Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

  KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

  Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

  “Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

  “Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

  Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

  “Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

  “Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

  “Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,” alisema.

  Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

  Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

  Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

  Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon, alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

  Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Jamaa ana POWER kweli... Inaonyesha JINSI asivyo na WASIWASI JUU YA KAZI YAKE.
   
 3. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kwa nini waandishi wa habari huwa mnawaauliza hawa mnaowauliza maswali mwongozo? kwa nini usimuulize ni makosa gani ambayo yanapaswa mtu akawajibika kama alivyosema kuna makosa ya kuwajibika?
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ukisikiliza kwa makini kauli yake utagundua jinsi serikali ilivyokosa uhalali wa kuongoza.
  yaani mpaka hapo haoni kosa na hawezi kujiuzulu hata kama polisi wake wakiua maelfu machoni pake.
  MPELEKEENI TAARIFA KUWA TUNAMSUBIRI URAIANI.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu jamaa atumia akili gani?

  Anapata wapi ujasiri wa kuongea upuuzi kama huu?

  Hapa ana maana kuwa watu wasipotii sheria adhabu yao ni kuuawa??
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Walimuuliza anayekosa kutii sheria bila shuruti huuwawa kwa kutumia kifungu kipi cha sheria?

  Kama hawakumuuliza, basi naieleweke leo kuwa waandishi wa habari ndio tatizo Pasco waambie wenzio.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Is that a new phrase for "murder"?
  Siku aliyouawa marehemu Mwangosi kulikuwa na maandamano?? I thought ilikuwa ni ufunguzi wa tawi la CHADEMA....... Anyway hapo RPC anajaribu kutuambia ule mkusanyiko wa CHADEMA ndo ulifanya yale mauaji au?
  Is he trying to say kwamba marehemu Mwangosi alikataa kutii sheria ndo polisi wakaamua kufanya walichofanya?Hio ni sahihi??
  Ushauri wa bure kwa RPC huyu........ Kadri anavyozidi kuongea anazidi kutia hasira watu kwa maneno yake...... Akae kimya tuu, itakuwa ni busara zaidi asijifanye jeuri
  Kweli nimeamini power corrupts, and absolute power corrupts absolutely!!!

   
 8. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Naona majibu yake ni yale yale kama kauli ya Hiza Tambwe ilivyokuwa. Kwa nn watu hawaandamani kushinikiza watu kama hawa kujiuzulu?? Yaani mnataka ajiuzulu mwenyewe?? Huo si utamaduni wa wetu, inabdi awekewe pressure kwa maandamano.
   
 9. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nasikia uchungu ningekuwa mimi ndo ananijibu hivyo ningekuwa mahabusu sasa hivi kwa kesi ya kumtandika ngumi ya uso na kuua RPC
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nazani damu ya Mwangosi imeanza zaa matunda maana mzee keshaanza changanyikiwa CDM walikuwa na mkutano wa ndani yeye anaongelea maandamano!
  Kamanda ni busara kukaa kimya otherwise unaaribu
  Alafu na huyu mwandishi yuko shallow na hakujiandaa kabisa au ndo uko katika harakati za kumsafisha Kamudandu?
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hapo nilipopigia mstari
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  naombeni namba yake tafadhali....
   
 13. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Astaghafrulah laana tu lah! Yaani huyu m.... ndo anaropoka hivi, ningekuwa karibu yake wakati anajibu ningemlima kichwa cha uso na ningekuwa mahabusu
   
 14. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  siku 40 za kutoandika habari za polisi zimeisha au zilipunguzwa?
   
 15. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni jibu au swali la rpc kwanini wasijiuzuru walioandamana nijiuzuru mimi? Mwangosi aliandamana? Je wajibu wa polisi ni kuuwa waandamanaji? Alitakiwa ajibu sio kuleta ulevi na ubabe wa madaraka
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia subordinates wake mpaka wakamfyatulia bomu mwangosi at zero distance.pia awajibike kwa mauaji yaliyofanywa na polisi huko songea.
   
 17. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna kijana wangu wa kike yuko darasa la pili, ana busara maradufu kuliko huyu RPC.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unaweza kusoma kitu fulani hapa kama hayati Nyerere alivyosema; "ukishaonja nyama ya mtu vigumu kuacha." Mwisho wa nukuru. Nilipokuwa nasikia kauli hiyo sikujua Nyerere alikuwa anamaanisha nini kwa vile nilikuwa bado mdogo sana.

  Kamuhada ameua Songea watu wanne mwaka huu, na kisha kuhamishiwa Iringa ameanza kuvuta kiti chake cha U-RPC kwa kuua Mwandishi wa habari mauaji ya kinyama yeye akishuhudia amebaki gari kando yake.

  Leo anakuja kwa kujiamini na bila wasiwasi kwamba hawezi kujiuzuru alikuwa anatekeleza kazi yake.

  Ukiona dalili za kuzeeka vibaya na kushia kustaafu kutokuwa na maisha ya raha na starehe huku ukiwazia tamu ulizozimwaga, basi ujue mambo kama hayo si ya umri wa sasa tunaouona, ila ni jambo alilolizoea na ndio maana anajiamini na hana wasiwasi kwa mauaji yake.

  Kiongozi mwenye dhamiri ya kujali maisha ya binadamu angeona aibu na kusikitikia tukio lile linalolaaniwa na watanzania na dunia nzima na hata kuisababishia serikali kupata matatizo kwa wahisani kama Umoja wa nchi za Ulaya uliyvotolea kauli jana.
   
 19. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  History inaonyesha, Makamanda wa Policcm wanaoua ndio hupanda vyeo.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,925
  Trophy Points: 280
  Mauwaji aliyoyafanya ni ya kisiasa,na kwahiyo majibu yake pia ni ya kisiasa.

  Hata asipojiuzulu,kuna wakati atajibu tuhuma hizi za mauwaji.Nchi za wenzetu kashfa kama hii wala asingethubutu kupanua mdomo,maana angekuwa keshajiuzulu na angeogopa maneno yake yasitumike dhidi yake wakati wa mashtaka.Kwa mfano kauli kuwa watu wakikusanyika kufunguwa tawi basi wauwawe kwasababu wamevunja sheria.Kauli kwamba walifanya maandamano ni ya kisiasa,kwasababu mwanzoni alisema ni mikutano haitakiwi kwasababu ya sensa,lakini cha ajabu ccm ilikuwa na mikutano,na pia kulikuwepo na fiesta.

  Only in Tanzania haya ndo yanaonekana kuwa ni ya kawaida.
   
Loading...