Kandambilimbili ametutoka RIP

Kandambilimbili ametutoka RIP

Ninja

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
361
Reaction score
722
Mwenzetu Kandambilimbili alitutoka tangu 26/12/2010 jumapili na amezikwa jana kwao Bukoba.

Alizaliwa mwaka 1971 hivyo ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa na tatizo la kisukari tangu muda mrefu lakini halikuwa kubwa sana na aliweza kulimudu vema kwa muda wa zaidi ya miaka 10. Wiki iliyopita sukari ilisumbua na kusababisha 'stroke' na akalazwa Mikocheni hospital na ndipo umauti ukamkuta.

Poleni wana JF wote kwa kuondokewa na mmoja wetu.

RIP Kandambilimbili (Real Name: Baruti, formely TAA member of staff).
 
Innalillah wainailaih rajiuun,
Bwana alitoa na bwana ametwaa,
 
dah! For some moments in life there are no words.
 
Poleni sana Wafiwa. Wish family,relatives and friends can remain strong in this difficult time.RIP Kanda2.
 
Pole sana wafiwa. Mungu awape moyo wa subira na uvumilvu wa kupotelewa na ndugu yenu.:embarrassed:
 
Mungu ailaze roho ya marehemu Kandambilimbili mahali pema peponi. Ameni
 
May the soul of our beloved brother REST IN PEACE! eee Mungu muumba Mbingu na ardhi wajarie nguvu na uvumilivu familia ya ndugu yetu Kanda2 hasa kipindi hiki kigumu cha kuomboleza maondokeo ya mpendwa wetu! amen
 
Upumzike kwa amani Kandambilimbili. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina la Bwana na litukuzwe.
 
Dah, Pole sana wafiwa, RIP Kandambilimbili

Tunaweza pata picha yake? Only if that is allowed at this stage
 
SAD ... RIP Kamanda Baruti ...

"...when my eyes shall close in death,
...when I soar to worlds unknown,
...see thee on Thy judgment throne,
... rock of ages, cleft for me,
... let me hide myself in Thee"
 
Mwenzetu Kandambilimbili alitutoka tangu 26/12/2010 jumapili na amezikwa jana kwao Bukoba.

Alizaliwa mwaka 1971 hivyo ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa na tatizo la kisukari tangu muda mrefu lakini halikuwa kubwa sana na aliweza kulimudu vema kwa muda wa zaidi ya miaka 10. Wiki iliyopita sukari ilisumbua na kusababisha 'stroke' na akalazwa mikocheni hospital na ndipo umauti ukamkuta.

Poleni wana JF wote kwa kuondokewa na mmoja wetu.

RIP Kandambilimbili ( Real Name: Baruti, formely TAA member of staff).
Ni ajabu sana hili jambo.
Ndio leo najua kuwa Baruti Mwesiga ndiye tuliyekuwa tunamwita Kandambilimbili!...
Kwa ufupi namfahamu vizuri sana huyu mkuu!...Alikuwa mhasibu kwa taaluma, na alikuwa mcheshi sana, ukiachilia mabandiko yake ya kusisimua.

Ama kweli dunia tunapita!..
Mungu ailaze roho ya Marehemu pahalapema peponi.
 
Back
Top Bottom