Mchungaji Msigwa kuongoza maandamano kumng'oa Kamanda Kamuhanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Msigwa kuongoza maandamano kumng'oa Kamanda Kamuhanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 21, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Tukio la kuuawa kwa mwandishi huyo bado limevuta hisia za wananchi wengi ambapo shinikizo linaelekezwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, likimtaka ajiuzulu kama sehemu ya uwajibikaji.


  Akihutubia wananchi hao, Mchungaji Msigwa, alilaani kitendo cha kuuawa kwa Mwangosi na kusema kuwa hatatoa kauli yoyote isipokuwa atafanya kazi kwa vitendo na kuhakikisha Kamanda Kamuhanda anaondoka.
  "Hatuwezi kulinda ujinga huu uendelee, mimi sitatoa tamko ila nitaanza kwa vitendo. Hatuwezi kuuacha uozo huu. Kamuhanda lazima aondoke," alisema.
  Alilitaka jeshi la polisi kumuogopa Mungu na kutenda haki badala ya kutii amri zinazohatarisha usalama wa raia na kuwakatisha uhai. "Nalaani vitendo vyote vya jeshi la polisi vinavyohatarisha usalama wa raia. Na wale wote wanaotoa amri kwa askari kwa ajili ya kuwapiga na kuwaua wananchi washindwe na walegee kwa jina la aliyehai Yesu Kristo, Iringa hatukuzoea matukio haya, sasa basi Kamuhanda lazima aondoke," alisema Msigwa.

  Aliwataka wananchi wa Iringa kushiriki katika maandamano ya amani yatakayofanyika leo kuanzia ofisi yake kuelekea katika ofisi ya Kamanda Kamuhanda kushinikiza aondoke Iringa.

  "Nyumbani kwetu kuna nyoka, huyu nyoka lazima aondoke. Kila Ijumaa tutakuwa na maandamano ya amani kumng'oa huyu nyoka na lazima polisi walinde maandamano hayo. Kamuhanda ni nyoka lazima aondoke," aliongeza.

  Polisi chupuchupu kupigwa na wananchi mkutanoni Iringa Mjini
  MAUAJI ya mwandishi wa kituo cha runinga cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi, aliyeuawa kwa kufyatuliwa bomu na polisi kijijini Nyololo mkoani Iringa, yameendelea kuliandama jeshi hilo, ambapo wananchi mjini hapa nusura wampige askari aliyevamia mkutano wa mbunge juzi.

  Katika mkutano huo wa mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), uliofanyika katika eneo la Soko Kuu mkabala na kituo cha polisi, askari mmoja alijitokeza na kutaka kuwapiga wananchi kwa virungu bila sababu.
  Wakati Mchungaji Msigwa akiendelea kuhutubia, askari huyo alitokea kituoni hapo na kwenda kutembeza virungu kwa watu, lakini kabla ya kuanza kazi yake, sauti za wananchi zilipazwa zikisema, "Muacheni huyo ndiye atakayetuonyesha Mwangosi leo hii."

  Wakati zogo hilo likiendelea, kundi la vijana lilianza kumsogelea huku likisema: "Hatuogopi mabomu wala bunduki za polisi."
  Purukushani hizo, ziliwafanya askari wenzake kufika na kumvuta huku wakimkimbizia kituoni kumnusuru na uamuzi waliotaka kuuchukua wananchi dhidi yake.

  na Gustav Chahe, Iringa
  imechapishwa: Tanzania Daima

  Iringa - Maandamano kushinikiza Kamuhanda ajiuzuru yapigwa stop

  [​IMG]

  Polisi wakizunguka mji wa Iringa kuzuia maandamano yaliyoandaliwa na Mbuge Msigwa kushinikiza Kamanda Kamuhanda ajiuzuru.

  [​IMG]

  Mbunge wa Iringa mjini Msigwa akitoka eneo la ofisi akielekea hospitali kwa matibabu ya mguu wake baada ya kusitishwa kwa maandamano
  Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Msigwa, akizungumza na wanachama na wapenzi wa chama hicho katika ofisi za Wilaya za chama hicho kuhusu kuahirishwa kwa maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike siku ya leo kushinikiza kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kujiuzulu kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten Daudi mwangosi kilichotokea tarehe 2 septemba mwaka huu.

  Msigwa amesema kutokana na barua aliyoipata toka kwa zikitaka kusitisha maandamano hayo, aneleza barua inawataka kusitisha na kueleza kuwa sababu kubwa ni kwamba maandamano hayo hayataweza kuwa na polisi wa kusimamia na kukataza kufikia katika ofisi ya RPC ambayo ni ofisi ya kiserikali.


  Hata hivyo Msigwa ameeleza kuwa msimamo wao uko pale pale ila anajiandaa kujibu hoja za barua hiyo na kuwataka wananchi wawe na subira mpaka atakapowatangazia tena kuwepo kwa maandamano hayo ya amani.
  Wakati huo huo wameonekana askari wakiwa katika magari yao kudhibiti wananchi kuandamana. Hali hiyo ilitokana na wananchi hao kumiminika kwenye ofisi za Chadema mjini hapa kwa ajili ya kujiandaa maandamano.   
 2. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  tuko pamoja
   
 3. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hali ya Mbunge Msigwa iringa mjini ni mbaya! ana jaribu kutembelea nyota ya Mwangosi kujijenga kisiasa!
   
 4. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Anataka wengine wamwangosiwe katika hayo maandamano.
  Kuongoka ni hiari ila kutubu ni lazima.
   
 5. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  kwahiyo una maanisha alichofanya kamanda kamuhanda ni sahihi?
   
 6. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wacha urongo wewe hali ya kisiasa kwa chadema na msigwa haina mashaka kabisa tofauti na ccm huu ndo ukweli
   
 7. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  chizi sio lazima akote makopo hata kutema pumba katika jambo serious nao ni uchizi tafakari chukua hatua
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Umeonaee. Wakati wa kampeni alikopa fedha kwa Abuu wa NBC na akaweka rehani gari yake. Bado hajaikomboa
   
 9. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Ningependa jeshi la polisi wafanye kazi zao kitaalamu, kikanuni na kwa kufuata taratibu zao zinavyowaelekeza, sio kufanya kazi kwa kushinikizwa, kupelekwa pelekwa na kulazimishwa kufanya kazi kama hili kundi la hawa watu (chadema) linavyotaka.

  Wasipotii amri ya polisi hawa wana-chadema, wembe huwe ni ule ule na ningelitaka jeshi la polisi wasiogope lawama, kudhihakiwa na hata kulaaniwa na kundi hili la hawa watu kwani watanzania tupo nyuma yao.

  Kama wapo katika harakati za kuthibitisha kuwa nchi haitatawalika, basi na serikali itaendelea kusimamia utawala bora na kuwathibitishia kuwa haiteteleki na bado ni imara katika kutawala nchi yetu.

  Dawa ya moto ni moto tu siku zote, huwezi kunibebea mawe, vitu vyenye ncha kali na malungu, mimi nije na speaker kukuambia tawanyika lazima nitakuwa kichaa. Kama watafanya maandamano yao kwa kufuata utaratibu hakuna mwenye shida nao, tumeona hili kwenye makundi mengine ya jamii kama waislamu walifanya ya kwao, wana-cuf nao wamefanya pia na waandishi wa habari.

  Hakuna hata kundi moja lililoguswa na jeshi la polisi.

  1. KWANINI CHADEMA KILA WAKATI WAWE WAO TU WAKUPIGWA NA POLISI?

  2.KWANINI WAO TU CHADEMA WAFANYIWE MAUJI?

  3.KUNA KIPI KILICHOJIFICHA HAPA KWA HAWA WANACHADEMA AMBACHO NAAMINI RAIA WENGI HAMKIJUI?

  Raia tuamke na tuzinduke kutoka katika usingizi mzito wa kupandikizwa na hilo kundi la hao watu wachache, hama hakika kuonyesha kama hawajali, vijana wanaouwawa katika maandamano yao, hawana hata utaratibu wa kuziangalia kwa kuzihudumia hizo familia zilizoachwa na marehemu hao, huu sio unyama unaofanywa na hiki chama cha CHADEMA?.

  Kwanini tujiingize kwenye giza kwa kuwaunga mkono hawa watu kwa roho mbaya hii?

  "BADILIKA UBADILI TAIFA".
   
 10. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Unajiona umechangiiiiiiiiiiiaaaa! Una bahati naogopa ban.
   
 11. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nimependa hapo kwenye blue! Well said.
   
 12. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama umetumia hata akili ya kawaida wakati unaandika, nani hajui polisi wanaua kwa maagizo ya ccm? Makundi uliyotaja watu hawauawi kwa sababu ccm hawajaagiza hivyo na makundi hayo hayana effect kwa ccm.
   
 13. J

  Jimy P Senior Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwaambia wanachadema Iringa. mkiandamana bila kibali mtashughulikiwa tu, na ninachukua nafasi hii kumpongeza Kamanda Kamuhanda kwa kusimamia Sheria za nchi vizuri yeyote atakayevunja mshughulikie ipasavyo Tupo nyuma yako...Asikutishe mtu wala chama chochote cha siasa ambacho badala ya kufanya kazi za siasa wamekuwa wanaharakati.
  Na ninapenda kuwaanbia waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa msiwe wanasiasa fanyeni kazi yenu ya uandishi wa habari kama mlivyosomea...Ethics za uandishi wa habari...

  Wananchi wa Iringa mkiandamana bila kibali wakati matukio yanatokea hamtamuona Mch Msigwa,, Mtaacha familia zenu..Chama chenyewa kimejaa Ukanda na Ukabila..Kikao cha ukoo hakina tofauti na kikao cha Chama
   
 14. J

  Jimy P Senior Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Excellent,, Kamanda kamuhanda yupo Sahihi kabisa kwa sababu CDM Wanaandamana bila kibali.. tena kwa usimamizi mzuri washeria Kamanda Kamuhanda anafaa kuwa IGP...
  CDM Wanatumia njia ya kuvunja sheria halafu wakivunja wakiachwa wanasema serikali ya CCM Dhaifu..
  Sasa ni kusimamia sheria tu...
   
 15. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Siasa ya matusi na kejeli ni sawa na siasa uchwara ambayo siku zote ina malengo ya kuleta vurugu na fujo, huwa haina nia njema hata kidogo.

  Siasa ya namna hii ailengi kujadili wala kupanga mbinu mbalimbali za kupata maendeleo ili lile lengo la kubadili hali za watanzania kuwa zenye unafuu zaidi kufikiwa.

  Bali zimekuwa ni siasa za kuzua vituko, kuleta mabishano na mapambano yasiyo na tija kwa watanzania, hili hali wanatambua fika watanzania hawayahitaji yote haya.

  Wapeni watanzania wanachotaka muone kama kuna atakaewapinga, mambo ya kuwajengea watanzania usugu katika miili yao na kuzitia giza akili zao hili zisiweze kufikiria kwa kina ni JANGA JIPYA KWA TAIFA LINAPIKWA HAPA.

  Kama serikali haitachukua hatua za haraka dhidi ya hili kundi la wana-chadema, basi kila upuuzi watakao ufanya wao litaonekana ni kosa la serikali. Hii itasababisha hekima na heshima ya serikali kushuka kwa mambo ambayo kimsingi haijafanya.

  HAMKA NA UZINDUKE KUTOKA KWENYE USINGIZI MZITO WA KUPANDIKIZWA NA HAO MAGWANDA. LENGO NA MADHUMUNI YAO NI KUKUTUMIA TU NA HAWANA LENGO JEMA NA WEWE.

  "BADILIKA UBADILI TAIFA".
   
 16. M

  Masikrodinga JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Dah....! Inaonekana MAGAMBA yanakulipa vizuri sana maana unawafanyia kazi nzuri
   
 17. j

  jigoku JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Magonjwa ya akili nayo ni tatizo kubwa kwa sasa,non communicable desease hii inamsumbua Hammy.
   
 18. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mahali unapostahili kuwa ni Mirembe... Nahisi kuna gololi zimelegea kwenye ubongo wako!
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Dislike!!!
   
 20. cbandiho

  cbandiho Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  wewe fanya uwezalo,iwe ni maandamano au maombi.....ili mradi aondoke na hatua za kisheria zifuatwe,tukianzia hapo hata wengine tutawafikia tu
   
Loading...