RPC wa Arusha anatuhumiwa kuficha tukio la askari polisi kumuua dereva wa magari ya watalii Omari Msamo

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Je ni sahihi wananchi kujichukulia sheria mkononi wakamuua RPC wa Arusha? Kama sio sahihi basi tunataka kuona askari wa usalama barabarani Arusha waliojichukulia sheria mkononi kwa kumuua Omari Msamo wanafikishwa mahakamani. Huu ujinga wa polisi kujiona wako juu ya sheria na wanaweza kufanya chochote ukomeshwe sasa.

Sisi kama wadau wa haki na utawala wa sheria tutaanza kuchukua hatua ambazo tutaona zitaleta uwajibikaji kwa RPC wa Arusha na askari waliohusika na mauwaji hao. Tumepata taarifa ambazo bado tunazifanyia kazi kwamba RPC wa Arusha na maafisa wengine wanafanya juhudi za kuzima jambo hili ili lisijulikane.

Haya matukio ya watu kufia mikononi mwa polisi yamekuwa mengi. Huu ni uthibitisho kwamba askari wengi ndani ya jeshi la polisi wanatumia nguvu nyingi kuliko akili. Pengine tatizo hili linatokana na mafunzo ambayo hayakidhi vigezo na wala hayaendani na wakati kipindi hiki ambacho technology inakua kwa kasi. Ndio maana tangu mwanzo nasisitiza kuwa hili jeshi limekosa sifa za kulinda raia na mali zao, hivyo kuna ulazima wa kulifanyia Overhaul .

Nitaelekea Arusha kuhakikisha haya mabumunda yanachukuliwa hatua haraka sana.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

GridArt_20240320_112324789.jpg

Pia soma - Arusha: Polisi wawakamata Waliohusika na Mauaji ya Dereva wa magari ya Watalii Omari Msamo
 
Mdude - "Tumepata taarifa ambazo bado tunazifanyia kazi".

Ingependeza zaidi kabla hujatuletea hii taarifa uwe umeshaenda kwanza Arusha kutafuta ukweli wa jambo husika, au kwanza umuulize mtu unayemuamini aliyepo Arusha akupe uthibitisho wa taarifa zenyewe, kuliko kuzileta kwanza halafu ndio unaenda Arusha kutafuta uthibitisho.

Nilitegemea ile taarifa yako ya mwisho uliyoileta hapa uliyodai upo mgodi wa dhahabu usiojulikana upo katikati ya msitu kule Tabora ikufungue macho, bahati mbaya naona bado una tabia ile ile, wacha mihemko, kwanza kusanya taarifa zakutosha ndio uwe unakuja kutoa ripoti zako hapa.
 
Ingependeza zaidi kabla hujatuletea hii taarifa uwe umeshaenda kwanza Arusha kutafuta ukweli wa jambo husika, au kwanza umuulize mtu unayemuamini aliyepo Arusha akupe uthibitisho wa taarifa zenyewe, kuliko kuzileta kwanza halafu ndio unaenda Arusha kutafuta uthibitisho.
Mvuta bangi hawezi akawa na mawazo kama hayo uliyomshauri. Yaani hana taarifa sahihi na ya ukweli na wala hana ushahidi lakini anakurupuka kutoa taarifa isiyo na ushahidi na kuanza kutukana na kukashifu jeshi letu la polisi. Kichwa na akili ya Mdude ilishaharibiwa na matumizi makubwa ya Bangi.
 
Push back ndio lugha wanayoitambua hawa watawala wetu,jeshi hili la police lipo kisiasa zaidi kuliko kisheria,ona kauli zote za hawa watawala ni kutishia kutumia police to settle the score,ukivaa jezi ya masandawana ...police watakuchukua na kwenda kukupumzisha huu ni ushenzi mkubwa,police wetu waitwe services badala ya forces,vizee vyote above 45 yrs ondoa,ingiza young blood ya 22yrs hadi 35yrs,train hawa kitaalamu ,traffic officer's peleka Botswana 🇧🇼 wakajifunze kwa miezi 6,wakirudi barabara zetu zitakua tofauti
 
Hatari sn
 
Mvuta bangi hawezi akawa na mawazo kama hayo uliyomshauri. Yaani hana taarifa sahihi na ya ukweli na wala hana ushahidi lakini anakurupuka kutoa taarifa isiyo na ushahidi na kuanza kutukana na kukashifu jeshi letu la polisi. Kichwa na akili ya Mdude ilishaharibiwa na matumizi makubwa ya Bangi.
Acha upumbavu huu,eti jeshi LETU la police,nani kakupa usemaji wangu?,jeshi hili Lina history ya mauaji mengi tu na pia lini IGP atanipa taarifa za crime statistics za nchi yangu hii?,je crime inapanda au kushuka ni haki yangu kujua hili
 
Tatizo ni chama police Arusha ni kundi la waalifu ukweli usemwe wakitaka kuuwa watuuwe sote tena hadharani kwa haki sio kwa kificho mimi huwa naona kabisa sikumoja nitakufa kwenye mikono ya hawa wa uwaji..
 
Kwako Mdude_Nyagali kuhusu RPC ni askari mwenye busara sana. kosa la polisi wa usalama barabarani mkoa wa Arusha, RPC asihusishwe kwa namna hiyo.
Inahitaji hekima na busara kwenye mambo ya aina hiyo, na huyo mzee(RPC) ni wa kaliba hiyo.
Asante
 
Je ni sahihi wananchi kujichukulia sheria mkononi wakamuua RPC wa Arusha? Kama sio sahihi basi tunataka kuona askari wa usalama barabarani Arusha waliojichukulia sheria mkononi kwa kumuua Omari Msamo wanafikishwa mahakamani. Huu ujinga wa polisi kujiona wako juu ya sheria na wanaweza kufanya chochote ukomeshwe sasa...
Weka ushahidi hapa wiki mbili zilizopita ulileta habari ya kuokoteza kama hii tukaenda kuchimba ikawa ni uongo na mod's wana acha makusudi nyuzi kama hizi zenye kuleta taharuki!
 
Back
Top Bottom