Kamlete - akibisha...

Nadhani bora tuombe ma MOD wabadilishe kichwa cha habari na kuwa "down memory lane"... maana mwisho tutakumbushana mambo ya "ukuti ukuti" na kitu hiki hapa ambako JokaKuu amekigusia. Nakushauri usibonyeze kusikiliza usije kunilaumu na kutaka JF ifungiwe bure!
 

Attachments

  • usisikilizehili.mp3
    385.7 KB · Views: 70
aaaaaaaaaaaaahhhhhhh badala ya vithlani sasa yamegeuka kuwa mambo ya vitabu? ni ajabu sana hii!!!! sasa hapa tujadili lipi?
 
Mwanakijiji,

..utanisamehe kwa kukuharia topic. lakini mmenikumbusha mbali sana.

..kabla ya kuanza kusoma vitabu, tulikuwa tukifaidi hadithi za kusimuliwa na bibi,babu,mjomba, au shangazi.

..tena basi kulikuwa na hadithi nyingine za kutisha. watoto wa siku hizi wanatazama horror movies!!

..vilevile usisahau kuimba. i dont see kids singing these days.
 
Mwanakijiji,

..utanisamehe kwa kukuharia topic. lakini mmenikumbusha mbali sana.

..kabla ya kuanza kusoma vitabu, tulikuwa tukifaidi hadithi za kusimuliwa na bibi,babu,mjomba, au shangazi.

..tena basi kulikuwa na hadithi nyingine za kutisha. watoto wa siku hizi wanatazama horror movies!!

..vilevile usisahau kuimba. i dont see kids singing these days.

Tatizo ni mijini. Huko vijijini, hadithi zinaendelea na watoto wanaimba sana. Tena hata mchakamchaka na bendi zipo wala mambo ya horror movies hakuna kabisa huko vijijini.
 
Tarehe 6 Disemba mwaka 2007 Helikopta ya Jeshi la Wananchi ilianguka kwenye ziwa Natron huku na kujeruhi watu kadhaa wakiwemo wale ambao walidaiwa kuwa ni "Wageni wa serikali" ambao walikuwa na vifaa vya kupigia picha za filamu katika ziwa hilo na taarifa za awali zilisema pia kupiga picha mlima wa Oldonyo Lengai.

Na jana Helikopta nyingine imeanguka mkoani Arusha na kuua watu wote sita waliokuwemo kwenye chopa hiyo ambayo ilikuwa inatoka Arusha kuelekea Dodoma.

Ndege zote hizo mbili zinaunganishwa na yule dalali maarufu Bw. Shaileth Pragji Vithlani ambaye ndiye aliyeshughulikia mchakato wa kuzipata ndege hizo na kuwaunganisha JWTZ huku yeye mwenyewe akiwa mabilioni ya shilingi mfukoni kama gharama yake ya udalali. Bw. Vithlani ndiye dalali huyo huyo aliyeshiriki katika ununuzi wa rada ambako inadaiwa kuwa alikatiwa karibu Shs. Bilioni 21 kama malipo yake ya udalali wa kazi yake.

vithlani2.JPG

Kwa vile sasa inaonekana helikopta zake hizo zote zina matatizo, jambo la kwanza ambalo tunapenda kutoa wito.

a. Kusitisha kuruka kwa helikopta zote za Jeshi hadi uchunguzi huru wa kitaalamu wa airworthness ufanywe na kuona kama zinafaa kuendelea na huduma.

b. Endapo helikopta hizo zilizoanguka na zile zilizopo bado zilionekana zina defects zozote za msingi basi Bw. Vithlani pia afunguliwe mashtaka ya manslaughter au criminal negligence kutokana na kuchangia vifo vya watanzania hao na pia kulisababisha Taifa hasara.

c. Maafisa waliohusika na ununuzi wa helikopta hizi wachukuliwe hatua mara moja ikiwemo kufunguliwa mashtaka ya kijeshi.

d. Serikali imtafute huyo dalali kabla na yeye hajafa na kuzikwa huko huko Uswisi siku chache zijazo na mwili wake kuteketezwa kwa moto kwa desturi za kwao!!

Vinginevyo kama kina Rashid Othman wanauwezo wa kukifanya kile Waisrael walikifanya baada ya mauaji ya Munich ya 1972 ambapo maafisa wake wa Usalama waliwafanyizia wale wote waliohusika na mauaji hayo bila kujali nchi walizopo. Ni wakati wa kutuma kikosi chetu (kama hakipo kianzishwe) cha kuwashughulikia watu kama hawa ambao wanafanya uhalifu Tanzania halafu wanakimbilia nje ya nchi.

Tuwatume waende "wakamlete.. akibisha... "

sssshhhhhhhh jamani semeni polepole wasiwasikieni maana nawaona wanauma meno. Kwani huyu mtanzania wa Asia wao hawafahamu kweli aliko?
Kwani deal zote wakati wa kuzipanga huwa hawajui wanam contact vipi?
Haya matangazo mengine yanawafanya tuwaone ni wajinga kweli! hivi wanamdanganya nani?
Haiwezekani kwamba jeshi linafanya deal na mtanzania tena wa Asia bila kuwa na lead ya mtu mkubwa fulani.
Sasa yaelekea na jeshi letu limekwisha kabisaaaaaaaa maana siri zetu zotee za ulinzi nje nje.
Alafu na hawa tunawaita usalama wa nini vile? Viongozi wa nchi na familia zao sijui? kwani kweli hawajui lolote? mbona wana na kamkono kao humo humo jeshini?
Tena hata hao wenyewe ni wanajeshi maana wana ranks za jeshi. AAAAAAAAa haya mambo ukiyafikiria nakuambia utatushangaa wadanganyika. Hivi nitumie nini ili nipate usingizi nisiendelee kukumbuka mambo ya nchi hii Danganyika?
 
jamani taratibuni kwani hili tangazo si kalibuni tu ndugu yetu mkjj au ndio polisi imetangaza na kutoa tangazo hili?


mie nnavyojua siku hizi mkjj anaitaka ile nafasi ya muigizaji yomba yomba si mnamkumbuka?
 
mtu wa pwani.. usilete mambo ya "Chale mnene na Chale Mwembamba".. hili tangazo ni la muda lakini kutokana na matukio ya kuanguka chopa jana nadhani kuna haja ya kumkamata huyu jamaa na kumtia pingu mapema iwezekanavyo.
 
aaaaah...nani aliwinda ndege hapa? mnakumbuka majina ya ndege nyie....mi vyangu vilikuwa visota tu......

Mi nakumbuka "sholwe." Kuna mtoto mmoja alikuwa mkali wa kutengeneza manati kwa sababu alikuwa anajua kuchonga 'vipago.' Halafu alikuwa anajua kuchagua mipira mizuri ya manati, manake ipo ya aina mbili, isiyo vutika na mingine premium inavutika. Baba yangu alikuwa akikuona na manati anaweza kukuua!

Umewahi kuendesha magari ya madebe yenye matairi ya vipande vya ndala?
 
speaking of manati.. kwanini tulikuwa tunapaka damu kwenye ile Y ya manati (hata jina limenitoka).. Halafu kuna yule ndege mwenye mkia mrefu ati ukimpata yule basi ukimgusa mdada tu...
 
speaking of manati.. kwanini tulikuwa tunapaka damu kwenye ile Y ya manati (hata jina limenitoka).. Halafu kuna yule ndege mwenye mkia mrefu ati ukimpata yule basi ukimgusa mdada tu...

Ile Y ya manati ndio "Kipago."

Siku hizi watu wanasema na Video games, na vi MP3 players. Nadhani sisi tuli have fun zaidi!
 
Ile Y ya manati ndio "Kipago."

Siku hizi watu wanasema na Video games, na vi MP3 players. Nadhani sisi tuli have fun zaidi!

mp3 player siku hizo tulikuwa na Sony Walkman. Yaani hiyo Trade Mark ya Walkman mpaka ikawa neno, ukiwa nayo hiyo mjanja wewe na mtaa mzima utajipanga kutaka kuiazima.
 
Mi nakumbuka "sholwe." Kuna mtoto mmoja alikuwa mkali wa kutengeneza manati kwa sababu alikuwa anajua kuchonga 'vipago.' Halafu alikuwa anajua kuchagua mipira mizuri ya manati, manake ipo ya aina mbili, isiyo vutika na mingine premium inavutika. Baba yangu alikuwa akikuona na manati anaweza kukuua!

Umewahi kuendesha magali ya madebe yenye matairi ya vipande vya ndala?

Ahahahahahaaaaa....Kuhani umeniacha hoi kishenzi!! Nakumbuka sana magari ya makopo na matairi ya vipande vya ndala. Usukani ni mti uliofungwa na kamba...kuna kamba flani hivi zilikuwaga bomba kishenzi...ila nimezisahau jina lake...

Halafu unakumbuka mipira iliyokuwa inatengenezwa na manailoni halafu unaifuma na kamba? Hii ndo ilikuwa alternative yetu ya magozi kwa vile yalikuwa adimu sana. Mdingi akienda kiwanja akikuletea gozi kama zawadi basi mwenyewe unataaamba...Lol.
 
Ukiona watu wanakumbushana sana vitu vilivyopita ujue washazeeka hao.

Whats next? Vita vikuu vya pili Burma, Sudan na North Africa?

Tutafungua tawi la Tanzania Legion sasa hivi hapa, na kuorodhesha askari Keya (King's African Rifle)
 
Ukiona watu wanakumbushana sana vitu vilivyopita ujue washazeeka hao.

Whats next? Vita vikuu vya pili Burma, Sudan na North Africa?

Tutafungua tawi la Tanzania Legion sasa hivi hapa, na kuorodhesha askari Keya (King's African Rifle)

Not necessarily....we're just wallowing in nostalgia....

At the same time, yes, umri unazidi kwenda....wengine washaoa na watoto sasa hivi....
 
Agoro Anduru umenikumbusha nadhani ndiyo alikuwa na ile "Rosa Mystica" siyo?

'Rosa Mistika' nafikiri pia ni kitabu cha Musiba bila kusahau Njama.Agoro Anduru kitabu chake kingine kilichonivutia ni 'Temptesheni' samahani namaanisha Temptation.Natamani nikipate sasa ili nikisome tena
 
Last edited:
Hivi Musiba alikuwa haibi artwork? I have a feeling kwamba alikuwa ana "tafsiri" novel za kizungu na kuziuza nyumbani kama kazi yake. Ebu niambie story zote za CIA, KGB, et la...na mambo ya uninja kwenye novel zake alikuwa haziibi kwenye novel za kizungu? Yaani novel zake zilikuwa kama movie vile...

By the way, yuko wapi huyu mtu siku hizi?

QM,
Musiba yupo. Amejaa pale Mikocheni mtaa wa Warioba.
 
Ile Y ya manati ndio "Kipago."

Ni kweli kabisa Y ya manati ilikuwa inaitwa 'Kipago' ila sasa hivi uwe makini hilo jina 'Kipago' lina maana tofauti kwa sasa hasa kwa vijana wa kiume wanapozungumzia bayolojia .

Lugha ni hai,huzaliwa,hukua na hufa.
 
Back
Top Bottom