Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.

Ya lwakatare iko wapi humu mbona cjaiona?
 
  1. kubenea saed
  2. dr.ulimboka stephen
  3. Daud Mwangosi
  4. dr.harrison mwakyembe
  5. fr.evarist mushi
  6. Dr.juan mwaikusa
  7. fr.ambroce mkenda
  8. absalom kibanda
  9. horace kolimba
  10. edward moringe sokoine
  11. prof.mark mwandosya
  12. kumwagiwa tindikali mufti
  13. Mauaji ya ndago (iramba0
  14. mauaji ya Arusha
  15. mauaji ya Songea
  16. mauji ya mwembe chai
  17. mauji ya morogoro
  18. mauji ya zanzibar
  19. mauji ya kada wa cdm arumeru
mkumbuke na mwandishi wa gazeti la 'Mfanyakazi' Hayati Stanislaus Katabaro (may he rest ni eternal peace). Huyu naye ni miongoni wa wahanga wa mwanzoni
 
Hiyo ya Obama imeniacha hoi kabisa. Teknolojia hatari! Mpaka hapo naanza kushawishika juu ya uwezekano wa video ya Lwakatare kuwa ya feki. Lakini mnaweza kunisaidia zaidi mimi Tomaso, maana ni miongoni mwa kile kizazi kinachotaka ishara. Naomba mtutengenezee moja ya Mwigulu Nchemba au Rizwani mumlishe maneno, au hata ya mkuu wa kaya kabisa tumsikie na kumwona akisema "nchi imenishinda, nimeamua kujiuzulu urais, nitaondoka ikulu wiki ijayo. Urais namkabidhi Lipumba, mimi nahamia Madagascar". Just to prove your point. Yaani hapo nitaamini 100%.
 
Sina muda na kubishana na watu walifundishwa kuvuta bangi zenye mchanganyiko wa mavi ya walevi. Napambana na hoja za watu makini wenye akili timamu.

Hii video kweli imewachanganya sana CHADEMA, tuwaachie POLISI wafanye kazi yao na ukweli utajulikana hakuna haja ya kutukana humu JF, mbona hii video iko wazi jamani hata tukijifanya kumtetea LWAKATARE ni kazi bure, ni gumu sana kushindana na ushahidi.
 
Teknolojia inafanya mpaka lips ziende sawa na maneno? Unajua kuna watu wanaweza kuzima sauti wakasoma lips tu hizo wakakwambia huyu kasema nini hapa?

Sasa lips nazo wamechakachua mwanzo mpaka mwisho? Sauti yake? Anavyoongea?

Au unataka kusema picha yote ni Lwakatare, ni avatar tu?

Muungwana akikosea kukubali kosa na kuomba msamaha ni ada.

Ama sivyo kukataa kosa wakati watu wamemnasa kwenye tape ni kuongeza kosa.

This is sheer thuggery and mischief. Hiki ndicho chama mbadala tunachokitegemea kije kuiondoa CCM?

Hii ni strategy inayokubalika kichama au uhuni wake huyu mmoja tu na vi underdogs vyake?

Usituletee ufia dini kwenye siasa.

Mkuu, hivi ile Picha ya Ze Utamu ya JK ilikuwa kweli???
 
Wana mapinduzi wanaamini kuwa ukiona mambo kama haya tambua kuwa ukombozi upo karibu. Uhuru na Ruto walifanya kama haya na sasa wameingia ikulu, aibu kwa ICC na mafia wao. Nadhani ni muda wa kushangilia ushindi na mapinduzi ya kweli, watanzania wenye akili, na hasa hawa wanaotumia mitandao ya kijamii na forum makini kama JF watatumia akili zao kuchambua hili. Maana mengi yamesemwa kuhusu CHADEMA yameshindwa....walianza na ukanda ukashindwa, wakaja na dini wakashindwa, wakaja na kadi ya dokta Slaa wakashindwa, sasa wemeibuka na mauaji...hakika MUNGU ni yule yule jana, leo na hata milele, ataendelea kutupigania wana CHADEMA.

Tualianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU
Ikiwa MUNGU, yupo upande wetu, nani atanyanyuka kinyume chetu?

Jamani mmesahau na ile ujumbe wa sms Nchemba alizosema katumiwa na wabunge wa CDM. sijui iliishaje nayo
 
Hiyo ya Obama imeniacha hoi kabisa. Teknolojia hatari! Mpaka hapo naanza kushawishika juu ya uwezekano wa video ya Lwakatare kuwa ya feki. Lakini mnaweza kunisaidia zaidi mimi Tomaso, maana ni miongoni mwa kile kizazi kinachotaka ishara. Naomba mtutengenezee moja ya Mwigulu Nchemba au Rizwani mumlishe maneno, au hata ya mkuu wa kaya kabisa tumsikie na kumwona akisema "nchi imenishinda, nimeamua kujiuzulu urais, nitaondoka ikulu wiki ijayo. Urais namkabidhi Lipumba, mimi nahamia Madagascar". Just to prove your point. Yaani hapo nitaamini 100%.
Haa haa haa, kiwanda cha kulisha watu maneno sifahamu kilipo, labda tumuulize Mwigulu, anaweza akatupeleka. Mimi pia ningependa kuona clip ya hivyo.
 
KWA KWELI KUNA HAJA YA KUUNGANISHA MATUKIO JUU YA CCM HII WADAU Hiii nchi saizi serikali ikibanwa wanatengeneza sinema DOWANS ilipopamba moto kikaja kikombe cha babu serikali ndio ikampa promo ya bure,mgomo wa madaktari ulipopamba moto dr.ulimboka akatekwa,matokeo ya kidato cha nne vijana wamefail kibanda anatekwa suala la kibanda limepamba moto video inatoka kuonyesha viongozi wa cdm wapanga mauaji,mnatengeza matukio ili kufuta ajenda zinazoibana serikali padre mushi alipouwawa kuzima mjadala mkaleta FBI ,Ccm yale majambia aliyotangaza igp omary mahita siku moja kabla uchaguzi kuwa ni ya cuf yaliishia wapi???hamuwezi kutufanya watanzania wajinga na wapuuzi,angalia matukio haya..halafu nikangalia hii list naona CCM wanyakyusa wamewageuza deal/kufanikisha mauchafu yao......




  1. kubenea saed
  2. dr.ulimboka stephen
  3. Daud Mwangosi
  4. dr.harrison mwakyembe
  5. fr.evarist mushi
  6. Dr.juan mwaikusa
  7. fr.ambroce mkenda
  8. absalom kibanda
  9. horace kolimba
  10. edward moringe sokoine
  11. prof.mark mwandosya
  12. kumwagiwa tindikali mufti
  13. Mauaji ya ndago (iramba0
  14. mauaji ya Arusha
  15. mauaji ya Songea
  16. mauji ya mwembe chai
  17. mauji ya morogoro
  18. mauji ya zanzibar
  19. mauji ya kada wa cdm arumeru
 
.......... sawa nachukulia unahoja pia lakini lazima uchunguzi ufanyike maanake hali tete saa hiii!
 
Hii video kweli imewachanganya sana CHADEMA, tuwaachie POLISI wafanye kazi yao na ukweli utajulikana hakuna haja ya kutukana humu JF, mbona hii video iko wazi jamani hata tukijifanya kumtetea LWAKATARE ni kazi bure, ni gumu sana kushindana na ushahidi.

Na wewe inaonekana uwezo wako wa kufikiri na kuchanganua hoja ni mdogo kuliko hata punje ya haradali. Mimi natamani hoja hii iende mahakamani, tuone wakili yupo mjinga na kichaa atakwenda kusema kuwa hii clip ina ukweli.
 
Chadema baada kwenda kumdhamini jasusi wenu anaoza lupango mnakesha hapa JF kukanusha ukweli.
 
Kaaazi kweli kweli, hicho ndo chama cha majambazi( ccm), wemeona watoke kimtindo huo, ila ukweli utajulikana tu.
 
Back
Top Bottom