Uchaguzi wa madiwani vurugu tupu;Chadema yashinda Ludewa, CCM yashinda Songea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa madiwani vurugu tupu;Chadema yashinda Ludewa, CCM yashinda Songea

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nngu007, Oct 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, OCTOBA 29, 2012 05:25 NA WAANDISHI WETU, DAR NA MIKOANI

  *Mkoani Arusha risasi za moto zarindima mchana kweupe
  *Songea, wafuasi wa CCM, CHADEMA wakatana mapanga
  *Chadema yashinda Ludewa, CCM yashinda Songea

  MBUNGE wa Viti Maalum, Rahel Mashishanga (CHADEMA) pamoja na Katibu wa Chadema Jimbo la Nyang'hwale mkoani Geita, Michael Ndege, wamenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa na kisha kupigwa na kukatwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Viongozi hao walivamiwa jana katika matukio tofauti, ambapo Mashishanga anadaiwa kuvamiwa jana asubuhi, alipokuwa akiangalia mwenendo wa uchaguzi wa udiwani katika vituo vya kupigia kura, katika Kata ya Mwawaza, mkoani Shinyanga.

  Akiwa katika kazi hiyo, inasemekana mbunge huyo alivamiwa na kundi la vijana, wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

  Akizungumza na MTANZANIA jana kwa simu kutoka mkoani Shinyanga, Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), alisema Mashishanga alivamiwa na kupigwa na gari lake liliharibiwa vibaya, kwa kupigwa mawe.

  "Ni kweli nimeambiwa Mbunge Rahel Mashishanga, amevamiwa na kupigwa na wafuasi wa CCM, wakati akitembelea na kuona zoezi la upigaji kura katika Kata ya Mwawaza.

  "Mbali na kumpiga, wameiponda kwa mawe gari yake na vioo vinaelezwa vimeharibika vyote. Mbaya zaidi alikuwa na mdogo wake, ambaye amepigwa na kuteguka bega la kushoto na ameumia mdomo.

  "Kwa sasa mimi nipo hapa kama mwangalizi wa uchaguzi, ambaye ninakisimamia chama changu katika uchaguzi wa Kata hii ya Mwawaza," alisema Nyerere.

  Vincent ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema kuwa vitendo hivyo kamwe havivumiliki, huku akilitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linawasaka na kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo.

  Kwa upande wake, Ndege inasemekana alivamiwa juzi usiku akiwa njiani kwenda kulala, ambapo alivamiwa na kundi la vijana waliokuwa wamevalia sare za CCM, kisha akakatwa kwa mapanga na visu.

  MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala, ili kuthibitisha kutokea kwa matukio hayo, alisema hana taarifa ingawa aliahidi kufuatilia.

  Arusha risasi za moto zarindima

  Taarifa kutoka mkoani Arusha zinaeleza kuwa, uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Daraja Mbili, Jimbo la Arusha, umeingia dosari katika eneo la Alinyanya, baada ya kutawaliwa na milio ya risasi.

  Milio hiyo ya risasi ilisikika jana wakati wananchi wakiendelea kujitokeza vituoni, kwa ajili ya kupiga kura.

  Tukio la kufyatuliwa risasi, linadaiwa kutokea katika Kituo cha kupigia kura cha Sekondari ya Felix Mrema na linasemekana liliwahusisha viongozi na wanachama wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM na CHADEMA.

  Inadaiwa kwamba, kundi la wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa CCM waliomaliza kupiga kura, waliendelea kubaki kituoni, hatua inayodaiwa kupingwa na wafuasi wa CHADEMA, ambao nao walikuwa kituoni hapo.

  Chanzo cha habari hizi kililiambia MTANZANIA, kwamba baada ya kuibuka vurugu hizo katika kituo hicho, askari polisi walilazimika kuingilia kati, kwa kuwaondoa watu wote kwenye kituo hicho.

  Ilidaiwa kwamba, wakati polisi wakifanya kazi hiyo, ndipo milio mitatu ya risasi iliposikika, baada ya risasi tatu kufyatuliwa hewani na kusababisha taharuki kwa baadhi ya wananchi, waliokuwa eneo hilo kwa ajili ya kupiga kura.

  Diwani wa Kata ya Levolos, Efatha Nanyaro (CHADEMA), alipoulizwa juu ya tukio hilo, alithibitisha kwamba lilitokea.

  "Ni kweli kumetokea vurugu za hapa na pale na kiongozi mmoja wa CCM, God Mwalusamba, inasemekana alihusika moja kwa moja.

  "Taarifa nilizozipata ni kwamba, yeye pamoja na watu wengine, wamechukuliwa na polisi, lakini pia gari la Lema (Godbless Lema, Mbunge za zamani wa Arusha), limechukuliwa na askari polisi," alidai Diwani Nanyaro.

  Hata hivyo, Diwani Nanyaro alipinga taarifa kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), ndiye aliyefyatua risasi katika eneo hilo.

  "Hizo taarifa si za kweli, Nassari na Lema wapo huku Daraja Mbili, wanaendelea na majukumu ya chama, aliyefyatua risasi pale, alikuwa ni Mwalusamba," alidai Nanyaro.

  Katika hatua nyingine, taarifa kutoka eneo la shule hiyo ya Felix Mrema, zilimtaja Nassari kuwa ndiye aliyefyatua risasi hewani, akidaiwa kutishia wananchi wasipige kura.

  Katika vurugu hizo, ilidaiwa kuwa, watu zaidi ya 10 wanadaiwa kukamatwa na askari polisi, kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo.

  Ilidaiwa kwamba, Nassari ambaye alikuwa eneo hilo huku kukiwa na umati wa watu, inasemekana alichomoa bastola yake na kufyatua risasi hewani, ili kuwatisha wananchi.

  Hata hivyo taarifa zinasema kuwa, baada ya vurugu hizo kutulizwa na askari polisi, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Arusha, Martin Munis, inasemekana alipotelewa na fedha pamoja na simu ya mkononi.

  Tayari tukio hilo linadaiwa kuripotiwa katika kituo cha polisi na kupewa namba AR/RB/13624/2012 ya shambulio la kudhuru mwili, dhidi ya watuhumiwa Nasari na Lema.

  Mgombea wa udiwani wa CCM katika kata hiyo, Philip Mushi, aliiambia MTANZANIA, kwamba ana uhakika wa kuibuka na ushindi kwa kuwa wapiga kura wengi walimwelewa wakati wa kampeni zake.

  "Hawa watu wamejaribu kuvuruga zoezi la upigaji kura ili lisimalizike vizuri, lakini binafsi sina shaka ninao uhakika wa kuibuka na ushindi, kwani wanachama na wapiga kura walituelewa vizuri wakati wa kampeni," alisema Mushi.

  CCM, CHADEMA watwangana Songea

  Wafuasi wa vyama vya CCM na CHADEMA, katika Kata ya Ruvuma, Mjini Songea, juzi walitwangana walipokuwa wakifunga mikutano ya kampeni Mjini Songea.

  Mapambano hayo yalisababisha watu Saba, kujeruhiwa kwa silaha za jadi, yakiwemo mapanga huku majeruhi wakikimbizwa hospitali kwa matibabu.

  Akizungumza na MTANZANIA, mmoja wa majeruhi ambaye pia ni kada wa CCM, Mashaka Mbawala (45), alisema vurugu hizo zilitokea wakati walipokuwa wakienda kumchukua mgombea wao na kwamba wakati wa tukio hilo, walivamiwa na wafuasi wa CHADEMA na kuanza kupigwa na mapanga.

  "Tulikuwa tunakwenda kumchukua mgombea wetu wa udiwani, Maurus Lungu na tulipofika karibu la Kanisa, tuliona kundi la vijana wa CHADEMA, wamekaa na waliamua kuziba njia ili tusipite.

  "Tulipoona wamezuia njia, tukawaomba watupishe, ili tupite tukamchukue mgombea wetu aende eneo lililoandaliwa kwa mkutano. Cha ajabu yalianza kutokea mabishano ambayo yalidumu karibu dakika tano hivi, ndipo zilianza vurugu na sikutambua kilichoendelea, kwani nilipigwa na kitu chenye ncha kali na kupoteza fahamu papo hapo," alisema Mashaka.

  Kwa upande wake Athuman Moyo (44) ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Ruvuma, alijeruhiwa kwa kupigwa na rungu mbavuni. Alisema kwamba, vurugu hizo zilisababishwa na wafuasi wa CCM na siyo CHADEMA kama ilivyokuwa ikielezwa.

  "Nilishangaa kuona kama kuna gari aina ya Land Cruser nyeupe, imefika kwa haraka na mkong'oto ukaanza, pale nikaona baadhi ya wenzangu wanalalamika kuwa, wamekatwa na vitu vilivyodhaniwa kuwa ni mapanga na mimi nikajikuta napigwa marungu na mateke, yalikotokea sikujua maana nilipoteza mwelekeo," alisema Moyo.

  Mwigulu Nchemba, ang'aka

  Katibu wa Halmashauri Kuu, Uchumi na Fedha wa CCM, Mwigulu Nchemba, amewataka wakazi wa Wilaya mpya ya Momba, kutokubali kushawishika na kauli za uchochezi zinazotolewa na CHADEMA, katika ujenzi wa halmashauri hiyo mpya.

  Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), aliyasema hayo juzi wakati akifunga kampeni za uchaguzi wa udiwani, katika Kata ya Mpapa, Kijiji cha Mwanjila, baada ya diwani wa kata hiyo kufariki dunia.

  Akimnadi mgombea wa CCM, Nalosko Simbeye, Nchemba aliwataka wakazi wa eneo hilo, kutokubali kushawishika na kauli za uchochezi zinazotolewa na vyama vya upinzani, hasa katika kipindi hiki cha kuijenga halmashauri hiyo mpya, kwani kauli hizo zina lengo la kuvuruga amani.

  Alisema kwamba, wilaya mpya inapoanzishwa, huhitaji mambo mengi muhimu, kama vile uboreshaji wa miundombinu zikiwamo barabara, hospitali, shule za msingi na sekondari na kwamba mchakato wa kuyakamilisha hayo, unahitaji utulivu na amani.

  "Wilaya mpya, kata na vijiji vyake, haviwezi kuendelea kama eneo hilo halina amani na utulivu. Hivyo nawaombeni wana Momba, msikubali kuruhusu kuchagua mgombea ambaye kazi yake kubwa itakuwa ni kuhamasisha watu kufanya vurugu na kuandamana, ili kumwaga damu," alisema Nchemba.

  Naye, Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, aliwataka wakazi wa eneo hilo, kutokubali kuchagua viongozi ambao watawasababishia maandamano hadi ngazi ya familia.

  "Mwana Momba nakuhakikishia kwamba, endapo utachagua kiongozi kutoka CHADEMA utakuwa umeruhusu maandamano hadi ndani ya familia zenu na jambo hili siyo zuri, kwa sababu tunachotaka sisi ni maendeleo wala siyo maandamano," alisema.

  Uchaguzi mdogo ngazi ya udiwani umefanyika jana katika kata 22 nchini kote.

  Habari hii imeandaliwa na Bakari Kimwanga (Dar), Eliya Mbonea (Arusha), Amon Mtega (Songea) na Pendo Fundisha (Mbeya).

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  POLICE wako wapi wenye hizi CHAGUZI za UDIWANI? Au wanajipanga na WanaCCM?
  Kwanini Wagombea kutishiwa na MAPANGA kuuwawa??? ILI wa CCM washinde?
   
 3. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  554245_448357071867354_54036771_n.jpg
  hii ndio kitu iko kichwani mwangu kwa sasa inanisumbua sana ubongo hesabu zake kama differentiation
   
 4. piper

  piper JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hahahaha haya bana.
   
Loading...