Karikenye
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 564
- 280
Bocho kwa sehemu uko sahihi lakini ujue huu ni mfumo (system) na mfumo hujengwa kwa sheria, kanuni na taratibu ambazo sheria mama yake ni Katiba! Katiba yetu mbovu hatujaweza kusimamisha mihimili 3 ya dola ambayo inajitegemea..Rais (Executive) ana mkono kwenye mhimili wa Sheria (Judiciary) na Wawakilishi wa wananchi (Parliament) hili ni kosa kubwa sana ambalo Katiba yetu inalo! Na usidhani hii ilikuja tu, iliwekwa na watu kwa lengo la kumfanya Rais atawale na siyo kuongoza! Sasa unayoyaona leo katika nchi hii ni matokeo ya katiba hiyo! Inakuwaje mfano waziri awe na uwezo wa kulifungia gazeti (Mf Mwanahalisi issue)? Serikali (Executive) ilitakiwa iende mahakamani kulalamika na ipeleke ushahidi utolewe Gazeti husika likionekana na hatia ndipo lifungiwe au lipigwe faini! Sasa unachokiona ndio kiini macho tulichonacho kwenye Katiba yetu! Watu hawawajibiki kwa sababu Executive haiwajibiki (Top-down), executive ipo corrupt so are other officials because that's what they see from their bosses up there!! Ukweli ni kwamba accountability Tanzania ipo kwa kiwango kidogo sana siyo zaidi ya 25%, kwingine kote ni ujanja ujanja tu! It is very pathetic! Gharama ya kuubadilisha mfumo inaweza kuwa detrimental kwa Chama tawala, hilo wanalijua na ndio maana wameamua ni heri hali ibaki kama ilivyo (STATUS QUO & BUSINESS AS USUAL) maana watakuwa na uhakika wa kuendelea kutawala!!Tatizo la Tanzania sio CCM tu ni watanzania wote kwa nafasi zetu mbali mbali tulizokuwa nazo.
Hebu niambie:
1) CCM itajuaje kama mimi nikiwa mtumishi wa TRA nimeshirikiana na wafanyabiashara katika kukwepa kodi (Collusion)?
2) CCM itajuaje kama nyara za serikali zimetoroshwa nje ya nchi ikiwa watanzania waliopewa nafasi kwenye maeneo hayo watashirikiana na maharamia kutosha nyara za serikali (collussion)?
3) CCM itajuaje kama kuna watumishi wa umma wanaoongeza bei katika manunuzi kwa kushirikiana na wauzaji na hivyo kupandisha gharama za manunuzi ya serikali (procurement frauds)?
4) Zile overtime mnazopewa wakati muda wa kawaida mnautumia kukesha JF na kucheza karata. Unafikiri ni CCM pia?
Tatizo sio CCM pekee na serikali, ni sisi watazania kwanza inabidi tubadilike kuwa na moyo wa uzalendo ndipo mambo yatakapobadilika for good katika nchi yetu.
Bila kuwajibika, si CHADEMA wala chama chochote cha upinzani kitakachoweza kuleta the so called mabadiliko ya kweli Tanzania.
Amka usidanganywe badilika wewe kwanza na umwambie mwenzako abadilike.
Pamoja tunaweza.