Karume atengwa, picha zake zachanwa Z’bar

Karume atengwa, picha zake zachanwa Z’bar

ya zanzibar hayatuhusu tuongelee ya kwetu hata wakiitwa mi-mamba kwao sawa tu.
 
Mkuu katika siasa, hakuna dhambi kubwa kama kuwatukana wananchi,hasa uliotokana nao.
Hicho ni kilele cha dharau na elitism.

Mimi nafikiri hii picha ndio kwanza inaanza, makubwa yako mbele.
Atadhurika vipi na hayo makubwa yanayofuata kutoka hapo. hivi kwa mfano wakifanya yote hayo halafu yeye akajinyamzia kimya kama alivyofanya mangula wakati ule anatukanwa na akina makamba kwani itakuwaje. Labda kama anatafuta tena uongozi serikalini. lakini sioni kama hayo yanayotokea hivi sasa yana impact yoyote kwake.
 
Nyerere alithubutu kumwita Kolimba na Malecela kama ni wahuni, kwahiyo Uhuni umejaa CCM na kwa kweli kama tutaendelea kuwa ndani ya utawala wao tujuwe nikuzama na wahuni hao wapo tayari kufanya lolote lile almuradi kupata maslahi yao, ikiwa kuuwa, kuiba, kufitini liwe lolote lile baya, muhimu wanaweza kulifikia lengo lao.
Ikiwa wana CCM kama kweli wanamthamini Abied Amani Karume kwa mila na tamaduni zetu za Kizanzibari mtoto wake na familia yake siku zote zitakuwa zinatukuzwa, lakini kinyume chake ndio hiki leo kumtukana Amani ni sawa kumtukana Baba Karume, tabu nikuwa mhuni hajui alifanyalo ndio tabu yake.
Hawa ni watu hatari sana na lazima kutafutwe suluhisho la mara moja la kuwadhibiti. Mwanamume huwa hana matusi ila awe baradhuli, hakika waandishi hawa wa Kisonge wengi wao ni kaumi hiyo wakiongozwa na Borafya, kutokana na malezi mema ya Kiislamu niliyopewa siwezi kutukana kama wao, lakini ni aibu kwa Borafya huko nyuma alivyowahi kuwa na mambo aliyoyafanya na kwa kweli kile ni chombo kilichokuwa kinakwenda mperampera karibu kitagonga mwamba, subra ni muhimu, ingawa mwenye kasema kala nyama ya mbwa dua hazimpati.
CCM Kisonge wajuwe dunia haibaki kama wanvyofikiria mabadiliko hutokea bila ya mtu kuelewa, wapi Iran na Shah, wapi DDR na Honicker, wapi Yugoslavia na Tito, wapi Romania na Sacisko, wapi Somalia na Said Barewapi zitakuwa ni nyingi na kutoweka kwake hakuna aliofikiria. Karibuni tumeona tawala kuporomoka kama Misri, Tunisia, Libya ambako hakuna mmoja alitarajia ipo siku yatakuwa hayo, tunajuwa waliofungika kiakili wanaamini CCM na Zanzibar ya kisonge kubakia milele, kwasababu hawajasoma na kutegemea fitna na ubahalula kuweza kuwafanya maisha yao yaweze kwenda. Wakati utawasuta watu na watake kujinyonga na kuiona dunia sio.
Amani hawezi kushtakiwa na madhalim, kwani kumshtaki Amani ni kukishtaki chama cha CCM, Zanzibar na Bara. CCM imejaa dhulma, walimdhulumu Bilali wakampa Amani, sasa leo wanasema nini? Frankenstein amemtengeneza kiumbe kaanza kuleta mashaka, sasa huku hawa wapumbavu wameshindwa kuelewa leo wanatukana nini?
Kumtukana Bibi Fatma Karume nikujiuliza ni kweli huyu alikuwa mke wa muasisi wa Mapinduzi? Hapa ndipo ninapofahamu Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, kuwa waliofanya Mapinduzi sio wenyewe Wazanzibari, matokeo kile kizazi kichafu cha kina Injini na Mfaranyaki ndicho hadi leo kinaisumbua Zanzibar. Hakuna marefu yasio na mapana na hakuna Kiza kisichopambanukiwa. Mapinduzi sio daima lakini haki ndio daim
 
Mkuu tusi na ukweli mara nyingine ziko kwenye sarafu moja yenye pande mbili.
Ukitaka kusema ukweli unaouma hekima inahitajika ili kutowatusi hata wazazi wako.

Ni dhahiri msemo wa " akili ya samaki" kama umekufurahisha , kuna ambao imewaudhi, tena kwa sababu nzuri tu.
Wengi Wazenji wanashangaa leo wanaambiwa wana akili ya samaki wakati walimbeba jamaa hata pale ambapo hakustahili.
Shukurani ya punda mateke!!!

Mimi siwezi kufurahishwa wala kuchukia kutokana na msemo kama huo ambao ulitolewa na mwana CCM katika hadhira ya wana CCM wenzake.......yaani hayanihusu......ila najua kuwa asilimia kubwa ya Wazenji sio wana CCM....kwa hiyo kama ni tusi basi kawatukana wana CCM wenzie waliokuwa wanamzomea..tean wakiwa Dodoma na wala sio Zanzibar
 
Acha hizo mkuu!
Waliompokea Dr Shein tena kwa wingi basi walikuwa CUF!
Tena wakaishia kurarua taswira za Sheikh Amani Karume?
 
Karume alikuwa na nafasi ya kufanya mageuzi wakati wa utawala wake wa miaka 10 kwa sasa anafanya vurugu kwa Rais wa sasa Dk. Shein.

ilitumika nguvu kubwa sana hadi serikali ya umoja wa kitaifa ikaundwa chini ya utawala wake na mauaji ya Pemba kwa mara ya kwanza wakawa wakimbizi.

mwendo anaokwenda nao sasa Karume ni kama hakuwahi kuwa Rais wa znz angewapa uhuru wazanzibar kuamua na kusikilizwa.

mm nafikiri ndicho alichokisema, kwamba maoni ya kila mmoja hata kama yanatuudhi tuvumiliane ili mwisho rasimu ya katiba itengenezwe na kujadiliwa na ss sote. tatizo ccm hawataki mawazo tofauti na yale yaliyosemwa na wao baada ya mkutano mkuu uliofanyika Dodoma. mm naona yuko sahihi ndio maana yy aliasisi serikali ya umoja wa kitaifa kwa faida ya wazanzibar ili kuwepo na amani na hata kampeni za 2010 zanzibar zilikuwa na utulivu kuliko miaka yote iliyopita. yy alijifunza kusikiliza mawazo tofauti na anayoyaamini ndiyo maana hatimaye alifikia hapo. kwann ccm hawataki kusikia mawazo tofauti na wao wanayoyaamini na kuyasimamia?
 
Karume alikuwa na nafasi ya kufanya mageuzi wakati wa utawala wake wa miaka 10 kwa sasa anafanya vurugu kwa Rais wa sasa Dk. Shein.

ilitumika nguvu kubwa sana hadi serikali ya umoja wa kitaifa ikaundwa chini ya utawala wake na mauaji ya Pemba kwa mara ya kwanza wakawa wakimbizi.

mwendo anaokwenda nao sasa Karume ni kama hakuwahi kuwa Rais wa znz angewapa uhuru wazanzibar kuamua na kusikilizwa.

Karume ameondoka madarakani Zanzibar ikiwa na Katiba mpya na Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Wahafidhina na akili samaki wanaompinga leo wanatambua kama siyo ujasiri binafsi wa Karume,maridhiano na umoja wa Wazanzibari usingewezekana. Karume alikuwa mwiba kwa viongozi wa CCM Tanganyika ambao wamekuwa hawataki umoja na mshikamano baina ya Wazanzibari.
 
Well, ukikata miti yote utazuia mvua, which renders the Sugu slogan senseless! Beyond that I agree with everything else you said.

Hapana, ila kuita mawazo ya wengine akili za samaki ndio akili zenyewe za samaki hizo. Mtu anaposema jamani kila mtu apewe nafasi ya kutoa mawazo yake kuhusu Muungano, hata wale ambao wanaona wangefanya vizuri zaidi kama nchi nje ya Muungano, hawataki Muungano, kuwafunga midomo hao wasitoe mawazo, hizo ndio akili za samaki.

Akili za samaki zinafanya kazi hivi: Chengu mmoja akiwa mbele ya msafara utakuta utitiri mzima wa samaki unamfata nyuma bila kujua manufaa ya ile safari. Wa mbele akiingi chaka wote wanaingia chaka. Mtu mmoja akasema mwaka 1964, wakati kuna watu milioni 8, kwamba kitu fulani kinatufaa, basi mpaka leo watu wamezaliana kama samaki wamefika milioni 40 na wote bado wanafuata ule utitiri bila kujiuliza tumefika wapi na safari ile, manufaa yake yako wapi? Akili za samaki!

Wanatokea baadhi wanasema jamani turuhusu mawazo huru kuhusu mustakabali wa nchi yetu, wanatukanwa. Ndio akili za samaki!

....good!critical analysis
 
Barubaru
Wadigo wanasema "wanukao hawajijui"
Naona una walikini mwingi tu ulienda shule kukusanya vyeti na sio kuelemika; na nakuthibitishia hilo kwa mifano yako unayotoa; kilichomfanya Barlow akutwe na mauti ni kutembea na mke wa mtu; kama Barlow angeuliwa na wanaharakati kama wa uamsho basi hapo ungeweza kuoanisha mfano huo na askari aliyeuliwa Zanzibar na wanaharakati wa uamsho;

Narudia tena kauli uamsho hauwakilishi maoni ya wazanzibari walio wengi; hilo lipo wazi; chokochoko za uamsho zilikuwa na nguvu Amani; alikuwa akimtumia sana shemeji yake Mansoor Himid kuleta chokochoko kwa tamaa zake za madaraka;

Amani na Ally ni wanandugu angalia mitazamo yao kuhusu muungano; dawa ya uamsho tayari imepatikana nyie kaeni na tamaa zenu huko mliko uarabu huna wewe ni mpemba tu hata hagal na kanzu nyeupe darzi bado utakuwa mpemba tu usisahau asili yako siku nyingine na mifano ya kipemba;

Wapemba wanahekima nyingi na mifano mingi ya maisha; kitovu chako cha asili ni pemba; daraja la uarabu huna usidanganye watu walimuona Jamshid kima mpaka ikamlazimu aishi ukimbizini Uingereza sijui watatumia vigezo gani kwa mpemba aliyezaliwa Pemba; usikimbie asili yako kwa kutaka kujikweza.

Chama
Gongo la mboto DSM
Kwanza kabisa pole sana kwani utabiri wako umekupoteza njia.

Nimezaliwa Shanghani Unguja kwa baba yangu ni mwarabu wa kiyanga mwera na mama mwarabu wa sikonge. Hivyo sina asli ya pemba hata kidogo. Kwani wazazi wangu ni waarabu asilia pande zote sina uchotara ndanimwe na hata watoto wangu ni hivyo hivyo. Na ndio maana nimerudi kwetu na kupokelewa kama raia kamili bila masharti. jaribu wewe kuomba uraia wa Oman uone!!!

Nashindwa kabisa kukuelewa kwanini UAMSHO inakunyima usingizi? kwanini wasiachiwe waZnz wayamalize wenyewe kama walivyomaliza tofauti zao za kisiasa baina ya CUF na CCM. kwani wa Bara mna maslahi gani kwayo?

Mimi kwa mtazamo wangu mfumo usio sahihi unaoongoza bara haiwezi hata kidogo kuongoza Znz kwa sababu ya asli za watu wa huko.

Utamaliza mabucha tu lakin nyama ni ile ile.

Tuombe kheir

Hivi blogu za huko kwenu hazipo ?
Huko utaeleweka vizuri, huku kwetu ni pilipili ya shamba kwako, haitakiwi kukuwasha.
 
Uraia wa kujaza fomu kama unaomba kazi ndio unakuofanya usahau asili? Uarabuni umekwenda ukiwa tayari balehe na mtu mzima hao Oman walikutumia tiketi na kukuomba urudi kwenu kama sio wewe ulikwenda kutafuta maisha? Afadhali leo umewadhihirishia wana JF kama wewe ni mtanzania. Na kama kweli wewe damu yako ni mwarabu haya Zanzibar yanakuhusu nini? Uamsho haujawahi kunyima usingizi hata siku moja; mtakosa nyie ambao azma yenu haikutimia; hakuna mfumo wa utawala usio na matatizo hata hapo Oman mfumo walionao si kweli kama unakubalika na wa Oman wote. Uamsho ni kikundi cha wahuni wachache; vibaraka waliokuwa wakitumiwa wapo jela hushangai kuona hali ni shwari visiwani? Hivi sasa tuone kama utawasikia viongozi wao; viongozi wa uamsho wanajulikana na nina uhakika wewe unawajua.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Hivi blogu za huko kwenu hazipo ?
Huko utaeleweka vizuri, huku kwetu ni pilipili ya shamba kwako, haitakiwi kukuwasha.

Fikra potufu hizi.
Hujui kuwa Yanga haiwezi kuwa yanga Bila Simba na vile vile kwa upande wa Simba.

lazima kuwe na mawazo mgongano ndio mnakasha unanoga.

Pole sana

Fikra potufu hizi.
Hujui kuwa Yanga haiwezi kuwa yanga Bila Simba na vile vile kwa upande wa Simba.

lazima kuwe na mawazo mgongano ndio mnakasha unanoga.

Pole sana

Mkuu kwa uchaguzi wako mwenyewe umeamua kwenda huko" kwenye heri".
Sasa tulia huko, na mimi binafsi naona maoni yako hayana mantiki maana huna la kutetea hapa nchini.

Sana sana waweza kuwa mamluki.
Huna haki ya ku comment nchi yetu ina vyokwenda.

CHADEMA hata wakitutukana tunajua ndugu zetu, likotokea la kutokea huwa tunakuwa pamoja.

Ndo maana ningekushauri ujikite zaidi na siasa za Oman
 
Usimfukuze Barubaru Oman yamempeleka maisha tu; 90% ya ndugu zake wa damu wapo Tanzania; Oman hakuna siasa ina mtawala Qaboos; siasa anazozijua Barubaru ni hapa za nyumbani kwao Tanzania; ni mwenzetu hizo hagal zisikutishe!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Fikra potufu hizi.
Hujui kuwa Yanga haiwezi kuwa yanga Bila Simba na vile vile kwa upande wa Simba.

lazima kuwe na mawazo mgongano ndio mnakasha unanoga.

Pole sana

hao vichogo ni maneno wanayozungumza ndo ushahidi tosha kwao.wanapenda kupinga mambo ya zanzibar As if wameshawahi kwenda.maneno aliyoyasema karume ni sawa kwa mwenye akili lakin hao vichogo vya watanganyika watakwambia hakuongea lolote ila ni uamsho.inaonesha watanganyika wanawanyima usingizi uamsho.na hapo ni mwanzo tu wanzanzibar tupo pamoja sote isipokua wachache ndo hawakubadilika.kinacho waumiza vichogo ni kwamba hawataki kuitwa watanganyika ndo maana wanaulinda muungano kwa hali na mali.
 
Usimfukuze Barubaru Oman yamempeleka maisha tu; 90% ya ndugu zake wa damu wapo Tanzania; Oman hakuna siasa ina mtawala Qaboos; siasa anazozijua Barubaru ni hapa za nyumbani kwao Tanzania; ni mwenzetu hizo hagal zisikutishe!

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu watanzania wengi, hasa kizazi cha Mwalimu ni masikini jeuri.
Tulizaliwa Tanganyika, tumeishi Tanganyika, matatizo yetu hapahapa Tanganyika na tutafia Tanganyika.

Watu wanasahau kuwa Ujerumani ya Magharibi wakati huo Ilitudengulia na tikaw aonyesha mlango wa kutokea.

Kilichonikera sana sana ni hiyo statement ya mamluki huyo akifikiri tunapenda sana kwenda huko walikoenda.
Tofauti kabisa hawajui raha ze tu , taabu zetu.

Mimi akiongea memba wa CDM au hata CUF nitamwelewa, lakini raia wa nje Anayetudengulia uraia wa kigeni namwona ni mamluki tu.
Kwanza kabisa pole sana kwani utabiri wako umekupoteza njia.

Nimezaliwa Shanghani Unguja kwa baba yangu ni mwarabu wa kiyanga mwera na mama mwarabu wa sikonge. Hivyo sina asli ya pemba hata kidogo. Kwani wazazi wangu ni waarabu asilia pande zote sina uchotara ndanimwe na hata watoto wangu ni hivyo hivyo. Na ndio maana nimerudi kwetu na kupokelewa kama raia kamili bila masharti. jaribu wewe kuomba uraia wa Oman uone!!!
 
hao vichogo ni maneno wanayozungumza ndo ushahidi tosha kwao.wanapenda kupinga mambo ya zanzibar As if wameshawahi kwenda.maneno aliyoyasema karume ni sawa kwa mwenye akili lakin hao vichogo vya watanganyika watakwambia hakuongea lolote ila ni uamsho.inaonesha watanganyika wanawanyima usingizi uamsho.na hapo ni mwanzo tu wanzanzibar tupo pamoja sote isipokua wachache ndo hawakubadilika.kinacho waumiza vichogo ni kwamba hawataki kuitwa watanganyika ndo maana wanaulinda muungano kwa hali na mali.

Swadakta kwa maneno yako muruwa. Nimekukubali sanaaaaaaaaaa.

Kweli UAMSHO inawanyima usingizi. Na watashindwa tu kwani siku zote batili haiwezi kuishinda Haki.

Similar Discussions

Back
Top Bottom