Kamlete - akibisha...

Hicho ndio wanacho maanisha "land of milk and honey"? Laiti ningelijua!

Kroger na Meijers ni grocery stores?

Maana kuna matunda ambayo hata Kariakoo huyapati lakini nenda Pathmark na Wegmans! Kariakoo kuna makungu au matunda nyoka? Mi nshaona makungu Pathmark! Ninashaona mpaka mabungo na mastafeli kwenye grocery stores. Sijui wanayaibua wapi. Huwezi kuona sega la nyuki barabarani lakini Asari hukosi kwenye grocery store! Duuuh! Laiti!

Wewe hujawahi kuisikia Kroger? unaishi wapi mwenzetu, West coast?
 
Hivi si tuliambiwa serikali ina mkono mrefu inakuwaje huo mkono hauwezi kumfikia huyu bwana??????? Au ni mkono wa nguo nguo hivyo ukipigwa upepo kidogo unapinda na kushindwa kufika unapotakiwa!!!!!!!!!!!!
Ina mkono ufikao sehemu unazozitaka; kwao hili halijawa high priority bado, ikifikia at the top of TO DO LIST, "Na suspect akisema yuko tayari kuwataja mafisadi wenye majina makubwa makubwa" then utasikia suspect kapatwa na shinikizo la damu na ameaga dunia. Wanafanya kazi zao kimafiamafia hawa wakuu.
 
Hamuwezi kuwa na kumbukumbu nzuri kama hamkumbuki "Usiku wa Balaa" na yule "Kibibi Gula" na "Mzee Ole".... sijui kama watu wanakumbuka hadithi kama "Dimbwi la Damu" na kisa cha "Helen Jeuri??" Mtasema nini tukiwakumbusha visa vya Lisabeti na Bulicheka katika nchi ya Wagagagigikoko? Hivi hata mnakumbuka mambo ya "Paulo usije kucheza na sisi" au mambo ya "Makari Hodari, katika Safari"....?
 
Hapa unaungumzia Sani chini ya Bwaji....Kipindi hicho Sani ilikuwa ikitoa burudani isiyo mfano...
Aidha hapo kwa Makari Hodari nafikili ni Omari Hodari.. ni baadhi ya mambo ambayo sio rahisi kuyasahau....
 
Last edited:
Down The Memory Lane.............!
Not Tanzanian Of Asian Origin......!
Tumuulize Miss Tanzania Atajua Tu Alipo .......!
 
Agoro Anduru umenikumbusha nadhani ndiyo alikuwa na ile "Rosa Mystica" siyo?

MKJ,

"RosaMystica" kilitungwa na Euphrase Kezilahabi (ambacho kilipigwa marufuku),Agoro Anduru (marehemu kwa sasa) alitunga vitabu vya kiingereza vyenye stori nyingi ndani...pia kina John M.S. Simbamwene ("Mauaji Lojingi",n.k.) kina Bwana Msa wa Znz,etc...

Anyway wanasema this is the dotcom era
 
Hivi Musiba alikuwa haibi artwork? I have a feeling kwamba alikuwa ana "tafsiri" novel za kizungu na kuziuza nyumbani kama kazi yake. Ebu niambie story zote za CIA, KGB, et la...na mambo ya uninja kwenye novel zake alikuwa haziibi kwenye novel za kizungu? Yaani novel zake zilikuwa kama movie vile...

By the way, yuko wapi huyu mtu siku hizi?

Musiba yupo,siku hizi anashughulika na chama cha TCCIA,mambo ya viwanda na kilimo nafikiri,muda fulani nilimuona ZNZ kwenye biz isssues,kawa mtu mzima but I wonder what happened to his "talent"...
 
mp3 player siku hizo tulikuwa na Sony Walkman. Yaani hiyo Trade Mark ya Walkman mpaka ikawa neno, ukiwa nayo hiyo mjanja wewe na mtaa mzima utajipanga kutaka kuiazima.

Huko kwetu tulikuwa tukiita "okumani" wengine "hokumani" mradi tu ilieleweka ni kitu gani
 
Ukiona watu wanakumbushana sana vitu vilivyopita ujue washazeeka hao.

Whats next? Vita vikuu vya pili Burma, Sudan na North Africa?

Tutafungua tawi la Tanzania Legion sasa hivi hapa, na kuorodhesha askari Keya (King's African Rifle)

Pundit,

umenikumbusha mzee mmoja alikuwa akija dukani kwetu kunywa soda,huyu mzee alipigana WWII sasa mi nilikuwa nikisikia tu neno "keya" na sikujua maana yake hadi niliposoma historia miaka ya baadaye sekondari...
 
Kwa hiyo mzee pundit unasuggest Joram Kiango akamtafute Sailesh????????? Suggest title basi ya hiyo kitabu mpya ya Ben Mtobwa.........lol
 
Jamani mimi mbona sijaona aliyesoma kijijini hata mwanakijiji naona kasoma mjini maana kasahau kuwa vijijini inabidi uondoke na chakula chako cha mchana asubuhi unapokwenda shule, unaendesha baikeli ya mbao inayowekwa mafuta ya kulainishia ya ng'ombe mkono mwingine umebeba mfuko wa daftari na chakula cha mchana maana shule ziko mbali sana.
 
angalau wenzetu mlikuwa na vitu vya kuchezea.. wenzenu kijijini.. mkono mmoja umeshika kaputula isidondoke huku kwapani umeweka daftari za "Mazoezi"; mkono mwingine una bonge la kijiti na ringi la baiskeli unakimbizana nalo kuwahi shule... uzuri wake jinsi ulivyokuwa unakatisha nayo kona mtu akikuambia uendeshe pikipiki hutaki!!

hapo sijakuambia kuhusu manati inayoning'inia shingoni for "after school activity"...

Nimemshtukia M.M Mwanakijiji ni the former "Madenge"

madenge.gif

Jamco.. Soma hapo juu na utaona kuwa hukupitia kurasa zote za Bandiko hili...:D

Jamani mimi mbona sijaona aliyesoma kijijini hata mwanakijiji naona kasoma mjini.......
 
MKJ,

"RosaMystica" kilitungwa na Euphrase Kezilahabi (ambacho kilipigwa marufuku),Agoro Anduru (marehemu kwa sasa) alitunga vitabu vya kiingereza vyenye stori nyingi ndani...pia kina John M.S. Simbamwene ("Mauaji Lojingi",n.k.) kina Bwana Msa wa Znz,etc...

Anyway wanasema this is the dotcom era

bwana Ibambasi kwa nini hiki kitabu cha Rosa Mystica kilipigwa marufuku?.kilikuwa na ishu gani mbaya? by the way mimi nilikisoma pale Tanganyika library, Dar.
 
Hivi Musiba alikuwa haibi artwork? I have a feeling kwamba alikuwa ana "tafsiri" novel za kizungu na kuziuza nyumbani kama kazi yake. Ebu niambie story zote za CIA, KGB, et la...na mambo ya uninja kwenye novel zake alikuwa haziibi kwenye novel za kizungu? Yaani novel zake zilikuwa kama movie vile...

Yaani ni kweli mimi nilikuwa na mawazo hayo hayo. Nina imani kabisa alikuwa anatuongopea, kama kaandika yeye vile, kumbe kazi yake yeye ilikuwa ni kubadilisha lugha tu, stori imekuwa ya kwake...
Hehehehe...Kwikwikwi
 
Back
Top Bottom