Kamanda Kamuhanda kuhamishwa Iringa, yadaiwa chanzo ni mauaji ya Mwangosi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Kamuhanda kuhamishwa Iringa, yadaiwa chanzo ni mauaji ya Mwangosi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzalendo JR, Sep 18, 2012.

 1. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  SIKU chache baada ya kutokea mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa dhidi ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi, habari zilizolifikia gazeti hili zinasema Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda, yupo mbioni kuhamishiwa Makau Makuu.

  Vyanzo mbalimbali vya kuaminika ndani ya jeshi hilo vilidai kuwa, Kamanda Kamuhanda atahamishiwa Makao Makuu, Dar es Salaam, lakini haijajulikana atapangiwa kazi gani.

  Inaelezwa kuwa, uhamisho huo utafanyika mara moja baada ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Mamno ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kumaliza uchunguzi wa mazingira ya kifo cha marehemu Mwangosi anayedaiwa kupigwa bomu.

  "Wakubwa wetu wamepima na kupitia rekodi ya utendaji wa Kamuhanda, hatua za awali atalazimika kuhamishiwa Makao Makuu, Dar es Salaam.

  "Kutokana na mazingira ya kifo cha Mwangosi ni wazi Kamuhanda hawezi kuendelea na kazi mkoani Iringa, pamoja na mashinikizo mbalimbali yanayotolewa na wanahabari kutaka awajibishe," kilisema chanzo hicho na kusisitiza kuwa; "Sababu nyingine ya kuhamishwa Makao Makuu ni mauaji yaliyotokea kwenye mikoa aliyokaa, alipokua mkoani Ruvuma watu wanne walipoteza maisha mjini Songea wakati wa maandamano," kilisema chanzo chetu cha habari.

  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Bi. Advera Senso, alipoulizwa kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alisema; "Taarifa hizo sina, kama zingekuwepo ningewaambia".

  Aliongeza kuwa, kama uhamisho huo utakuwa wa kweli ni utaratibu wa kawaida kwa makamanda kuhamishwa vituo vya kazi na kupelekwa sehemu zingine.

  Hivi karibuni, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linadaiwa kufanya mauaji ya Mwangosi katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, wakati viongozi wa CHADEMA, wakifungua matawi na kufanya mikutano ya ndani.

  Baada ya kutokea mauaji hayo, Kamanda Kamuhanda alisema polisi walilazimika kutumia nguvu ya ziada kutokana na wananchi kukaidi amri halali ya kuwataka watawanyike.  Source: Gazeti la Majira


  My words:
  Sijawahi kuona wala kusikia Askari hata mkuu wa kituo akifukuzwa kazi kwa makosa ya kuua, kutesa, au kwenda kinyume na maadili. SIJASHANGAZWA NA TAARIFA HII. Laweza kua ajabu la8 la dunia akifukuizwa huku alishatoa kauli ya anaipenda kazi yake hivyo anahitaji Staafu kwa amani.

  Hapa inaonekana kuna watu anatekeleza hila zao japo moyo wake hautaki, ni dhiki tu za kutofanya maamuzi ya ujanani hata kutegemea kibarua hadi miaka 56.
   
 2. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FEAR OF THE UNKNOWN hunts poor minded persons.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Hiyo itakuwa Promotion ama demotion?
   
 4. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Motivation kaka
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,806
  Trophy Points: 280
  Duuuuh! Hii ndio serikali sikivu bhana , wakurugenzi wakiharibu hapa wana hamishiwa pale hili wakaharibu tena. Kamanda kaharibu iringa badala ya kuwajibishwa analetwa makao makuu!

  Huu uwoga wa kuwawajibisha watu ni kutoka na kuwatuma watekeleze matakwa yao. Kamanda alitumwa atekeleze ilani ya kuchafua cdm ndio maaana hawawezi kumuwajibisha,

  sishangai sana hata yule askari mtuhumiwa(kiini macho) alipewa ulinzi mkali na akapakiwa kwenye shangingi utafikiri yeye ana haki kuzidi wengine kumbe inabidi wamlide maaana wlimhaidi na alikuwa anatekeleza ilani ya kuichafua cdm kwa kuuwa raia wasio na hatia!

  "Sijui kwanini watanzania ni maskini-jk"
   
 6. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jeshi letuu la Polisiiiiiii
  Ni chombo cha wananchiiiiii
  Kukamataaa waharifuuu ndiokazi yajeshiletu.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa polisi ukipelekwa makao makuu ni kama demotion!
  Ila huyu ilibidi apigwe chini!
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Huo si Utamaduni wa Serikali yetu kaka..
   
 9. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Makao makuu panaitwa kijiweni.

  Nilisoma ushuhuda wa Abdallah Khamisi nikawa na maswali mawili
  1. Kwanini yule 0CS peke yake ndo aliumia?
  2.Je wakati bomu linalipuka RPC alikuwa ameshaondoka?

  Ushuhuda wa Senga umejibu maswali yangu.
  1.OCS hakujua mchongo ndo maana alikuwa akimtetea marehemu Mwangosi. Hivyo baada ya kufyatua lile bomu wauaji kwa haraka wakakimbia wakijua kuna mlipuko wa pili. OCS hakujua habari ya bomu it caught him unawares you can even tell by his scream "wananiuwa hawa"

  2.Kamuhanda alishuhudia harassing ya marehemu lakini hasa alikuwepo hapo kuhakikisha watu wake wanatimiza lengo pamoja na kuhakikisha clean up of the crime scene ili aje kupotosha ukweli kwenye ripoti tofauti na kama angeondoka mapema

  My point is, we must demand Kamuhanda prosecution. In jail is where he belongs
   
 10. MWANAMTAA

  MWANAMTAA Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huko sijui ata muuwa nani.........................
   
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,535
  Likes Received: 10,453
  Trophy Points: 280
  mimi nilijua anafikishwa mahakamani kwa kuhusika na mauaji ya Mwangosi.!?
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  kama akihamishiwa daslmamu basi tutegemee damu nyingine hasa ya pale chuo cha naniliu kumwagika...si unajua tena haipiti mwaka wale jamaa wako barabarani......
   
 13. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,005
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Mimi sielewi naona rangi rangi th kwa yatendwayo na hili jeshi la intelijensia ma serikali yake. Yaani huyi rpc nk wa kuhamishwa au ni wa kuvuliwa madaraka aliyo nayo na kupandishwa kizimbani kujibu kesi ya mauaji? Jamani, jamani watawala ole wenu siku yaja mtajibu kwa Mungu haya muyafanyayo
   
 14. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  dah siamini masikio yangu anahamishiwa makao makuu, so mission accomplished!!
   
 15. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nilijua atahamishiwa Segerea, hii ndio serikali ya JK
   
 16. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Anapandishwa cheo kwa kuua mwandishi wa habari aliyejihusisha na mkutano wa Chadema
   
 17. eumb

  eumb Senior Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Demotion hiyo, anakuja kusoma magazeti tu, hapo Makao Makuu wapo wengi Wa level yake!
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kama ndio hivyo sitoshanga na yule askari mkatili aliyelipua bomu ndio anakuwa RPC wa Iringa!
  [​IMG]
   
 19. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Jeshi letu la polisi lina kosa uwajibikaji na utawala bora ,ila tuna ofisi na waziri anayehusika na utawala bora cha ajabu hatuoni huo utawala bora .kimsingi hapa utawala bora ulikuwa uanzie hapa .watazamaji tunaoangalia tunaona bora utawala na si utawala bora .
   
 20. M

  Man 4 Move Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anayemhamisha na anayehamishwa one day they will be going to their home"the hague"
   
Loading...