndani ya nyumba ile ni part of the mission? Impossible. U wapi huo usiri?
3. Tena njemba (Richie) inaibuka kwa nyuma ya master Rwakatare na kusalimia, huku akimpa mgongo anaitikia bila hata ya kugeuka kuhakiki ni nani? Then story zinaendelea! Everybody in the house is a killer!
4. Halafu katikati ya mazungumzo yanatajwa matukio ya mauaji ya kisiasa yaliyotekelezwa katika harakati za CHADEMA na kupelekea serikali ya CCM kuhusishwa nayo! What a way kwa serikali kutua mzigo na kung'aa tena mbele ya watanzania waliolala!
5. Master Rwakatare anaonekana ni mzoefu wa mbinu mbalimbali za mauaji kiasi kwamba anaonekana kutaja toka kichwani na kuandika notice! Jasusi la hatari hili.
Mtazamo wangu:
Tukio zima linaonekana kuwa staged kwa sababu zifuatazo:-
1. Eneo liliporekodiwa tukio hili hapa-support uhalisia kwamba kuna mipango ya mauaji inapangwa. Mipango hatari kama hiyo inayohusu maisha ya high profile figures haiwezi kupangwa kipuuzi namna ile. Security iko wapi hapo? Mhudumu wa chai, karani, Richie wanapita tu. Huwezi kumwamini kila mtu, big no! Unless ni movie za kina Ray ili condition fulani itimie!
2. Matukio ya mauaji ya Morogoro, Igunga, Mwangosi na Kubenea yalipangwa makusudi yatajwe kwenye tamthilia hii ili kuisafisha serikali dhidi ya shutuma ambazo zimekuwa zikielekezwa huko. Na ndio maana hakuna mtiririko unaoshawishi kwamba kulikuwa na jambo linapangwa kutekelezwa bali kuwaibia siri ndugu watazamaji kwamba mchawi wenu si serikali bali ni CHADEMA. Lengo kuu ni kuiunganisha CHADEMA na vifo hivi vya kutisha! Halafu mengine yaliyobakia (Ulimboka na Kibanda) tutajenga taswira automatic na kuwaunganisha humo, na mengine yatakayofuata jicho letu kwanza itabidi lianze kuimulika CHADEMA!!!!! Na ndio kisa cha swali ambalo hata si la kimbinu la anayedhaniwa muuaji kuihusisha CCM ili ionewe huruma. Ni mchezo wa kijinga kweli huu.
3. Kwenye ile karatasi Lwakatare alikuwa anaandika nini? Wewe unadhani alikuwa anaandika? NO way! Alikuwa anasoma dondoo alizoziandaa (script) kuhakikisha mambo ya msingi hayaachi. Alikuwa anasoma kwanza kisha anaongea huku akijifanya kuandika. Mwangalie vizuri tu (mfano kuanzia dak. 8 na sek. 33 mpaka dak. 8 na sek. 45--- angalia macho kisha angalia kalamu. Anaangalia straight wakati kalamu inaandika pembani kulia!!!)
Who did this?
Maoni yangu:
Lwakatare is behind all of this bullshit! Yes, I said it! Huyu bwana ametumika kuiangamiza CHADEMA. Angalia kwa makini ku-determine position ya kamera. Pale hakuna ujasusi wala nini, kamera iko kati ya actor wa uuaji na Lwakatare! Huyu bwana alijua kabisa kuwa anarekodiwa, wala si mkakati wa siri! Kuanzia dak.19 na sek. 21 muuaji anaanza kustruggle na kamera kwani scene inatakiwa iishe abruptly. Upuuzi kabisa huu.
Msikilize actor anayewakilisha wengine, ni mwandishi zaidi kuliko muuaji. Muda wote yuko kuitikia "mmmh." Haulizi details za kumsaidia kutekeleza jukumu lake? Ni ajabu na kweli.
Kitakachofuata ni either Lwakatare ata-confess, na kuwaunga top layer wa CHADEMA au atatoa maelezo yenye kupelekea watu woooote kuamini ni mpango wa CHADEMA. Halafu atawataja vijana wake wa kazi ambao tayari wameandaliwa. Watakiri kuhusika na unyama huo. Then? There is ana exit strategy kwa hawa, huku wakiwaacha top layer wa CHADEMA wakiwa slowly annihilated!!!!
REMEMBER Wassira alisema nini kuhusu CHADEMA? Wakati mnasherekea kuwaondoa kina Shonza, kumbe kuna mitego mingi tu imetegwa ndani ya chama. Pia nina mashaka sana na kiongozi mmoja ndani ya CHADEMA ambaye anahusishwa humu kutaka kuuliwa na viongozi wenzake! Na watu wa system waliomo ndani ya chama!! Watch out hata kama ni wana sheria wazuri kiasi gani, kumbuka historia zao walikotoka walifanya nini!!
THE ENERMY WITHIN!