Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,762
- 40,987
Tarehe 6 Disemba mwaka 2007 Helikopta ya Jeshi la Wananchi ilianguka kwenye ziwa Natron huku na kujeruhi watu kadhaa wakiwemo wale ambao walidaiwa kuwa ni "Wageni wa serikali" ambao walikuwa na vifaa vya kupigia picha za filamu katika ziwa hilo na taarifa za awali zilisema pia kupiga picha mlima wa Oldonyo Lengai.
Na jana Helikopta nyingine imeanguka mkoani Arusha na kuua watu wote sita waliokuwemo kwenye chopa hiyo ambayo ilikuwa inatoka Arusha kuelekea Dodoma.
Ndege zote hizo mbili zinaunganishwa na yule dalali maarufu Bw. Shaileth Pragji Vithlani ambaye ndiye aliyeshughulikia mchakato wa kuzipata ndege hizo na kuwaunganisha JWTZ huku yeye mwenyewe akiwa mabilioni ya shilingi mfukoni kama gharama yake ya udalali. Bw. Vithlani ndiye dalali huyo huyo aliyeshiriki katika ununuzi wa rada ambako inadaiwa kuwa alikatiwa karibu Shs. Bilioni 21 kama malipo yake ya udalali wa kazi yake.
Kwa vile sasa inaonekana helikopta zake hizo zote zina matatizo, jambo la kwanza ambalo tunapenda kutoa wito.
a. Kusitisha kuruka kwa helikopta zote za Jeshi hadi uchunguzi huru wa kitaalamu wa airworthness ufanywe na kuona kama zinafaa kuendelea na huduma.
b. Endapo helikopta hizo zilizoanguka na zile zilizopo bado zilionekana zina defects zozote za msingi basi Bw. Vithlani pia afunguliwe mashtaka ya manslaughter au criminal negligence kutokana na kuchangia vifo vya watanzania hao na pia kulisababisha Taifa hasara.
c. Maafisa waliohusika na ununuzi wa helikopta hizi wachukuliwe hatua mara moja ikiwemo kufunguliwa mashtaka ya kijeshi.
d. Serikali imtafute huyo dalali kabla na yeye hajafa na kuzikwa huko huko Uswisi siku chache zijazo na mwili wake kuteketezwa kwa moto kwa desturi za kwao!!
Vinginevyo kama kina Rashid Othman wanauwezo wa kukifanya kile Waisrael walikifanya baada ya mauaji ya Munich ya 1972 ambapo maafisa wake wa Usalama waliwafanyizia wale wote waliohusika na mauaji hayo bila kujali nchi walizopo. Ni wakati wa kutuma kikosi chetu (kama hakipo kianzishwe) cha kuwashughulikia watu kama hawa ambao wanafanya uhalifu Tanzania halafu wanakimbilia nje ya nchi.
Tuwatume waende "wakamlete.. akibisha... "