Karume atengwa, picha zake zachanwa Z’bar


KIGENE

KIGENE

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
1,113
Points
1,250
KIGENE

KIGENE

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2011
1,113 1,250
WATU wasiojulikana wamechana mabango yenye picha za Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Zanzibar, huku umati mkubwa ukijitokeza kumpokea Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM Zanzibar, Rais Dk. Ali Mohammed Shein. Mabango hayo yakiwa na ujumbe wa harakati za maendeleo wakati wa uongozi wake yamechanwa na kuchomwa moto siku chache tangu kutokea mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.

Picha za rais huyo mstaafu na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar zilionekana kuchanwa katika makunato ya barabara ya Kiembesamaki, Michenzani na kuibua shangwe kutoka kwa wanachama wa CCM Zanzibar jana. Dk. Shein alipokewa juzi kwa kishindo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar na wanachama na viongozi wa serikali baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Mabango hayo yenye nguzo za chuma yalipambwa na serikali katika kuunga mkono juhudi za maendeleo zilizokuwa zikifanywa na Karume na kuweka ujumbe wa maneno na picha kubwa "Rais Amani Karume kinara wa maendeleo Zanzibar," yalisomeka kabla ya kuchanwa.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili mjini Zanzibar umebaini kuwa kumekuwapo na maelewano mabaya kati ya kiongozi huyo mstaafu na wanachama wa CCM Zanzibar kutokana na kutofahamika msimamo wake kuhusu Muungano tangu Jumuiya ya Uamsho ilipoanza kufanya kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani visiwani Zanzibar.

Wakizungumza kwa wakati tofauti baadhi ya Wana CCM jana walisema kwamba kitendo cha Karume kuwafananisha na akili za samaki wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM katika hotuba yake ya shukrani pia kumechangia wanachama kupoteza imani dhidi yake na kuamua kuchana mapambo ya picha zake mitaani. Haji Ali Kombo, mkazi wa Amani, Zanzibar (45), alisema mafanikio ya Karume ya kisiasa na yake binafsi yasingefanikiwa bila ya wanachama kumpa ridhaa ya kuwaongoza, licha ya kuanguka katika kura za maoni mwaka 2000.

Mussa Hashim Mussa (65), mkazi wa Dimani, alisema pamoja na Karume kuanguka katika kura za maoni mwaka 2000, bado viongozi Tanzania Bara walimbeba, lakini sasa anashindwa kutetea hata misingi ya Muungano wa Tanzania.
Alisema wanachama na viongozi walimpa ridhaa ya kuaongoza kwa heshima ya baba yake, licha ya kuangushwa vibaya katika kura za maoni na wanasiasa wakongwe Zanzibar, akiwamo Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Karume aliamua kuwafananisha na akili za samaki wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM walipoanza kukatisha hotuba yake na kumzomea baada ya kuonekana mzito kuzungumzia kwa uwazi vurugu za Uamsho Zanzibar. Makada hao wa CCM walianza kukatisha hotuba yake na kumtupia lawama kuwa alishindwa kutetea misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kuwa mzito kukemea vurugu zilizokuwa zikifanywa na Uamsho na kuchafua hali ya kisiasa na kusababisha makanisa, baa na mali za serikali kuchomwa moto Zanzibar.

Hata hivyo, tayari viongozi wanane wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya uharibifu wa mali na kuhatarisha usalama wa taifa, ambapo dhamana zao zimefungwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim.

Hata hivyo, kauli ya Karume kuwafananisha wajumbe wa mkutano huo na akili za samaki imepokewa kwa shangwe na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), ambao wamekuwa wakishangilia, wakimaanisha kuunga mkono kauli hiyo.

source :Tanzania Daima
HALI imezidi kuwa tete visiwani Zanzibar kutokana na watu wasiojulikana kuendelea kusambaza vipeperushi vya kumkashifu Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi, Aman Abeid Karume, kutokana na hotuba yake aliyoitoa mjini Dodoma.

Matamshi ya kuwafananisha baadhi ya wajumbe na samaki, yameonekana kuwakera wakazi wa Zanzibar, ambapo sasa kasi ya kusambaza viperushi vya kumpinga na kumkashfu imeongezeka.
Jana, gazeti hili lilishuhudia baadhi ya vipeperushi hivyo ambavyo vilikuwa vikisambazwa kwa ustadi wa hali ya juu vikiwa na ujumbe tofauti kwa kiongozi huyo, huku vingine vikiwa na matusi ambayo hayaandikiki.

Mathalan kipeperushi kimojawapo kiliandikwa hivi: "Karume asante kwa kutuita samaki lakini kumbuka samaki hao walikuchagua kwa vipindi viwili vya miaka 10. Usimtukane mamba kabla hujavuka mto!"

Pia vilikuwepo vingine vilivyoandikwa vikidai kuwa Karume alimwangukia sana Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ili kuweza kuteuliwa kuwania kipindi cha pili.

Huku vingine vikisomeka kuwa Amani si mtoto halali wa Mzee Abeid Aman Karume na vinginevyo.
Juzi mabango yenye picha za Karume na ujumbe wa harakati za maendeleo wakati wa uongozi wake, yalichanwa na kuchomwa moto siku chache tangu kutokea mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.

Source : Tanzania Daima.
 
J

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Messages
2,758
Points
2,000
J

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2012
2,758 2,000
na huo ndio mwisho wake kisiasa. hatabebwa tena. UAMSHO NA YEYE WOTE BYEBYE!!
 
K

Kadogoo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2007
Messages
2,072
Points
1,195
K

Kadogoo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2007
2,072 1,195
na huo ndio mwisho wake kisiasa. hatabebwa tena. UAMSHO NA YEYE WOTE BYEBYE!!
Halafu wanachama, wafuasi, mashabiki na wakereketwa wa Uamsho wote wafukuzwe Zanzibar au wafungwe wote ndipo Zanzibar itatulia?
 
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
4,214
Points
0
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
4,214 0
Haaa,kweli zanzibar kazi bado mbichi!
 
mopaozi

mopaozi

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
3,308
Points
1,250
mopaozi

mopaozi

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
3,308 1,250
Bado haibadilishi ccm kuendelea kutawala milele
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225
Sasa yule MDOGO wake aliyekuwa BALOZI Ujerumani kwa MUDA MREFU Sana atagombea URAIS????
Sababu ndani ya FAMILIA yake kuna MADOSARI kibao; Pia SHEMEJI yao... Jamaa aliyeoa Dada yao PIA ana UAMSHO na yuko CCM...

FUNNY... MADARAKA MATAMU KWELI!!! Tatizo ndio hilo CCM wanabebana Sana...
 
K

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Messages
1,150
Points
2,000
Age
39
K

Kwameh

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2011
1,150 2,000
Wapi nitapata nakala au audio/video ya speech ya mwisho ya Karume mkutano wa CCM?
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,196
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,196 2,000
HIvi kweli Karume bila Muungano angekuwa hapo alipo? Miye hotuba yake ya juzi ile ilinishangaza kuwa kulikuwa na watu wanassikiliza...
 
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
Nairobi husema kimeumana. Ni vizuri kuwa CCM inaanga kumeguka ambapo wanageuziana mitutu. Baada ya Karume kufichuliwa kuwa ni mwanachama wa Uamsho alighafirika na kutukana kama vile si kiongozi. Aliwaita wana CCM wenye akili ndogo yaani ubongo wa samaki. Maskini hakujua kuwa wanamjua na jeuri aliyo nayo imetoka kwao nao wanalijua hilo. Sasa wameanza kumvua nguo. Natamani wamshughulikie na Kikwete na genge lake ili tupate ukombozi. Badala ya kukanusha tuhuma anadandia matusi. Sasa ona aibu imemkuta ambapo picha zake zinachanwa chanwa utadhani ni Mubarak wa Misri alipopigwa teke. Tunaomba wazenj watwambie hata yule aliyesaidia Iran kutumia bendera yetu kufanya biashara yake ya mafuta baada ya kuwekewa vikwazo.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,203
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,203 2,000
Hivi na yule bingwa wa matusi, Ismail Jusa Ladu, naye kapotelea wapi?
 
T

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Messages
1,917
Points
2,000
T

Taso

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2010
1,917 2,000
Miye hotuba yake ya juzi ile ilinishangaza kuwa kulikuwa na watu wanassikiliza...
Samahani Mkubwa, nashindwa kujizuia kurudia alichosema Karume, kwamba hizi ndio zenyewe "akili za Samaki." Mlimpa nafasi ya kutoa nasaha zake ili aseme nini ambacho chama kizima au Watanzania wote mngekubaliana nae, Neno la Uzima na hadithi za Mtume? Unashangaa waliendendelea kumsikiliza, ulitaka wampopoe mayai-viza ashuke jukwaani? Kutaka kuhubiriwa imani yako ya mawazo yale yale tu ndio alizosema "akili za samaki!"

To the more substantive matter, would Karume be where he is were it not for the Union? Most definitely. For starters, Karume got where he is because of his pedigree, his father's name ramrodded him to leadership even when his party bucked him (Billal actually shellacked him miserably in party polls). And his father is far from a creature of the Union. The elder Karume was President of a country before he was demoted to a vice in the advent of the Union. In the same sense, it is not farfetched to say that outside the Union Karume could have given the farewell speech as the head of Afro Shiraz Party, not as a second fiddle to Dodoma's party hochos.

Amani Karume owes the Union nothing!

Down with the Union!
 
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
4,214
Points
0
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
4,214 0
Ni yaleyale ya kujuana ya ccm, kikwete anapendelea kwao, mfano barabara ya kutoka tanga kwenda bagamoyo imekaa tu kama pambo haitumiki ipasavyo lakini imejengwa kwa lami. Ni upendeleo wa wazi.
 
masopakyindi

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Messages
14,547
Points
2,000
masopakyindi

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2011
14,547 2,000
HIvi kweli Karume bila Muungano angekuwa hapo alipo? Miye hotuba yake ya juzi ile ilinishangaza kuwa kulikuwa na watu wanassikiliza...
Mkuu MMKJJ mbona wajumbe walimuimbia " Uamsho bye bye"!
 
masopakyindi

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Messages
14,547
Points
2,000
masopakyindi

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2011
14,547 2,000
Hivi na yule bingwa wa matusi, Ismail Jusa Ladu, naye kapotelea wapi?
Wafadhili wa uamsho wamesambaratika kiaina.
Hebu cheki safu yao:
  • Karume-Nje CCM!
  • Sheikh Khalid-lupango
  • Waziri Himid-uwaziri Zanzibar nje
  • Sheikh Sherrif Hamad-amebaki kulalama kuwa kuna uonezi Zanzibar(lakini hakulalamika askari polisi alipouwawa)
Ismail Jussa alijua analindwa na wafadhili wake au kuelekezwa kutamka matusi yale.

Na Nyerere was right, cheki vizuri safu hyo, hakuna mmbantu hapo!
Wanakula nyama ya mtu hao!!
Waliwabagua Wabara sasa wanawabagua waafrika Zanzibar!!!
 
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Points
195
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 195
Huyo ndo karume a.k.a Mtoto wa diria,mwana uamsho mkubwa asiye na chembe hata ya shukrani kwa muungano uliombeba,atakula jeuri yake sasa.
 

Forum statistics

Threads 1,283,904
Members 493,869
Posts 30,805,593
Top