Kamanda Kamuhanda: 4 Songea, 1 Iringa

Last I checked, Kamuhanda kasema anakaribia kustaafu na pia amepokea maagizo toka ngazi fulani za juu kuwathibiti CHADEMA (read at all costs).

Elimu sifuri, maadili sifuri hao ndio polisi wa Tanzania. Hasara wanazosababisha tunaziona na kupata machungu sana. Kikwete akitaka kujua anavyodharaulika si tu na wananchi abali hata na watendaji wake athubutu kuangalia mtiririko wa matukio ya hivi karibuni. Tokea mwezi wa sita lile tukio la Dk Ulimboka hadi jana hili la Mwangosi, ni unyama, uhuni na kutotii sheria. Nchi ilishamshinda ila kwa vile hakuwa na exit plan basi ana hang-around!
Kumbe ukiona haya mamtu yenye sura mbaya yamekimbilia upolisi yameenda kutimiza azma yao ya ubaya na ujambazi bwana eeh!!. Muwe makini ndugu zangu kila kitu kimeshaharibika, ukikutana na haya majambazi pasipo na mtu porini kimbia kama una usafiri. Nimeshashuhudia uporaji unaofanywa usiku wakiwa wenyewe au wakiazima silaha majambazi.
Tuna hitaji dunia ijue kuwa hatuna serikali wala vyombo vya dola tena!!
 
Nasikia eti hawa polisisiemu wamejitetea kuwa hicho kitu kilichomuuwa mwandishi wa habari kilirushwa kutoka upande walipokuwa wanachama wa Chadema..........kwa mtazamo wangu huu ni utetezi wa kipuuzi unaotolewa na viongozi wetu wapuuzi kila siku ili kuhalalisha mauaji na uongozi wao wa kipuuzi. Nadhani sasa wakati umefika kwa wananchi kusema 'NO', tumechoka na upuuzi wa serikali yetu.
 
Jina la Michael Kamuhanda nilipolisikia tu nilihisi kama nimewahi kulisikia tena siku si nyingi. Nina uhakika na wengine wamelikumbuka pia k Natamani wamlete Dar-es-Salaam pia ili watu waelewe tatizo tulilonalo. Nikimuita ni mhalifu sijui kama nitakuwa nimetia chumvi sana... haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kamanda unasimamia mauaji ya raia kisa wanataka kuandamana tu! Hivi hana mbinu nyingine zozote kichwani mwake zaidi ya kuwa trigger
happy!
wamlete mbeya apate joto ya jiwe
 
Si yeye peke yake. Hata mkuu wa polisi Mwuwaji Saidi Mwema ana orodha ndefu sana ya wananchi wasio na hatia waliouawa na jeshi lake. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaani serikali ya CCM.
 
Poleni watanzania wenzangu. Huku USA hali ya Democrasia imekuwa kwa kiasi kikubwa na hivi hayo ni yakawaida pindi yanapotokea. Lakini huko nyumbani ni matatizo matupu. Ila ndio tupo katika kipindi cha mpito. Yote hayo yatapita na tutakomaaa tu. Ila kwa hili Kamhanga yupo sahihi katika kutekeleza majukumu yao. Kumbuka Dola wana kwenda kwa amri tena amri ya mwisho ndio mara zote hufuatwa. Tatizo la baadhi ya Watanzania hawataki kukubali ukweli kwamba kuna wakati ukifika yapasa kutii dola. Mimi sijaona sana sababu ya M4C KUSHINDANA NA DOLA. Serikali ikisema yatupasa kusikiliza. Tukileta ubishi madhara yake ndo kama haya. Wenyewe wanasema "UTII WA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA" Kwa kuwa hatutii sheria na sasa tunashurutishwa na kwenye kusurutishwa kunakuwa na matokeo mabaya ndo hayo sasa. Tujifunze kutii dola na si kulazimisha mambo. Poleni!

We kweli huelewi unacho ropoka,wapi ambapo hakuna utii??kamanda mwenyewe alisema maandamano hapana ila mikutano ya ndani ok,pale walikuwa wanafungua tawi bila maandamano,(2)walikwisha mkamata na kumpiga vilivyo,ilitoka wapi tena haja ya kumpiga bomu?we hujaona kuwa polisi ndio waliokosa kutii sheria?kama hukumu ya kifo imefutwa hii ya bomu imesainiwa wapi?huko uliko yaelekea hawajui kiwango cha akili yako!!wangeshakutimua kitambo.
 
Jina la Michael Kamuhanda nilipolisikia tu nilihisi kama nimewahi kulisikia tena siku si nyingi. Nina uhakika na wengine wamelikumbuka pia kuwa ndiye aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Ruvuma ambapo mapema mwaka huu (Februari) wananchi 4 waliuawa napolisi walipokuwa wakijaribu kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Natamani wamlete Dar-es-Salaam pia ili watu waelewe tatizo tulilonalo. Nikimuita ni mhalifu sijui kama nitakuwa nimetia chumvi sana... haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kamanda unasimamia mauaji ya raia kisa wanataka kuandamana tu! Hivi hana mbinu nyingine zozote kichwani mwake zaidi ya kuwa trigger happy!

Hee huyu ndiye aliyekuwepo kile kipindi watu wakiuawa wakiwa chini ya mikono ya Polisi? Kwanini nayeye asiuawe?
 

Attachments

  • Capture.JPG
    Capture.JPG
    20.6 KB · Views: 22
Mkuu Mwanakijiji Polisi ya sasa,hii ya kutenda kazi kwa kutotumia weledi bali kwa lengo la kujipendekeza kwa chama tawala haitashangaza kuona Kamuhanda safari hii akapandishwa cheo c kuhamishwa mkoa tena
Sitoshangaa kwani hata wakati wa Mkapa wale waioua Zanzibar walisifiwa kwa "kazi nzuri" na wengine kupandishwa vyeo.
 
Hatuna jeshi la polisi. Every man/woman for him/herself!
 
Budget ya mabomu na risasi za moto imeongezeka.. makamanda wanashindana Burn rate
 
sipati picha ukikutana na usiku wa giza nene na msangi, zoka, rama ighondu na kamuhanda! uwiiiiiiiiiiiii utatamani zirail akutoe roho kabla hata hujasalimiana nao! ni wauaji live, wanatembea na makoleo ili kung'oa watu kucha, meno na kusambaratisha matumbo ya watu bila ganzi!.
 
Jamani inauma sana...Lini amani ya kweli iatapatikana Tanzania????Naona tunataka kuwapiku Syria kwa nguvu zote...
 
Inasikitisha sana, sasa hapo sinema nyingine ya kichina itachezwa muda sii mrefu. Ataletwa mkenya sasahivi kuhusika na tuhuma hizi za kupiga na kuuwa
 
INGEKUWA zamani Nyerere angekemea uovu huu wa polisi na kuamru watafute njia mbadala za kukabiliana na waandamanaji wasio na silaha yoyote.unajua wakati wanakabilianana waandamanaji hawachukui tahadhari ya kulinda mabomu yao yasifyatuke.

Walinde yasifyatuke tena?? Yule askari angalia picture alikuwa analenga, au ndio ilikuwa inafyatuka, kuna moshi unaonekana kabisa...
 
Polisi wanafanya wanachokijua kwa kuwa hakuna mahali wanapowajibika...
Hiyo ndiyo kazi waliyoelekezwa kuifanya na wanaifanya kwa juhudi zote...
Hakika wamesahau jukumu namba moja la Jeshi la Polisi...
Nalo ni kulinda na kutetea haki za raia dhidi ya waovu na maovu...

Hauko sahihi. Wanafanya hivyo kwa kuwa wanawajibika kwa chama tawala. La sivyo wasingekuwa wanafanya wafanyayo
 
Tuanze kwa kutazama upya mafunzo wanayopata huko CCP.
Ninaamini hawa polisi ktk mafunzo yao wanafundishwa ukatili na roho mbaya badala ya kufundishwa roho ya imani na utendaji wa kazi zao kwa roho safi na kwa nia njema.
 
Tutarajie mengi ya kusikitisha!
wavutaji Bangi na Madawa ya kulevya + upungufu wa akili na ufinyu wa fikra zao= Mauaji ya Raia wasiokuwa na hatia!
 
Back
Top Bottom