Karume atengwa, picha zake zachanwa Z’bar

Karume atengwa, picha zake zachanwa Z’bar

Karume hakutukana wananchi....bali aliwaambia ukweli wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM (ambao hawawakilishi wananchi wote)
Mkuu tusi na ukweli mara nyingine ziko kwenye sarafu moja yenye pande mbili.
Ukitaka kusema ukweli unaouma hekima inahitajika ili kutowatusi hata wazazi wako.

Ni dhahiri msemo wa " akili ya samaki" kama umekufurahisha , kuna ambao imewaudhi, tena kwa sababu nzuri tu.
Wengi Wazenji wanashangaa leo wanaambiwa wana akili ya samaki wakati walimbeba jamaa hata pale ambapo hakustahili.
Shukurani ya punda mateke!!!
 

[TD="bgcolor: #ffffff"][/TD]

HALI imezidi kuwa tete visiwani Zanzibar kutokana na watu wasiojulikana kuendelea kusambaza vipeperushi vya kumkashifu Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi, Aman Abeid Karume, kutokana na hotuba yake aliyoitoa mjini Dodoma.

Matamshi ya kuwafananisha baadhi ya wajumbe na samaki, yameonekana kuwakera wakazi wa Zanzibar, ambapo sasa kasi ya kusambaza viperushi vya kumpinga na kumkashfu imeongezeka.
Jana, gazeti hili lilishuhudia baadhi ya vipeperushi hivyo ambavyo vilikuwa vikisambazwa kwa ustadi wa hali ya juu vikiwa na ujumbe tofauti kwa kiongozi huyo, huku vingine vikiwa na matusi ambayo hayaandikiki.

Mathalan kipeperushi kimojawapo kiliandikwa hivi: “Karume asante kwa kutuita samaki lakini kumbuka samaki hao walikuchagua kwa vipindi viwili vya miaka 10. Usimtukane mamba kabla hujavuka mto!”

Pia vilikuwepo vingine vilivyoandikwa vikidai kuwa Karume alimwangukia sana Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ili kuweza kuteuliwa kuwania kipindi cha pili.

Huku vingine vikisomeka kuwa Amani si mtoto halali wa Mzee Abeid Aman Karume na vinginevyo.
Juzi mabango yenye picha za Karume na ujumbe wa harakati za maendeleo wakati wa uongozi wake, yalichanwa na kuchomwa moto siku chache tangu kutokea mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.

Source : Tanzania Daima.

hamna kipya kwani ndio siasa za ccm, mtu akiwaambia ukweli humzulia hata uongo usiokuwepo. sishangai wao kusema Amani sio mtoto wa Karume kwani hata Nape alipowaambia ukweli ccm makamba/ccm walitamka kuwa sio mtoto wa Nnauye,

ccm wanashangaza kila siku kwa maneno na matendo yao
 
Hawa siku zote wanabebwa tu na yule mdogo wake alivyokuwa balozi kwanza alikuwa haelewi cheo chake na madaraka yake. kazi walikuwa wanafanya makaimu wake yeye akilala ofisini, sasa aje kuongoza ZNZ nani anamtaka? Kwanza na familia yeyewe haitakiwi Zanzibar kutokana na madosari kibao ndani ya familia yao kama vile ubakaji, na vitu kibao ambavyo wazanzibari wengi wanajuwa na kunung'unika mitaani, hawafai na hawatakiwi Zanzibar, waishukuru CCM tu.

Nilisikia Huyo KAKA Mtoto wa KARUME aliyekuwa RAIS; Mkwewe alinunua JENGO MJINI Maeneo ya STONE TOWN Reserved Building... Nasikia alishalichukua na Wakati Karume anamaliza Madaraka yake, Wakaambiwa SIO LAO

Najua Mwanae Mmoja wa KIKE ni WAKILI sijui aliichukua hiyo kesi Kumsaidia MAMA yake?
 
karume ameodhi sana zanzibar amekwiba sana huyu jamaa sheli zote za mafuta Znz kipindi chake lazima kuna fungu kila mwaka wapeleke kwake na ardhi amechukua sehem kubwa huyu jamaa amefanya ufisadi, CCM wana uwezo mkubwa wa kumshusha na kuwa kapuku kabisa, kama alivyomfanyia Dr Salmin basi naye yatamkuta asipojitazama mapema. Hakustahili kusema sababu sera ya chama chake inambana so hata kama ameshapita Urais wake lakini bado hajavuka mto, jamaa wana uwezo mkubwa wa kumfanya akalia zaidi ya Salmin, karume anaamini uwepo wa Serikali 3 basi yeye ni rahisi kupata tena madaraka uku akiwa amemsahau Seif Shariff kuwa naye anayataka madaraka hata kwa kisu, hii ni hatari Viongozi wamekuwa waroho sana, me naona ni Udhaifu na tamaa kila mtu anatekeleza sera ya chama chake na kukijenga chake,sera ya serikali 3 ni ya CHADEMA so Karume anawapigia Debe bila kujijua, Seif Sharif hawezi kupewa Nchi hata mara moja kwa kupitia chama cha CUF kwa sababu za kintelejesia, Cuf hawapewi daima mpaka labla wachange roho zao.

Chama cha CUF upande wa Zanzibar ni chama cha ubinafsi chama kisichotaka watu wa bara chama kinalingania maslahi ya watu kutoka Pemba kwa hudi na uvumba Seif sharif anataka madaraka na akiyashka Nchi lazima aipeleke kipemba pemba na kufanya ubinasi kama asili yao....Ili aliliona R.IP Abeid Karume katika hotuba yake moja alisema maneno hayo.
 
Diria na Karume wamepishana miaka minne...Wazanzibar wapo wachache sana sijui kwa nini wanashindwa kuwa na umoja.

Mh, ina maana Diria alimzaa Karume akiwa na miaka minne? hapo sasa, endelezeni majungu, ngoja nikasome kidogo
 
Mkuu tusi na ukweli mara nyingine ziko kwenye sarafu moja yenye pande mbili.
Ukitaka kusema ukweli unaouma hekima inahitajika ili kutowatusi hata wazazi wako.

Ni dhahiri msemo wa " akili ya samaki" kama umekufurahisha , kuna ambao imewaudhi, tena kwa sababu nzuri tu.
Wengi Wazenji wanashangaa leo wanaambiwa wana akili ya samaki wakati walimbeba jamaa hata pale ambapo hakustahili.
Shukurani ya punda mateke!!!

Acha wavune walichopanda. Kwani mtu anachaguliwa kwa kubebwa au kwa sera zinazokidhi wanaomchagua???
 
Karume ana haki ya kutoa maoni yake.Hao wahafidhina wanaingia kichwa kichwa .wataumbuka

Kuna mfumo kristo zanzibar ndio sababu itakayotumika kukwepa kuwajibika.

Tutaambiwa ni mfumo kristo umesambaza vipeperushi.
 
Mh, ina maana Diria alimzaa Karume akiwa na miaka minne? hapo sasa, endelezeni majungu, ngoja nikasome kidogo

Kumbe na zanzibar kuna uzinzi nilidhani kwa kuwa asilimia kubwa 99% ni waislamu na Mahakama ya kadhi ipo hakutakuwa na uzinifu ambao ni kwa ajili ya makafri tu.
 
Source yenyewe ndo hiyo gazeti la vitumbua.Tupa kwa toilet huko
 

[TD="bgcolor: #FFFFFF"][/TD]


Mathalan kipeperushi kimojawapo kiliandikwa hivi: "Karume asante kwa kutuita samaki lakini kumbuka samaki hao walikuchagua kwa vipindi viwili vya miaka 10. Usimtukane mamba kabla hujavuka mto!"



Source : Tanzania Daima.

Mi nakumbuka tabia ya kusambaza vipeperushi vinavyowachafua watu tulikuwa nayo darasani wakati nikiwa darasa la tatu... Na nakumbukuka niliwahi kucharazwa viboko vingi sana na mwalimu aliyefahamika kama Stella baada ya kipeperushi changu kugundulika...
Ni tabia ya kitoto na ya kijinga sana ambayo najiuliza kama wanaofanya hivyo huko Zanzibar ni watu wazima au watoto, na kama wanawakilisha akili za Wazanzibari...
 
Wandugu hivyo ndiyo picha halisi ya CCM ilivyo. Ni mwana CCM gani anaweza kupoint baya moja tu ambalo Karume alisema katika speech yake?

So kama alichosema ni kweli, maana yake ni kuwa CCM haitaki uhuru wa maoni, inatubabaisha tu. For any reasonable person, ile ilikuwa ni starting point ya kufikiria kama yuko katika chama ambacho kina mustakbali mzuri kwa taifa hili.

Kama ule ulikuwa ni mkutano mkubwa wa chama kinachoongoza taifa, na viongozi wote wakuu walikuwepo lakini hakuna hata mmoja ambaye alikuwa na ujasiri wa kusimama na kusema, 'HAPANA, HII SI CCM TUITAKAYO', huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu kuongozwa na viongozi hawa!
 
hamna kipya kwani ndio siasa za ccm, mtu akiwaambia ukweli humzulia hata uongo usiokuwepo. sishangai wao kusema Amani sio mtoto wa Karume kwani hata Nape alipowaambia ukweli ccm makamba/ccm walitamka kuwa sio mtoto wa Nnauye,

ccm wanashangaza kila siku kwa maneno na matendo yao

Karume alikuwa na nafasi ya kufanya mageuzi wakati wa utawala wake wa miaka 10 kwa sasa anafanya vurugu kwa Rais wa sasa Dk. Shein.

ilitumika nguvu kubwa sana hadi serikali ya umoja wa kitaifa ikaundwa chini ya utawala wake na mauaji ya Pemba kwa mara ya kwanza wakawa wakimbizi.

mwendo anaokwenda nao sasa Karume ni kama hakuwahi kuwa Rais wa znz angewapa uhuru wazanzibar kuamua na kusikilizwa.
 
Kumbe na zanzibar kuna uzinzi nilidhani kwa kuwa asilimia kubwa 99% ni waislamu na Mahakama ya kadhi ipo hakutakuwa na uzinifu ambao ni kwa ajili ya makafri tu.

Umesahau kuvaa nguo za kufunika maeneo yote, si inazuia uzinzi? au
 
Mi nakumbuka tabia ya kusambaza vipeperushi vinavyowachafua watu tulikuwa nayo darasani wakati nikiwa darasa la tatu... Na nakumbukuka niliwahi kucharazwa viboko vingi sana na mwalimu aliyefahamika kama Stella baada ya kipeperushi changu kugundulika...
Ni tabia ya kitoto na ya kijinga sana ambayo najiuliza kama wanaofanya hivyo huko Zanzibar ni watu wazima au watoto, na kama wanawakilisha akili za Wazanzibari...

Jibu rahisi utaambiwa ni mfumo kristo unaoyumbisha znz, syria, afghastan nk.
 
Karume alimfanyia fitina Salim na kumsingizia alishiriki katika kumuua baba yao, sasa dhambi ileile aliyo mfanyia mwenzake ndo inamtafuna, mtazamo wangu huyu mlevi atakufa muda sio mrefu kwa depression.

anavuna alichopanda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom